Baadhi Ya Sifa Za Sauti Zoloto Zinazotumiwa Na Baadhi Ya Wahubiri Wa Kipentekosti Kuwasilisha Injili Na Umuhimu Wake
Loading...
Date
2023
Authors
Nyambura, Teresiah
Githinji, Peter
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
EANSO
Abstract
Makala haya yalilenga kubainisha baadhi ya vigezo vinavyobainisha sauti
zoloto zinazotumiwa na baadhi ya wahubiri wa Kipentekosti kama mtindo wa
kuwasilisha injili. Tulilenga waumini wa madhehebu tofauti ya Kipentekosti
katika eneo la Gilgil katika kaunti ya Nakuru. Tulitumia mihimili miwili ya
nadharia ya “Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji” (Bell, 1984, 2014).
Mhimili wa kwanza unadai kuwa Mtazamo wa wasikilizaji hutumika katika
viwango vyote vya lugha iwe ni lugha moja au wingi lugha kwani haiangazii
tu kubadilisha mtindo wa utamkaji wa sauti, bali pia uchaguzi wa jinsi ya
kutamka sauti na upole wa mazungumzo. Mhimili wa pili hudai kuwa mtindo
wa matumizi ya lugha katika uzungumzaji huwa chanzo cha mabadiliko katika
mahusiano ya mazungumzo. Usampulishaji wa kimaksudi ulitumika kwa
sababu ya urahisi wa kupata walengwa wa makala haya. Kiasa kikubwa cha
data kilitokana na kanda za sauti za mahubiri mbalimbali kutoka kwa wahubiri
tofauti. Hatimaye, kanda tatu ambazo wahubiri walizolota na tatu ambazo
wahubiri hawakuzolota zilitumika. Kanda za mahubiri zilichujwa kwa
kutumia programu ya PRAAT ili kupata sifa za kiakustika zinazobainisha
sauti zoloto. Mbinu za hojaji, mahojiano na wahubiri binafsi, uchunzaji na
mahojiano na makundi legwa zilitumika katika uchanganuzi na ufasili wa
data. Matokeo ya utafiti yalibainisha vigezo vikuu vitano ambavyo ni kipimo
cha hezi, urefu wa mawimbi ya sauti, kiwango cha desibeli, mpumuo wa sauti,
kiwango cha tambo na tofauti kati ya fomanti ya kwanza na ya pili kama
baadhi ya sifa zinazobainisha sauti zoloto za wahubiri wa Kipentekosti.
Description
Article
Keywords
Kanisa za Kipentekosti, Kanisa zisizo za Kipentekosti, Sauti Zoloto, Uzolotaji, Wapentekosti, Wasikilizaji
Citation
Nyambura, T. & Githinji, P. (2023). Baadhi Ya Sifa Za Sauti Zoloto Zinazotumiwa Na Baadhi Ya Wahubiri Wa Kipentekosti Kuwasilisha Injili Na Umuhimu Wake East African Journal of Swahili Studies, 6(1), 68-83. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1166.