Usomaji na Ufasiri Sasa wa Utenzi wa Mwanakupona

Loading...
Thumbnail Image
Date
2017-06
Authors
Munyole, Simiyu Dennis
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulichunguza usomaji na ufasiri sasa wa Utenzi wa Mwana Kupona sasa. Uchunguzi huu uliongozwa na malengo, maswali ya utafiti, pengo la utafiti na mihimili ya nadharia. Malengo ya utafiti huu yalikuwa: kubainisha mazingira chipuzi ya Utenzi wa Mwana Kupona, kueleza maudhui yaliyowasilishwa na mtunzi katika Utenzi wa Mwana Kuponzi na kueleza usomaji na ufasiri wa utenzi huu kwa kuzingatia aina ya wasomaji mbalimbali katika mazingira ya sasa. Utafiti huu ulitokana na hali kuwa vipindi tofauti vya kihistoria vimepita tangu utunzi wa utenzi huu. Katika vipindi hivi vya kihistoria, kumekuwa na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Kutokana na mabadiliko haya ilikuwa ni vyema kuchunguza usomaji na ufasiri wa utenzi huu katika mazingira ya sasa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uhistoria Mpya na nadharia ya Mwitikio wa Msomaji. Nadharia ya Uhistoria Mpya huangalia matini ya jadi katika muktadha wa wakati uliopo. Nadharia hii ilitumika katika kuchunguza nafasi ya mazingira katika usomaji na ufasiri wa Utenzi wa Mwana Kupona. Aidha nadharia ya Mwitikio wa Msomaji hutathmini upokezi wa wasomaji wa kazi mbalimbali za fasihi. Nadharia hii ilitumika kuchunguza usomaji na ufasiri. Nadharia hizi ndizo zilizouongoza utafiti huu. Muundo wa utafiti ulikuwa wa kisoroveya. Sampuli lengwa katika utafiti huu ilikuwa wasomaji kutoka jimbo la Lamu na Nairobi. Mbinu ya kusudio ilitumika ambapo wasailiwa ishirini (20) kutoka Lamu na wengine ishirini (20) kutoka Nairobi walishughulikiwa na watafiti kupitia mwongozo wa maswali. Utafiti huu ulifanywa maktabani na nyanjani. Mbinu kuu ya kukusanya data ilikuwa ni usomaji maktabani na mahojiano nyanjani. Data iliyokusanywa maktabani na nyanjani ilipangwa kulingana na vigezo maalum na uchanganuzi wake kuongozwa na maswali ya utafiti, malengo, pengo la utafiti na mihimili ya nadharia. Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Ilibainika kwamba mazingira ya usomaji wa kazi fulani ya fasihi pamoja na tajiriba za msomaji huathiri kwa kiasi kikubwa jinsi anausawiri na kuona ulimwengu. Mtazamo wa msomaji wa kazi fulani ya fasihi humwelekeza jinsi anavyoifasiri kazi mahususi ya fasihi ambayo ameisoma. Aidha ilibainika kuwa ufasiri wa wasomaji mbalimbali wa utenzi huu umebadilika. Kwa hivyo, kadri mazingira na mienendo ya jamii inavyoendelea kubadilika ndivyo usomaji, ufasiri na upokezi wa kazi hiyo unavyobadilika.
Description
Tasnifu Iliyowasilishwa Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta Juni 2017.
Keywords
Citation