Usawiri wa mishororo katika ushairi wa Kiswahili
Loading...
Date
2016
Authors
Ndirangu, Teresa Wanjiku
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulitathmini kuchunguza usawiri wa mishororo katika ushairi wa Kiswahili.
Diwani mbili zilirejelewa: Tamthilia ya Maisha (2005) iliyohaririwa na Kyallo Wadi
Wamitila na Diwani ya Karne Mpya (2007) ambayo imehaririwa na Ken Walibora.
Utafiti huu ulidhamiria kutimiza malengo matatu makuu. Kwanza, tulilenga kuainisha
mishororo katika mashairi teule kutoka diwani hizo. Pili, kuchunguza dhima mbalimbali
za mishororo hiyo. Aidha, tulilenga kuchunguza jinsi usawiri wa mishororo
ulivyofanikisha usawiri wa dhamira na maudhui. Nadharia ya Kiutanzu iliongoza utafiti
huu ambapo mihimili yake ilitumiwa kuhakiki mishororo kama sifa ya msingi ya utanzu
wa ushairi. Imetusaidia kuhakiki sura mbalimbali za mishororo na nafasi zake katika
usawin wa mashairi. Data ilikusanywa kwa kusoma kwa kina na kunukuu mistari
iliyotuelekeza kwenye malengo ya utafiti wetu. Data hiyo imechanganuliwa na
kuwasilishwa kwa mbinu ya kimaelezo kuambatana na malengo, maswali ya utafiti na
nadharia iliyozingatiwa. Uwasilishaji umefanywa kwa sura tano. Sura ya kwanza ina
sehemu zifuatazo: utangulizi, mada ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka,
yaliyoandikwa kuhusu mada na misingi ya nadharia. Sura ya pili imechunguza historia
na mabadiliko ya ushairi wa Kiswahili. Sura ya tatu imelenga kuainisha mishororo na
sura ya nne imeshughulikia dhima za mishororo hiyo. Sura ya tano imeshughulikia
muhtasari, hitimisho na mapendekezo ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu yatawafaa
wanafunzi, wahakiki na watunzi wa mashairi kwa jumla.
Description
Tasnifu hii imetolewa ill kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika chuo Kikuu cha Kenyatta