Usawiri wa maswala-ibuka katika hadithi za watoto
Loading...
Date
2012-07-24
Authors
Karanja, Dorcas Wanjiku
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Tasnifu hii inajadili usawiri wa maswala-ibuka katika hadithi za watoto. Vitabu vya hadithi vilivyoteuliwa ni miongoni mwa vile ambavyo vimependekezwa na Tume ya Elimu nchini Kenya, visomwe na wanafunzi wa darasa la nne hadi la nane katika shule za msingi, na vivyo ni 'Mnyama mwenye Huruma (2005) na Rebecca Nandwa, 'Ndoto ya Riziki' (2005) na Razwana Kimutai., 'Mama wa Kambo' (2005) na Catherine Kisovi,'Yalianza kimchezomchezo' (2000) na Angelina Mdari, 'Mchuuzi wa matambara' (2006) na Edward Were na 'Ngano za mfalme Tapwara Tapwara'. Nadharia iliyotumika ni ile ya kimtindo na ile yauhalisia. Mihimili ya nadharia hizi ilitumika kama dira ya kuuongoza utafiti huu katika kuyaafiki malengo yake.
Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kuainisha maswala-ibuka katika vitabu vya hadithi vya watoto vilivyoteuliwa, lengo la pili lilikuwa ni kuonyesha mitindo iliyotumiwa na waandishi katika kuyasawiri maswala-ibuka na mwisho kabisa utafiti huu ulilenga kutathmini ufaafu wa mitindo hii katika fasihi ya watoto.
Data iliyotumika katika utafiti huu, ilikusanywa maktabani ambapo mapitio ya vitabu, majarida, magazeti na tasnifu, yalisaidia katika kuupa msingi utafiti huu, kinadharia na kimpangilio wa data. Data iliyopatikana ilichanganuliwa. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo.
Tasnifu hii ina jumla ya sura tano. Utafiti umeonyesha kuwa waandishi wa fasihi ya watoto wamefaulu katika kuangazia maswala-ibuka katika kazi hizi. Aidha mitindo iliyotumika inafaa na inaafiki kiwango cha watoto.
Description
Department of Kiswahili and African Languages Department: 135p. The PL 8702 .K37 2012
Keywords
Swahili language, Grammar, Study and teaching