Methali za Kiswahili kama chombo cha mawasiliano: mtazamo wa kisiimu - Jamii
Loading...
Date
2012-06-06
Authors
Maitaria, Joseph N.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Tasnifu hii imejadili Methali za Kiswahili kama chombo cha mawasiliano. Kazi hii inajaribu kuonyesha kwamba Methali kama vile lugha, ni zao la jamii na hutokana na utamaduni wa jamii mahsusi. Haya yote yamechunguzwa chini ya msingi wa Isimu-Jamii.
Katika kutekeleza lengo langu nimegawanya tasnifu hii kwa sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi. Sura hii inaonyesha malengo ya tasnifu hii, sababu za kulichagua somo hili na nadharia ya tasnifu hii. Aidha nimeeleza kazi ambazo zimefanywa kuhusu methali kwa ujumla.
Sura ya pili inajadili historia ya Waswahili na utamaduni wao. Imani yangu ni kuwa Waswahili ni jamii yenye makazi yake pwani ya Afrika Mashariki ni uvumi kwamba jamii hii iliibuka baada ya wageni (Waarabu) kuja na kutamakani sehemu hizo. Fauka ya hayo nimeelezea namna methali za Kiswahili huibuka katika mazingira na utamaduni mahsusi.
Sura ya tatu nimejadili sifa mbalimbali zinazobainika katika baadhi ya methali za Kiswahili. Sura ya nne imeshughulikia matumizi ya methali za Kiswahili katika mawasiliano ya kijamii. Katika kufanya hivyo inabainika kuwa matumizi ya methali katika mawasiliano huathiriwa na miktadha na utamaduni wa jamii.
Sura ya tano ndiyo hitimisho. Nimetoa msimamo wangu kwamba methali kama vile lugha, huibuka katika mazingira maalum. Kwa hivyo matumizi ya methali katika mawasiliano huathiriwa siyo tu na miktadha bali pia na tamaduni zilimoibuka.
Description
The PL 8704.A2 M3
Keywords
Kiswahili Literature--Proverbs//Proverbs--Kiswahili