Ufundi katika riwaya za Mohammed Said Abdulla
Loading...
Date
2012-05-09
Authors
Kamau, Margaret
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Tasnifu hii imejadili ufundi katika riwaya za Mohammed Said Abdulla. Kazi hii inajaribu kuonyesha ufundi alioutumia mwandishi katika kuwasilisha ujumbe wake.
Sura ya kwanza ni utangulizi was utafiti wetu. Hapa tumejadili somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, upeo na pia sababu za kulichagua somo hili. Hali kadhalika tumegusia yale yaliyoandikwa na wengine kuhusu somo hili pamoja na machache kuhusu nadharia inayotuongoza katika uchunguzi wetu. Mwisho tumejadili njia za utafiti ambazo tumetumia kufanikisha utafiti wetu.
Sura ya pili inaangalia maisha ya mwandishi ili kuona ni mambo yapi yalimwathiri katika utunzi wake. Sura hii pia yaangalia sifa za fasihi ya upelezi ili kusaidia msomaji kuelewa mkondo wa riwaya za mwandishi. Muhtasari wa vita alivyoandika mwandishi pia umetolewa katika sura hii.
Sura ya tatu inajadili mbinu za unahishaji wa maana zilizotumiwa na mwandishi Abdulla. Tamathali zilizojadiliwa ni methali, misemo tashhisi na stiari. Tumebaini jinsi tamathali hizi zilivyotumiwa na mwandishi katika kuwasilisha ujumbe wake.
Sura ya nne imejadili ubunifu katika kazi za mwandishi Abdulla. Tamathali tulizojadili ni takriri, mazungumzo, tabaini, lafidhi, maelezo, tashbihi na tanakali. Tmebaini jinsi tamathali hizi zilivyotumia kwa njia ya ubunifu kuleta ufasaha wa kazi ya sanaa na kufanya usomaji uwe na kuvutia.
Sura ya tano ni hitimisho ya uchunguzi wetu. Katika sura hii tumetoa muhtasati wa kazi yetu kwa jumla na kuonyesha kwamba hata ingawa mwandishi hana maudhui mazito ametumia lugha kwa ufundi wa hali ya juu kisanaa. Zaidi ya hayo, tumejadili matatizo yaliyotukumba na kutoa mapendekezo ya maeneo yanayostahili kufanyiwa utafiti zaidi hapo baadaye.
Description
The PL 8704.U43 K3
Keywords
Swahili literature