Matumizi ya taswira na ishara katika sauti ya dhiki

Loading...
Thumbnail Image
Date
2012-01-09
Authors
Nyanchama, Marion
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia matumizi ya taswira na ishara katika Sauti ya Dhiki. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuhakiki diwani ya Sauti ya Dhiki ili kutaoa jinsi Abdilatif alivyotumia taswira na ishara katika kuwasilisha maudhui yake. Utafiti huu uliongozwa na nadharia changamano: semiotiki na nadharia ya uhakiki wa kitamaduni. Kimsingi, nadharia ya semiotiki inashughulikia ishara na uashiriaji, (maana zao) katika matini za kifasihi. Kwa upande mwingine, nadharia ya uhakiki wa kitamaduni ni nadharia itumikayo kueleza, kuainisha, kuchanganua na kufasiri kazi za kifasihi kwa kuzingatia mtazamo wa kiutamaduni. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti na madhumuni ya utafiti. Pia, sura hiyo imegusia yale yaliyoandikwa kuhusu mada pamoja na nadharia zilizoongoza utafiti huu. Sura ya pili imeshughulikia yanayohusu mwandishi na utamaduni wa Waswahili, hususan eneo la k*grafia la Waswahili, mpangilio wa jamii ya Waswahili, imani, dini na matumizi ya lugha, shughuli za kiuchumi, umuhimu wa ushairi, pamoja na uhusiano wa historia na Sauti ya Dhiki. Maelezo haya yanachangia katika kuweka msingi bora wa kuelewa yanayozungumziwa katika Sauti ya Dhiki, katika kutoa muktadha unaofaa. Sura ya tatu imeshughulikia lugha na utamaduni, pamoja na ishara na uashiriaji. Sura hii pia inasaidia kuelewa Sauti ya Dhiki kupitia uchanganuzi wa matumizi ya taswira na ishara kwa kuzingatia mihimili ya nadharia changamano. Sura ya nne imechanganua Sauti ya Dhiki. Uchanganuzi huu umebainisha matumizi ya taswira na ishara katika kuwasilisha maudhui ya diwani hiyo. Katika kufanya hivyo, sura hii imechanganua baadhi ya tungo ili kubainisha taswira na ishara ya: mnazi, mamba, jimbi, jipu pamoja na ishara ya mama. Katika sura ya tano, utafiti huu umezingatia tungo zinazobainisha taswira na ishara ya: mtoto aliye tumboni, nyundo, safari, mvua, kujinyoa, moyo pamoja na ngome. Matumizi ya taswira na ishara katika diwani hii yamesaidia kuona jinsi Abdilatif alivyotumia fani hizo, na hivyo kufanikisha uelewa wa maudhui yanayozungumziwa. Sura ya sita imejikita katika kutoa mahitimisho, matokeo na mapendekezo ya utafiti.
Description
Department of Kiswahili and African Languages, 196p. The PL 8704.M3N9 2004
Keywords
Swahili poetry--Study and teaching
Citation