Taswira ya mwanamke kama inavyojitokeza katika nyimbo za kisasa za Rap

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-12-16
Authors
Wachira, James Waweru
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia taswira ya mwanamke kama inavyojitokeza katika nyimbo za kisasa za Rap. Mtafiti amehakiki tungo za wasanii wa kike na wa kiume ambazo ni mojawapo wa tanzu mpya za fasihi simulizi. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha usanii ambayo ni nadharia ya uchanganuzi-nafsia katika mtazamo-kike. Nadharia hii hujishughulisha na hali za kinafsi hasa kupitia kwa matumizi ya lugha. Nadharia hii imetumika kwa kuzingatia lugha kama utaratibu wa kiishara katika utafiti huu. Tasnifu hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambapo mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, pamoja na upeo wa utafiti huu zimeshughulikiwa. Pia, udurusu wa maandishi yanayohusu mada hii pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti huu imejadiliwa. Sura ya pili inashughulikia itikadi mbalimbali zinazojitokeza katika nyimbo za wasanii wa kiume wa nyimbo za kisasa za rao kuhusu taswira ya mwanamke katika jamii. Katika sura ya tatu, taswira ya mwanamke kama inavyosawiriwa na wasanii wa kike wa nyimbo hizi imejadiliwa. Sura ya nne imeshughulikia baadhi ya mambo ya kitamaduni yanayoathiri jinsi mwanamke anavyosawiriwa na wasanii hawa. Sura ya tano ni hitimisho linalotoa muhtasari na matokeo ya utafiti huu, pamoja na mapendekezo ya utafiti. Mwisho kabisa, kuna marejeleo na kiambatisho cha data iliyotumika katika utafiti huu
Description
Department of Kiswahili and African Languages, 171p. The PL 8704.W3T3 2006
Keywords
novel
Citation