Uchambuzi wa matini: matumizi ya lugha katika sajili ya matatu

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-12-08
Authors
Kihara, David Kung'u
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Katika tasnifu hii, tumechambua matini ili kubaini matumizi ya lugha katika sajili ya matatu kwa ujumla. Tumechanganua data kutoka vituo vikuu vya magari ya matatu na njiani abiria waliposafirishwa. Utafiti huu ulikuwa na malengo manne ambayo ulitekeleza. Kulikuwa na kuchanganua sifa zinazobainisha sajili ya matatu, kuchanganua aina za maana zinazowasilishwa na matini zinazotumika, kubainisha athara za maana na ujumbe, na kuchunguza msimbo wa maana. Kwa kutekeleza haya, nadharia ya isimu amilifu na hasa mtazamo bayana wa Isimu Amilifu Mfumo ulitumika. Sarufi Amilifu Mfumo (SAM) inajivunia uyakinifu wa kiisimu. Pamoja na uyakinifu wa kiisimu SAM inadai uhalisia wa Kipragmatiki sawia Kisaikolojia. Uwiano wa mambo haya ni msingi wa dhana ya udokezi maana. Utafiti huu umehusisha mbinu mbili kuu za utafiti wa maktabani na ule wa nyanjani. Uchanganuzi wa data ulihusisha uanishaji wa makundi ya msimbo, sifa bainifu na athara za matumizi ya lugha katika sajili ya natatu. Matokeo ya utafiti yamejumuishwa katika sura tatu. Utafiti umeonyesha kuwa sajili ya matatu ina msimbo wake. Imedhihirika pia ya kwamba sajili hii hubainishwa kwa sifa za aina mbalimbali, sifa wazi zaidi zikihusu umbo, muundo na matumizi ya lugha. Aidha, utafiti umedhihirisha kuwa matumizi ya lugha katika sajili ya matatu huwa na athari mbalimbali zinazowaathiri wahudumu na abiria kimawazo na kihisia.
Description
The PL 8702 .K54
Keywords
Swahili language//Transportation--Kenya--Nairobi
Citation