Lugha ya kimafumbo katika riwaya za katama mkangi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2014-10-09
Authors
Kamachu, Mercy Waruguru
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu utashughulikia matumizi ya lugha ya kimafumbo katika riwaya za Mkangi Mafuta (1984) na Walenisi (1995). Kutokana na udurusu wa maandishi ya wahakiki na watafiti mbalimbali wa riwaya za Mafuta (1984) na Walenisi (1995) imebainika kwamba kuna pengo linalohitaji utafiti zaidi. Matumizi ya lugha ya kimafumbo inayojumuisha istiari, tashbihi, jazanda, majazi, methali na nahau haijashughulikiwa kama mada mahususi ya utafiti katika riwaya hizi mbili. Malengo ya utafiti huu ni; kubainisha mifano ya matumizi ya lugha ya kimafumbo katika riwaya teule, kukadiria mchango wa lugha ya kimafumbo katika kuibulia na kuendeleza maudhui, mwisho ni kutathmini jinsi lugha ya kimafumbo inavyotumiwa katika usawiri na uainishaji wa wahusika katika riwaya hizi. Mada hii ya "lugha ya kimafumbo" katika riwaya za Mafuta (1984) na Walenisi (1995) iliteuliwa kwa kuzingatia sababu kadhaa. Kwanza, lugha ya kimafumbo ni miongoni mwa vipengele muhimu vya lugha katika kazi za fasihi. Pili, riwaya za Mkangi hufunzwa vyuoni na shuleni. Katika kuwasaidia wasomaji wa riwaya hizi kuelewa zaidi, haina budi kutathmini na kubainisha lugha ya kimafumbo iliyotumiwa na mwandishi katika riwaya teule. Mwisho ni kwamba, utanzu wa riwaya unaendelea kukua, hivyo basi utafiti unafaa kufanywa ili kutathmini mitindo ya lugha aliyotumia mwandishi. Utafiti huu utaongozwa na nadharia nadharia ya kimafumbo ya kisasa ambayo waasisi wake ni Lakoffna Johnson (1992). Data itakayokusanywa itachanganuliwa kwa kuzingatia lugha ya kimafumbo kwa usaidizi wa mihimili ya nadharia ya kimafumbo ya kisasa. Utafiti huu utasaidia katika uhakiki wa fasihi kwa upande wa riwaya.
Description
Keywords
Citation