Osore, Miriam2023-11-222023-11-222018Miriam Osore (2018): ‘Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo ya kukuza na kuendeleza Kiswahili’ in Lugha na Maswala Ibuka’, edited by Kandagor M. Obuchi, S. M. and Mwanakombo, N. M., Nairobi, Chama cha Kiswahili cha Taifa, pp 123 – 135. ISBN: 978-9978-5058-56.http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27178Book ChapterMatumizi ya Kiswahili yametanuka kimaeneo kutoka pwani na maeneo ya Bara Hindi na kuendelea kutumika katika nchi nyingine barani Afrika na mabara mengineyo. Kiswahili sasa kinatumika katika nchi ya Kongo, Afrika Kusini, Rwanda, Burundi, Gabon, Marekani, Ujerumani, Bara la Ulaya, Uchina na kwingineko. Kiswahili kinatambulika miongoni mwa lugha kuu za kimataifa kama vile Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kihispaniola, na hata Kireno. Kati ya lugha za Kiafrika kama Hausa na Kilingala, Kiswahili ndiyo lugha ambayo imeenea kwa kasi na kuvuka mipaka ya bara la Afrika hadi kwingineko ulimwenguni. Awali, wamisionari walipofika Afrika Mashariki, walijifunza Kiswahili. Waliporejea kwao, walianzisha mafunzo ya Kiswahili kwa wale ambao walinuia kuzuru Afrika Mashariki kwa shughuli mbalimbali kama biashara, dini na utawala. Wataalamu wengi wa bara la Ulaya, walijitolea kufanya utafiti na kuandika vitabu kuhusu Kiswahili. Kwa mfano, Askofu Steere, Whiteley, Ashton na Krapf. Waliandika vitabu kama vile Handbook of Swahili Language (1870) cha Steere na Swahili Dictionary (1850) .cha Krapf. Uandishi wa vitabu hivi ni miongoni mwa hatua za mwanzo za kukiendeleza Kiswahili. Huko Marekani, Wamarekani wenye asili ya Kiafrika na Wazungu wamekuwa wakijifunza Kiswahili kama mojawapo ya masomo katika vyuo vikuu. Kwa Wamarekani weusi, hatua hii ni kama kielelezo cha urithi wa utamaduni wao. Barani Afrika, Kiswahili kinatumiwa kuleta utangamano kati ya jamii mbalimbali. 123 Kiswahili kimeteuliwa kama lugha mojawapo iliyo rasmi ya Umoja wa Afrika (VA). Lugha nyingine ni Kiingereza, Kifaransa, Kiispaniola, Kireno na Kiarabu. Aidha, Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika. Katika kiwango hiki, Kiswahili ni lugha ya kimataifa. Kiswahili kimepanda hadi ngazi ya kimataifa kwa sababu mbalimbali. Kwa mujibu wa Mbaabu (1979) baadhi ya sababu hizo ni kwamba Kiswahili ni lugha ambayo haina mihemko ya kisiasa; inakubali mabadiliko ya istilahi mpya na unyambuaji wa maneno. Aidha, Kiswahili hakina vikwazo vya kimazingira; kina maandishi, historia na fasihi yake (Chiraghdin na Mnyampala, 1977).otherTeknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo ya kukuza na kuendeleza Kiswahili’ in Lugha na Maswala IbukaBook chapter