Hamisi, Omar Babusa2011-12-222011-12-222011-12-22http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/2093Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi Yamahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo kikuu cha kenyatta 2005 The PL 8704.V5B3Tasnifu hii imeshughulikia uainishaji wa mashairi ya Kiswahili kwa kutumia vigezo badalia. Imechanganua historia ya mashairi ya Kiswahili kiwakati na vile yalivyoainishwa kabla ya kuzuka kwa mashairi huru. Pia imetoa sababu za kubadilika kwa tanzu za ushairi ambazo zimesababisha kubadilika kwa uainishaji wa ushairi wa Kiswahili. Sura ya kwanza ni utangulizi na ni muhtasari wa mwongozo uliotusaidia katika utafiti wa kuainisha mashairi ya Kiswahili. Mambo yaliyojadiliwa katika sehemu hii ni: swala la utafiti, madhumuni ya tasnifu, nadharia tete, misingi ya nadharia na upeo wa utafiti. Sura ya pili inaainisha mashairi ya Kiswahili kabla ya kuja kwa maandishi. Katika kipindi hiki tukagundua ya kwamba kulikuwa na matapo mawili ya mashairi. Yaliyofuata arudhi na yasiyo na arudhi. Nyimbo za Waswahili za wakati huo hazikufuata arudhi za vina na mizani. Tulikubaliana ya kwamba mashairi ambayo hayakufuata arudhi yalikuwepo hata kabla ya majilio ya wageni. Na mashairi ya kipindi hiki yaliainishwa kwa kigezo cha maudhui. Katika sura ya tatu, tumechambua tanzu za mashairi ya Kiswahili baada ya kuja kwa hati za Kiarabu. Tukaeleza athari ya Waarabu kwa Waswahili na vile Waarabu walivyokuja na ushairi wa arudhi. Tanzu nyingi za dini ya IGislamu ziliibuka katika kipindi hid. Mashairi yakahifadhiwa katika hat za lGarabu. Mashairi yote ya Kiswahili katika kipindi hiki yalifuata arudhi na yaliainishwa kwa kigezo cha muundo. Sura ya nne imechambua mashairi yaliyofuata arudhi za Urasimi Mkongwe baada ya kuja kwa hati za Kirumi. Tulieleza vile washairi wa tapo hill walivyoshikilia kuwa shairi la Kiswahili lazima liwe na urari wa vina na mizani. Pia tukaona vile - - washairi haws walivyojaribu kufufua sheria za utungaji za mashairi ya kimapokeo. Wanajopo hili waliainisha mashairi kwa kigezo cha muundo. Katika sura ya tano, tumeeleza chimbuko la mashairi huru ya kiswahili na waasisi wake. Tukaeleza sababu za kuzuka kwa tanzu hizi mpya ambazo zilileta mgogoro na kupendekeza vigezo badalia vya kuainisha mashairi haya. Vigezo tuiivyopendekeza vilijumuisha mashairi yote; ya arudhi na yasiyo na arudhi na kupendekeza sheria mpya za kutunga mashairi ya kiswahili. Sura ya sita ni hitimisho. Sura hii imeelezea matokeo ya kuainisha upya mashairi ya Kiswahili ambapo ni kupunguza mgogoro na kupndekeza fasihi ya IGswahili. Pia katika sura hii tumependekeza juu ya utafiti zaidi juu ya kuainisha tanzu za mashairi ya Kiswahili.enSwahili poetryVigezo badalia kuhusu uainishaji wa mashairi ya kiswahiliThesis