Sichangi, Geoffrey Mukhono2011-11-152011-11-152011-11-15http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/1641The P 96 .L34S5Utafiti huu umechambua matini ili kutathmini mafanikio ya uarifu katika taarifa za habari zinazosomwa kwa Kiswahili kwa madhumuni ya kuonyesha utoshelevu wa uarifu. Tumechanganua data kutoka kwenye vituo vya utangazaji vya KBC na Redio Citizen. Watafitiwa ambao walishirikishwa katika utafiti huu waliteuliwa kutoka eneo la Kahawa Sukari, wilayani Thika. Vigezo vya wasikilizaji wenye umri, elimu na jinsia tofauti vilitumika. Mchango wa kazi hii ulilenga kuziba pengo katika isimu lililosababishwa na tatizo la ukosefu wa uarifu katika taarifa za habari zinazosomwa kwa Kiswahili. Ili kufanikisha utafiti huu, nadharia ya isimu amilifu ilitumika. Maana zinazotambuliwa na mtazamo wa Sarufi Amilishi Mfumo kwa mujibu wa Halliday zilitumika katika kuchanganua uarifu, huku vigezo vya umatini kwa mujibu wa Dressler na Beaugrande vikitumika katika kutathmini umatini wa taarifa za habari. Matokeo ya utafiti huu yamewasilishwa kwa njia ya maelezo, katika sura tatu. Imedhihirika katika utafiti huu ya kwamba taarifa za habari zinazowasilishwa katika Kiswahili huarifu kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, uarifu katika taarifa za habari hutingwa zaidi na ukosefu wa kina katika habari, ukosefu wa ujumbe mpya pamoja na matumizi ya sentensi zisizofasirika kwa uwazi. Hatimaye, tumependekeza taratibu za kuboresha uwasilishaji wa taarifa hizo ili kufanikisha uarifu.otherMass media and language -- Kenya//Swahili language -- Social aspects//Radio broadcasting -- KenyaUarifu katika taarifa za habari : mtazamo wa isimu amilifuThesis