King'ei, Kitula Osore, MiriamAnyango, Pamela A.2018-03-142018-03-142016http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/18242Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha KenyattaUtafiti huu umelenga kuelezea uovu katika jamii kama unavyosawiriwa na Ben R. Mtobwa. Maswala yanayotendeka ni nyeti na ibuka katika jamii ya sasa. Riwaya ambazo zimeshughulikiwa ni Salamu Kutoka Kuzimu (1984) na Tutarudi na Roho Zetu (1987). Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kubainisha aina ya maovu, kueleza kiini cha uovu huo, kuonyesha athari ya uovu huu na kuangalia mbinu za upelelezi zinazotumiwa na mwandishi kukabiliana na uhalifu. Mwandishi huyu anatumia fasihi kuyasawiri maovu yanayotokea katika jamii. Mwandishi huyu anatumia fasihi kuyasawiri maovu yanayotokea katika jamii. Aidha, anaonyesha namna wahusika katika riwaya hizi wamesukumwa na jamii zao kuwa waovu. Utafiti huu umeongozwa na mihimili ya nadharia mbili kutimiza malengo yake. Nadharia ya Maadili na ile ya Uhalisia. Nadharia ya Maadili iliasisiwa na wanafalsafa Plato (c443) na Jean Jacques Rousseau (1712-1778). Waitifaki wa nadharia hii ni Tolstoy (1960), Hough (1966), Palmer (1992), na wengine. Nadharia hii ya Maadili imekusudiwa kushughulikia mtazamo wa mwandishi kuhusu uovu. Nadharia ya Uhalisia iliasisiwa na Hegel. Waitifaki wa nadharia hii ni Georg Lukacs (1972) na wengine. Nadharia hii imeshughulikia mambo ya kihalisia katika jamii. Mihimili ya nadharia hizi imeuongoza uhakiki wa riwaya zilizoteuliwa ili kupata data inayotosheleza utafiti huu. Data hiyo imerekodiwa na kuchanganuliwa kulingana na maswali ya utafiti pamoja na mihimili ya nadharia. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mada, sababu za kuchagua mada, misingi ya nadharia, mbinu za utafiti na uchanganuzi wa data. Sura ya pili imejadili historia ya mwandishi na kuandika machache kuhusu dhana ya uovu. Sura ya tatu imejadili kiini, athari na mbinu za upelelezi zinazotumika kumaliza uovu katika Salamu Kutoka Kuzimu (1984). Sura ya nne imejadili kiini, athari ya uovu huo kwa wanajamii na mbinu za upelelezi zilizotumika kuzuia uovu katika Tutarudi na Roho Zetu (1987). Sura ya tano imejumuisha muhtasari wa utafiti, matokeo ya utafiti, mchango wa utafiti na mapendekezo. Utafiti huu unanuiwa kuwa wenye manufaa kwa wahakiki wa fasihi, wakuza mitaala, wapenzi wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa jumla.enUsawiri wa Uovu Katika Riwaya Teule za Ben R. MtobwaThesis