Alice Nyambura MwihakiMbaabu, I. G.Mumbua, David Jane2011-11-152011-11-152011-11-15http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/1638Department of Kiswahili and African Languages,124p.The PL 8351 .D3 2008.Utafiti huu ulidhamiria kuchanganua mchakato wa kisemantiki kwa kuegemea maneno mkopo ya Kikamba kutoka Kiswahili. Uchanganuzi huu hasa ulilenga kubainisha kanuni zinazotawala taratibu mbalimbali za utohozi maana. Tafiti awali zimeangazia zaidi utohozi fonolojia na utohozi mofolojia bila kuzingatia kanuni katika mchakato wa utohozi maana. Aidha kazi hii ilinuia kufidia upungufu wa tafiti awali kwa dhamira ya kupanua ufahamu zaidi katika mfumo wa maana, na semantiki ya Kikamba. Utafiti ulifuata nadharia msingi ya Tahakiki Usemi na kushirikisha Sarufi Amilishi Mfumo. Kwa jumla nadharia hizi hutazama lugha kama mfumo wenye maana na unaodhibitiwa na mfumo wa kijamii. Utafiti huu pia ulihusisha njia mbili kuu za utafiti: utafiti wa nyanjani na ule wa maktabani. Tasnifu ya utafiti imewasilishwa kwa njia ya maelezo, mifano na vielezo katika sura nne. Sura ya kwanza maswala ya kimsingi yanajitokeza: usuli wa mada, swala la utafiti, upeo na mipaka ya utafiti, tahakiki ya maandishi, misingi ya nadharia na uchanganuzi wa data. Sifa za kifonolojia, kimofolojia na kisemantiki zimeangaziwa katika sura ya pili yaani muundo wa maneno ya Kikamba. Matokeo kuhusu taratibu za utohozi semantiki na kanuni husika katika maneno mkopo yaliyochanganuliwa yamefafanuliwa katika sura ya tatu. Jumla ya mahitimisho, matokeo ya utafiti na mapendekezo ya utafiti yamejadiliwa katika sura ya nne. Imani na falsafa za kijamii ni miongoni mwa maswala yaliyodhihirika kuelekeza maana za maneno mkopo.otherKamba language -- Foreign words and phrasesLanguage and languages -- Foreign words and phrasesUchanganuzi semantiki wa maneno mkopo ya kikamba kutoka kiswahiliThesis