Sululu, Simiyu BensonWafula, Richard MakhanuMaitaria, Joseph Nyehita2023-07-122023-07-122021Sululu, S. B., Wafula, R. M., & Maitaria, J. N. (2021). Mchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi Katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Kufa Kuzikana. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 3(1), 91-99.http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/26189ArticleUsomaji wa fasihi katika kipindi cha sasa unabainisha idadi kubwa ya waandishi kutoka jamii zisizo Waswahili ambao wameandika kazi katika tanzu mahsusi za fasihi simulizi ya Kiswahili. Waandishi hawa wameendelea kutumia maudhui, ploti na vipengele vingine vya utamaduni wa fasihi simulizi za jamii zao katika kubuni kazi zao za fasihi andishi ya Kiswahili. Vipengele vya fasihi simulizi za jamii za waandishi hawa, wasiokuwa Waswahili, vimeingizwa katika riwaya ya Kiswahili na kuwa sehemu ya riwaya hii. Makala hii imechunguza jinsi uingizaji wa vipengele hivi vya fasihi simulizi za watunzi wa riwaya ya Kiswahili, wasiokuwa Waswahili, unaifanya riwaya hii kuwa ya kimahuluti. Mahsusi, makala hii imedadavua mchango wa tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi katika umahuluti wa riwaya ya Kiswahili kupitia mfano wa riwaya ya Kufa Kuzikana(2003) iliyoandikwa na Ken Walibora. Tathmini hii imetumia Nadharia ya Umahuluti wa Utamaduni inayoshikilia kwamba panapotokea hali ya mtagusano baina ya tamaduni tofauti, matokeo yake si wingi-tamaduni bali ni mchanganyiko wa vipengele kutoka tamaduni hizi mbalimbali ambao ni bora na imarazaidi kuliko tamaduni asilia. Nadharia hii imetumiwa kufafanua jinsi umahuluti wa riwaya ya Kiswahili umechangiwa na uingizaji wa vipengele vya tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi kutoka jamii za watunzi wake teule wasiokuwa Waswahili. Katika kufanya hivyo, makala hii imebainisha jinsi kuingizwa kwa vipengele hivi vya fasihi simulizi za jamii za waandishi teule katika riwaya ya Kiswahili kumeirutubisha riwaya hii kwa kuifanya kuwa changamano na nyumbufu kwa ambavyo inameza tanzu kutoka tamaduni tofauti na kujiimarisha kupitia kwazo bila kupoteza sura yake asilia.enWaswahiliFasihi SimuliziTanzu za KimaigizoRiwaya ya KiswahiliUmahulutiMchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi Katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Kufa KuzikanaArticle