King'ei, Kitula Osore, MiriamMwangi, Teresia Wanjiku2019-04-042019-04-042018http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/19401Tasnifu Hii Imewasilishwa Ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili, Katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. 2018Utafiti huu ulishughulikia mabadiliko ya nafasi na mtazamo wa wahusika wanaume katika riwaya mbili teule za Said A. Mohamed:Utengano (1980) na Dunia Yao (2006). Utafiti umebanisha kwamba kuna mabadiliko katika nafasi zao kwenye jamii hasa katika familia. Pia, mtazamo wao kuhusu wanawake na masuala mbalimbali katika maisha umebadilika. Aidha utafiti ulionyesha sababu zilizochochea kuzuka kwa mabadiliko hayo katika kusawiri wahusika wanaume. Ni wazi kuwa fasihi huchota mali ghafi yake kutoka kwa jamii na hivyo hali za kiuchumi, kisiasa, kijamii na vile vile tajriba yake mwandishi kwenye mazingira anamoishi, huathiri uandishi wake. Pia, utafiti ulijaribu kuonyesha athari za mabadiliko hayo katika uendelezaji wa riwaya kimaudhui. Ili kutekeleza hayo, tuliongozwa na nadharia ya uhalisia iliyoasisiwa na Gustave Flaubert na wengineo. Nadharia hii inajikita kwenye vitu thabiti vinavyohisika na mishipa ya fahamu ya mwanadamu na pia ukweli unaodhihirika katika kazi ya fasihi. Uhalisia wa kifasihi huonyesha uwezo wa kazi ya fasihi kuelezea hali kwa kuzingatia uyakinifu wa maisha. Kupitia kwa nadharia hii, ni wazi kuwa uhalisia wa mazingira anamoishi mwandishi na hata tajriba yake kwenye mazingira hayo, humwathiri pakubwa kwenye uandishi wake kama vile jinsi anavyowachora wahusika wake. Utafiti huu ni wa kimaelezo na ulifanyiwa maktabani. Sampuli iliteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio kwani ililenga vitabu mahsusi vya riwaya vinavyoonyesha mabadiliko hayo. Mtafiti alisoma kwa kina riwaya teule, vitabu, makala, majarida, tasnifu na hata tafiti na makala mtandaoni yenye ukuruba na mada ya utafiti huu. Aidha, vitabu na tafiti zilizofanywa kuhusiana na nadharia ya uhalisia zilisomwa. Baada ya kukusanya data na kuichanganua kutegemea malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia, mtafiti aliwasilisha matokeo kwa njia ya maelezo kwenye sura mbalimbali. Mtafiti anakisia kuwa matokeo ya utafiti huu yatadhihirisha kuwa mabadiliko ya nafasi na mtazamo wa wahusika wanaume yalisababishwa na mabadiliko ya mazingira alimokulia na alimoishi mwandishi, mabadiliko ya kijamii, kisiasa na hata tajriba na ukuaji wake kama mwandishi. Inatarajiwa kuwa wasomi, waandishi wa fasihi na hata watafiti wa kifasihi watanufaika kutokana na kazi hii.otherMabadiliko ya Nafasi na Mtazamo wa Wahusika Wanaume Katika Riwaya za Said A. Mohamed: Utengano (1980) na Dunia Yao (2006)Thesis