Osore, Miriam2023-11-222023-11-222023Miriam Osore (2023): ‘Itikadi ya Kuumeni katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi in Kiswahili Utaifa na Elimu Nchini Kenya, Njogu K. & Momanyi C. (edits), Nairobi, Twaweza Communications & UNESCO ISBN 978-9966-128-13-3 PP. 108 – 119.978-9966-128-13-3http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27171Book ChapterUtaifa hujengwa kutokana na mihimili ya usawa na haki kwa wote. Lakini, aghalabu; kutokana na itikadi za udume, wanawake hujikuta wananyanyaswa na kukandamizwa. Hali hii inawazuia kutoa mchano wao kikamilifu katika ujenzi wa taifa..Hatahivyo, kupitia fasihi.rnielekeo inayokandamiza inaweza kupunguzwa katika jamii. Usomaji wa fasihi unaobainisha udhaifu wa itikadi ya kuumeni unaweza kuchangia katika kubadili ubaguziwa kijinsia na kuimarisha usawa. Itikadi ya kuumeni imebainishwa na Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi kupitia mbinu ya ukiushi. Dhana ya ukiushi (dejamfZiarization) ina maana ya kudhihirisha kitu au hali kwa njia isiyokuwa ya kawaida, au isiyo dhahiri. Dhana hii hutumiwa kueleza kijumla hali ambapo kitu fulani hudhihirishwa kwa njia isiyo kuwa ya kawaida. Stacy (1977:178) anaeleza kuwa mbinu ya ukiushi hutumiwa kwa malengo mbalimbali; kwa mfano katika kuchekesha, kushangaza, kuhuzunisha, kukasirisha au kumfanyia mtu mzaha. Hata hivyo, mbinu hii imetumiwa kueleza uvumbuzi mpya ambao umebadilisha maisha, na fikra .za binadamu. Mbinu hii inapotumiwa katika fasihi huwa kimaksudi ili kudhihirisha jambo fulani. Mbinu ya ukiushi ina historia ndefu katika utunzi wa fasihi. Wananadharia na wanafasihi wamekiri, kwa mfano, kwamba mbinu ya ukiushi haiwezi kuepukika katika utunzi wa ushairi. Tangu awali, matumizi ya mbinu hii ya ukiushi yameelekea kusisitiza wazo kwamba, hutumiwa kwa malengo mawili: kiujumi na kudhihirisha 108 maana katika fasihi. George Steiner (1976:217-218), kwa mfano, anasema, "Lugha ndicho kifaa muhimu ambacho binadamu anaweza kutumia kukataa kuuona ulimwengu jinsi ulivyo" Anachosisitiza katika madai haya ni kwamba lugha hutumiwa kukiuka maana ya kawaida na kuvumbua njia mpya za kuuona ulimwengu. Dhana ya ukiushi katika fasihi iliasisiwa na mwanamaumbo mrusi Viktor Shklovsky ambaye aliunda dhana ya Kirusi 'Ostranenie' ambayo ilitafsiriwa katika Kiingereza kama "kueleza kwa njia ya ajabu" (making strange). Aliamini kwamba jukumu la fasihi lilikuwa kueleza au kubainisha ulimwengu kwa njia isiyokuwa ya kawaida. Alikirikwamba jukumu lafasihi lilikuwa kuchochea hisia za msomaji. Kwake 'Ostranenie' ilijumlisha mbinu zote ambazo mwandishi wa fasihi anaweza kutumia ili kubainisha kitu cha kawaida kwa njia ya kukifanya kieleweke kwa njia mpya. Kwa hivyo, alichukulia kwamba mbinu za ukiushi zililenga sio tu kudhihirisha maana, ,bali pia kutoa picha ya kipekee ya kile ambacho kilikuwa kikielezwa (Shklovsky,' 1965). Mbinu hizi zinapotumiwa katika fasihi,: hutufanya kuona m'ambo kwa njia iliyo tofauti kabisa na jinsi tunavyoyajua. Mbinu za ukiushi ni muhimu kwa, sababu msomaji wa fasihi huzitambua moja kwa moja anaposoma. Anapokutana na mbinu hizi, yeye hulazimishwa kutafakari na kisha kutambua ilemaana mpya inayokusudiwa na mwandishi. Mbinu hizi ni nyingi na huweza kuwa za kitamathali kama vile jazanda, taswira, tashihisi, tashbihi na methali. Makala hii inafafanua jinsi Euphrase Kezilahabi na Said Ahmed Mohamed wanavyoshughulikia na kubainisha itikadi ya kuurrieni (patriarchal ideology) kupitia mbinu za ukiushi. Watafiti wengi wameshughulikia mbinu mbalimbali za fasihi lakini si wengi ambao wamejaribu kuonyesha jinsi uhakiki wa mbinu za ukiushi unavyoweza kutumiwa kuelewa maana katika kazi za fasihi. Msimamo wetu ni kwamba mbinu za ukiushi ni muhimu katika utunzi wa fasihi na uchunguzi wa mbinu hizi unaweza kubainisha maudhui ya mwandishi kwa njia nzuri zaidi.otherItikadi ya Kuumeni katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi in Kiswahili Utaifa na Elimu Nchini KenyaBook chapter