Leonard Chacha MwitaAyiega, Mofart Onyoni2022-09-262022-09-262022http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/24291Tasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Februari, 2022Utafiti huu ulilenga kuchunguza ukiukaji wa Kanuni ya Kufuta Mabano katika uundaji wa nomino ambatani za Kiswahili. Nomino ambatani ni mofu changamano (Mgullu; 1999). Kanuni ya Kufuta Mabano huonyesha hatua zinazotumiwa kuunda neno sahihi kwa kutumia viambajengo. Mabano katika kanuni hii hudhihirisha mipaka na hufutwa kuashiria kuwa sheria za uundaji wa maneno hazina ufikiaji wa umbo la neno linalotokana na ngazi za awali. Uchunguzi huu ulifanywa baada ya kubaini kuwa baadhi ya nomino ambatani za Kiswahili hukiuka Kanuni ya Kufuta Mabano hasa pale ambapo mabadiliko hutokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa. Data ya uchunguzi huu ilikusanywa kutoka kwenye Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015) ambapo nomino ambatani thelathini zinazoghairi thelathini zisizoghairi Kanuni ya Kufuta Mabano mtawalia zilitumika. Nomino hizi zilichaguliwa kwa kuzingatia uwepo wa sifa za ukiukaji wa Kanuni ya Kufuta Mabano (KKM). Malengo ya uchunguzi huu yalikuwa ni: kudhihirisha nomino ambatani za Kiswahili zinazoghairi KKM ya Mofolojia Leksia (ML). Kudhihirisha maumbo ya nomino ambatani za Kiswahili yanayokiuka KKM ya Mofolojia Leksia, kubainisha sababu za baadhi za nomino ambatani za Kiswahili kukiuka KKM ilhali zingine hazikiuki, na kueleza mchango wa ukiukaji wa KKM ya Mofolojia Leksia kwa wanaleksikografia wa Kiswahili. Ili kufanikisha utafiti huu, nadharia ya Mofolojia Leksia iliyoanzishwa na Kiparsky (1982) na kufafanuliwa zaidi na Katamba & Stonham (2019): Kanuni ya Kufuta Mabano na Kanuni ya Mzunguko Kamili iliongoza uchunguzi huu. Data ya uchunguzi huu ilikusanywa maktabani. Baadhi ya makala zilizotumika katika uchunguzi huu ni tasnifu, makala yaliyosakurwa mtandaoni na majarida. Usampulishaji kimakusudi uliongoza uchunguzi huu ili kufikia maneno husika ya nomino ambatani yaliyodhihirisha ukiukaji wa KKM. Matokeo ya uchunguzi huu yamedhihirisha kuwa ukiukaj wa Kanuni ya Kufuta Mabano husababishwa na mofu ya pili ya nomino ambatani kuonekana na mofu ya kwanza, na muktadha wa matumizi ya nomino ambatani katika mawasiliano ya kila siku. Utafiti huu ni nafasi bora ya kuchangia isimu hasa kupitia kufahamu na kufafanua mwambatano katika Kiswahili, kuwahami waundakamusi za Kiswahili na maarifa, kukuza mofolojia ya Kiswahili na kuchochea uchunguzi zaidi.enUkiukaji wa KanuniKufuta MabanoUundajiNomino AmbataniKiswahiliMtazamoMofolojia LeksiaUkiukaji wa Kanuni ya Kufuta Mabano katika Uundaji wa Nomino Ambatani za Kiswahili: Mtazamo wa Mofolojia LeksiaThesis