Nyongesa, Daniel Masika2014-10-102014-10-102014-10-10http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/11431Utafiti umechunguza mtindo na dhamira katika mashairi ya Kiswahili ya washairi chipukizi kutoka kaunti ya Bungoma. Kwa kutumia mbinu kusudio, Toili Khisa, Martin yongesa na Brian Mutambo waliteuliwa ili kuwawakilisha washairi wengine chipukizi kutoka kaunti ya Bungorna nchini Kenya. Malengo ya utafiti yalikuwa kubainisha mtindo katika mashairi ya washairi chipukizi kutoka kaunti ya Bungoma, kubainisha dhamira zilizofumbikwa kwenye mashairi ya washairi hawa na kuchunguza jinsi mitindo iliyotumiwa na washairi hawa ilivyofanikisha uwasilishaji wa dhamira lengwa katika ushairi wao. Kwa ambavyo mtindo unahusu jinsi mtunzi anavyojieleza kwa kutumia lugha na hufanikisha mawasiliano ya kifasihi ukiwerno ushairi, utafiti huu uliongozwa na rnihimili miwili ya nadharia ya mtindo na mwingine mmoja wa nadharia ya maadili. Kwa mujibu wa Leech (1969), nadharia ya mtindo inashughulikia jinsi lugha inavyotumiwa na mtunzi katika kuwasilisha rnaudhui ya kazi yake. Kwa upande mwingine, Tolstoy (1960) anasema kuwa ujumi na uzuri wote wa sanaa hutegemea maadili ambayo hupitishwa kwa wanajamii. Vile vile, sanaa nzuri ni ile ambayo inaweza kupitisha ujumbe kwa watu wengi na inaeleweka na kila mtu. Kwa kutumia mihirnili ya nadharia hizi, utafiti huu umeyachanganua mashairi yaliyokusanywa kutoka kwa washairi chipukizi ili kupata data iliyokidhi mahitaji ya utafiti. Data iliyopatikana ilirekodiwa na kuchanganuliwa kulingana na malengo na maswali ya utafiti pamoja na mihimili changamano ya nadharia zilizotumiwa katika utafiti huu. Uwasilishaji data umefanywa kimaelezo. Utafiti huu umelenga kuwafaa wasomi, watafiti wa ushairi na wakuza mitaala nchini Kenya. Tasnifu hii imegawanywa kwa sura tano. Sura ya kwanza ya tasnifu imetanguliza mada, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka. yaliyoandikwa kuhusu mada, sababu za kuchagua mada na misingi ya nadharia. Sura ya pili imeshughulikia chimbuko na maenezi ya ushairi nchini Kenya. Katika sura hii, kando na kutoa fasili mbali rnbali za ushairi na shairi, tumefafanua asasi na njia mbalirnbali zilizochangia ushairi kuenea hadi maeneo ya bara ikiwemo kaunti ya Bungoma kwani inaaminika kuwa asili ya ushairi ni pwani. Katika sura ya tatu, tumechanganua maumbo mbali mbali yanayojitokeza kupitia mashairi ya washairi chipukizi kutoka kaunti ya Bungoma. Sura ya nne imeshughulikia tamathali za usemi na jinsi uteuzi wake mwafaka ulivyofanikisha uwasilishaji wa dharnira lengwa. Mwisho ni sura ya tano ambayo imetoa hitimisho, matokeo ya utafiti na mapendekezo ya utafiti.enMtindo na dhamira katika mashairi ya kiswahili ya washairi chipukizi kutoka kaunti ya BungomaThesis