King'ei, Kitula Osore, MiriamMukonambi, Kekonen Stanley2026-02-232026-02-232025-11https://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/32542Tasnifu Hii Imewasilishwa ili Kutimiza Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, Novemba 2025. Supervisor 1. Titus KauiUtafiti huu ulichunguza wakaa, uwasilishaji usemi na wahusika katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Baadhi ya wanasiasa hutumia hotuba zinazovuta makini ya wasikilizaji na wafuasi wao kwa mitindo tofauti. Mojawapo ya mbinu hizi za kimtindo ni usimulizi. Utafiti huu ulichunguza vipengele vya usimulizi; wakaa, uwasilishaji wa usemi na wahusika. Wakaa ni mpangilio wa matukio katika hadithi. Uwasilishaji wa usemi ni namna ambavyo maana hutolewa kwa kutumia lugha ilhali wahusika ni viumbe wa kisanaa wanaoendeleza kazi ya kifasihi. Malengo ya utafiti huu ni: kubainisha vipengee vya wakaa, uwasilishaji wa usemi na wahusika katika hotuba teule na kujadili dhima ya wakaa, uwasilishaji usemi na wahusika katika hotuba teule. Nadharia iliyotumika ni ya Naratolojia kwa kuzingatia mawazo yake Rimmon-Kenan. Mtazamo wake ni wazi kwani huwasaidia wasomaji kutofautisha kwa urahisi viwango vya masimulizi na kuchanganua matini kwa hatua. Aidha, haujatumika na tafiti nyingi ikilinganishwa na ule wa Gerald Genette. Mihimili yake ilifaa kwani iliweka wazi vipengele ambavyo vilishughulikiwa na kutathmini nafasi yavyo katika uelewekaji wa hotuba teule. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumika kuteua hotuba teule za Rais mstaafu Uhuru Kenyatta wa chama cha TNA na JP, Mhes. Raila Odinga wa chama cha ODM na Rais Dkt. William Ruto wa chama cha URP, JP na UDA zilizotolewa kati ya mwaka 2013 hadi 2023. Utafiti ulifanyika maktabani ambako data ilikusanywa kwa njia za usomaji makini kwa kupitia makala, nyaraka, majarida, tasnifu za awali na kutazama na kusikiza makala ya mtandao wa YouTube. Ufafanuzi wa kimaelezo kwa kuzingatia nadharia ulitumiwa kutolea matokeo ya utafiti ambayo yamewasilishwa kwenye vijimada vilivyomo katika sura tano za tasnifu hii. Matokeo ya utafiti huu yanatoa mchango katika taaluma ya fasihi kwa wahakiki na wanafunzi kufahamu nafasi ya vipengee hivi katika hotuba. Aidha, unawafaidi wahakiki na watafiti wa fasihi kwa kuwaelekeza jinsi ya kuhakiki hotuba.enWakaa, Uwasilishaji Usemi na Wahusika katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa KenyaThesis