King'ei, Kitula Osore, MiriamNasimiyu, Christine M.2016-11-232016-11-232016http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/15175Tasnifu hii imew asilishw a kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya Uzamili ya Chuo Kikuu Cha Kenyatta, 2016Utafiti huu ulichunguza athari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika uwasilishaji wa maudhui ya diwani ya Dhifa ya E. Kezilahabi (2008). Malengo yalikuwa, kubainisha maudhui yaliyowasilishwa na mtunzi wa Dhifa, kubainisha narnna maudhui haya yalivyowasilishwa na kueleza narnna maudhui haya yalivyoibua mazingira ya kijamii na kihistoria. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uhistoria Mpya ambayo huangalia umuhimu wa muktadha katika utunzi na uhakiki wa kazi za kifasihi. Pia, huonyesha ya kwamba kadiri jamii zinavyoendelea, utamaduni hubadilika kiwakati na jambo hili huathiri utunzi, uwasilishaji na uhakiki wa kazi za kifasihi. Utafiti huu ulizingatia muundo wa kimaelezo kuhusu suala la utafiti, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Utafiti huu ulifanywa maktabani. Sampuli iliteuliwa kimakusudi ambapo mashairi ishirini na moja yaliteuliwa ili saba yashughulikie kipengele cha siasa, uchumi na masuala ya kijamii. Data ilikusanywa kutokana na usomaji wa kina wa mashairi teule. Uchanganuzi wa data ulizingatia uainishaji wa aina ya maudhui, uwasilishaji wake pamoja na matukio ya kihistoria. Aidha, ulizingatia chimbuko la maudhui, namna yalivyowasilishwa, dhamira na falsafa ya mtunzi. Hayo yote yalifanywa kwa kuzingatia pengo lililonuiwa kujazwa na utafiti huu kwa kuongozwa na nadharia ya utafiti. Utafiti ulibaini na kutambua kwamba, siasa ya Tanzania, baada ya Azimio la Arusha ilichukuwa rnkondo mpya. Aidha, mazingira mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi yalichangia pakubwa katika kuwasilisha maudhui ya diwani ya Dhifa. Inatarajiwa kuwa utafiti huu utawafaa wanafunzi wa shule za upili, vyuo, watafiti wa ushairi na wakuza mitalaa. Tasnifu hii iligawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza ilishughulikia mada ya utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mad a, sababu za kuchagua mada na misingi ya nadharia. Sura ya pili ilichunguza historia na falsafa ya mtunzi. Sura ya tatu iliangazia maudhui ya kisiasa. Sura ya nne ilichambua maudhui ya kiuchumi. Sura ya tano iliangalia maudhui ya kijamii. Sura ya sita ilijumuisha muhtasari, hitimisho,matokeo ya utafiti na mapendekezo.KiswahiliAthari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika uwasilishaji wa maudhui ya dhifa (E. Kezilahabi)Thesis