Maitaria, Joseph NyehitaWafula, Richard Makhanu2023-07-172023-07-172018http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/26267ArticleMakala haya yanafafanua maudhui yaliyomo katika tungo za mashairi ya Abdilatif Abdalla kwa kuzingatia namna masuala ya utamaduni waWaswahili yanavyowasilishwa. Masuala hayo yanahusu namna wenyeji hao wanavyotangamana na wanavyoshughulikia maisha yao kwa ujumla. Kadhalika, ubainishaji wa vipengele hivyo vimewasilishwa kwa kuzingatia taijriba ya mtunzi kama mmoja katika jamii hiyo. Mashairi hayo yanapozingatiwa, inabainika kuwa; hisi za mtunzi zimedhibitiwa kwa lugha teule ya mafumbo inayojikita katika zaidi katika ‘lugha’ au ‘lafudhi’ yake ambayo ni lahaja ya Kimvita. Katika muktadha huu, jumbe hizo zinahitaji fasiri na maelezo kutokana na utamaduni wa mtunzi. Kwa mapana, mashairi hayo yana mwangwi unaogusia historia yataifa lake (hasa katika miaka ya baada ya 1963 nchini Kenya). Kwa maana hii, ushairi wa Abdilatif Abdalla unaweza kwa kihifadhi na kibainishaji cha vielelelzo vya utamaduni na uhalisi wa maisha ya jamii ya mtunzi. Katika kushughulikia uhusiano uliopo kati ya fasihi na utamaduni, makala haya yanaangazia baadhi ya mifano ya mashairi yaliyohifadhiwa katika Diwani ya Sauti ya Dhiki (1973). Mwishowe, inapependekeza namna mashari teule ya Kiswahili yanavyoweza kuwa hifadhi ya ‘viashiria’ vya ‘viishara’ vyatamaduni asilia katika jamii ya sasa.enmashairiAbdilatif AbdallautamaduniWaswahilimtunzilughauhalisiviashiriaviisharaUshairi wa Abdilatif Abdalla katika Kubainisha Utamaduni wa WaswahiliArticle