Dorcas Muendi Musyimi2026-04-232026-04-232017-09https://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/32955Tasnifu hii Imetolewa kwa Shule ya Fani na Sayansi za Jamii ili Kutosheleza Mahitaji ya Shahada ya Uzamifu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, September 2019. Supervisors. 1. Dkt. Leonard, M. Chacha 2. Dkt, Jacktone. O. OnyangoUtafiti huu umechunguza utohozi fonolojia wa maneno ya mkopo ya Kiswahili kutoka Kiingereza. Azima kuu ikiwa ni kuchanganua michakato ya kifonolojia inayofanikisha utohozi huo kulingana na fonolojia ya lugha pokezi. Pia, utafiti huu umebainisha ubadilishaji wa fonimu za Kiingereza hadi Kiswahili katika maneno mkopo yaliyoteuliwa. Isitoshe, utafiti umeangazie upungufu unaosababishwa na utohozi huu wa kifonolojia na kutoa mwelekeo wa jinsi upungufu huo unavyoweza kusuluhishwa. Mtafiti alitumia nadharia ya Fonolojia Leksia ambayo hushughulikia sauti za lugha pamoja na nadharia ya Kanuni za Usilabishaji ili kuchanganua suala la silabi. Isitoshe, mtafiti alitumia vigezo vya PEGITOSCA katika kutathmini ufaafu wa msamiati unaobuniwa kwa kutumia mbinu ya utohozi. taaluma ya Utafiti huu ulifanywa nyanjani ambapo mtafiti alipata maneno mkopo kutoka sajili ya teknolojia ya habari na mawasiliano, spoti hasa mchezo wa kandanda, dini, afya, usafiri na biashara. Kamusi ya Karne ya 21 (Toleo la Pili) iliyochapishwa na Longhorn (2013) ilitumiwa ili kuthibitisha kwamba maneno mkopo husika yalikuwa na asili ya Kiingereza. Pia, mtafiti alitumia Kanmusi ya Kiswahili Sanifu (Toleo la 3) iliyochapishwa na TATAKI (2014) ili kuthibitisha usanifu wa maneno mkopo yaliyotumika, Utafiti huu ulifanywa maktabani kwa kupitia vitabu, tasnifu, majarida na huduma za mtandao ili kupala habari zaidi kuhusu maneno kutazama. ya Maneno ilichanganuliwa kwa makopo. ya Mbinu mkopo za utafiti yaliandikwa kufuata maswali ya zilizotumiwa na pia ni kushiriki yakarekodiwa. utafiti na mihimili na Data nadharia zilizotumikizwa kisha ikawasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Utafiti huu ya uliweka wazi michakato ya kifonolojia inayoongoza utohozi wa maneno mkopo kwa kutegemea lugha pokezi. Michakato hii ni uchopekaji wa sauti, udondoshaji wa vokali, ufupishaji wa vokali, ubadilishaji wa sauti, udumishaji wa maumbo na ubadilikaji wa maumbo ya silabi, Utafiti ulidhihirisha kwamba, ingawa mbinu hii ya uundaji wa msamiati ni faafu, huwa na utata kwani baadhi ya maneno ya mkopo si dhahiri na wala hayafuati utaratibu maalum na ulio sawa. Suluhisho la utata huu ni kwamba utohozi ufanywe kwa kufuata matamshi ya lugha lengwa wala si maandishi ya lugha chanzi. Matokeo ya huu yatachangia katika usomi wa Kiswahili, isimu za lugha kwa ujumla na kwa watafiti wa Isimu Historia. Mtafiti anapendekeza utafiti ufanywe kwa kuzingatia matawi utafiti mengine ya isimu; sintaksia, mofolojia, semantiki na pragmatiki. Pia utafiti unaweza Kiswahili au kufanywa kuhusu fonolojia arudhi ya maneno mkopo katika katika lugha zingine. Mtafiti anapendekeza utafiti ufanywe ili kuchunguza istilahi zote zilizowasilishwa kutoka lugha ya Kiingereza hadi ya Kiswahili iwapo zina ufaafu kwa misingi ya kimataifa kama inavyopendekezwa na kanuni za PEGITOSCA. Aidha, utafiti unaweza kufanywa kuhusu istilahi zilizomo lwenye kamusi za Kiswahili na zitumiwazo na wahadhiri wa lugha ya Kiswahili wanapofunza isimu katika vyuo vikuu, Nadharia ya Usilabishaji inaweza kutumikizwa katika utafiti wa fonolojia wa lugha zingine ambazo hazina msingi wa Kibantu ili kuchunguza jinsi zinavyosilabisha maneno ya mkopo.enUtohozi Fonolojia wa Maneno Mkopo ya Kiswahili kutoka KiingerezaThesis