Wafula, R. M.Mugambi, PeterMwirabua, Andrew Kairi2015-02-262015-02-262014http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/12311Department of Kiswahili & African Languages, 115p. 2014Utafiti huu umechunguza jinsi ukoloni mamboleo unavyodhihirika katika muktadha wa utandawazi kwa kurejelea tamthilia mbili teule: Posa za Bikisiwa (2008) ya S. A. Mohamed na K. King'ei na Sudana (2006) ya Alamin Mazrui na K. Njogu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Baada Ukoloni. Utafiti ulifanyiwa maktabani. Mtafiti alisoma makala mengi yaliyohusiana na mada ya utafiti ili kupata data iliyokusudiwa. Mtafiti pia alifanya utafiti wa nyanjani kwa kuwahoji watunzi. Vilevile, mtafiti aliwahoji wataalamu na wanafunzi wenzake. Aidha mtafiti alichanganua tamthilia hizi mbili teule ili kupata data iliyokusudiwa ili kutimiza matakwa ya utafiti huu. Data iliyokusanywa ilirekodiwa na kuchanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti na nadharia ya Baada Ukoloni. Data zilizokusanywa zimewasilishwa kwa njia ya maelezo. Kazi hii imewasilishwa kwa sura tano. Utafiti huu umeonyesha kwamba utandawazi ni mbinu mpya ya kisasa ya kuendeleza ukoloni mamboleo dhidi ya mataifa maskiniotherUkoloni mamboleo na utandawazi katika tamthilia teuleThesis