Mutembei, Doreen Nkatha2026-02-042026-02-042025-11https://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/32263Tasnifu hii Imewasilishwa kwa Ajili ya Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, Novemba 2025. Supervisor 1. Jessee MurithiUtafiti huu ulilenga kulinganisha itikadi katika mashairi ya Muyaka na Utenzi wa Mwanakupona. Dhana ya itikadi ni dhana changamano na pana na imeibua mijadala mingi baina ya wataalamu mbalimbali. Itikadi ni muhimu kwa sababu huelekeza matendo yote ya mtunzi kuhusu yale atakayowasilisha na namna atakavyowasilisha kazi yake. Kwa hivyo, itikadi ndio huongoza misimamo, mielekeo na imani ya mtunzi. Vitabu teule vya kufanikisha utafiti huu ni mashairi ya Muyaka na Utenzi wa Mwanakupona. Vitabu hivi viliteuliwa kwani ingawa kazi hizi ziliandikwa katika kipindi kimoja, ni tofauti kimtindo na kimaudhui. Hivi ni kusema kuwa watunzi hawa waliongozwa na itikadi tofauti. Kwa hivyo, ni muhimu kuchunguza na kuzilinganisha zile itikadi katika mashairi ya Muyaka na Utenzi wa Mwanakupona na jinsi itikadi husika zinazowaongoza watunzi hao zinavyolingana na kujitokeza katika kazi zao. Utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo: kubaini itikadi katika Utenzi wa Mwanakupona na mashairi ya Muyaka, kutathmini jinsi athari za itikadi zinavyopelekea uwasilishaji wa maudhui kwenye Utenzi wa Mwanakupona na mashairi ya Muyaka na kuchunguza athari za itikadi katika uwasilishaji wa mtindo katika mashairi ya Muyaka na Utenzi wa Mwanakupona. Nadharia ya itikadi, mikabala ya Karl Marx (1977 na 1979), Louis Althusser (1981) na Antonio Gramsci (1985) ilitumika. Mkabala wa Karl Marx umetumika kwani unashikilia kuwa itikadi ni ‘ungamuzi potoshi.’ Mkabala wake Louis Althusser umetumika kwani aliorodhesha vyombo vya kiitikadi ambavyo alivigawa katika vikundi viwili. Vinavyo endeleza itikadi moja kwa moja kama vile polisi, jeshi, mahakama na serikali. Pia, vyombo visivyo vya moja kwa moja kama dini, elimu, vyombo vya habari na familia. Mwisho, mkabala wake Antonio Gramsci umetumika kwani Gramsci anaieleza dhana hii ya itikadi kama fikra, mitazamo na mielekeo ambayo binadamu huchukulia kuwa za kawaida hivyo kujikandamiza kwa hiari yake mwenyewe. Data husika ilitolewa maktabani ambapo shairi, beti, mishororo na vipande vya mishororo vilivyo na dhana za kiitikadi zilikusanywa. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo ili iweze kueleweka. Kutokana na data ya utafiti huu, imebainika kuwa Muyaka na Mwanakupona waliongozwa na itikadi tofauti ingawa walikuwa watunzi wa kipindi kimoja cha kirasimi. Itikadi hizo zilipelekea uwasilishaji wao wa maudhui na mtindo vitofauti.enMtazamo Linganishi WA Itikadi Katika Utenzi WA Mwanakupona na Mashairi Ya MuyakaThesis