Wendo, Fadhili Hamisi2026-02-042026-02-042025-11https://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/32267Tasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Novemba 2025. Supervisor 1. Titus KauiUtafiti huu umechunguza jinsi maudhui ya ukungwi yanavyojitokeza katika nyimbo teule za taarab. Malengo yafuatayo yalinuiwa kutekelezwa; kubainisha dhima ya kungwi katika jamii ya Waswahili, kuchunguza maudhui ya ukungwi katika nyimbo teule za taarab na kulinganisha dhima ya kungwi na maudhui ya ukungwi katika nyimbo teule za taarab. Sampuli iliteuliwa kimaksudi ambapo kati ya nyimbo nyingi za taarab, nne ndizo ziliteuliwa kutumika katika utafiti huu. Nyimbo hizi ni: Maji ya Uvuguvugu (Wachonga Vinyago), Nenda salama (Omar Kopa), Ndoa (Aslay na Khadija Kopa), Bi Harusi (AT). Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya kimakusudi. Kati ya maeneo mengi katika jamii ya Waswahili, eneo la Msambweni ndilo lililoteuliwa kutumika katika utafiti. Mbinu hii ilifaa katika kuwateua makungwi waliochangia data muhimu ya kuchanganuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili; nadharia ya Simiotiki na nadharia ya Uamilifu. Nadharia ya Simiotiki iliasisiwa na Ferdinand Dessaussure (1913) na Charles Pierce (1977) na inahusu uhusiano uliopo kati ya kitaja na kitajwa na matumizi ya ishara, picha na msimbo. Nadharia hii ilisaidia katika kufafanua mbinu za uwasilishaji wa ujumbe katika nyimbo teule za taarab. Kwa upande mwingine nadharia ya Uamilifu iliasisiwa na Emile Dukheim (1912) na inahusika na uchambuzi wa dhima zinazojitokeza katika kazi za fasihi. Hii ilituongoza katika kubainisha dhima ya kungwi katika jamii. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba na wa nyanjani ambapo maktabani; mtafiti aliweza kusoma tasnifu, makala na majarida yanayohusiana na mada. Nyanjani, mtafiti alitembelea eneo lengwa ili kuwahoji baadhi ya makungwi kuhusu dhima yao. Matokeo yalionyesha kuwa kungwi ana jukumu la kuwafundisha wanawali kuhusu maswala ya unyumba yakiwemo usafi wa mwili na nyumba, namna ya kumhudumia mume, namna ya kusema na marafiki na jamaa za mume, matumizi ya vifaa vya kiasili kama vile mbuzi, kinu, mchi ufagio miongoni mwa mengine. Aidha, maudhui haya ya ukungwi yanafundishwa na waimbaji wa nyimbo teule za taarab na kuonyesha namna kipera cha nyimbo na mawaidha vinaingiliana kimaudhui. Utafiti huu unatarajiwa kutoa mchango wa kuonyesha jinsi vitanzu vya mawaidha na nyimbo huingiliana kidhima.otherMaudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za TaarabArticle