Karuga, Mary Njeri2011-12-222011-12-222011-12-22http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/2114The PL 8701.K4 K37Lengo la kazi hii ni kuchambua vitabu vya fasihi ya Kiswahili vya watoto kwa misingi ya vigezo vya uteuzi wa vitabu vya watoto. Aidha,upokezi wa watoto wa vitabu hivyo ni jambo lililotiliwa maanani. Vitabu vilivyofanyiwa uchambuzi ni; Jinsi Chui Alivyopata Madoadoa (Kola,1994); Kaka Sungura na Wenzake (Michuki ,2003); Mlima Kenya Kajifungua (Kimunyi, 1997) na Mfalme na Majitu (Omollo,1994). Watoto walioshiriki katika utafiti huu ni wa Manispaa ya Kiambu na wako katika darasa la taro na la sita. Umri wao ni kati ya miaka 9-13. Kwa kurejelea nadharia za uhakiki wa kimtindo na mwitikio wa msomaji,uhakiki na upokezi wa vitabu hivyo umejadiliwa. Kazi hii imegawanyika katika sehemu tano. Sura ya kwanza inatanguliza kazi yote. Hapa, mada ya utafiti, malengo ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka ya utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii, ukusanyaji na uwasilishaji wa data zimeshughulikiwa. Sura ya pili inashughulikia vigezo vinavyopaswa kuongoza uteuzi wa vitabu vya fasihi vya watoto. Vigezo vilivyozingatiwa ni maudhui, wahusika, ploti, mtindo, umbo na mandhari. Katika sura ya tatu, data imewasilishwa na hoja muhimu kujadiliwa ambapo uchambuzi wa kiuhakiki kuhusu vitabu viwili - Jinsi Chui Alivyopata Madoadoa na Kaka Sungura na Wenzake umefanywa. Vile vile upokezi wa vitabu hivyo nwatotoumechanganuliwa. Uhakiki na upokezi huu umeegemea upande wa maudhui, wahusika, ploti, mtindo, umbo na mandhari katika vitabu hivyo. Kwenye sura ya nne, vitabu viwili vilivyosalia yaani Mlima Kenya Kajifungua na Mfalme na Majitu vimeshughulikiwa kwa kufuata utaratibu ule ule wa sura ya tatu. Hatimaye sura ya tano inatoa muhtasari wa kazi yote ambapo matokeo ya utafiti huu pamoja na mapendekezo yameshughulikiwa. Imedhihirika kuwa watoto huvutiwa na vitabu vilivyoandikwa kwa kuwazingatia kama hadhira lengwa kwa jinsi ambavyo vipengele vya kifasihi tulivyovichunguza vinahusiana na kiwango chao cha umri na uelewa.enKiswahili--language--KenyaUhakiki na upokezi wa fasihi ya kiswahili ya watoto katika shule za msingi nchini KenyaThesis