KUCHUNGUZA UFUNDISHAJI WA KUSOMA KWA SAUTI KATIKA MADARASA YA KWANZA, PILI NA TATU KATIKA SHULE ZA MSINGI. BEA TRICE WAMBUIrKOBA IDARA YA KISW AHILI NA LUGHA ZA KIAFRIKA CHUO KIKUU CHA KENYA TTA Tasnifu hii imetolewa Hi kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shah ad a ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. 2008 Okoba,Beatrice Kuchunguza ufundishaji wa 11 KENYATIA U~.VERSITY l BRARY UNGAMO Tasnifu hii ni kazi yangu binafsi na haijatolewa kwa mahitaji ya shahada katika Chuo Kikuu kingine. , BEATRICE WAMBUI OKOBA Tasnifu hii imetolewa kwa idhini yetu kama wasimamizi wa kazi hii katika chuo hiki. ~\ DKT. C. W. RYANGA NA DKT. J.O. ONYANGO 1 TABARUKU Kwa Marehemu babangu Solomon Karanja aliyenihimiza kuendelea na masomo yangu, NA Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kukamilisha shahada hii, Utukufu wote umuendee. SHUKRANI Kwanzanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uwezo wa kukamilisha kazi hii. Shukraniza kipekee ziwaendee Dkt.Ryanga na Dkt. Onyango kwa kusimamia utafiti huuna pia kwa ushauri wao ambao ulifanikisha utafiti huu. Nawashukuru wahadhiri wote wa idara ya Kiswahili na lugha za Kiafrika kwa kunifundisha na kwa ushauri wenu na mwongozo ambao ulinifaa wakati wa masomo yangu. Naishukuru Tume ya kuajiri Walimu (T.S.C.), kwa kunipa ruhusa ya kusoma. Ninawashukuru wanafunzi wenzangu Musembi, Mayodi, Ann, Kaui, Mandina, Sichangi, Kawila, Kavuria, Ondara, Dorcas, Gaitho na Mugambi kwa ushirikiano wao ambao ulinipa moyo. Asanteni nyote Ningependa kuwashukuru walimu wakuu na walimu wa madarasa ya chini katika shule za Gatura, Chomo, Gatunyu, Kirwara, Rwegetha na Gichumbu kwa kukubali kushiriki katika utafiti huu. Mwenyezi Mungu awabariki nyote mlionifaa katika juhudi zangu za kufanya utafiti huu. Mwisho, ningependa kushukuru sana familia yangu haswa kwa mume wangu Dkt. Barrack Okoba aliyenihimiza kuendelea na masomo yangu. Pia msaada wake ulikuwa rnkubwa wakati wa kupiga chapa kazi hii na kwa kunipa msukumo wa kuikamilisha shahada hii. Namshukuru mamangu Naomi, kwa maombi yake yaliyonipa imani ya 11 kuendelea na masomo yangu. Nawashukuru pia wanangu Bildad, Baraka na Bilha kwa uvumilivu na maombi yao nilipokuwa masomoni. ASANTENI III IKISIRI Utafiti huu umeshughulikia kuchunguza ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika rnadarasa ya chini katika shule za msingi, Utafiti huu ulilenga kuonyesha rnbinu na nyenzo zilizotumiwa katika kutekeleza ufunzaji wa kusorna kwa sauti. Aidha, vitabu na tathmini zilichunguzwa na kuonyesha rnchango wake katika kuimarisha usornaji. Kadhalika, matatizo yaliyowakabili watoto katika usomaji yaliangaziwa na ufaafu wa rnikakati iliyotumiwa na walirnu. Utafiti ulinuia kuonyesha rnatatizo katika stadi ya kusoma na kuchunguza mikakati iliyotumiwa na walimu kukabiliana na changamoto hizi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Krashen pamoja na Modeli Husishi. Nadharia ya Krashen inaeleza uzingativu wa taratibu mbalimbali ili kufanikisha ujifunzaji kusorna L2. Nayo, modeli Husishi inasisitiza umuhirnu wa kukuza ujuzi wa kupambanua sauti na ufahamu wa maana ya sauti hizo kwa pamoja. Hi kufanikisha rnalengo ya utafiti, walirnu walijaza hojaji na uchunguzi wa darasani ulifanywa ili kuchunguza utekelezaji wa funzo la kusoma kwa sauti. Walirnu waliteuliwa kutoka shule sita za umma katika tarafa ya Gatanga, wilaya ya Thika. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwa watoto walikosa rnsingi rnzuri katika stadi hii. Watoto wengi waliendelea na madarasa ya juu kabla ya kuirnarika katika vipengele vya kirnsingi katika stadi ya kusoma kwajumla. Imedhihirika kuwa walimu katika madarasa haya wanahitaji kuhamasishwa zaidi kuhusu hatua za kusoma zinavyofanyika. Hii ni kwa sababu baadhi ya walirnu walikosa ubunifu katika utekelezaji wa shughuli za darasani katika stadi ya kusorna kwa sauti. IV UFAFANUZI WA ISTILAID Shule za malezi Aina ya shule ambazo hutayarisha watoto kuhusiana na mambo ya kimsingi kabla ya kuingia shule za msingi. Hii inachukuliwa kwa maana ya watoto ambao wana uwezo wa chini katika kuelewa mambo ya kiusomi darasani. Huu ulichukuliwa kuwa uwezo wa kupambanua herufi na sauti zake. Ujuzi huu unajikita katika mbinu ya abjedi, kutamka herufi na silabi. Huu unaashiria ule uwezo wa kuelewa kinachosomwa. Ujuzi huu unajikita katika mbinu ya kutazama na kusema neno, kusoma kirai, kusoma sentensi na kusoma hadithi. Akili nzito Ujuzi wa chini Ujuzi wajuu v YALIYOMO Ukurasa TABARUKU i SHVKRANI ii UFAF ANUZI WA ISTILAHI v SURA YAKWANZA 1.0 Utangulizi 4 1.1 Swala la Utafiti 7 1.2 Malengo ya Utafiti 8 1.3 Maswali ya Utafiti 9 1.4 Nadharia Tete 9 1.5 Sababu za Kuchagua Mada 9 1.6 Upeo na Mipaka 11 1.7 Misingi ya Nadharia 13 1.7.1 Nadharia ya Krashen 13 1.7.1.1 Kitengo cha Upataji - Ujifunzaji Lugha 14 1.7.1.2 Kitengo cha Utaratibu wa Kiasili 15 17.1.3 Kitengo cha Urekebishaji Makosa 16 1.7.1.4 Kitengo cha Uteuzi wa Makala 17 1.7.1.5 Kitengo cha Hisi 18 1.8 Modeli Husishi 19 1.8 1 Modeli Chini-Juu 20 1.8.2 Modeli ya Juu-Chini 21 1.9 Tahakiki ya Maandishi 22 1.10 Mbinu za Utafiti :· 25 1.10.1 Sampuli 26 1.10.2 Ukusanyaj i Data 27 1.10.3 Uchanganuzi na Uwasilishaji waData 27 SURA YA PILI: MBINU NA NYENZO ZA KUFUNDISHIA KUSOMA 2.0 Utangulizi 29 2.1 Stadi ya Kusoma 29 2.1.1 Sifa bainifu za Usomaji wa Sauti 30 2.2 Mbinu za Kusoma 36 2.2.1 Njia ya Uchanganuzi 37 2.2.2 Utaratibu Changamano 43 2.3 Nyenzo/Vifaa 49 2.3.1 Aina za Nyenzo 49 2.3.2 Umuhimu wa Nyenzo/Vifaa 51 2.3.3 Kuteua Nyenzo 52 2.3.4 Uhifadhi wa Nyenzo 53 2.4 Aina za Usomaji 54 2.4.1 Kusoma Darasa Lote 54 2.4.2 Kusoma Mmoja Mmoja 54 2.4.3 Kusoma Katika Makundi 55 2.4.4 Kusoma Kimya 57 2.5 Maandalizi ya Kusoma 58 2.5.1 Mazoezi Kabla ya Kusoma 59 2.6 Tathmini 60 2.7 Kazi ya Marudio 63 SURA YA TATU: UWASILISHAJI WA UFUNZAJI WA STADI YA KUSOMA KWASAUTI 3.0 Utangulizi 65 3.1 Uwasilishaji wa Matokeo 66 3.1.1 Maelezo Kuhusu Watoto Katika Hojaji 66 3.1.2 Maelezo Kuhusu Walimu Katika Hojaji 68 3.1.3 Maelezo Kuhusu Kiwango cha Elimu ya Walimu 68 3.2 Majibu ya Walimu Kuhusu Ufundishaji wa Kusoma 72 3.2.1 Malengo Yaliyozingatiwa na Walimu Katika Ufundishaji 72 3.2.2 Mbinu za Kufundisha Kusoma kwa Sauti 74 3.2.3 Maoni Kuhusu Umuhimu wa Kila Mbinu 76 3.2.4 Vitangulizi vya Kusoma 77 3.2.5 Mtindo wa Usomaji 78 3.2.6 Mpangilio wa Makundi Darasani 80 3.3 Aina ya Vitabu na Makala ya Kusoma 81 3.4 Mbinu za Kutathmini Usomaji wa Watoto 84 3.4.1 Idadi za Tathmini 85 3.4.2 Umuhimu wa Kuweka Rekodi za Tathmini 87 3.4.3 Asilimia ya Watoto Wenye Ufasaha 88 3.5 Uchanganuzi wa Matokeo ya Hojaji ya Walimu 90 3.6 Uchunguzi wa Darasani 91 3.6.1 Aina za Vitangulizi 92 3.6.2 Mbinu za Kufundishia 93 3.6.3 Mpangilio wa Darasani 98 3.6.4 Mazingara ya Darasani 100 3.6.5 Aina ya Vitabu 101 3.6.6 Tathmini 102 3.7 Uchanganuzi wa Matokeo ya Uchunguzi wa Darasani 105 SURA YA NNE: MATATIZO YANAYOWAKABILI WATOTO KATIKA UJIFUNZAJI WA KUSOMA 4.0 Utangulizi 108 4.1 Matatizo katika Darasa la 1 109 4.2 Matatizo ya Darasa la 2 121 4.3 Matatizo ya Kusoma kwa Watoto wa Darasa la 3 127 4.4 Namna Walimu Walivyotatua Matatizo ya Usomaji 130 2 4.5 Uchanganuzi wa Matatizo ya Watoto 134 SURA YA TANO: MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO 5.0 Muhtasari 136 5.1 Hitimisho 137 5.2 Mapendekezo 142 MAREJELEO 145 KIAMBATISHO 1 149 KIAMBA TISHO 2 154 KIAMBA TISHO 3 156 KIAMBATISHO 4 157 KIAMBATISHO 5 158 ORODHA YA MAJEDW ALl NA MICHORO Jedwali 3.1: Idadi ya Wanafunzi Katika Kila Darasa 67 Mchoro 3.1: Idadi ya Walimu Kulingana na Jinsia Katika Darasa 1-3 68 Mchoro 3.2: Asilimia ya Kiwango cha Elimu ya Walimu (N=18) 70 Jedwali 3.2: Tajriba ya Mwalimu Katika Ufundishaji wa Kiswahili 70 Jedwali 3.3: Malengo Yaliyozingatiwa na Walimu Katika Darasa la 1-3 73 Jedwali 3.4: Idadi ya Walimu Waliotumia Mbinu Mbalimbali Katika Darasa la 1-3.75 Jedwali 3.5: Maoni ya Walimu Kuhusu Mbinu Mbalimbali Katika Darasa la 1-3 76 Jedwali 3.6: Aina ya Vitangulizi Vilivyotumiwa na Walimu Kutanguliza Funzo 78 Jedwali 3.7: Mitindo ya Kusoma Iliyotumiwa na Walimu Katika Darasa la 1-3 79 Jedwali 3.8: Aina ya Makundi Yaliyotumiwa na Walimu katika Darasa la 1-3 80 Jedwali 3.9: Vitabu Vilivyotumiwa na Walimu Katika Darasa la 1-3 82 Jedwali 3.10: Aina za Tathmini Talizopewa Watoto Katika Darasa la 1-3 85 Jedwali 3.11: Idadi za Tathmini Katika Muhula 86 Jedwali 3.12: Maoni ya Walimu Kuhusu Umuhimu wa Rekodi 88 Jedwali 3.13: Makadirio ya Usomaji wa Watoto Kulingana na Walimu 89 Jedwali 3.14: Namna Walimu Walivyofundisha Silabi 94 Jedwali 3.15: Namna Watoto Walivyoendeleza Maneno Katika Imla 97 Jedwali 3.16: Namna Watoto Walivyoandika Katika Zoezi la Imla 104 Jedwali 4.1: Matatizo ya Kusoma kwa Watoto Darasa la 1 110 Jedwali 4.2: Maneno Yaliyosomwa na Watoto Darasa la 1 112 Jedwali 4.3: Usomaji wa Watoto wa Majina Kwenye Picha Darasa la 1 117 Jedwali 4.4: Matatizo ya Watoto Katika Usomaji Darasa la 2 122 Jedwali 4.5: Mfano wa Makala Yaliyosomwa na Watoto Darasa la 2 125 Jedwali 4.6: Matatizo ya Watoto ya Kusoma Katika Darasa la 3 128 Jedwali 4.7: Namna Walimu Walivyokabiliana na Matatizo ya Watoto ya Kusoma 131 3 SURA YA KW ANZA 1.0 Utangulizi Kiswahili ni mojawapo ya lugha zinazofunzwa katika shule za msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la nane. Kulingana na mtalaa wa elimu kutoka kwa Taasisi ya Elimu (K.I.E. 2002) Kiswahili kinatumiwa katika madarasa ya chini kufundishia masomo katika shule za mjini, na lugha ya eneo kufundishia katika shule za mashambani. Kiswahili kimepiga hatua kubwa kimaendeleo nchini Kenya kuanzia kipindi cha pili cha karne ya ishirini na kuendelea. Mbali na Kiswahili kuwa lugha ya taifa, imekuwa lugha ya lazima na ya kutahiniwa katika viwango vya shule za msingi na sekondari kwa mujibu wa Ripoti ya Mackay (1981) iliyotekelezwa kwa kuanzisha mfumo wa elimu wa 8-4-4 mwaka wa 1985. Aidha kumekuwa na mabadiliko ya mtalaa kuimarisha kiwango cha elimu ili kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu. Kumekuwa na marekebisho ya silabasi mara kwa mara ambayo yamefanyiwa masomo hususan katika kiwango cha shule ya msingi. Marekebisho yaliyofanywa katika somo la Kiswahili kwa mujibu wa silabasi mpya (K.I.E. 2002), yameonyesha vile mafunzo yanavyogawika kwenye stadi nne za lugha yaani kusikiliza na kuongea, kusoma, na kuandika. Mbinu na nyenzo za kufunzia pamoja na namna ya kutathmini zimeonyeshwa. Mbali na maendeleo haya kiwango cha somo hili katika shule za msingi, sekondari na hata vyuo vikuu hairidhishi. Haja ya kuinua viwango hivi inadhihirika kutokana na machapisho mengi ya vitabu vya kiada hasa katika shule za msingi. Baadhi ya vitabu hivi ni kama vile, Kiswahili Mufti, Masomo ya Msingi, Kiswahili Sanifu, Kiswahili 4 Teule. Hivyo kuna haja ya kuchunguza ufundishaji wa stadi hizi mara kwa mara ili kuona maendeleo ya lugha hii. Kusoma ni mojawapo ya stadi za lugha andishi. Mwanafunzi akimudu stadi hii anaweza kujitimizia mahitaji yake ya kimawasiliano bila kutegemea msaada wa mtu mwingine. Kwa kawaida mtu akisoma anaweza kufanya hivyo kimya au kwa sauti kulingana na muktadha wa kimawasiliano unaohusika. Kama kuna haja ya watu wengine kusikia ujumbe wa mwandishi, msomaji atasoma kwa sauti, lakini ikiwa hakuna haja atasoma kimoyomoyo ili ujumbe huo uwe siri yake (Kawoya na Ryanga, 2003). Gage (1967) anasema kuwa kitendo cha kusoma kinaweza kugawika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni ile ya kutambua maumbo na ya pili ni kule kuweza kupata maana kutokana na maumbo yenyewe. Bila njia hizi mbili kitendo cha kusoma hakiwezi kukamilika. Anaendelea kusema kuwa mtoto anapojifunza kusoma, mwalimu ana jukumu la kumsaidia mtoto kutambua herufi, silabi, maneno na hata kifungu cha sentensi fupi. Wanyoike (1982) anaeleza kuwa kusoma ni kitendo cha kufasiri maumbo yaliyojikita katika maandishi, kutambua maumbo, kuyanakili akilini na kisha kuyatamka. Uwezo wa kutambua maumbo na kuyatamka ndio wa kimsingi katika stadi ya kusoma hasa katika kiwango cha chini cha ujifunzaji kusoma. 5 Zoezi la kusoma kwa sauti ni muhimu kutokana na ukweli kwamba kupitia zoezi hili mwanafunzi anapata fursa ya kuirnarisha hali ya matamshi yake. Kila anaposoma kwa sauti anafanya mazoezi ya kutamka maneno ya Kiswahili na kiimbo cha Kiswahili kwa jumla. Mazoezi haya yanakuwa msingi mzuri kwa zoezi la kusoma kimoyomoyo. Ikiwa anaweza kusoma ujumbe uliyoandikwa kwa njia ambayo inaleta maana hiyo ni ishara kwamba ana uwezo wa kusoma vizuri kwa sauti (Kawoya na Ryanga, 2003). Mbaabu (1987:27) anasema kuwa Kiswahili kimatamshi kina ukuruba na lugha nyingi za Kiafrika hasa za Kibantu. Hii ina maanisha kuwa kuna uwezekano wa watoto kufanikiwa kwa kiwango cha juu katika kusoma na kuandika Kiswahili; kwa sababu maneno yanasomwa kama yanavyoendelezwa. Anapendekeza kuwa Kiswahili kikipewa nafasi zaidi katika mtalaa wa shule za msingi watoto wataweza kuimarika katika stadi hizi zaidi. Njia mojawapo ya kuinua hadhi ya lugha hii ikiwa ni kuhakikisha inatumiwa kama lugha ya kufundishia masomo katika madarasa ya chini. Anaendelea kusema kuwa walimu waliopitia mfumo wa 8-4-4 wangechangia kuinua kiwango cha somo hili ikichukuliwa kwamba wamefunzwa Kiswahili kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Miaka kadha imepita tangu maoni haya kutolewa, ingawa Kiswahili hakitumiwi kufundishia masomo katika shule zote nchini Kenya, idadi ya vipindi vya somo hili vimeongezeka hadi tano katika madarasa ya chini na ya juu. Hata hivyo, kuna malalamishi kuhusu matokeo mabaya ya somo hili kwa mujibu wa vijitabu vinavyotathmini matokeo ya mtihani wa darasa la nane (K.C.P.E). Vijitabu hivi vinachapishwa kila mwaka na Baraza la Mtihani la Kitaifa (K.N.E.C). 6 Watoto hujifunza lugha mpya kwa urahisi kuliko watu wazima ikiwa mazingara ya kujifunzia ni ya kufaa. Mtoto alivyo mchanga ndivyo alivyo na uwezo mwingi wa kujifunza lugha mpya. Hii ni kwa sababu ubongo wa mtoto ni mwepesi kwa kushika mambo (Wanyoike, 1982). Beaty (1988) akimnukuu (Mclaughlin, 1978) anasema kuwa mtoto huimarika kwa urahisi katika matamshi kuliko mtu mzima. 1.1 Swala la Utafiti Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane, somo la Kiswahili hayaridhishi. Haya yanaashiria changamoto ambazo zinaikabili lugha hii mbali na juhudi nyingi ambazo zimefanywa na wizara ya elimu kuinua kiwango chake. Dhana za kimsingi katika masomo mbalimbali hujengwa katika madarasa ya chini. Hii ndiyo sababu ni muhimu kuangazia ufundishaji wa stadi za lugha katika madarasa haya. Ni dhahiri kuwa stadi ya kusoma kwa sauti inachangia pakubwa katika kukuza uwezo wa watoto wa kuweza kupambanua sauti na maana ya kinachosomwa. Vile vile ndiko kunakomwingiza mtoto katika ulirnwengu wa kusoma. Usomaji wa baadaye wa mapana unatokana na msingi huu wa kusoma kwa sauti. Aidha utafiti huu unalenga kubainisha pen go zilizopo katika ufundishaji wa stadi ya kusoma kwa sauti .Kuna haja ya kuchunguza mikakati inayotumiwa na walimu kuimarisha stadi ya kusoma kwa sauti ili kuweza kuikabili kwa njia ifaayo. Katika silabasi mpya ya Kiswahili K.I.E. (2002) usomaji unahusisha kusoma kimoyomoyo kimya na kusoma kwa sauti. Aidha usomaji wowote utilie mkazo matamshi bora, viimbo, mkazo, uakifishaji na mahadhi. Usomaji umepangwa katika makundi sita: usomaji wa sauti, kusoma kwa ufahamu, kusoma kwa ziada, matumizi 7 ya maktaba na kamusi. Katika darasa la kwanza hadi la tatu kuna usomaji kwa sauti ambao unalenga kuimarisha stadi ya kusoma na kutamka fonimu au sauti inavyofaa. Kusoma kwa sauti kunapungua katika madarasa ya juu kwa sababu inachukuliwa kwamba wameimarika katika matamshi na kwa hivyo kusoma kunalenga zaidi kwenye ufahamu. Utafiti huu utajikita katika ufundishaji wa kusoma kwa sauti, mbinu na nyenzo za kufundishia, vitabu vilivyoteuliwa kwa kusoma na tathmini ambazo watoto walipewa kwa mujibu wa mapendekezo ya silabasi. Aidha matatizo yaliyowakabili watoto katika utekelezaji wa kusoma kwa sauti na namna walimu walivyokabiliana na changamoto hizo. 1.2 Malengo ya Utafiti Utafiti huu una malengo yafuatayo: 1. Kubainisha mbinu zilizotumiwa katika ufundishaji wa kusoma kwa sauti. 2. Kubainisha vitabu na makala yaliyotumiwa katika kufundisha kusoma kwa sauti. 3. Kutambua nyenzo walizotumia katika ufundishaji wa kusoma kwa sauti. 4. Kuchunguza aina za tathmini za kusoma kwa sauti zilizotumiwa na walimu. 5. Kubainisha matatizo yaliyotokea na namna yalivyokabiliwa ili kupendekeza mbinu mwafaka. 8 1.3 Maswali ya Utafiti 1. Ni mbinu na nyenzo zipi zilizotumiwa katika ufundishaji wa kusoma kwa sauti? 2. Ni vigezo vipi vilivyotumiwa katika kuchagua vitabu na makala ya kusoma? 3. Ni tathmini zipi zilizotumiwa katika kupima kiwango cha usomaji wa watoto? 1.4 Nadharia Tete Utafiti uliongozwa na yafuatayo: 1. Walimu wanashirikisha mbinu na nyenzo mbalimbali katika ufundishaji wa kusoma kwa sauti. 2. Walimu wanakagua vitabu na makala yaliyosomwa darasani. 3. Walimu wanatathmini viwango vya kusoma kwa sauti vya watoto. 1.5 Sababu za Kucbagua Mada Mbaabu (1996) anasema kuwa kupita mtihani wa Kiswahili na Kiingereza ni mojawapo ya masharti ya mwanafunzi kuhitimu ili kuweza kujiunga na chuo kikuu au kuchukua taaluma fulani chuoni. Kwa sababu ya umuhimu wake kuna haja ya kuchunguza ufundishaji wa stadi za lugha mara kwa mara ili kutatua matatizo yanayotokea ili wanafunzi wasiendelee kuathiriwa na somo hili. Hali ya lugha Kenya ni tatanishi kwa sababu nchini kuna zaidi ya lugha arobaini (Abdulaziz, 1982). Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, katika madarasa ya chini lugha inayotumiwa kufundishia masomo ni lugha inayozungumzwa katika eneo la shule. Katika shule za mjini walimu wanatumia Kiswahili na mashambani wanatumia lugha 9 ya eneo la shule. Yamkini shule za mashambani, Kiswahili na Kiingereza ni baadhi ya lugha zinazofunzwa kama masomo mengine katika kiwango hiki. Hii inamaanisha mtoto anakabiliana na ujifunzaji wa lugha tatu kwa wakati moja. Lugha hizi zinatumia herufi zinazofanana isipokuwa tofauti chache ya matamshi katika baadhi ya herufi. Utafiti huu ulijikita katika usomaji kwa sauti wa Kiswahili kwa wanafunzi Wagikuyu. Kuna haja ya kuchunguza kama ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika madarasa ya chini unazingatia mapendekezo ya silabasi. Pia kuchunguza matatizo yanayowakabili walimu wanapotekeleza malengo ya silabasi; namna wanavyotatua matatizo hayo tukichukulia kuwa idadi kubwa ya watoto nchini Kenya hufunzwa Kiswahili kama lugha ya pili. Watoto wa darasa la kwanza, la pili na la tatu walichaguliwa. Nthiga (2002) anasema kuwa msingi mzuri wa lugha unajengwa katika kiwango hiki ili kuendeleza usomaji wa baadaye. Kulingana na silabasi (K.I.E., 2002) watoto katika madarasa haya hupewa mazoezi mengi ya kusoma kwa sauti ili kukuza stadi ya kusoma. Aidha watoto katika darasa la tatu huchukuliwa kuwa wana umilisi wa kusoma kwa sauti ikilinganishwa na darasa la kwanza na la pili. Umilisi wa stadi za lugha, kusikiliza, kuongea, kusoma na kuandika hufuata utaratibu fulani. Hizi stadi zinaingiliana na kila kiwango kinajengwa na kiwango kilichotangulia. Dhana za kimsingi hufunzwa kwa usahili katika madarasa haya. Krashen (1988) anasema kuwa watoto hujifunza lugha kwa hatua kutoka miundo sahili hadi changamano, kwa hivyo madarasa haya yatafaa kuona maendeleo ya kusoma kwa sauti. 10 Tafiti nyingi zimeshughulikia kusoma kwa ufahamu zikipima ufahamu wa watoto katika kuelewa makala waliyosoma (Onyamwaro, 1990; Kirigia, 1991; Nyamasyo, 1992; Mbua, 2000; Matuu, 2000; Mberia, 2002). Utafiti huu ulichunguza umilisi wa kusoma kwa sauti. Kuna haja ya kuchunguza sifa bainifu za kusoma kwa sauti kama vile; matamshi bora, viimbo, shadda, uakifishi na mahadhi yanavyozingatiwa. Aidha, sifa hizi zinasaidia katika kuelewa ujumbe wa makala yaliyosomwa. Kadhalika matamshi ni muhimu, kwa sababu huathiri kinachowasilishwa. Matamshi kama vipengele vingine vya lugha kama vile sarufi, msamiati husaidia kuelewa ujumbe unaowasilishwa (Musau, 1993). Utafiti huu utasaidia walimu wa Kiswahili kuhusisha mbinu mbalimbali kuimarisha usomaji wa sauti wa watoto. Utafiti huu pia utawafaa wapanga mitalaa ambao wataweza kulenga mahitaji ya watoto. Kutokana na uchunguzi huu waandishi wa vitabu wataweza kuzua makala na mazoezi mwafaka wakizingatia viwango tofauti vya watoto. Kadhalika, wakaguzi wa shule wataweza kutoa mwongozo na mikakati ya kuimarisha stadi ya kusoma kwa sauti ili kujenga ufasaha wa watoto na kuwatia ari kupenda kusoma. 1.6 Upeo na Mipaka Kuna aina nyingi za usomaji baadhi yake ni; kusoma kwa sauti, kusoma kimoyomoyo, kusoma kwa ziada na maktaba (K.I.E., 2006). Utafiti huu umejikita katika kuchunguza ufundishaji wa kusoma kwa sauti. Yamkini namna mwanafunzi anavyosoma huathiri stadi zingine za lugha kama vile kuandika na ufahamu. Utafiti huu ulijikita katika stadi ya kusoma kwa sauti katika madarasa ya chini katika shule 11 za msingi. Madarasa haya yalichaguliwa kwa sababu katika silabasi imependekeza watoto wafundishwe alfabeti, silabi, kusoma sentensi fupi na sahili nk. Hii inaashiria kuwa watoto hawa hawajaimarika katika usomaji. Aidha katika madarasa haya ya chini walimu hushirikisha usomaji kwa sauti zaidi ya madarasa ya juu. Eneo la tarafa ya Gatanga, wilaya ya Thika lilichaguliwa kimaksudi kama eneo wakilishi la maeneo ya wazungumzaji wa lugha ya Kigikuyu nchini Kenya. Utafiti huu ulilenga wanafunzi Wagikuyu wanaojifunza lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili (L2). Asilimia kubwa ya watoto nchini ni wale wanaojifunza Kiswahili kama L2. Walichaguliwa kwa sababu ni wabantu kwa hivyo wanawakilisha idadi kubwa ya jamii nchini Kenya. Aidha inaaminika wanafunzi wa jamii ya kibantu hawana matatizo mengi wakilinganishwa na jamii-lugha zingine kwa sababu ya ukuruba wa fonolojia na fonimu ya lugha zao na lugha ya Kiswahili. Shule sita za msingi ziliteuliwa kwa kutumia sampuli bahatishi. Shule hizo ni Chomo, Gatura, Gatunyu, Kirwara, Gichumbu na Rwegetha. Tarafa hii ya Gatanga ilichaguliwa kwa sababu watoto hawana athari kutoka kwa jamii zingine. Tarafa hizo zingine katika wilaya hii, Kakuzi na Thika-Ruiru zina mchanganyiko wa wakaazi kutoka sehemu zingine za nchi. Utafiti ulizingatia kusoma kwa sauti ukilenga sifa zake bainifu kama vile: kuzingatia matamshi sahihi, kusoma kwa mwendo mwafaka na kwa ufasaha, kiimbo, mkazo na alama za kuakifisha. Pia ulichunguza mbinu na nyenzo zilizotumiwa na walimu na aina ya tathmini walizowapa watoto. 12 1.7Misingi ya Nadharia Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Krashen (1985). Nadharia hii inaonyesha kuwa, kuna taratibu za kuzingatiwa ili mtoto kuweza kujifunza ujuzi wa kusoma na kufahamu makala anayosoma ama kwa sauti au kimoyomoyo. Krashen anaeleza umuhimu wa uteuzi wa makala kama mojawapo ya vipengele muhimu katika kufanikisha ujifunzaji wa L2. Ujifunzaji wa L2 hufanyika kwa urahisi ambapo uteuzi mwafaka wa makala unafanywa huku ukihusisha hisi za walengwa. Kadhalika modeli Husishi ilitumiwa katika utafiti huu. Modeli Husishi ni modeli ya kijumla ambayo inajumuisha modeli ya Juu-Chini na modeli ya Chini-Juu katika kukuza stadi ya kusoma. Modeli ya Juu-Chini inazingatia ujuzi wa juu wa kusoma ambao ni ufahamu wa makala yanayosomwa. Modeli ya Chini-Juu inatilia mkazo ujuzi wa chini wa kusoma ambao unahusisha upambanuzi wa maumbo na sauti zake kisha kuishilia na ufahamu. Modeli hizi zinajengana katika kukuza ujuzi wa usomaji. Hii ina maana modeli Husishi ni bora zaidi kwa sababu inahusisha sifa zote ambazo zinapatikana katika modeli ya Juu-Chini na Chini-Juu badala ya kuzitenganisha na kuipa modeli moja uzito kuliko nyingine. 1.7.1Nadharia ya Krashen Nadharia hii iliasisiwa na Krashen miaka ya sabini katika makala mbalimbali iliyochapishwa (Krashen 1982, Krashen 1985; Krashen and Terrel 1988; Mclaughlin, 1987). Nadharia hii inajikita katika ujifunzaji wa L2 ambapo inashikilia umuhimu wa t kuteua kifungu au makala ambayo itawafaa walengwa. Kadhalika inaelezea kuwa hisi za mwanafunzi huathiri upokezi wa kifungu ama chanya au hasi. Yamkini habari au 13 makala ndio kipengele muhimu katika kujifunza L2. Vipengele hivyo vingine hutumika kuendeleza upokezi wa lugha mahsusi. Nadharia ya Krashen ina vipengele au vitengo vitano. Vitengo hivi ni: kitengo cha Upataji-Ujifunzaji, kitengo cha Utaratibu wa Kiasili, kitengo cha Ujaribiaji, kitengo cha Uteuzi wa makala na kitengo cha Hisi. 1.7.1.1 Kitengo cba Upataji - Ujifunzaji Lugba Krashen (1985) anachukulia lugha ni mfumo wenye taratibu mbili za kujifunza lugha zinazohitilifiana. Utaratibu wa kwanza, ni upataji wa lugha kwa njia ambayo si waziwazi. Hii ni njia ambayo hufanana na namna ambavyo watoto hujifunza lugha ya kwanza (Ll). Aidha, ni zao la kupata lugha kwa kuingiliana na wenyeji wa lugha hiyo. Utaratibu wa pili ni ujifunzaji lugha kupitia njia dhahiri. Njia hii hufuata utaratibu rasmi ambao huishilia na kujua lugha iliyokusudiwa ambayo huwa L2. Katika njia ya kwanza mtu hutumia lugha kwa minajili ya kuwasiliana na hufahamu vipengele vya lugha kutokana na uhusiano wake na watumiaji wa lugha hiyo. Wazungumzaji hawajali usahihi wa lugha bora tu maana imeeleweka. Namna ya pili, ujifunzaji huwa ni matokeo ya kujifunza vipengele vya lugha katika mazingara rasmi na hutilia mkazo matumizi sahihi ya lugha. Kulingana na Krashen utaratibu wa pili ndio mahsusi kwa sababu sheria za lugha zinabainika waziwazi kutokana na mazingara rasmi. Hata hivyo, kuna upungufu unaojitokeza katika kitengo hiki ambapo dhana hizi mbili upataji na ujifunzaji hazijabainishwa na Krashen. Kadhalika, hajaonyesha taratibu za kuzingatiwa katika utekelezaji wake. 14 Kwa mujibu wa maelezo ya Mclaughlin (1987) kuna mwingiliano wa taratibu hizi mbili ambapo kwa mfano, katika mazingara yasiyo rasmi watu wazima wanaweza kujifunza sheria za lugha kwa kuuliza maswali marafiki zao. Vilevile katika darasa wanafunzi wanaweza kupata lugha ambapo wanashiriki katika mijadala, maigizo darasani na kusemezana nje ya darasa. Kama tulivyodokeza, utafiti wetu umehusu ujifunzaji wa Kiswahili kama L2. Kitengo hiki kilitufaa katika kuchunguza ufundishaji wa stadi ya kusoma kwa sauti lugha ya Kiswahili. Watoto hawawezi kupata ujuzi wa kusoma kwa ufasaha na kwa kiimbo cha Kiswahili bila kufundishwa kirasmi. Isitoshe watoto wanaoshughulikiwa katika utafiti huu ni watoto wa mashambani, hawana mwingiliano na wasemaji wa lugha hii kwa hivyo wanategemea mwalimu kuwafunza namna ya kusoma na kuwasiliana kwa lugha hii. 1.7.1.2 Kitengo cha Utaratibu wa Kiasili Kitengo hiki kwa mujibu wa Krashen kinachukulia kuwa upataji wa sheria za lugha hufuata utaratibu unaobashirika ambapo upataji wa baadhi ya sheria hufuata moja baada ya nyingine. Hata hivyo, utaratibu huu hauonyeshi mpangilio maalum unaofaa kufuatwa katika utekelezaji wake. Kitengo hiki hujikita katika kuelezea upataji wa vipengele vya kisarufi kama vile nomino, viarifa, vimilikishi, mnyambuliko wa vitenzi na kadhalika. Kando na vipengele vya sarufi, ujuzi wa kusoma pia hufuata utaratibu maalum, kwa hivyo kitengo hiki kilitufaa katika utafiti wetu kwa sababu tulishughulikia taratibu za 15 kufuatwa katika ujifunzaji wa kusoma kwa sauti. Kadhalika ni muhimu walimu kufahamu hatua za usomaji ili kuweza kuandaa shughuli ili kuimarisha usomaji kwa sauti. 17.1.3 Kitengo cha Urekebishaji Makosa Kulingana na Krashen (1985) hiki ni kifaa ama chombo kinachoonyesha namna upataji na ujifunzaji wa L2 unavyofanyika. Chombo hiki kinahakikisha marekebisho yanafanyika katika muundo wa usemi wa lugha baada ya kufahamu sheria za lugha hiyo. Uwezo wa kutoa usemi katika lugha fulani inatokana na uwezo ambao mtu amezaliwa nao. Ujuzi unaotokana na ujifunzaji wa lugha katika mazingara rasmi unabainisha sheria za lugha mahsusi. Ujuzi wa sheria hizi, inakuwa chombo cha kufanyia marekebisho usemi kabla ya kuongea au kuandika. Kitengo hiki kina umuhimu wake katika ufundishaji wa lugha kama anavyoeleza Krashen. Anaelekeza kuwa kuna masharti mawili ya kuzingatia ili kuweza kutumia chombo hiki vizuri. Sharti ya kwanza, msemaji azungumze lugha kwa usahihi na pili, , afahamu sheria za lugha ile.Hata hivyo, masharti haya mawili ni vigumu kutekeleza. Kitengo hiki hakikutumika katika utafiti huu kwa sababu hatukushughulikia usahihi wa matumizi ya lugha. Utafiti wetu ulijikita katika madarasa ya chini ambapo misingi ya dhana mbalimbali za lugha zinajengwa. Hii ina maana kuwa watoto katika kiwango hiki walikuwa hawajaimarika katika ujuzi wa sheria za lugha ili kuweza kuj irekebisha. 16 1.7.1.4 Kitengo cha Uteuzi wa Makala Kitengo hiki kinadai kuwa binadamu hupata lugha kwa njia moja tu, ambayo ni kwa kufahamu ujumbe au kupokea habari inayoeleweka. Krashen anasema kuwa ujuzi huu huimarika kwa kufuata utaratibu wa kiasili. Maendeleo ya ujuzi wa lugha huimarika ambapo msomaji anabainisha makala yenye miundo tofauti yenye kuimarika kuzidi kiwango cha makala iliyotangulia Krashen anaendelea kusema kuwa, hata ujuzi wa sarufi ya lugha hufuata mkondo huu. Msomaji anaweza kubainisha vipengele vya sarufi kwa kuhusisha muktadha na sifa zisizo za kiisimu kung'amua matumizi yake. Kadhalika mwalimu wa lugha anaweza kufunza makala kwa kuhusisha nyenzo mbalimbali (picha, vifaa halisi) katika ufundishaji. Kitengo hiki kinajikita katika mambo mawili: 1. Usemi ni zao la upataji. Usemi hauwezi kufunzwa moja kwa moja bali ni matokeo yanayotokana na uteuzi wa habari mwafaka inayoishilia na kujenga umilisi wa lugha. 2. Ikiwa makala iliyoteuliwa inafahamika na inatosheleza, aidha vipengele vya sarufi vitajitokeza moja kwa moja. Mwalimu wa L2 hatasumbuka kufikiria atafunza nini katika kiwango kinachofuata yamkini haya yatajitokeza kwa kiasi inayotosheleza na anaweza kukagua kama mwanafunzi amepata iliyokusudiwa. Inadhihirika wazi kuwa aina ya habari inayoteuliwa katika ujifunzaji wa lugha ni muhimu ikiwa mwanafunzi ataimarika katika lugha ile. Kwa mujibu wa Chomsky kila binadamu amezaliwa na chombo ambacho kinamwezesha kupata lugha. Mbali na kusikiliza habari, chombo hiki pia kinachangia katika ujifunzaji wa lugha. Hata hivyo, 17 KENYA U VE madai kuwa ujifunzaji wa lugha unafanyika kwa njia moja tu hautoshelezi katika kipindi tulichomo. Kuna tafiti nyingi ambazo zinaonyesha kuwa watu wanatofautiana na tofauti hizi huathiri ujifunzaji wa lugha. Kitengo hiki kilifaa utafiti wetu kwa sababu kilituwezesha kuonyesha umuhimu wa kuteua makala ya kusoma ambayo inalingana na uwezo wa watoto. Kadhalika kilionyesha umuhimu wa kuteua nyenzo mwafaka katika ufundishaji wa kusoma kwa sauti ili kutosheleza tofauti za uwezo katika watoto. 1.7.1.5 Kitengo cha Hisi Kitengo hiki kinajihusisha na athari za hisi katika ujifunzaji wa lugha. Uteuzi wa makala ya kusoma ni muhimu lakini si kipengee cha kipekee katika ujifunzaji wa lugha. Msomaji itambidi kuwa katika hali nzuri ili kupokea kile anachosoma. Kwa mujibu wa Krashen (1985) kuna haja ya kuchuja habari zinazomfaa mwanafunzi. Pia kuna haja ya kujua kiasi gani cha habari kinachoweza kupokelewa na kwa muda upi. Aidha inaaminika kuwa hisi za mwanafunzi huathiri upokezi wa habari. Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kumuathiri mwanafunzi ni kama vile: kukosa motisha, kutojiamini na hofu wakati wa ujifunzaji. Kulingana na Yule (1996) akichangia kitengo hiki cha Hisi anasema kuwa watoto wanaweza kuwa katika umri unaofaa kujifunza lugha lakini kunaweza kutokea vizingitimkuti vya kumzuia kuimarika katika lugha. Anaeleza kuwa mazingira yenye kuaibisha mtoto, mazingara ya darasani yasiyosisimua, na ratiba za vipindi zenye 18 kuchosha zitaathiri hasi ujifunzaji wa lugha. Nyenzo na vitabu visivyovutia, vitazuia uimarishaji wa lugha. Ikiwa mtoto ana uchovu, njaa, hofu na hajiamini itakuwa vigumu kwake kujifunza chochote katika lugha. Kitengo hiki kilitufaa katika kuchunguza vigezo ambavyo walimu wanatumia kuteua makala ya kusoma kwa mfano urefu, ugumu wa makala. Aidha ilitufaa katika kuchunguza mbinu na nyenzo mbalimbali zilizotumiwa, na namna zilivyochangia katika ujifunzaji wa kusoma kwa sauti. Kadhalika ilitusaidia kutathmini mazingara ya darasani yalivyochangia katika ufundishaji wa kusoma kwa sauti kama vile kiwango cha motisha darasani. 1.8 Modeli Husishi Modeli hii imekuzwa na wataalamu mbalimbali (Rumelhart, 1977 ; Stanovich, 1980 ; Ulijn, 1980). Modeli hii inahusisha modeli ya chini-juu na juu-chini katika usomaji. Kila mojawapo inachangia katika kuelewa kwa kifungu kinachosomwa. Wataalamu wenye mwelekeo huu wanaamini kuwa usomaji unahusisha bongo lakini si uradidi tu wa silabi ambao unakuza ujuzi wa kusoma. Hii ina maana ikiwa watoto watafunzwa kufahamu, kutathmini, kupambanua anachosoma basi itabidi ujuzi wa aina zote mbili ukuzwe mapema ili mtoto aone maksudi ya kusoma. Eskey (1988) anasema kuwa modeli hii inaweza kufafanua namna kusoma kunavyofanyika kwa wanaojifunza L2. Anasema kufasiri kwa mfumo mmoja wa lugha hadi mwingine ni muhimu hasa katika stadi ya kusoma kama ilivyo stadi zingine zajuu. 19 Modeli hii ilitumika katika utafiti huu ili kuonyesha umuhimu wa kusoma kuanzia mwanzo mtoto anapoingia shuleni. Hii ni kwa sababu mtoto asipofurahia kusoma mapema, atakosa motisha na atatatizika katika ujuzi wa juu wa kusoma. Watoto katika madarasa ya chini wanatayarishwa katika ujuzi wa chini ambao unahusisha kupambanua herufi mbalimbali na kuweza kuzitamka kwa usahihi pia kutamka maneno kwa ufasaha. Kadhalika stadi ya kusoma inahusisha ufahamu wa kinachosomwa ujuzi huu wa juu itabidi ukuzwe mapema ili mtoto aone fahari ya usomaji. Modeli hii ilitusaidia kuonyesha umuhimu wa kuzingatia viwango vyote viwili vya usomaji ikiwa yatapatikana maendeleo mazuri ya usomaji katika madarasa ya chini. Modeli hii ni jumlishi kwa hivyo ilitufaa zaidi katika utafiti wetu, hii ni kwa sababu kusoma kunahusisha mambo hayo mawili kupambanua herufi na ufahamu. 1.81 Modeli Chini-Juu Waasisi wa modeli hii Gough (1972) na pia Laberge na Samuel (1975) wanasema kuwa kuna umuhimu wa watoto kuimarika katika ujuzi wa kufasiri maumbo na kuyatamka, kupambanua maneno, ili kuweza kufahamu matini wanayosoma. Wote wanakubaliana na kusisitiza haja ya kufasiri kila neno kwanza na kuishilia na ufahamu wa kilichosomwa. Mwasisi mwingine Newman (1979) anashikilia kuwa utambuzi wa sauti za maumbo tofauti ndio ujuzi wa kimsingi katika utambuzi wa neno. Aidha, anasema kuwa ikiwa mtoto hawezi kutambua neno kwa kulitazama itakuwa vigumu kwake kuelewa habari aliyosoma. Kule kujua kanuni za kifonetiki kutamwezesha kufasiri maneno. 20 Mbinu za kufunzia kama vile kutamka sauti, abjedi, silabi zinazingatia modeli hii. Modeli hii ilitufaa katika utafiti wetu kwa sababu watoto wanaojifunza kusoma katika madarasa ya kwanza na ya pili wanazingatia ujuzi huu wa kuweza kufasiri maumbo na kupambanua maneno ambao ndio wa kimsingi katika kusoma kwa sauti. Silabasi pia inapendekeza matumizi ya mbinu zilizotajwa hapo juu ili kuimarisha usomaji. Mbinu hizi zimejikita katika ujuzi wa chini wa kusoma kwa sauti. Ujuzi huu ni muhimu kwa sababu bila ujuzi huu haiwezekani mwanafunzi kuingia katika kiwango kinachofuata cha ujuzi wa juu ambao unajikita katika ufahamu. Aidha, kupambanua herufi huchukua muda kuzimudu. Hivyo basi modeli hii imetumiwa katika utafiti wetu kuchunguza athari za uchaguzi wa walimu katika matumizi ya mitindo fulani katika ujifunzaji wa kusoma kwa sauti. Pia imetumiwa kuonyesha uzuri na upungufu wa mbinu zilizopendekezwa katika ujifunzaji wa kusoma kwa sauti. 1.8.2 Modeli ya Juu-Chini Goodman na Burke (1972) wanashikilia kwamba ufahamu wa kifungu hautokani na kuelewa kwa neno kivyake, bali muktadha wa neno huchangia katika kuelewa kwa neno lenyewe. Pia ujuzi wa lugha na mazingara nje ya matini huchangia katika ufahamu wa ujumbe. Modeli hii inajikita katika ujuzi wajuu ambao unahusu ufahamu wa kile kinachosomwa. Ujuzi huu unaendelezwa na mbinu kama kutazama na kusema neno, kusoma kirai, kusoma sentensi na kusoma hadithi. Modeli hii itafaa zaidi wanafunzi wa kiwango chajuu ambao tayari wana umilisi wa kusoma na hawana matatizo ya kufasiri maumbo, na wenye uwezo wa kutumia 21 mikakati mbalimbali kuelewa ujumbe uliosomwa. Kwa hivyo, ujuzi huu unahitaji kukuzwa mapema. Kusoma kwa sauti kunatilia mkazo matamshi bora, ufasaha, viimbo, mkazo, mahadhi na uakifishaji. Sifa hizi ndizo husababisha uelewa wa kinachosomwa. Kwa hivyo haina budi kwa kiasi kuchunguzajinsi ujuzi huu wajuu ulivyokuzwa katika madarasa ya chini. Ikumbukwe watoto katika darasa la tatu kulingana na silabasi huchukuliwa kuwa wamemudu ujuzi wa chini. Hii ina maana kuwa walimu katika darasa hili huzingatia zaidi kukuza ufahamu wa makala. Modeli hii itafaa utafiti wetu katika kuonyesha athari za kutilia mkazo mitindo fulani na kupuuza ile mingine. 1.9 Tahakiki ya Maandishi Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu kusoma kwa jumla katika lugha ya Kiingereza na lugha zingine lakini chache katika lugha ya Kiswahili. Teal (1994) anasema kuwa kusoma kwa sauti ni muhimu san a kwa watoto. Njia hii hukuza vipengele vingine vya usomaji ambavyo ni muhimu katika mawasiliano. Kumsomea mtoto kwa sauti ni njia moja ya kusisimua na mwafaka katika kumwiingiza mtoto katika ulimwengu wa kusoma. Utafiti wa Wario (1981) ulichanganua ujuzi wa kusoma unavyoingiliana na mazingara ya shule. Utafiti ulinuia kubainisha athari za mijengo ya shule, ukubwa wa darasa, maeneo ya shule, vitabu na maktaba katika usomaji. Alipata kuwa mambo hayo huzuia watoto kufikia kiwango chajuu cha usomaji. Tofauti iliyopo kati ya utafiti huu 22 na wetu ni kuwa utafit wa Wario haukuzingatia mbinu, nyenzo na tathmini zinavyochangia katika kuimarisha stadi ya kusoma. Alirejelea kwa jumla stadi ya kusoma, lakini utafiti wetu umejikita katika ujifunzaji wa kusoma kwa sauti. Wanyoike (1982) alishughulikia utaratibu wa kufundisha stadi ya kusoma katika madarasa ya kwanza na ya pili. Ameelezea kwa jumla mbinu ambazo zinafaa kutumiwa na walimu katika ufunzaji baadhi yake ni kama vile abjedi, silabi, tazama na kusema. Utafiti huu ni tofauti na wetu kwa sababu huu ulidhamiriwa kuwa mwongozo wa walimu wa kufundishia stadi ya kusoma katika madarasa ya kwanza na ya pili. Aidha, utafiti huu haukuhusisha moja kwa moja kusoma kwa sauti na haukujikita katika nadharia ya ujifunzaji L2. Kadhalika haukujikita katika utafiti wa nyanjani. Hata hivyo, ulitusaidia katika utafiti wetu kuelewa uzuri na udhaifu wa mbinu mbalimbali za ujifunzaji wa kusoma. Aidha, shughuli ambazo walimu wanaweza kushirikisha watoto katika usomaji zimejadiliwa. Naye Onyamwaro (1990) alitafiti mambo ambayo huathiri ufunzaji wa kusoma lugha ya Kiswahili, kwa jumla katika madarasa ya chini. Utafiti huu ulichunguza mambo yanayoathiri ufundishaji wa kusoma. Alishughulikia maswala k.v. ujuzi wa mwalimu, mazingara ya mtoto, nyenzo na mbinu za kufundishia kusoma. Alipata kuwa walimu walikuwa wamehitimu katika vyuo vya walimu lakini walikosa msingi mzuri katika lugha ya Kiswahili katika shule za msingi na sekondari. Utafiti huu ulibainisha ukosefu wa vitabu na nyenzo za kutosha kufundishia. Walimu walikosa ujuzi wa kuandaa mafunzo ya kusoma kwa njia mwafaka kama ilivyopendekezwa kwenye silabasi. Utafiti huu haukuchunguza matatizo ya watoto ya kusoma kwa sauti na 23 namna walimu walivyoyatatua. Kadhalika, huu ulijadili kusoma kwa jumla na haukujikita katika misingi ya nadharia ya ujifunzaji wa L2. Utathmini wa kusoma ufahamu kwa watoto wa darasa la nane ulifanywa na Kirigia (1991). Utafiti huu ulichunguza ufundishaji wa ufahamu kwa lugha ya Kiingereza. Aidha ulijaribu kupima ufahamu wa watoto kuhusu mada mbalimbali walizopewa. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa watoto wengi hawakuelewa walichosoma. Utafiti huu ni tofauti na wetu kwa sababu ulihusu watoto katika madarasa ya nane. Aidha, ulipima ujuzi wa juu katika stadi ya kusoma ambao ni ufahamu katika lugha ya Kiingereza. Huu wetu ulishughulikia kusoma kwa sauti kwa watoto katika madarasa ya chini. Kadhalika, nadharia iliyotumiwa ni tofauti na yetu. Kirigia alitumia nadharia ya isimunafsia na sisi tulitumia nadharia ya Krashen. Utafiti huu ulitusaidia kufuatilia shina la matatizo katika stadi ya kusoma. Mberia (2002) alitafiti ufundishaji wa kusoma katika lugha ya Kiingereza kwa madarasa ya chini. Alichunguza mbinu zilizotumiwa na walimu na njia walizotumia kuteua makala ya kusoma. Aidha, nyenzo ambazo zilitumiwa na walimu na namna walivyopima viwango vya usomaji wa watoto vilichunguzwa. Utafiti huu ni tofauti na wetu kwa sababu huu ulijikita katika kuchunguza kusoma kwa ufahamu kwa lugha ya Kiingereza na huu wetu ulishughulikia kusoma kwa sauti katika lugha ya Kiswahili. Utafitii huu ulichangia utafiti wetu katika uteuzi wa baadhi ya nadharia zilizoongoza utafiti wetu. 24 1.10Mbinu za Utafiti Utafiti huu ulihusisha mbinu mbili kwa upande mmoja utafiti wa maktabani na wa nyanjani kwa upande mwingine. Utafiti Maktabani: Usomaji mpana wa vitabu, makala, tasnifu, majarida na machapisho yanayohusiana na mada ulifanywa maktabani. Usomaji huu ulimsaidia mtafiti kuelewa zaidi kuhusu nadharia za utafiti wetu pamoja na maoni mbalimbali ya wataalamu kuhusu dhana katika stadi ya kusoma. Utafiti Nyanjani: Baada ya usomaji wa maktabani, utafiti wa nyanjani ulifanywa kwa nia ya kuchunguza namna walimu walivyotekeleza ufundishaji wa kusoma kwa sauti. Data ilikusanywa kutoka kwa walimu sita kutoka kwa kila darasa la kwanza, la pili na la tatu kutokana na shule sita katika tarafa ya Gatanga, wilaya ya Thika. Idadi hii i1ichaguliwa kwa sababu ingetupa data ya kutosha. Kwa mujibu wa Milroy (1987) ni kwamba sampuli ndogo ndiyo mwafaka katika utafiti wa lugha. Hii ni kuwa sampuli kubwa katika utafiti wa lugha huzua data nyingi yenye urudufu. Shule sita za umma zilizoteuliwa ni Chomo, Gatura, Gatunyu, Kirwara, Gichumbu na Rwegetha. Darasa moja la kwanza, la pili na la tatu zilichaguliwa kutoka kwa kila shule. Madarasa haya yaliteuliwa kwa sababu stadi ya kusoma kwa sauti ilizingatiwa zaidi kuliko katika madarasa ya juu. Pia dhana za kimsingi zilifundishwa katika 25 madarasa haya. Isitoshe, watoto walipewa tathmini za kusoma kwa sauti katika tathmini rasmi katikati na mwisho wa muhula. Walimu katika madarasa haya walijibu maswali ya hojaji. Kadhalika, mtafiti alichunguza kipindi kimoja cha stadi ya kusoma katika kila darasa kwa kutumia ratiba ya kukagua funzo. Kwa njia hii matokeo ya majibu ya hojaji yaliweza kuthibitishwa. Aidha, kinasa sauti kilitumiwa kurekodi funzo ili kumpunguzia mtafiti kazi ya kuandika kila kitu ili aweze kuzingatia zaidi mazingara ya darasa na namna ufundishaji ulivyotekelezwa. Majadiliano yasiyo rasmi yalitumiwa kuangazia baadhi ya hoja zilizotolewa kwenye hojaji na yaliyochunguzwa darasani. 1.10.1 Sampuli Tarafa ya Gatanga ina maeneo matatu ya kielimu, Gatanga, Kihumbuini, na Kariara. Tarafa hii ni pana sana na ina shule arobaini na saba za umma. Eneo la Gatanga liliteuliwa na shule sita kati ya kumi na nne ziliteuliwa kwa kutumia mbinu bahatishi. Shule hizi zilichaguliwa kuwakilisha tarafa ya Gatanga. Shule ziliteuliwa kwa kutumia mbinu bahatishi kwa sababu watoto hawa walikuwa wamelelewa katika mazingara yaliyofanana, kama vile; Ll, umri na tajriba ya lugha ilikaribiana. Aidha shule zote katika eneo la Gatanga zilipangwa katika makundi mawili; shule zenye darasa moja kwa kila kiwango na zenye zaidi ya darasa moja. Kisha kwa kutumia sampuli bahatishi tuliteua shule tatu katika kila kikundi. Kwa jumla, shule sita ziliteuliwa kuwakilisha tarafa hili. Kisha shule ambazo zilikuwa na zaidi ya darasa moja, mbinu bahatishi i1itumiwa kuteua darasa moja. 26 1.10.2 Ukusanyaji Data Walimu kumi na wanane waliofunza madarasa yaliyoteuliwa walijibu maswali ya hojaji. Pia majadiliano yasiyo rasmi yalitumiwa na mtafiti kuangazia majibu katika hojaji na uchunguzi wa darasani. Mtafiti alikagua kipindi kimoja kwa kila darasa akiongozwa na ratiba ya kukagua funzo. Usomaji ulirekodiwa, hii i1isaidia mtafiti kuwa mwangalifu wakati wa kuchanganua data kwa sababu aliweza kuchunguza matamshi, viimbo, mkazo na uakifishaji katika ufundishaji darasani. Kadhalika ilimpunguzia mtafiti kazi ya kuandika kila kitu kwa sababu si rahisi kunakili kila kitu na kusikiliza kwa wakati mmoja. Kwa njia hii mtafiti aliweza kupata data muhimu na ya kutosha. Aidha data kutoka kwa maswali yasiyo rasmi yalibainisha majibu ambayo yalitolewa. Kadhalika tuliweza kutazama kazi ya watoto kwenye daftari zao. Daftari chache ziliteuliwa kwa kutumia mbinu bahatishi ili kuzikagua ilimradi kuonyesha matokeo ya ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika madarasa ya chini. 1.10.3 Uchanganuzi na Uwasilishaji wa Data Utafiti huu ulilenga kuchanganua ufundishaji wa kusoma kwa sauti. Data kutoka nyanjani ilichanganuliwa kwa kuzingatia maswali kwenye hojaji iliyojazwa na walimu. Idadi ya majibu ya walimu yalionyeshwa katika majedwali. Majedwali yalipangwa kuonyesha kila darasa Iilivyoendelezwa. Kwa njia hii, maendeleo ya usomaji yalionekana dhahiri kutoka kwa darasa moja kwenda lingine. Kadhalika aina za matatizo ya watoto katika usomaji na namna ya kutatua matatizo yale yalionyeshwa katika majwedali kwa kila darasa. Hojaji hizi zimeonyesha utekelezaji 27 wa kusoma kwa sauti ulivyofanywa na mikakati iliyotumiwa na walimu kuimarisha usomaji. Data iliyotokana na uchunguzi wa darasani iiichanganuliwa ili kuthibitisha majibu kutoka kwa walimu kwenye hojaji. Aghalabu, matokeo ya uchanganuzi yalitolewa kwa njia ya maelezo. Idadi ya majibu ya walimu katika hojaji kuhusu maoni fulani ikizidi nusu ya jumla za majibu yaliyotolewa, ilichukuliwa hiyo ndiyo mielekeo inayozingatiwa na walimu wengi kuhusu stadi ya kusoma kwa sauti. Muhtasari. Sura hii, imeweka msingi wa utafiti huu kwa kuzingatia sehemu mbalimbali za utafiti huu. Sehemu hizi ni k.v. swala la utafiti, sababu za kuchagua mada, malengo ya utafiti, upeo na mipaka na misingi ya nadharia. Kadhalika yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti zimeshughulikiwa. Sura inayofuata inabainisha dhana muhimu katika stadi ya kusoma kwa sauti na njia mbalimbali za kutekeleza ufundishaji wa stadi hii. 28 LIB SURA YA PILI: MBINU NA NYENZO ZA KUFUNDISHIA KUSOMA 2.0 Utaugulizi Sura hii inatoa maelezo kuhusu mbinu za kufundishia kusoma ambazo ni za aina mbili ya uchanganuzi na changamano. Aidha kuna maelezo kuhusu: • Sifa bainifu za stadi ya kusoma kwa sauti. • Mbinu na nyenzo za kufundishia kusoma kwa sauti. • Mitindo ya usomaji. • Vitangulizi kabla ya usomaji. • Tathmini na kazi ya marudio. Maelezo haya yanapambanua na kubainisha stadi ya kusoma kwa sauti na kuonyesha uzuri na upungufu wa baadhi ya taratibu zilizoshughulikiwa. 2.1 Stadi ya Kusoma Dhana ya kusoma imekuwa ikibadilika katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita kadri utafiti wa stadi hii unavyoendelea. Kusoma ni utaratibu wa upokezi wa lugha kama ilivyo kusikiliza. Utaratibu huu unahusisha isimunafsia ambayo huanza kwa kubainisha namna maumbo yanayowakilisha sauti yanavyopokelewa na msomaji ambaye anang'amua maana iliyokusudiwa na maandishi (Goodman, 1969). Yamkini kuna uhusiano baina ya lugha na mawazo katika usomaji. Mwandishi hueleza mawazo yake kupitia lugha naye msomaji anafasiri lugha na kung'amua mawazo yaliyokusudiwa. Aidha, Pearson (1981) anasema kuwa kufasiri maumbo ni jambo la kimsingi katika usomaji. Hata hivyo, shughuli za usomaji haziwezi kukamilika bila 29 kuwepo uelewa wa kile kinachosomwa. Hii ina maana kuwa ujuzi wa aina zote mbili ni muhimu kuzingatiwa katika usomaji kwa sababu zinaingiliana. Usomaji unaofaa ni ule wenye kuleta matokeo yanayotarajiwa. Yamkini, kuweza kusoma kwa usahihi na kwa ustadi ni kuweza kufahamu yanayosomwa ili kutimiza makusudio ya kusoma (Gathumbi na Ssebbunga, 2005; 32). Walimu wa lugha wana malengo mawili mahsusi: ambayo ni kuhakikisha watoto wanaweza kutumia lugha kwa usahihi na kwa ufasaha. Ufasaha huu hutokana na mtoto kuwa katika mazingira yenye wingi wa lugha ya kuongea na lugha ya maandishi (Claessen na Stephen, 1988). Homer (1974) anasema kuwa kuna mambo ambayo huchangia katika ujifunzaji wa kusoma. Baadhi ya mambo yanayoathiri ujifunzaji wa kusoma ni: • Uwezo wa akili wa mwanafunzi. • Uwezo wa kuwasiliana. • Mazingara mwafaka ya nyumbani na shuleni. • Ukomavu wa kimwili. • Ukomavu wa kihisia. 2.1.1 Sifa bainifu za Usomaji wa Sauti Kusoma kwa ufasaha kunamaanisha kusoma bila kusitasita au kuacha mapengo katika usomaji, msomaji kujua maneno anayotaka kusema bila kizuizi chochote, neno moja likiongoza na kufuatwa na neno lingine. Kusoma kwa mwendo wa wastani, kusoma bila kugusa kila neno kwa kidole wala kumumunya neno kabla ya kutamka, kusoma 30 bila kuruka maneno na hakuna kujirudia rudia anaposoma (Gathumbi na Ssebbunga, 2005:33). Aidha wanasema kuwa walimu na hata wazazi hutarajia watoto wao kuwa wasomaji hodari. Ufanisi wa watoto katika usomaji utategemea wao kupata uwezo na ujuzi ambao huonekana dhahiri kwa wasomaji hodari. Ni jukumu la mwalimu kuhakikisha kuwa watoto wanakuza uwezo wa kumudu kusoma kwa ustadi. Kulingana na K.I.E (2006) baadhi ya mambo ambayo yanafaa kukuzwa katika usomaji wa sauti ni kama yafuatayo: • Matamshi • Kiimbo • Mkazo (1) Matamshi Kwa mujibu wa Dalton na Barbara (1994) matamshi ni muhimu sana kama jinsi ishara uso, mkao wa mtu na mavazi zina uwezo wa kuathiri namna ya kumchukulia mtu fulani kadhalika lugha na matamshi yetu. Matamshi yanaweza kuashiria umri, jinsia, tabaka, kiwango cha elimu, na kama ni mtu ama wa kupendeka au la Kuna ithibati nyingi kutokana na wataalamu kuwa watoto wenye umri wa chini huimarika katika matamshi kwa sababu bongo zao bade changa na kuwa sehemu zote mbili za bongo bade kubobea katika jambo moja maalum. Maelezo ya Schumanns (1975) akiendeleza nadharia Hisi anasema kuwa watoto ni viumbe vya kijamii, kwa hivyo kutokana na hulka yao hisia hupenya kwa urahisi na kuwaathiri watoto kihisia na kijamii. Kadhalika, vivyo ndivyo walivyotayari kupokea lugha kwa urahisi kuliko vijana waliobalehe na watu wazima. 31 Aidha jambo linalotajwa na wataalamu ni kuwa kuna umuhimu wa matamshi sahihi kwa wanaojifunza L2. Hata hivyo, hii haina maana ya kuwa na lafudhi inayofanana moja kwa moja na ya wazawa wa lugha ile. Hii ni kwa sababu si rahisi kufanikiwa kwa watu wazima hasa ikiwa mazingara yenyewe hayana wingi wa lugha ile. Kwa hivyo, matamshi sahihi ni yale yanayoeleweka kwa yule aitumiaye na wale wanaosikiliza (O'Connor, 1967). Anaelezea kuwa kama ilivyo vigumu kukuza tabia nzuri, ndivyo ilivyo vigumu kufunza matamshi sahihi. Hivyo kuna haja ya wanaohusika na ufundishaji wa lugha kujitahidi sana kufanyisha mazoezi ya kusikiliza kwa makini ili kukuza matamshi sahihi. Kusikiliza, ni stadi muhimu ya kuzingatiwa katika juhudi za kufundisha matamshi. IIi mwanafunzi aweze kutamka maneno vizuri ni lazima kwanza awe na uwezo wa kupambanua sauti zinazohusika katika usikizi wake. Bila uwezo huu ataishia kwa kutamka maneno na kuzungumza kwa namna ambayo inakanganya (Kawoya na Ryanga, 2003). Kusoma kwa usahihi na kwa ufasaha kutamfanya mtoto kujiamini na kumwezesha kujifanyia mambo yake bila kuhitaji usaidizi. Ufasaha una maana ya kuweza kusoma matini bila kukosea, haraka na kwa hisia. Ufasaha unatokana na mtoto kuzungukwa na lugha ya kuongea na kuandika. 32 (2) Kiimbo Kila lugha ina mahadhi/tuni inayoitofautisha na lugha nyingine. Aidha hakuna lugha inayozungumzwa kwa tuni moja kila wakati. Sauti husikika ikipanda na kushuka na vidatu tofauti hushikana kujenga tuni. Namna neno Iinavyosomwa Iinaweza kudhihirisha furaha, huzuni, chuki n.k. Maneno hayabadilishi maana bali tuni ama huongeza au hupunguza athari kutegemea yanayozungumzwa na hali ya wanaozungumza. Kulingana na Wamitila (2003) kiimbo ni dhana inayotumiwa kueleza jinsi sauti inavyosikika katika uongeaji au usomaji. Huhusisha mipando na mishuko ya sauti hizo. Dhana ya kiimbo huambatana na dhana ya vidatu yaani kiwango cha juu, cha chini au cha kati cha sauti katika usemaji. Vidatu vinatumiwa katika kiwango cha sentensi katika kutofautisha maana inayosemwa. Kiimbo husaidia kubainisha kusudi la usemaji lililokusudiwa na mzungumzaji kama vile kutoa maelezo, kuuliza swali, kuonyesha mshangao, na kutoa amri kulingana na namna kiimbo kinavyobadilika badilika. Kiimbo kwa hivyo ni sifa inayobainika katika sentensi nzima wala si neno kama ilivyo katika toni ( Habwe na Karanja, 2004). Kwa mujibu wa Mohammed (2001) na Habwe na Karanja (2004) kiimbo ni kipengele muhimu ambacho hutumiwa kutoa utata wa kuelewa maana katika sentensi. Pia hutofautisha maana ya sentensi yenye maana zaidi ya moja. Tutatambua iwapo msemaji anauliza swali, mshangao au kutoa taarifa kwa mfano katika sentensi hizi: i) Mpishi anapika ? ii) Mpishi anapika. iii) Mpishi anapika ! 33 Ingawa maneno yaliyotumiwa katika sentensi hizo juu ni yale yale, kiimbo kinachotumika ni tofauti katika kila usemi. Kwa hivyo, kiimbo hutubainishia hali za watu wanapozungumza kwa mfano mtu anapozungumza akiwa na furaha, huzuni, hofu au chuki kwa kubadilisha badilisha vidatu vyake i1i kudhihirisha mambo hayo. Kiimbo pia kina uzuri wa sauti na sifa zingine zote za uzungumzaji. Ni kupitia kwa kiimbo ambapo tunapata utamu wa lugha inapozungumzwa. Kiimbo ndicho ambacho huwabainisha watu mbalimbali wanapoongea. (3) Mkazo Mgullu (1999) na Mohammed (2001) wanakubaliana kuwa mkazo ni ile hali ya kulitamka neno au silabi fulani kwa nguvu zaidi kuliko nguvu zinazotumiwa kutamka maneno na silabi zingine. Silabi yenye mkazo husikika zaidi, huwa ndefu zaidi na huwa na kidatu cha juu zaidi kuliko maneno na silabi zingine. Silabi inayotamkwa kwa mkazo ina msikiko mkubwa zaidi kuliko silabi nyingine za neno hila hilo. Massamba na wenzake (2001) wanaeleza mkazo kama utamkaji wa nguvu zaidi katika sehemu ya neno au katika fungu la maneno. Katika lugha ya Kiswahili mkazo huwekwa katika silabi ya pili kutoka mwisho wa neno. Ifahamike kwamba ni yale maneno yenye asili ya Kiswahili tu yanayochukua mfumo huu. Hata hivyo, kuna maneno ya kukopwa kutoka lugha ya Kiarabu ambapo mkazo huwekwa kwenye silabi ya kwanza ya neno kwa mfano: 'dhambi, 'takribani, 'ghafula. Vilevile maneno mengine ya kukopwa yanadhihirisha mitindo mbalimbali ya kuweka mikazo kama vile ta'fadhali au tafa'dhali, 'ahadi au a'hadi, ho'tuba au 'hotuba. 34 Mkazo katika lugha ya Kiswahili inadhihirika katika kiwango cha neno na sentensi. Maana za maneno hutegemeajinsi msemaji anavyoweka mkazo (Mohammed, 2001). Katika kiwango cha neno mkazo unaweza kutumiwa kuonyesha tofauti ya maana ya maneno yanayofanana kwa mfano : Ba'rabara (sawasawa) 'ala (kifaa cha kuwekea kisu) wa'lakini (dosari) bara,bara (njia kuu) a'la (mshangao) wala'kini (hata hivyo) Katika kiwango cha sentensi, mkazo unaweza kubainika katika kusisitiza jambo au kinyume chake. Mikazo katika sentensi huwekwa katika neno fulani wanalotaka kulikazia wakalitamka kwa nguvu zaidi kama vile: a. Wataka 'kazi c. Wacheza 'mpira e.Waenda 'kasi b. Wa'taka kazi d. Wa'cheza mpira f. Wa'enda kasi Wanaisimu wanaamini kuwa neno ambalo hukaziwa zaidi katika sentensi huelekea kuwa na umuhimu zaidi kuliko maneno mengine. Mkazo katika sentensi ni huru kwa mfano; a. Hamisi analilia 'wembe. b. Hamisi anali'lia wembe. c. Ha'misi analilia wembe. Sentensi tatu hizo zina maana tofauti, sentensi ya kwanza inajibu swali Hamisi analilia nini ? sentensi ya pili inajibu swali Hamisi anafanya nini ? Hatimaye sentensi ya tatu inajibu swali ni nani analia? Mkazo ni muhimu sana katika kiwango cha sentensi. Mkazo wa sentensi katika lugha ya Kiswahili hautabiriki kama ilivyo katika kiwango cha neno, huwekwa popote. Mkazo katika sentensi ya maelezo ni tofauti na mkazo katika sentensi ya kuuliza na kutoa amri. 35 2.2 Mbinu za Kusoma Kusoma ni stadi ambayo ni ngumu kung'amua namna hufanyika. Hakuna anayeelewa kwa hakika namna mtu anavyofahamu kusoma. Wataalamu wa isimu wanaendelea kufanya utafiti ili kupata ujuzi ambao utatuwezesha kujua namna akili inavyofanya kazi kufahamu maana ya maandishi yaliyochapishwa. Hadi sasa hakuna utafiti ambao unaweza kuchukuliwa kuwa umetamatisha namna kusoma kunavyofanyika. Hata hivyo, kila mtu mwenye akili timamu ana uwezo wa kujifunza kusoma akipewa nafasi, mazingara mwafaka na mwongozo. Kwa mujibu wa wataalamu hakuna njia moja ya kipekee ya kufundisha au kujifunza kusoma. Mbinu yoyote ile ichaguliwe kwa kuzingatia uwezo wa mtoto. Vilevile shughuli zozote zitakazoteuliwa zielekezwe kwa mtoto ili kufanikisha malengo ya kusoma. Kulingana na Claessen na Stephen (1988) mbinu mwafaka ya kufundisha kusoma inafaa kuzingatia baadhi ya mambo yafuatayo: i) Watoto wanastahili kufuzu katika kila kiwango waliomo cha darasa. ii) Mwalimu afahamu kuwa ujuzi wa stadi za lugha hufuata mpangilio fulani. iii) Watoto wanahitaji mazingara mazuri ili kuamsha ari na mshawasha wa kujieleza kupitia lugha. iv) Mwalimu awe mnyumbufu mwenye kuweza kutumia nyenzo na mbinu tofauti kulingana na watoto alionao. 36 v) Mwalimu awe na njia mbalimbali za kutathmini ujuzi wa watoto bila kungojea mtihani rasmi. vi) Watoto sharti wasikilize na kucheza na lugha kabla ya kujaribu kusoma na kuandika. Kuna mbinu kadha za kufundisha kusoma. Wanyoike (1982) ameziweka katika makundi mawili. Kila mojawapo ikiwa na mbinu mbalimbali nazo ni: 1. Njia ya uchanganuzi (vipengele vya neno). 2. Njia changamano (huhusisha maana ya kila kisehemu cha sentensi). 2.2.1 Njia ya Uchanganuzi Kuna mbinu zifuatazo katika kikundi hiki : a) Mbinu ya abjedi b) Mbinu ya kutamka herufi kwa sauti c) Mbinu ya silabi a) Mbinu ya Abjedi Mbinu hii husisitiza umbo la herufi na majina ya herufi. Kwa njia hii watoto hukariri herufi zinazounda neno, kisha kutamka neno. Mtoto kwanza, hujifunza herufi kubwa na ndogo kama zinavyofuatana. Kisha inafuatwa na kushikanishwa kwa herufi mbili ambapo zinakaririwa na watoto. Kadhalika, herufi tatu, nne, tano zinafuata na kukaririwa ili kuunda neno lenye ama maana au la kiupuzi. Baada ya kumudu herufi hizi, silabi na maneno yaliunganishwa kuunda kirai na sentensi fupi. Kukariri kwa muda herufi, silabi, na maneno mwishowe humwezesha mtoto kupata ujuzi wa kusoma. Hii inamaanisha kuwa kusoma kulijikita katika kukariri. Mbinu hii hata 37 hivyo ilizingatia utambuzi wa maneno kuliko maana yake. Aidha, mbinu hii humwezesha mwanafunzi kufahamu mfuatano wa herufi, kusaidia kusoma kutoka kushoto kwenda kulia na hatimaye tahajia. Pia mbinu hii hujulikana kama mbinu ya tahajia kwa sababu humsaidia mtoto kufahamu mfuatano wa herufi katika neno (Gray, 1956). Utaratibu huu ulichukulia kuwa watoto wakitazama herufi hizi kama zinavyofuatana katika maneno na kuzikariri herufi hizi mara kwa mara wataweza kusoma kwa sababu herufi nyingi za konsonanti huambatana na sauti zake (Hughes, 1978:19). Utaratibu huu unahusisha mtoto kuweza kutambua na kubainisha sauti zinazotolewa na herufi mbalimbali. Kiswahili hutumia foni ishirini na tatu za Kiingereza kati ya hizi kuna vokali a, e, i, 0, U pamoja na ving'ong'o 'm, n, ng ny ' hubainika kwa sauti zake mahsusi. Fonimu kumi na nane za Kiswahili sharti kuambatanishwa na vokali ili kuunda sauti zenye maana au kuwasilisha maana. Aidha herufi hizi zinafanana katika lugha zote tatu ambazo mtoto hufundishwa katika shule za msingi; Kiswahili, Kiingereza na lugha za jamii mbalimbali. Hata hivyo kuna tofauti ya matamshi katika baadhi ya herufi kwa mfano, Kikuyu herufi kama vile: /g/ na /b/ inatofautiana na Kiswahili na Kiingereza. Mbinu hii imetumiwa kwa miaka mingi kufundisha kusoma. Ingawa watoto wengi miaka ya zamani walijifunza kusoma kwa kutumia mbinu hii inayo udhaifu wake. Kuna, baadhi ya majina ya herufi na sauti zake ambazo huhitilafiana na pia kuna herufi ambazo huwakilisha sauti mbalimbali kulingana na mazingira inapotokea hivyo kukanganya watoto katika jitihada zao za kujifunza kusoma, kwa mfano lugha ya 38 Kiingereza. Kadhalika mbinu yenyewe inachosha kwa sababu inabidi mtoto kukariri herufi zisizo na maana badala ya usomaji wenye maksudio na kwa hivyo haina umaarufu sana katika ufundishaji. Kinyume na upungufu wa mbinu hii, inaweza kutumika kuwawezesha watoto kumudu herufi na uwezo wa kuendeleza maneno kwa usahihi. Kiswahili hakitumii mbinu hii sana katika usomaji kwa sababu maneno hutamkwa kama yanavyoendelezwa. b) Mbinu ya Kutamka Herufi kwa Sauti Mbinu hii hulenga sauti binafsi, yaani fonimu zinazounda neno. Kwa kutumia mbinu hii mtoto hushikanisha sauti mbalimbali zinazounda neno. Kwa kutamka kila herufi kutoka kushoto kwenda kulia neno nzima hukamilika. Kwa mfano, neno la Kiingereza cat litatamkwa kama vile: c-Ik/, a-rce/, t-Itl. Kulingana na mbinu hii, watoto huanza kwa kufunzwa maneno mepesi na machache na idadi ya maneno huongezwa kadri wanavyoendelea kufunzwa kusoma. Kwa kuwa mbinu hii imejikita katika sauti haina budi shughuli zitakazofanywa katika ufunzaji kuhusisha kusoma kwa sauti. Mbinu hii husemekana husaidia watoto kutambua neno kwa haraka na usahihi kuliko mbinu ya abjedi. Udhaifu mkubwa wa mbinu hii, ni kule kuambatanisha neno geni na sauti isiyokuwa na maana. Hii mbinu inaelekeza katika ukariri usio na maana. Ikiegemewa sana watoto wanaweza kuwa wenye kukariri maneno na kupuuza ufahamu. Udhaifu mwingine ni kuwa mbinu hii aghalabu huchukulia kuwa kila herufi inawakilisha sauti moja. 39 Lakini kuna baadhi ya herufi ambazo huchukua sauti tofauti katika maneno, kwa mfano katika Kiingereza : o Cat lkatJ face /feis/ o C!!P Ik"pl full Iful/ Upungufu mwingine ni kuwa herufi pekee haitoi vidokezo vya kutosha kuitambulisha na kukumbukika kwa herufi upesi. Kwa hivyo, ni vyema kuwapa watoto shughuli zaidi ambazo zitawapa vidokezo vingi kuweza kubainisha herufi zinazokaribiana. Kama asemavyo Pearson (1981) kusoma ni mchezo wa kubahatisha. Lugha ya Kiswahili haiwezi kufaidika na mbinu hii kwa sababu haitamki herufi bali hutamka silabi na ikitumiwa hukanganya watoto. Kwa mfano ikiwa mwalimu atatumia mbinu hii itambidi kwanza awafunze watoto kutamka kila herufi kisha kuzishikanisha sauti hizo pamoja na vokali, jambo ambalo ni ngumu katika lugha ya Kiswahili kwa sababu nyingi ya herufi zake hazitamkwi kivyake. Kwa mfano neno 'kuku' likitenganishwa fonimu zake itasomwa lid na lul lid na lu/, yaani watoto watakuwa na shida ya kushikanisha hizo herufi. c) Mbinu ya Silabi Silabi huwakilisha tamko kamili ambalo huleta mfanyiko wa neno. Silabi ni sehemu ya matamshi ambayo kwa kawaida ni pana kuliko sauti moja lakini ndogo kuliko neno (Crystal, 1992). Mgullu (1999) anasema kuwa silabi ni kipashio kimojawapo ambacho hutumika kuelezea muundo wa lugha hasa katika kiwango cha fonolojia arudhi. Habwe na Karanja (2004) wakirejelea kamusi ya TUKI (1981) wanasema silabi ni kipashio cha utamkaji ambacho kwa kawaida ni kikubwa kuliko fonimu na 40 kidogo kuliko neno. Aghalabu wote wanakubaliana kuwa ni kipashio cha fonolojia ambacho kwa ukubwa kipo kati ya fonimu na neno. Mathalani silabi ni sehemu ya neno ambalo linatamkika na husikika kama sehemu tofauti na nyingine katika msingi wa neno. Lugha tofauti tofauti huwa na njia tofauti za kutamka na kuunda silabi na hivyo ubainifu wa lugha hizo hujitokeza. Lugha ya Kiswahili hujikita katika silabi. Silabi za Kiswahili hazibadiliki kulingana na muktadha kwa hivyo hutamkwa kwa namna moja bila kujali yanapotokea. Kwa njia hii watoto wanaweza kufunzwa sauti za silabi, wakizimudu itakuwa rahisi kwao kusoma maneno ya Kiswahili. Kiswahili kina konsonanti 18 ambazo ni: p, b, t, d, k, g, j, f, v, S, Z, h, m, n, /, r, w, y. Kisha kunazo herufijozi 11; eh, th, dh, sh, gh, ny, ng, ng', nd, nj, mb. Pia kuna nusu-irabu /w/ ambayo huambatanishwa na herufijozi kuunda sauti kama vile: shw, mbw, nyw. Yamkini /w/ hutumika katika utendakazi wa kimofolojia ambapo huwekwa kabla ya kiishio katika vitenzi kama vile: Pigwa Chezwa Itwa Semwa Pendwa Pikwa Konsonanti na herufijozi huambatanishwa na vokali 5 za Kiswahili kuunda silabi. Lugha ya Kiswahili hupendelea muundo ambapo konsonanti hufuatwa na vokali. Aidha kunayo maneno yenye kuundwa kwa vokali pekee kama vile: ua, oa, au, aoa, lakini hakuna yenye kuundwa kwa konsonanti pekee. Mengi ya maneno aghalabu huanza kwa konsonanti lakini kuna machache yenye kuanzia kwa vokali lakini yote huishia kwa vokali. 41 Hata maneno ya mkopo hufuata mpangiiio wa fonolojia ya Kiswahili kama vile: Kiingereza Kiswahili Kiarabu Kiswahili Record Hospital Bicycle Rekodi Hospitali Baiskeli Bint Ardh Waqkt Binti Ardhi Wakati Wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanakubaliana kuwa mbinu hii ndio mwafaka kutanguliza usomaji wa Kiswahili kinyume na mbinu hizo zingine katika utaratibu changanuzi. Hata hivyo kuna mifano michache ya maneno yanayoandikwa tofauti na matamshi kwa mfano; 1. Mbu hutamkwa kama m+mbu 2. Mvi hutamkwa kama m+mvi 3. Nge hutamkwa kama n+nge Uzuri wa mbinu hii ni kuwa mwanafunzi anaweza kusoma neno jipya kwa urahisi bila usaidizi. Ni rahisi wanafunzi ambao wameimarika katika silabi kufunza wengine ambao uwezo wao ni wa chini. Kadhalika ni rahisi kuandaa funzo hata ikiwa mwalimu hana ujuzi mwingi wa lugha ile. Walimu wenye uzoefu wa mbinu hii huipendelea sana. Inakuwa vigumu kwao kuwa wabunifu na kutumia mbinu zingine za kufundishia kusoma kwa sauti. Wataalamu wengi wametoa maoni yao kuhusu upungufu wa mbinu hii katika ufundishaji kwenye viwango vya ujuzi wa chini. Baadhi ya maoni ni kuwa mbinu hii hukuza mwenendo mbaya wa macho kwa sababu hata kisaikolojia mtu huona kwanza neno nzima kabla ya visehemu vinavyounda neno. Pia inachangia umumunyaji wa 42 midomo katika usomaji kimya. Aidha ikitumiwa mapema watoto hufa moyo na kukosa mshawasha wa kusoma kwa sababu silabi hazina maana yoyote. Wanasema kuwa mtindo huu unafaa kutumiwa zaidi katika kuchanganua neno au maneno. 2.2.2 Utaratibu Changamano Kuna mbinu kadha katika kitengo hiki cha ufundishaji kusoma kama zifuatazo: a) Mbinu ya kutazama na kusema b) Mbinu ya kusoma kirai c) Mbinu ya kusoma sentensi d) Mbinu ya kusoma hadithi a) Mbinu ya Kutazama na Kusema Neno Njia hii husaidia utambuzi wa neno zima. Kipengele cha kimsingi katika mbinu hii ni neno. Waasisi wa mbinu hii, huchukulia kuwa neno lina vidokezo vingi ambavyo vinaweza kuchangia hali ya kulikumbuka kuliko herufi. Watoto hukariri sentensi au kirai ambapo neno mahsusi hutiliwa mkazo hadi mtoto kuweza kulitambua neno kwa kutazama tu. Kupitia mbinu hii mtoto husikiliza, hutazama na kusema neno. Watoto hujifunza neno nzima kabla ya kulikatakata visehemu. Watoto hufunzwa kutamka kabla ya kufunzwa herufi na sauti zinazounda neno. Ni rahisi kufunza maneno kuliko sheria za kuunda sauti au silabi. Watoto hujifunza kwa kukumbuka neno zima hasa ikiwa maneno yanatofautiana katika umbo na ukubwa wa herufi. Kusoma neno nzima husaidia kusoma kirai au sentensi na kusoma kunakuwa na maana. 43 Maneno sharti yafunzwe moja baada ya nyingine na kwa mpangilio. Ili kukumbukika maneno haya sharti yaoanishwe na picha, michoro na vifaa halisi. Baada ya kurudia mazoezi kama haya kwa muda mtoto ataweza kuoanisha majina na vitu vinavyorejelewa. Mazingara ya mtoto darasani kupachikwe majina pamoja na vitu vinavyowakilishwa kwenye chati, ubao, kuta, na vifaa halisi kwenye mradi wa darasani. Maneno yanayofunzwa yawe na maana yanayoafikiana na tajriba ya mtoto. Mwalimu baadaye anaweza kutumia kadi za maneno kufundisha majina yaleyale, akayachanganya na kuwauliza baadhi ya watoto kuchagua kadi yenye jina fulani. Au anaweza kuwapa watoto mazoezi kama vile kuambatanisha picha na jina katika jedwali ama kuwapa majina yenye mapengo kujaza herufi mwafaka. Kwa njia hii watoto wataweza kukumbuka maneno waliyofunzwa. Kwa hakika wataalamu wanakubaliana kuwa watoto hujifunza kwa mapana kwa kuingiliana na mazingara yao kule kugusa, kuhisi, kuona na kusikiliza. Kusoma kunajikita katika utambuzi wa maumbo. IIi kusoma kwa ufasaha na ufahamu itabidi mtoto kukuza uwezo wake wa kutambua maneno. Kiwango hiki kitafikiwa ikiwa watoto watafunzwa idadi fulani ya maneno ili kuwawezesha kusoma moja kwa moja. Mtoto mwanzoni ataweza kutambua maneno fulani ya kila siku. Mtoto aweza kutumia njia mbili au zaidi kati ya hizi hapa chini kutambua neno: o Umbo la neno o Urefu wa neno o Kiambishi cha neno o Mwambatano wa herufi fulani o Mazingara ya neno. 44 Mbinu hii ina upungufu wake kama ilivyo mbinu zingine. Kuna uwezo wa watoto kukanganywa na maneno yanayokaribiana. Pia watoto wanaweza kubahatisha majina kwa sababu ya picha badala ya kutambua neno kwa hivyo kupuuza uelewa wa herufi na kujenga ubahatishi. Aidha, watoto watamtegemea sana mwalimu katika kusoma maneno mageni kwa sababu njia hii haina mbinu ya kumwezesha mtoto kusoma neno jipya. Kadhalika si rahisi watoto kujifunza idadi kubwa ya maneno kwa kipindi fulani kwa hivyo watakuwa na upungufu wa msamiati jambo ambalo litawatatiza katika kusoma. Vile vile, ili watoto kuweza kujua kiwango fulani cha maneno watahitaji kukariri zaidi ili kukumbuka, jambo ambalo huchosha watoto kama ilivyo mbinu ya abjedi na kutamka sauti. b) Mbinu ya Kusoma Kirai Mbinu hii inachukulia kuwa kirai kina maana zaidi ikilinganishwa na neno, kwa hivyo mtoto anayejifunza kusoma atashika kirai kwa urahisi kuliko neno. Kupitia njia hii, kirai huandikwa ubaoni na kukaririwa. Watoto huweza kutambua maneno fulani yaliyorudiwa katika virai walivyofunzwa. Kisha vipengele vilivyounda neno vinaweza kufundishwa na kutumiwa kutambua maneno mengine watakayofunzwa kama ilivyo katika mbinu ya kusoma neno. Aghalabu virai huambatanishwa na picha na michoro yenye maelezo. Uzuri na upungufu wa mbinu hii ni kama zile za mbinu ya kutazama na kusema neno c) Mbinu ya Kusoma Sentensi Mbinu hii inajikita katika kirai na sentensi. Mbinu hii inasemekana kuwa imechimbuka kutoka kwa mbinu ya kutazama na kusema neno. Waasisi wa mbinu hii 45 wanasema kuwa hata neno halina mengi ya kuarifu msomaji kama i1ivyo kirai au sentensi. Kwa hivyo, sentensi ndio kipengele cha kimsingi katika ufundishaji wa kusoma kwa sababu ina maana kamili. Kwa njia hii hamu ya watoto ya kusoma pamoja na makala ya kusoma yenye kuvutia inaweza kupewa watoto iIi kuharakisha usomaji wa ufasaha. Mwanzoni mwalimu anaweza kutanguliza kusoma sentensi fupi na sahili. Sentensi ibebe maudhui rahisi yenye kueleweka na kupatikana kwa mazingira ya mtoto. Baadhi ya maudhui yanaweza kuwa ya darasani, shuleni, jamaa, nyumbani, nk. Maneno yanayotumiwa katika sentensi yachaguliwe kwa makini na baadhi ya maneno yarudiwerudiwe katika sentensi iIi watoto wawe na uzoefu na kujiamini katika shughuli za kusoma. Mbinu hii inaweza kushirikishwa na kutazama na kusema neno kwenye kadi au ubaoni ili kuendelea na mazoezi ya kutambua maneno katika sentensi walizofunzwa. Kwa njia hii msamiati wa watoto utaongezeka na usomaji wa watoto utaendelea kupananuka. Aidha itawezesha watoto kusoma kwa ufasaha ili kujenga ufahamu wa wanayosoma kwa kuzingatia matamshi, kiimbo, shadda na uakifishaji. Ni muhimu kuzingatia fonolojia arudhi kama ilivyodhihirika katika madarasa ya pili na tatu kwa sababu inachukuliwa wamemudu kusoma kwa sauti kulingana na silabasi. Vilevile kule kujua maneno mengi kutawawezesha kusoma kwa ufasaha kwa sababu maana hutangulia fonologia arudhi. Kwa hakika maana ya lugha ya mazungumzo inabebwa na kiimbo. Hata hivyo, ni makosa kuchukulia kuwa uakifishaji ndio 46 unaashiria kiimbo. Hii ni kwa sababu uakifishaji aghalabu huja baadaye katika sentensi kuashiria chochote. lkumbukwe kiimbo hubebwa na maana kwa kuwa unapojua maana utajua namna ya kusoma sentensi au kifungu ipasavyo (Smith, 1971). Aidha ikiwa msomaji hajui maana ya sentensi hatajua kama usomaji wake unatatiza. d) Mbinu ya Hadithi Mbinu hii ni upanuzi wa mbinu ya sentensi. Hii ina maana kuwa hadithi ni muungano wa sentensi. Aidha, inatoa maelezo kamili kuliko sentensi. Kwa kawaida watoto hupenda hadithi. Inasemekana kuwa njia hii huamsha hamu ya. kusoma. Watoto hupenda kusimuliwa hadithi hasa za kijasiri na uhalisia ajabu. Mwalimu anaweza kuamsha ari na hamu ya kusoma kwa kuwasimulia watoto hadithi zenye kusisimua mawazo yao na kuwaburudisha. Hadithi yenyewe ifuatanishe vitushi kwa njia ya kimantiki, iwe fupi, maneno mepesi na yenye sentensi sahili. Kwa njia hii watoto j •watafuata hadithi bila shida na kunga'amua maudhui ya hadithi. Pia itawafanya watoto kupenda kusoma vitabu. Watoto ambao wanaweza kusoma sentensi wanaweza kuanzishwa kusoma vitabu. Kuna haja ya kuwa na vitabu vya hadithi ambavyo vinawiana na viwango vya watoto. Vitabu viwe vya viwango mbalimbali na vyenye maudhui yanayolingana na tajriba ya watoto. Kunayo maudhui ya watoto wa mjini na watoto wa mashambani. Mbali na maudhui mwalimu azingatie yafuatayo anapoteua vitabu vya kusoma: 1) Msamiati uwe wa kiwango cha watoto. 2) Taipografia kubwa ili kurahisisha usomaji. 3) Vielelezo ikiwezekana vyenye rangi 4) Aina za sentensi, ziwe sahili na fupi. 47 Vitabu hivi vitawawezesha watoto kujenga ufasaha katika usomaji. Ikumbukwe kusoma kwenye maana na kwenye kuvutia kutawafaidi watoto zaidi. Kufanikisha mbinu hii haina budi ishirikishwe na mbinu zingine kama vile kutenganisha maneno kuyatamka na kueleza maana yake katika hadithi. Pia picha na michoro itawasaidia watoto kuelewa zaidi hadithi. Watoto darasani wana uwezo tofauti wa kusoma kwa hivyo njia hii itatosheleza mahitaji mbalimbali ya watoto. Tofauti hizi zinaweza kusababishwa na mambo mengi kama umri, hulka, maumbile, mazingara ya nyumbani, mambo ya kihisia na kisaikolojia. Baadhi ya mambo haya si rahisi kuyang'amua lakini yatajidhihirisha katika vitendo vya watoto kwa mfano mambo ya kisaikolojia. Isitoshe, mbinu moja inaweza kumfaa mtoto mmoja zaidi ya mwingine katika wakati fulani kwa hivyo ni muhimu mwalimu kubadilisha mbinu zake kulingana na mahitaji ya darasani. Kulingana na wataalamu wa lugha, kuchanganya mbinu za kufundishia kusoma huleta matokeo bora kuliko kutumia mbinu moja. Kuna watoto wanaojifunza kwa wepesi kwa kuona wengine kusikia na kadhalika. Kwa hivyo watoto wengi watafaidi kukiwa na mbinu changamano. Mbinu changamano, inamaanisha mwalimu kuzingatia maslahi ya mtoto binafsi anapotayarisha kazi yake. Hii pia itamaanisha kazi nyingi kwa mwalimu ili kuweza kukabiliana na mahitaji ya darasa lake. 48 2.3 NyenzoNifaa Ujifunzaji ni njia isiyoelezeka kwa urahisi kwa hivyo nyenzo ni muhimu sana katika kuchochea ujifunzaji wa L2 (Bwen, 1982). Mwanafunzi hutumia masikio na macho katika ujifunzaji, hata hivyo, macho ndio njia ya kimsingi ya ujifunzaji. Nyenzo nzuri huchangia katika kuamsha hamu wakati wa somo. Kwa mujibu wa K.I.E. (2006) nyenzo ni vifaa ambavyo hutumiwa darasani ili kurahisisha ufundishaji na kuwawezesha wanafunzi kukumbuka kilichofundishwa. Aidha imeorodhesha baadhi ya nyenzo zinazoweza kutumiwa katika kila darasa. 2.3.1 Aina za Nyenzo Baadhi ya nyenzo ni kama vile: a) Vifaa halisi b) Chati c) Picha d) Michoro e) Kadi zenye silabi au maneno a) Vifaa Halisi Hivi ni kama matunda, nafaka, mimea, vinyago vya kuchongwa au kufinyangwa. Hivi ni vitu ambavyo vinapatikana kwa urahisi katika mazingira ya shule na nyumbani. Watoto wanaweza kuvikusanya vitu hivi na kuvileta shuleni. Vitu hivi viwekwe vizuri katika pembe moja ya darasa. Maj ina ya vitu hivyo yaandikwe kwenye kadi na kuambatishwa na kifaa mwafaka. Vitu hivi vinafaa kutumiwa na mwalimu katika ~ ufunzaji ili watoto waone umuhimu wake. Aidha vitu vinavyoweza kuharibika vinahitajika kubadilishwa mara kwa mara ili sehemu hiyo iwe yenye kuvutia. 49 Kadhalika kuna vifaa vingine kama ramani, dira na vitu vingine ambavyo vinaweza kutumiwa kulingana na kile kinachofundishwa. b) Chati Chati au mabango yanaweza kutumiwa kufanikisha funzo la kusoma. Chati inaweza kupachikwa picha zilizokusanywa na chini yake kuandikwa majina. Pia inaweza kuwa na michoro pekee au iambatanishwe ama sentensi fupi au majina. Pia chati inaweza kuwa na sentensi chache ambazo zinaafikiana na funzo. Nyimbo, mashairi yanaweza kuandikwa kwenye chati. Mwalimu anayetayarisha awe makini Hi asikanganye watoto. Maandishi yaandikwe kwa usahihi, nadhifu na yenye kusomeka kwa urahisi na watoto wote hata wale walioketi nyuma. Ikiwa atatumia rangi ziafikiane na rangi ya kitu kile kama inavyotarajiwa kwa mfano ikiwa ni mto uonyeshwe kwa rangi ya samawati. Jambo la muhimu ni mwalimu kujua atatumia kifaa kile wakati gani, kwa hivyo hili lijitokeze kwenye maandalizi ya funzo na hasa katika hatua gani ambapo itaingizwa. c) Picha Mwalimu anaweza kutumia picha za wastani au kubwa. Picha za wastani anaweza kuzitoa kwenye magazeti, majarida, vitabu vikuu kuu na picha za matangazo ya biashara. Picha hizi ikiwezekana ziwe za rangi na ambazo zinaonyesha mambo katika tajriba ya mtoto. Picha za kitu kimoja kimoja ni bora kuliko zile ambazo zina mkusanyiko wa mambo kwa kuwa zinaweza kuwakanganya watoto. Picha kubwa zinaweza kupatikana kutoka kwenye kalenda au kwenye pakiti za bidhaa mbalimbali. 50 Picha hizi zinaweza kuambatishwa na majina au hata sentensi zilizoandikwa kwenye kadi. Picha hizi zinaweza kutumiwa kujenga sehemu ya udadisi kwenye pembe moja ya darasa (curiosity corner). d) Kadi za Silabi/Maneno Kadi ni za aina mbalimbali. Mwalimu anaweza kutayarisha kadi zenye herufi,silabi, neno, picha, maumbo yenye kufanana. Kadi zenye picha zinaweza kuwa na majina chini yake na jina jingine nyuma ya picha. Kadi hizi zinaweza kuwa na umbo mbalimbali. Mwalimu atumie kadi za maneno kwa njia ya ubunifu. Anaweza kuibua michezo kwa kutumia kadi hizi kwa mfano mchezo wa kuvua samaki au kujipanga na kuunda sentensi kisha kuisoma. IIi watoto wafanye mazoezi ya kutosha itabidi mwalimu atayarishe jozi za kadi nyingi. Mazoezi kama haya yatamwezesha mtoto kuwa na uwezo wa kutambua picha, herufi, silabi, maumbo na hata maneno. 2.3.2 Umuhimu wa NyenzoNifaa Kulingana na Bwen (1982) na K.I.E. (2006) baadhi ya umuhimu wa kutumia nyenzo ni: i) Kukuza usikivu wa mwanafunzi. ii) Kuongezea na kuchangia yale ambayo mwalimu amefundisha darasani. iii) Kutoa ule uchovu wa sauti moja ya mwalimu darasani kwa kuwahusisha watoto. 51 iv) Huwafanya watoto kumtazama mwalimu na hivyo kurahisisha mawasiliano. v) Hubadilisha badilisha mwendo wa funzo. vi) Kuleta uhalisia darasani wakati mada mbalimbali zinapofundishwa. vii) Huibua mawazo tofauti watoto wanapojaribu kuelewa na kufasiri michoro. viii) Husaidia kuwasiliana na wanafunzi wa umri na uwezo mbalimbali. ix) Husaidia kushirikisha stadi zote za lugha kusikiliza, kuongea, kusoma na kuandika. 2.3.3 Kuteua Nyenzo Mwalimu anapotayarisha ratiba ya kazi mwanzoni mwa muhula ni vyema afikirie ni nyenzo zipi atahitaji kufundishia na namna wanafunzi watakavyovitumia. Inahitajika mwalimu ateue nyenzo kwa makini na kufikiria njia ya kuzitumia kwa kuwa matumizi yake ndiyo yatakayodhihirisha ufaafu wa kifaa chenyewe na kuwavutia watoto kulipenda somo. Pia itabidi aweze kutumia aina mbalimbali za nyenzo ili aibue hamu ya watoto na kutilia nguvu walichoj ifunza. Nyingi ya nyenzo hizi zinaweza kutengenezwa na mwalimu kwa kutumia vitu vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira yake. Walimu wanaweza kushirikiana katika kutengeneza nyenzo za kutosha na za aina mbalimbali ili ziwafae kwa pamoja. Mwalimu anaweza kuibua nyenzo kwa njia mbalimbali kwa mujibu wa K.I.E. (2006) ambazo ni: 52 i) Awashirikishe watoto kutafuta baadhi ya vifaa halisi vinavyopatikana nyumbani. ii) Kuyachunguza mazingara na kutambua baadhi ya nyenzo zinazopatikana hapo. iii) Kushirikisha watoto katika kuchora na kufinyanga na hata kuandaa sehemu mbalimbali za kuvutia katika darasa. iv) Anaweza kupata kwa njia ya kuazima kutoka shule jirani. v) Iwapo nyenzo zitanunuliwa atafute zile zonazouzwa kwa bei nafuu. 2.3.4 Uhifadhi wa Nyenzo Aidha kuna haja ya uhifadhi mzuri wa nyenzo kwa sababu hugharimu wakati mwingi kukusanya, kutayarisha, kuunda na hata kununua baadhi ya nyenzo. Vifaa hivi vikitunzwa vizuri vinaweza kutumiwa kwa muda mrefu na kwa watoto tofauti. Baada ya kutumiwa darasani, zile ambazo zinafaa kubandikwa ukutani ziwekwe kwa njia mwafaka. Hizi husaidia watoto kuendelea kujifunza hata bila usaidizi wa mwalimu. Hata hivyo, zisiwekwe kwa muda mrefu, baada ya watoto kumudu kazi ile ziondolewe na kuhifadhiwa. Kunazo zingine kama kadi za maneno, picha na kadhalika zinaweza kuwekwa kwenye sanduku au kabati na mwalimu ahakikishe zinawekwa katika hali nadhifu. I• Vilevile mwalimu anaweza kuwahusisha watoto katika kutunza vifaa hivi. Anaweza kufanya hivyo kwa kuwauliza kuvigawa na kukusanya baada ya kutumia. Ni vyema pia mwalimu kuweka orodha kamili ya nyenzo ambazo ziko chini ya ulinzi wake. 53 2.4 Aina za Usomaji Kulingana na Grant (1960), Williams (1973), Wanyoike (1982) na Quist (2000) kuna mitindo mbalimbali ya kusoma. Kuna kusoma kwa darasa nzima kwa sauti, kusoma mmoja mmoja kwa sauti, kusoma katika makundi kwa sauti na kusoma kimya. Kila mtindo una uzuri na udhaifu wake. 2.4.1 Kusoma Darasa Lote Huu ni mtindo ambapo mwalimu anaweza kuwauliza watoto wenyewe wasome kwa sauti maneno au sentensi. Mtindo huu unafaa zaidi katika usomaji wa makala mafupi, hasa kwenye ubao. Udhaifu wa mtindo huu ni kuwa watoto wanaweza kuzembea katika usomaji. Kwa hivyo mwalimu ahakikishe anawatazama watoto wanaposoma. Tena, mtindo wenyewe usitumiwe kwa muda mrefu kwa sababu watoto hupoteza usikivu haraka sana. Mtindo huu hutumiwa zaidi wakati ambao mwalimu anawataka watoto wasome nyuma yake kwenye kitabu au ubaoni inaweza kuwa kusoma maneno au sentensi. Pia anaweza kutumia katika utangulizi wa kusoma kwa sauti kifungu fulani. 2.4.2 Kusoma Mmoja Mmoja Hii ni njia nzuri pia ya usomaji. Mwalimu anaweza kuwauliza watoto kadhaa wasome maneno, sentensi au mistari michache ya kifungu. Ikiwezekana kila mtoto apewe nafasi ya kusoma. Lakini pia isitumiwe kwa muda mrefu kwa sababu inaweza 54 kuchosha. Mtindo huu unaweza kutumiwa katika mazoezi na hata kutathmini usomaji. Kwa njia hii ya kusoma mtoto ataweza kuona umuhimu wa mabadiliko ya sauti namna inavyochangia katika maana. MwaIimu anaweza kutumia fursa hii kumtuza mtoto kwa jitihada yake ili kumtia motisha ya kujitahidi zaidi. Kadhalika, mwalimu anaweza kutumia nafasi ile kunakili makosa ya mtoto ili kupanga baadaye namna ya kumsaidia, kazi ya marudio yanaweza kufanywa katika kikundi badala ya mtoto binafsi. Udhaifu wa mtindo huu ni kuwa watoto wachache sana watasoma katika kipindi. Hata hivyo, mwalimu anaweza kuweka orodha ya waliosoma ili wasirudiwe katika kipindi kingine cha kusoma kinachofuata. Pia watoto ambao hawajamudu kusoma wanaweza kukosa ari kwa sababu ya kuchekelewa na kukosolewa sana na hivyo kuwaathiri zaidi. 2.4.3 Kusoma Katika Makundi Hata katika darasa ambalo lina watoto wenye umri unaokaribiana bado utakuta watoto wana uwezo tofauti na kwa hivyo kuweka watoto katika makundi kutasaidia kuwapa kazi tofauti tofauti na kuongezea uelewaji. Katika mtindo huu watoto wanawekwa kwenye makundi kulingana na uwezo wao wa kusoma. Makundi haya yanaweza kupewa majina ya abjedi, ya rangi au ya wanyama. Makundi matatu huwa mwafaka zaidi, kikundi kimoja cha watoto wen ye uwezo mkubwa wa kusoma, ikifuatwa na wenye uwezo wastani na mwisho wenye akili nzito. Ni vyema kubadilisha badilisha makundi haya baada ya muda fulani ili kuwatia watoto motisha katika ufunzaji. 55 Ikumbukwe kuwa kuwatuza watoto kwa mafanikio hata madogo huwatia motisha ya kusoma. Haiwezekani mwalimu kuwepo katika kila kikundi kwa wakati moja. Itabidi, mwalimu achague kiongozi katika kila kikundi wa kuwaelekeza wengine wanachofaa kufanya. Kiongozi anafaa kuwa mtoto ambaye anawazidi kidogo wengine kwa uwezo wa kusoma. Pia kiongozi anaweza kutumiwa kugawa vitabu, nyenzo na chochote kingine na kisha kuvikusanya ten a na kuvirejesha kwa mwalimu. Kiongozi asibadilishwe mara kwa mara. Mwalimu itambidi kuandaa funzo lake kwa makini. Sharti ahakikishe kila kikundi kina kazi na nyenzo za kutosha kutumia wakati anaposhughulikia kikundi kimoja. Mwalimu atoe mwongozo na nyenzo za kutumiwa kabla ya funzo kuanza ili kusiwe na kelele darasani. Aidha, afuatilie kila kikundi kinafanya kazi ifaavyo. Uzuri wa mtindo huu ni kuwa watoto wote watahusika katika kujifunza kulingana na uwezo wao. Isitoshe, mwalimu atapata nafasi ya kusaidia kila kikundi kwa wakati wake. Hata hivyo, mtindo unaweza kutatiza ambapo idadi ya watoto ni kubwa mno. Baadhi ya matatizo ni: • Ukosefu wa nafasi darasani. • Ukosefu wa muda wa kutosha kuandaa kazi. • Ukosefu wa nyenzo na vifaa vya kutosha. • Ugumu wa kuchagua mbinu zifaazo. 56 WilIiams (1973) ametoa njia za kusuluhisha matatizo haya. Kuhusu nafasi darasani mwalimu itambidi kuwa na ubunifu kama vile kuwapeleka watoto uwanjani mara kwa mara. Pia anaweza kuteua sehemu kadhaa za ukuta darasani na kuweka vivutio. Kuhusu nyenzo na vifaa itabidi mwalimu kushirikisha walimu wengine na watoto kutayarisha ili wawe na nyenzo za kutosha. Kuhusu muda mwalimu awe mnyumbufu si lazima kufuata mpangilio wa vipindi kama vilivyoratibiwa. Katika madarasa ya chini mwalimu anaweza kuunganisha vipindi, tena mwalimu anaweza kufundisha masomo mawili kwa wakati ule ule kwa kuwapa watoto kazi tofauti hasa za hesabu kwenye kundi fulani. Ni muhimu mwalimu kujua kuwa ikiwa watoto hawajui kusoma itakuwa vigumu hata kufundisha masomo mengine. 2.4.4 Kusoma Kimya Mtindo huu unafaa zaidi watoto wa kiwango cha juu na hutumiwa baada ya watoto kupata ujuzi wa kutambua maumbo. Mwalimu anaweza kuutumia baada ya kupitia maneno na sentensi fulani kwa sababu watoto ambao tu ndio wameanza kujifunza kusoma wanaweza kutatizika wanapokutana na neno jipya kabisa. Pia itabidi mwalimu kuzunguka darasani na kuwasaidia watoto wanaposoma. Ni muhimu kwa watoto kupewa nafasi ya kusoma kimya ili kukuza desturi ya kusoma vizuri Kwa kuwa mbali na kutaka watoto waweze kutambua na kufasiri maumbo ni vyema wakiweza kusoma kwa ufahamu. Gathumbi na Ssebunga (2005) wanasema kuwa kusoma kwa sauti hufanya watoto wasimakinike katika usomaj i kwa sababu walimu huwa makini kurekebisha makosa ya matamshi, kiimbo, mkazo nk. kila yanapotokea na hivyo kuwavunja moyo watoto wenye matatizo mengi. Vile vile 57 inambidi mtoto kupunguza mwendo wa kusoma kuhakikisha hafanyi makosa. Yamkini mtoto atatilia maanani anavyosoma badala ya ufahamu wa kile anachosoma. Mwendo wa kusoma huandamana na kusoma kwa ufasaha. Kwa hivyo, kuna haja ya mwalimu kukuza ujuzi huu kwa huwasaidia watoto kusoma kwa mwendo unaofaa kwa sababu mtu husoma haraka anaposoma kimya kuliko kusoma kwa sauti. Hii itawezekana ambapo mtoto anaposoma hamumunyi midomo au kutoa sauti. Msomaji aliyemakinika hasomi neno moja moja bali macho yake huangazia maneno au kifungu cha maneno. Tena msomaji hatumii kidole kuashiria neno analosoma. 2.5 Maandalizi ya Kusoma Kuna viwango mbalimbali katika usomaji. Mwalimu ahakikishe watoto wanaimarika katika kila kiwango kabla ya kuingia kiwango kingine. Ikumbukwe mwalimu hafunzi kusoma anafunza watoto kusoma. Kila mtoto ni tofauti na mwingine; kila mtoto ana uwezo wake na maendeleo ya mmoja yanatofautiana na mwingine. Mwalimu anapoanza kujiandaa kufunza kusoma akumbuke mambo haya mawili: • Kuna watoto ambao watakuwa tayari kusoma kabla ya wengine. • Wengine wataendelea vyema na kwa kasi kuliko wengine. Williams (1973) anasema kuwa ni muhimu kwanza watoto wanapoingia shuleni mara ya kwanza mwalimu atathmini kama watoto wako tayari kusoma. Kuanza, mwalimu awafundishe watoto kwa pamoja ili waweze kumzoea na kuzoeana wenyewe. 58 Mwalimu anaweza kuwahusisha katika michezo na nyimbo na kuona namna wanavyoshiriki. Pia anaweza kuwasomea hadithi wakisikiliza hata kama ni kwa Ll , kuongea nao kuhusu picha na mambo mengine. Mtoto ambaye anashiriki katika kujibu maswali ya mawalimu na michezo atakuwa tayari kwa kusoma. kwa njia hii mwalimu anaweza kuunda makundi kadri watoto wanavyoonyesha maendeleo na baada ya majuma machache mwalimu atakuwa tayari na makundi yake. Katika kiwango hiki mwalimu asijifunge na idadi fulani ya watoto katika kikundi. Kuna mazoezi mbalimbali ambayo watoto wanaweza kufanyishwa kabla ya kusoma katika makundi ili kuwa na uzoefu wa mambo yafuatayo: • Kupambanua anayoona • Kupambanua anayosikia • Kusoma kutoka kushoto • Kutazama ukurasa juu-chini. 2.5.1 Mazoezi Kabla ya Kusoma Kulingana na Wanyoike (1982) na Claessen (1988) kuna mazoezi aina nyingi ambayo mwalimu anaweza kuwapa watoto ili kuwasaidia kuwa tayari kwa ujifunzaji wa kusoma baadaye. Baadhi ya mazoezi haya ni: a) Picha kwenye kadi: Mwalimu anaweza kutayarisha picha mbili mbili, watoto wazishikanishe mpaka ziishe. Pia maumbo yanaweza kuchorwa kwenye kadi ili watoto wachague yenye kufanana au hata ile ambayo haifanani na zingine. Kadhalika wanaweza kuchagua vitu ambavyo vinaanza kwa sauti fulani kisha wataje vitu vingine ambavyo vinaanza kwa sauti ile. 59 b) Anaweza kuweka vitu kwenye safu mbili kama vile herufi kubwa au ndogo, silabi, picha, maumbo,na maneno, kisha kuwauliza watoto kupigia mstari vitu vinavyofanana. c) Aweza kuweka kadi zenye maneno wazi, maneno ambayo watoto wamezoea. Kisha kuwauliza watoto kuchagua neno ambalo mwalimu amesoma au kuchagua neno lingine kama lililochaguliwa na mwalimu. Pia anaweza kuwauliza neno moja Iinaloanza kwa herufi kama vile 'b'na nyingine inayoanza na herufi 'd'. 2.6 Tathmini Tathmini ni kufanya uamuzi kuhusiana na jambo ili kuamua thamani au ufaafu wake (Ogunnyi, 1984; Reason, 1990). Anaendelea kusema kuwa mwalimu anaweza kubainisha maendeleo ya watoto kupitia tathmini kadhaa. Kutokana na uchanganuzi wa tathmini hizi anaweza kufanya uamuzi wa kubadilisha au kutupilia mbali mbinu fulani ya ufundishaji au kurudia tena funzo lile kwa kutumia nyenzo zingine mwafaka. Hii inadhihirisha mwingiliano unaoendelea kati ya tathmini na mazoezi katika mkabala wa ufundishaji na ujifunzaji wa kusoma. Watoto wanapoanza masomo, mara moja tofauti za watoto zinaibuka. Mwanzo kabisa utathmini wa maendeleo ya watoto unaweza kujikita katika mazoezi wanayopewa darasani kama vile: • Kuwatazama wanaposoma kwa sauti na kimya, mwalimu azingatie kama wanafurahia au kinyume chake. • Uwezo wa kusoma kadi za silabi, maneno, sentensi au kusoma. 60 • Uwezo wa kujaza mapengo kwa sauti. • Kujibu maswali yanayohitaji ndio au la. Kisha kuna tathmini za kusaidia kuchunguza shida za mtoto binafsi ili kutayarisha mazoezi ya ziada. Shipley na wengine (1968) wanasema mwalimu kama daktari anaweza kutambua shida ya mtoto kutokana na dalili zinazodhihirika kwa kutumia vifaa mwafaka vya kumwezesha kutambua shida hasa ya mtoto. Hivyo wanashikilia kuwa kubahatisha, kutazama kusiofaa na tathmini ambazo zimeandaliwa ovyoovyo haziwezi kufaidi chochote. Maswali ya kuzingatia ni je, mwalimu atajuaje shida za watoto ambao hawajafikia kiwango kinachofaa au wanao uwezo mkubwa zaidi darasani? Je, atajuaje ni watoto gani wanahitaji mazoezi ya ziada? Tathmini hizi zinafaa kufanywa mapema iIi mwalimu apate nafasi ya kurekebisha makosa ambayo yanadhihirika kwa kubadilisha mbinu za ufundishaji na kuandaa shughuli mwafaka kwa makundi mbalimbali darasani. Shida za watoto zinaweza kusababishwa na mambo mengi ambayo si rahisi kutambua kama yale ya kisaikolojia. Kabla mwalimu kuamua kama matatizo ni ya kisaikolojia kwanza mtoto apewe tathmini ya kuthibitisha hayo. Matatizo yanayosababishwa na ugumu wa somo au mbinu za kufundishia hizo ni rahisi kushughulikia zikitambulika. Aina za Tathmini Tathmini hizi ni za aina mbili : • kununuliwa • kutungwa na mwalimu. 61 KENYATTA UNIVERSITY LIBRARY Tathmni ambazo ni za kununuliwa zinajikita katika ushindani ambapo watoto hupangwa kulingana na werevu darasani au shule katika eneo fulani. Manufaa ya tathmini hizi ni kule kupambanua udhaifu wa kijumla unaopatikana kwa watoto wanapoendelea kukumbana na mada tofauti. Pia zinaweza kuonyesha mada ambazo zinatatiza watoto katika masomo mbalimbali. Lakini tathmini zilizotungwa na mwalimu zinaweza kusaidia hasa kutambua kipengele kipi kinachomsumbua mtoto kwa sababu hizi hutungwa zikijikita katika mada moja kwa wakati mmoja. Hizi humwezesha mwalimu kujua ni sehemu gani ya inamaanisha mtoto yule hayuko tayari kwa mada iliyofunzwa. Matokeo yakionyesha ~ ~ j• 11 :1, kusoma inayomtatiza mtoto. Ikiwa mtoto ana matatizo mengi katika ule mtihani sehemu moja ya mada ambayo mtoto haelewi, basi mazoezi ya ziada yanaweza kufanywa kwa kutumia mbinu mwafaka kufanya marudio. ••~ I 11,, " Matokeo ya mtihani yakichanganuliwa mwalimu anaweza kugundua mambo mengi kwa mfano matokeo yakionyesha watoto wengi walianguka, hii itamaanisha kurudia kipengele kile katika darasa lote. Pia ikiwa watoto wawili au watatu walipata baadhi ya maswali magumu na kuanguka mengine ya aina ile itamaanisha watoto watahitaji kusaidiwa kuwa makini zaidi. Aidha, watoto wenye kufanya makosa ya kiupuzi, itamaanisha pengine wana matatizo ya kisaikolojia. Hawa watahitaji mwalimu kuwatia ari na awe mwenye subira ili kuwasaidia watoto hawa kujiamini kuliko kuwarundikia kazi ya marudio. Mtoto mwenye uwezo wa wastani akikosa kufanya vizuri, ni vyema mwalimu kuchunguza sababu ; yawezekana mtoto alikuwa mgonjwa, mchovu ama ana jambo linalomsumbua, huyu anaweza kupewa mtihani mwingine. 62 2.7 Kazi ya Marudio Mwalimu mzuri atajaribu kusahihisha makosa ya kila aina yanapotokea. Marudio yenye faida ni yale yanayojikita katika stadi fulani. Mwalimu itambidi kuzingatia njia au utaratibu mwafaka utakaomwezesha mtoto kurekebisha makosa yake. Ni vyema mwalimu akijaribu njia mbalimbali za kumsaidia mtoto. Baadhi ya mambo ambayo mwalimu anaweza kuzingatia ili kuboresha mazoezi ya marudio ni kama yafuatayo : • Usirudie mtindo na kazi uliyokuwa umepitia awali. • Pima kiwango cha kazi ambayo mtoto ana uwezo wa kufanya na kumaliza. • Chagua kazi ama shughuli ambazo zitaibua hamu ya mtoto badala ya kufuata urasmi mwingi. • Jadiliana na mtoto kuhusu kazi aliyopewa kwa makini na hakikisha mtoto anajua jinsi na nini anafaa kufanya kwenye zoezi. • Mtoto apewe kazi aina mbalimbali. • Hakikisha mtoto anamaliza kazi aliyopewa na anatumia ujuzi aliofunzwa. • Usianze jambo jipya kabla mtoto hajamakinika katika zoezi alilofanya kwenye marudio. • Kile ambacho kinaweza kufundishwa kwa mtoto mmoja hata kikundi au darasa nzima linaweza kufundishwa. 63 Ikiwa marudio yatafanikiwa mtoto ataimarika zaidi, atajionea fahari na kila mafanikio yatamhimiza zaidi na atajiamini zaidi. Aghalabu watoto wanaofanyiwa marudio wataendelea kuhitaji usaidizi kutoka kwa mwalimu kwa kila mada mpya. Ifahamike mwalimu hawezi kuepuka marudio kwa kikundi cha watoto au mtoto binafsi. Hata hivyo, mwalimu ambaye anajikuta mara kadhaa akifanya marudio kwa darasa nzima, ajaribu kutathmini mbinu zake. Pengine anafunza mambo mengi katika kipindi kimoja au mbinu anazotumia haziwatii watoto motisha au yeye mwenyewe hawatii watoto mshawasha wa kupenda kusoma. Muhtasari Katika sura hii, tumejadili sifa bainifu katika stadi ya kusoma kwa sauri. Kadhalika tumeonyesha mbinu na nyenzo zinazotumiwa katika ujifunzaji wa kusoma kwa sauti. Kwa njia hii, sehemu hii imebainisha uzuri na upungufu wa kila mbinu zilizorejelewa. Aidha tumejadili namna ubunifu katika matumizi ya nyenzo unavyoweza kufaidi funzo la kusoma kwa sauti. Kadhalika kubainisha matatizo yanayowakabili watoto ni muhimu katika kuimarisha usomaji kwa sauti. Aina za tathmini zimeangaziwa na umuhimu wake kwa mwalimu katika kusuluhisha matatizo ya watoto. Katika sura inayofuata tutajadili data i1iyokusanywa nyanjani kuhusu ufundishaji wa kusoma kwa sauti unavyoshughulikiwa na walimu darasani. 64 SURA YA TATU: UWASILISHAJI WA UFUNZAJI WA STADI YA KUSOMA KWASAUTI 3.0 Utangulizi Sura ya pili tumejadili vipengele muhimu katika stadi ya kusoma kwa sauti. Baadhi ya mambo yaliyoangaziwa ni sifa zake bainifu, mbinu na nyenzo za kufundishia. Kadhalika umuhimu wa tathmini umeangaziwa katika stadi ya kusoma kwa sauti. Kwa kutumia tathmini mwalimu anaweza kutambua matatizo ya watoto ya usomaji. Aidha, ufahamu huu utamwezesha kuibua mikakati mwafaka kutatua na kuimarisha usomaji. Sura hii imedhamiria kueleza, kuchanganua na kujadili data ya utafiti iliyokusanywa nyanjani. Walimu kumi na wanane wa madarasa ya chini waliteuliwa kutoka shule ~".'~ sita za msingi katika tarafa ya Gatanga, wilaya ya Thika. Shule hizi ni Chomo, Gatura, Gatunyu, Kirwara, Gichumbu na Rwegetha, zilizoteuliwa kwa kutumia mbinu ••.' ~ ~bahatishi. Darasa moja lilichaguliwa katika kila kiwango ambapo kulikuwa na zaidi ya darasa moja mbinu bahatishi ilitumiwa kuteua darasa moja. Pia, sura hii imegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza inahusu majibu ya walimu katika hojaji ambayo yanahusiana na namna walivyoshughulikia funzo la kusoma kwa sauti darasani. Walimu walipewa hojaji kujaza ambazo ziliwataka kubainisha namna walivyofundisha stadi ya kusoma kwa sauti. Pia walihitajika kueleza namna walivyokabili matatizo yaliyotokea katika stadi ya kusoma kwa sauti. Sehemu ya pili imejadili matokeo ya uchunguzi wa darasani uliofanywa na mtafiti. Madhumuni ikiwa ni kuthibitisha majibu ya walimu yaliyotolewa kwenye hojaji. 65 Uchunguzi wa darasani ulifanyika kwanza kabla ya walimu kujaza hojaji. Kwa njia hii maswali ya hojaji hayakuathiri utekelezaji wa funzo darasani. 3.1 Uwasilishaji wa Matokeo Matokeo yalijadiliwa kwa kufuata vitengo mbalimbali vilivyoonyeshwa kwenye maswali ya hojaji. Vitengo vilivyoshughulikiwa ni kama vile; maelezo kuhusu watoto na walimu, maelezo kuhusu mbinu na nyenzo zilizotumiwa, namna usomaji ulivyotekelezwa na aina za tathmini zilizotumiwa na walimu. Utaratibu wa kuwasilisha ulibainisha matokeo ya kila darasa kama yalivyoelezewa na walimu ili kuweza kuona maendeleo ya watoto kutoka kila kiwango hadi kingine kama nadharia ya Krashen inavyotueleza kuwa, ufahamu wa lugha hukua kihatua. 3.1.1 Maelezo Kuhusu Watoto Katika Hojaji Matokeo katika Jedwali 3.1 yalionyesha kuwa madarasa ya kwanza yalikuwa na idadi ya watoto kati ya 30-58 kwa kiwango cha wastani watoto walikuwa ni 46. Katika madarasa ya pili idadi ya watoto i1ikuwa kati ya 33-65. Kwa kiwango cha wastani watoto walikuwa 47. Madarasa ya tatu idadi yao ilikuwa kati ya 33-50. Kwa kiwango cha wastani watoto walikuwa 44. Matokeo haya yalionyesha kuwa idadi ya watoto ilikuwa kubwa. Kadhalika watoto wa madarasa ya kwanza walikuwa kwa kiwango cha wastani na umri wa miaka 6. Madarasa ya pili walikuwa na miaka 7 na madarasa ya tatu walikuwa na miaka 8. Hata hivyo, kulikuwa na watoto katika madarasa haya waliozidi miaka iliyotajwa kwa sababu ya mambo tofauti. Umaskini, watoto walijiunga na shule baada ya karo ya shule kuondolewa na serikali mwaka wa 2003, 66 kurudia darasa kwa sababu ya kuwa na akili nzito na watoto wenye akili punguani. Hata hivyo, watoto wengi walikuwa katika madarasa yanayoafikiana na umri wao J d r 3 1 Id d' W f .K tik Kil De wa I . : a I ya ana unzi a I a a arasa Shule Idadi ya Watoto La Kwanza La Pili La Tatu Chomo 42 42 47 Gatura 56 50 46 Gatunyu 46 46 50 Kirwara 30 33 33 Rwegetha 58 65 37 Gichumbu 45 48 50 Jumla ya umri 6 7 8 Matokeo (Jedwali 3.1) ilidhihirisha kuwepo katika baadhi ya shule idadi kubwa sana ya watoto ikilinganishwa na zile zingine. Baadhi ya sababu zilizotolewa na walimu zilikuwa tofauti kama vile kuwepo vifaa bora katika shule moja kuliko zile zingine na ukosefu wa walimu wa kutosha kwa hivyo kuunganisha madarasa mawili. Kama ionekanavyo shule ya Rwegetha katika darasa la tatu lilikuwa na watoto wachache kwa sababu ya kutenganisha watoto baada ya kupata mwalimu mpya. Kulingana na wizara ya Elimu, idadi ya watoto darasani, inafaa kuwa mwalimu mmoja kati ya watoto 40 ingawa ilibatilishwa hivi karibuni na kuwa 50. Hii ilitokana na ongezeko la watoto baada ya kuanzishwa elimu ya msingi bila malipo. Ongezeko la watoto ina maana kuwa kazi ya mwalimu iliongezeka katika kutayarisha shughuii 67 na nyenzo mwafaka kutosheleza uwezo tofauti wa watoto. Kulingana na wataalamu hata kwa walimu wenye tajriba kufunza idadi kubwa ya watoto huwa changamoto kubwa. 3.1.2 Maelezo Kuhusu Walimu Katika Hojaji Majibu ya hojaji yalionyesha kuwa walimu wanawake ndio waliokuwa wengi kuliko wanaume katika madarasa ya chini (Mchoro 1). Wanawake ilichukuliwa ni wenye subira na wanaweza kuwashughulikia watoto wa umri huu kwa makini zaidi wakilinganishwa na wanaume. Hata hivyo, kuna haja ya utafiti kuthibitisha madai haya. Aidha, mwanamume katika darasa la pili alikuwa akifunza madarasa ya juu hapo awali. Mwalimu alisukumwa katika darasa hili kama adhabu. .Wanawake ~Wanaume 7 6 ::::s.5 5; 4 ca 3~ " 2ca:2 0 Kwanza Pili Tatu Madarasa Mchoro 3.1: Idadi ya Walimu Kulingana na Jinsia Katika Darasa 1-3 3.1.3 Maelezo Kuhusu Kiwango cha Elimu ya Walimu Matokeo yalionyesha kuwa asilimia 98 ya walimu walihitimu kiwango cha kidato cha nne (Mchoro 2). Kati ya hawa asilimia 50 walikuwa wa mfumo wa elimu ya 8-4-4. 68 Inachukuliwa kuwa hawa ndio wenye msingi bora katika somo la lugha ya Kiswahili kwa sababu walifunzwa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne (Mbaabu, 1987). Walimu 17 (98%) walikuwa na cheti cha PI isipokuwa mmoja ambaye alikuwa ameongezea masomo na kuwa na cheti cha shahada. Mwalimu mwenye shahada alikuwa wa mfumo wa 8-4-4. Mwalimu hata baada ya kupata shahada hakupendelea ama kufunza Kiswahili au madarasa ya chini. Kadhalika walimu waliofuzu katika mfumo wa elimu wa E.A.C.E walieleza kuwa hawakufunzwa lugha ya Kiswahili katika shule za msingi na za upili. Mmoja wao ingawa alikuwa na matatizo mwanzoni lakini baada ya kuhudhuria vipindi vya mwalimu mwingine aliyekuwa na tajriba katika madarasa haya alipata ujuzi wa kufundisha somo hili kwa watoto wa madarasa ya chini. Aidha, katika mifumo yote kuna walimu waliopenda kufundisha somo la Kiswahili na kuna wengine ambao hawakupenda. Hii ina maana kuwa mtazamo wa mwalimu kuhusu lugha ya Kiswahili ilikuwa muhimu mbali na tajriba au mfumo wa elimu. Ifahamike kuwa, walimu wote walikuwa wamefunzwa somo la Kiswahili katika vyuo vya walimu. Vile vile Kati ya walimu hawa 17 kuna baadhi yao walikuwa wanasomea cheti cha Diploma katika masomo yanayohusiana na ufunzaji wa watoto wadogo 'Early Childhood Development (E.C.D). Wengine walisomea 'Special Education' ambayo ni masomo yanayohusiana na watoto wenye changamoto katika ujifunzaji. Aidha, walimu wan ne walikuwa wakifanya mazoezi ya kufundisha wakati wa utafiti huu. Ni matumaini yetu kuwa ujuzi watakaopata utachangia katika kuwasaidia watoto wenye uwezo tofauti katika ujifunzaji. 69 K.C.S.E. 50% E.A.C.E. 22% Mchoro 3.2: Asilimia ya Kiwango cha EIimu ya WaIimu (N=18) Kulingana na wataalamu tajriba ni muhimu katika ufunzaji. Katika shule za msingi aghalabu huwa kuna walimu wanaofunza madarasa ya chini na wengine madarasa ya kwanza hadi la tatu. Ifahamike katika madarasa ya chini, aghalabu mwalimu mmoja juu. Mwalimu wa darasa la chini huandamana na watoto anaofunza kutoka darasa la 'I; hufunza masomo yote. Aidha katika madarasa ya juu aghalabu mwalimu hupewa masomo kadri ya uwezo wake. J d r 3 2 T . ob M r Ka ika VC dish O. Ki hTe wa I . ajri aya wa rmu ti un IS aJI wa swa I I.. Miaka 0-3 4-6 7-10 11 na zaidi Idadi 4 3 3 8 Kulingana na Jedwali 3.2 walimu ambao walikuwa wamefunza chini ya miaka mitatu walikuwa wanne. Hawa waliwakilisha walimu ambao hawana tajriba kwa sababu walikuwa wamefundisha madarasa haya kwa kipindi kimoja. Walimu waliokuwa 70 wamefundisha kati ya miaka 4-6 walikuwa na tajriba wastani kwa sababu walikuwa katika kipindi kingine cha pili katika madarasa haya. Aidha, walimu wenye zaidi ya miaka saba hawa walichukuliwa kuwa na tajriba kubwa kwa sababu walikuwa wamefunza madarasa ya chini kwa muda mrefu. Walimu hawa walikuwa wamepata ujuzi wa kutumia mbinu mbalimbali na kuibua mikakati ya kukabiliana na changamoto katika ufunzaji. Pia inachukuliwa kuwa walikuwa wameibua mikakati ya kukabiliana na hali tofauti za watoto. Matokeo yanaonyesha kuwa walimu wengi walikuwa na tajriba kubwa. I1idhihirika kuwa walimu wachache hawakupenda kufundisha madarasa ya chini. Walifunza bila hiari yao kwa sababu ama waliajiriwa au walipata uhamisho ili kuchukua nafasi za waliostaafu. Hata hivyo, kulikuwa na mwalimu mmoja ambaye alipenda kufunza Kiswahili lakini aliomba kufundisha madarasa ya chini ili apumzike kusahihisha insha. Lakini alikiri kuwa kuwafundisha watoto katika kiwango hiki i1ikuwa si rahisi kama alivyofikiria. Pia kulikuwa sababu za kinidhamu ambapo ,.. mwalimu alisukumwa kufunza darasa la chini kwa sababu ya utendakazi mbaya kama alivyosema mwalimu mkuu mmoja. Pengine ilichukuliwa kuwa ufundishaji wa madarasa ya chini ni rahisi. Ifahamike, kuna baadhi ya shule ambapo walimu wa madarasa ya chini walipewa kusahihisha insha za Kiswahili na Kiingereza ili kuwasaidia wale wa madarasa ya juu pengine kwa sababu ilichukuliwa kuwa hawana kazi nyingi. 71 3.2 Majibu ya Walimu Kuhusu Ufundishaji wa Kusoma Sehemu ifuatayo ilionyesha maswali yaliyonuia kuonyesha namna walimu walivyotekeleza ufundishaji wa kusoma kwa sauti. Maelezo ya walimu yamewasilishwa kwa mujibu wa madarasa mbalimbali ili kubainisha tofauti yoyote katika ufunzaji. 3.2.1 Malengo Yaliyozingatiwa na Walimu Katika Ufundishaji Kabla ya kuandaa shughuli za funzo mwalimu humbidi kufikiria malengo ya funzo ili kuandaa kazi itakayoafikiana na malengo ya mada itakayofunzwa. Kulingana na silabasi K.I.E (2002:131) malengo katika stadi ya kusoma huwa ni: kusoma silabi, kuunda maneno na kusoma, kutambua silabi, kusoma kwa matamshi sahihi, kusoma kwa ufasaha na kuzingatia uakifisho na kusoma kwa ufahamu. Inavyodhihirika ni kuwa malengo haya yanaoanisha ujuzi wa chini na ujuzi wa juu katika stadi ya kusoma kwa sauti. Malengo ya funzo huathiri shughuli na tathmini zitakazoteuliwa na mwalimu ili kufanikisha funzo lililoandaliwa. Malengo (Jedwali 3.3) yalitolewa na walimu na yaliafikiana na yale ya silabasi. 72 Jd r33MI y r ti wr Kafk D I 1 3e wa I . : a engo a IYOZID2arwa na a unu I a arasa a - Malengo Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Kusoma Silabi 3 2 0 Kutambua silabi 1 0 0 Matamshi sahihi 2 2 2 Ufasaha 1 0 4 Uakifishaji 0 3 1 Kusoma maneno 4 5 2 Kujibu maswali 1 4 4 Jumla ya malengo 12 16 13 Matokeo yanaonyesha kwamba walimu katika madarasa yote walikuwa na zaidi ya malengo moja katika ufunzaji wa kusoma kwa sauti (Jedwali 3.3). Katika darasa la kwanza inadhihirika kuwa walimu waIizingatia malengo ya kusoma silabi na kusoma maneno zaidi. Hawakuzingatia sana malengo yaliyozingatia ujuzi wajuu k.v. ufasaha, uakifisho na kujibu maswali. Hata hivyo, kuna mwaIimu mmoja ambaye alitoa malengo ambayo hayakuafikiana na yale yaliyotolewa kwenye silabasi kama vile • Kusoma Vivumishi • Kusoma msamiati • Kusoma hadithi Malengo haya yanaonyesha kuwa mwaIimu hakubainisha kati ya malengo na mada katika funzo. Malengo yanatakiwa kupima ujuzi mahsusi katika funzo. Hii ni kwa sababu watoto katika darasa hili hawajamudu kupambanua herufi na sauti zake zote 73 Aidha, ujuzi wa kiwango cha chini haudhihiriki kabisa. Malengo ni kama dira ya kumwelekeza mwalimu kuendesha funzo ifaavyo. Malengo mwafaka ni yale yanayoweza kupimika na kutimilika mwishoni mwa funzo. Katika darasa la pili na la tatu matokeo yalionyesha kuwa walimu hawakuzingatia malengo ya kusoma silabi na kutambua silabi kama malengo yao (Jedwali 3.3). Walimu wawili katika darasa la pili ndio waliolenga kusoma silabi. Hii inaonyesha kuwa walimu wengi katika madarasa haya walipima zaidi ufahamu. Hii inaashiria kuwa watoto hawa walikuwa wamemudu ujuzi wa chini wa kusoma. Aidha, walimu katika madarasa ya tatu walizingatia zaidi kusoma kwa ufasaha na kujibu maswali. Hii ina maana kuwa malengo yalijikita katika ujuzi wajuu zaidi. Kulingana na Modeli Husishi ni muhimu walimu kuhusisha ujuzi wa chini na wa juu katika kusoma kwa sauti. Kwa njia hii watoto wataweza kupambanua silabi na sauti zake na pia kujenga I,I. matamshi na ufasaha sahihi. lAI•, ,I I,. 3.2.2 Mbinu za Kufundisha Kusoma kwa Sauti Matokeo katika Jedwali 3.4 yalionyesha mbinu mbalimbali zilizotumiwa na walimu katika ufunzaji wa kusoma kwa sauti. Mbinu katika jedwali hili, zimepangwa kwa kuzingatia viwango vya ujuzi wa kusoma kwa sauti kuanzia vile vya ujuzi wa chini kuelekea vile vya ujuzi wajuu. 74 Jedwali 3.4: Idadi ya Walimu Waliotumia Mbinu Mbalimbali Katika Darasa la 1-3 Mbinu Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Abjedi 2 1 0 Silabi 6 6 6 Kusemaneno 6 5 5 Kusoma sentensi 2 4 5 Kusoma hadithi 0 4 6 Matokeo yanaonyesha kuwa walimu katika madarasa ya kwanza, pili na tatu walitumia mbinu ya silabi na kutazama na kusema neno (Jedwali 3.4). Maelezo haya I "I yanadhihirisha kuwa walimu katika viwango vyote walizingatia ujuzi wa chini wa kusoma kwa sauti. Ilidhihirika kuwa walimu katika darasa la kwanza walipuuza " ".' "umuhimu wa ufahamu katika stadi ya kusoma kwa sauti. Hii ni kwa sababu mbinu ya kusoma sentensi ilitumiwa na walimu wawili na mbinu ya hadithi haikutumiwa , ~,~ " kamwe. Walimu katika darasa la pili na tatu walionekana kutumia mbinu changamano ~I' " " "/1 ",f - katika ufunzaji wa stadi ya kusoma kwa sauti. Kulingana na silabasi watoto katika darasa la tatu walichukuliwa kuwa tayari wamemudu ujuzi wa chini wa kusoma kwa sauti. Matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna watoto ambao walikuwa hawajamudu ujuzi wa chini kwa sababu walimu wote sita walieleza kuwa wao hutumia mbinu ya silabi. Modeli Husishi inasisitiza kuhusisha viwango vyote vya ujuzi wa kusoma kuanzia mwanzoni ili kuimarisha stadi hii. Kwa njia hii watoto watakuwa na hamu ya kusoma kwa sababu usomaji una maksudio. 75 3.2.3 Maoni Kuhusu Umuhimu wa Kila Mbinu Walimu walikuwa na maoni mbalimbali kuhusu mbinu za kusoma kwa sauti. Matokeo yalionyesha kuwa walimu katika madarasa yote hawakutilia mkazo matamshi na uakifishaji (Jedwali 3.5). Hii inaonyesha kuwa ama watoto walikuwa hawana matatizo au walipuuza sifa hizi. Huu unaweza kuwa upungufu mkubwa kwa sababu haya yote mawili ni muhimu katika uelewa wa kinachosomwa. Jd r35M wr Kh MbO Mb r b r K tik D I 1-3e wa I . : aom ya a imu u usu mu aim a I a I a arasa a Umuhimu Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Kutambua herufi 1 1 0 Kumudu silabi 4 5 4 Matamshi 1 2 1 Ufasaha 4 5 5 Kujibu maswali 1 2 4 •"• •/•• (Mpangilio huu unaafikiana na mpangilio wa mbinu za kusoma katika Jedwali 3.4) (Jedwali 3.5). Walimu katika darasa la kwanza, la pili na la tatu walionekana kutilia ••, •! Matokeo yalibainisha kuwa walimu walifahamu umuhimu wa mbinu walizotumia mkazo upambanuzi wa silabi (Jedwali 3.5). Walimu walieleza kuwa sababu za kutumia mbinu hizi ni kuwawezesha watoto kupambanua herufi na silabi ili kuunda na kusoma maneno. Aidha, wengine walitaja umuhimu wa watoto kumudu silabi ili kuwaandaa kwa mitihani. Walimu wanne katika darasa la kwanza walieleza kuwa ni muhimu kwa watoto kumudu silabi kwanza kabla ya kuzingatia ufahamu. Katika darasa la pili kuna walimu wawili waliosema kuwa kiwango cha watoto cha ufahamu kilikuwa bado cha chini sana kufahamu walichokuwa wakisoma. Yamkini walimu 76 hawa walizingatia Modeli ya Chini-juu. Vile vile, matokeo yalionyesha kuwa kuna walimu wawili waliohusisha ujuzi wa juu wa kusoma katika ufunzaji wao. Walimu katika darasa la tatu walizingatia ujuzi wa chini na ule wa juu katika usomaji. Hii ina maanisha kuwa kulikuwa na watoto ambao walikuwa hawajamudu ujuzi wa chini wa kusoma (Jedwali 3.5). Maelezo haya hayaafikiani na mapendekezo ya silabasi katika darasa la tatu ambayo yanaonyesha kuwa watoto katika darasa hili walikuwa wamemudu ujuzi wa chini. 3.2.4 Vitangulizi vya Kusoma Matokeo yanaonyesha aina za vitangulizi ambavyo walimu walitumia katika vipindi vya kusoma kwa sauti. Ilidhihirika kuwa walimu walitumia zaidi ya kitangulizi kimoja kama inavyoonyeshwa katika Jedwali 3.6. Yamkini kuna walimu wengi katika madarasa ya kwanza, pili na tatu ambao walipendelea kutanguliza mafunzo yao kwa nyimbo na mashairi. Kwa maoni ya walimu ujumbe wa mashairi na nyimbo unafaa kuchukuana na mada itakayofunzwa. Kadhalika, ilionekana kwamba walimu katika darasa la kwanza na la pili walikuwa na aina nyingi za vitangulizi ikilinganishwa na wale wa darasa la tatu. Matokeo haya yanaonyesha upungufu wa ubunifu kadri walimu walivyoendelea katika madarasa yaliyofuata. Kando na hayo, walimu katika darasa la tatu walitoa vitangulizi ambavyo vilitofautiana na vilivyotajwa na walimu wa madarasa yaliyotangulia na ilidhibitika kuwa walimu hawakuzingatia matumizi ya nyenzo. 77 ENYA A iVERSITY J d r 3 6 A' li . VT t wr K t r F o.e wa I .. maya I angu lZI I rvyo umrwa na a rmu u anau tza unz Utangulizi Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Nyimbo 5 2 2 Vitendawili 2 2 3 Picha 2 2 0 Michezo 1 1 0 Chati 0 1 0 Mashairi 3 1 0 Hadithi I 1 0 Kadi 0 0 1 Vifaa halisi 0 0 1 Michoro 6 1 0 •"'~ ~ I•• Vitangulizi hivi ni: kueleza maana ya msamiati katika kifungu, kutunga sentensi wakitumia msamiati waliojifunza, na kusoma kifungu. Aidha walimu walieleza kuwa walitumia vitangulizi ili kuwatia mshawasha watoto katika ufunzaji. Maoni haya yanaafikiana na maelezo ya Kitengo cha Hisi ambacho kinaeleza kuwa ni muhimu kuzingatia hisi za watoto katika ufunzaji. 3.2.5 Mtindo wa Usomaji Kulingana na wataalamu wa lugha kuna aina mbalimbali za kusoma kwa sauti. Kila mtindo una uzuri wake na upungufu wake. Kwa mujibu wa matokeo, ilidhihirika kuwa walimu walitumia mitindo mbalimbali (Jedwali 3.7). 78 J d li 3 7 MO ° d K Ir t wr K tik D I 1-3e wa I .. dID 0 ya usoma iyo umrwa na a unu a I a arasa a Mtindo wa Kusoma Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Darasa lote 4 3 0 Mtoto mmoja mmoja 6 4 5 Kusoma kimakundi 2 2 1 Kusoma kimya 0 0 0 Matokeo yalionyesha kuwa walimu walipendelea kutumia mtindo wa kusoma wa mtoto mmoja mmoja (Jedwali 3.7). Walimu walieleza kuwa walitumia njia hii ili kuhakikisha kila mtoto alishiriki katika kusoma. Kupitia njia hii ni rahisi mwalimu kujua matatizo ya mtoto. Walimu wawili kati ya sita katika darasa la pili walieleza kuwa walichagua watoto ambao walijua kusoma ili kuwaongoza wengine. Kadhalika waliwapa watoto nafasi ya kujisomea kwa sauti huku mwalimu akizunguka na kuwasaidia watoto. Darasa la pili na la tatu kuna mwalimu mmoja kwa kila darasa aliyeeleza kuwa alitumia mtindo wa watoto wawili wawili kusoma. Hii ni kwa sababu kuna watoto walioogopa kusoma peke yao. Maoni ya walimu hawa yanaafikiana na maelezo ya Kitengo cha Hisi kinachoelezea umuhimu wa mwalimu kuzingatia hisi za watoto anaofundisha. Kadhalika mtindo wa darasa lote ulitumiwa na baadhi ya walimu katika madarasa ya kwanza na ya pili. Katika darasa la tatu walimu hawakutumia mtindo wa darasa lote kusoma kwa sauti. Watoto katika madarasa yote yaliyohusika hawakupewa nafasi ya kusoma kimya. Walimu pengine hawakufikiria mtindo huu unaweza kushirikishwa hata wakati watoto wanaposoma kwa sauti 79 3.2.6 Mpangilio wa Makundi Darasani Walimu walionekana kutumia aina tofauti ya makundi darasani wakati wa kufundisha kusoma kwa sauti (Jedwali 3.8). Makundi haya yalisoma kwa zamu huku mwalimu na watoto wengine wakisikiliza. Jd 1"38 A' M k di Y I" t WI" k tik D I 1 3e wa I .. ma ya a un I a ryo unuwa na a nnu a I a arasa a - Aina ya Makundi Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Wawili Wawili 1 0 0 Watatu Watatu 1 1 2 Safu 4 4 0 Matokeo yalionyesha kuwa walimu wanne katika darasa la kwanza na la pili waliweka watoto katika safu (Jedwali 3.8). Watoto katika safu hizi walipangwa kulingana na uwezo. Walimu walieleza kuwa kikundi kilichokuwa na matatizo mengi kiliwekwa karibu na meza ya mwalimu ili wapate nafasi ya kuwatazama na kuwasaidia zaidi. Mwalimu mmoja katika darasa la kwanza alieleza kuwa aliwaweka watoto katika makundi ili kuzuia watoto wenye uwezo kuathiriwa na wenye uwezo wa chini. Hii ina maana ya kuwa watoto werevu wanaweza kuvutwa nyuma katika maendeleo ya usomaji. Walimu wawili walitumia ama makundi ya watoto wawili wawili au watatu watatu. Mtoto mmoja kati yao akiwa mwenye uwezo kuliko wale wengine ili aweze kuwasaidia. Katika darasa la pili kulikuwa na mwalimu mmoja ambaye alikuwa bado hajapanga watoto katika makundi kwa sababu alikuwa amewafunza muhula mmoja pekee. Pia, walimu walieleza kuwa walitumia kigezo cha uwezo kuwapanga watoto. Katika darasa la tatu walimu hawakutumia makundi ya safu kuwapanga watoto. Walimu wawili kati ya sita walitumia makundi ya watoto 80 watatu watatu ambapo walichanganya mtoto mmoja mwenye uwezo wa kusoma kati ya wawili ambao walikuwa na akili nzito (Jedwali 3.8). Mmoja wao alieleza kuwa mara nyingine ni rahisi watoto kufunzwa na wenzao hususani wenye kuogopa mwalimu. Mwalimu mmoja alieleza kuwa aliwapanga watoto katika makundi saa nane wakati wa kuwapa mazoezi ya ziada kulingana na uwezo wao. Aidha walimu wengine watatu hawakutumia makundi, watoto walikuwa wamechanganyika darasani. Mwalimu mmoja kati ya hawa alifafanua kuwa watoto wenye uwezo wa chini wakitengwa hukosa motisha. Yamkini walimu waliotumia makundi walieleza kuwa makundi yalikuwa si ya kudumu, kadri watoto walivyoendelea kuimarika yalibadilishwa. Walimu walitumia matokeo ya mazoezi na tathmini rasmi walizopewa " watoto kupima maendeleo. 11i 3.3 Aina ya Vitabu na Makala ya Kusoma III '"ill 11 Vitabu na makala ni muhimu katika kuimarisha stadi ya kusoma. Kulingana na "'1111 '".'I1,' :11wataalamu vitabu na makala yanayotumiwa yanaweza kuendeleza au kutinga usomaji. Kwa mujibu wa kitengo cha Krashen cha Uteuzi Makala; uteuzi wa makala unafaa ",11',., kuzingatia uwezo na tajriba ya watoto. Matokeo ya Jedwali 3.9 yanaonyesha vitabu III,I I•• "I II1'il ,I.' aina mbali mbali vilivyotumiwa na walimu. Vitabu vyote vilivyoorodheshwa vimependekezwa na Taasisi ya Elimu (K.I.E). 81 J d r 3 9 vu b VT t wr Kat·k D I 1 3e wa I . : I a u I IVYO umrwa na a unu I a arasa a - Vitabu Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Kiswahili Mufti 4 4 4 Masomo ya Msingi 3 3 3 Kiswahili Sanifu 3 2 2 Kiswahili kwa Darasa 1 1 0 Kiswahili Teule 0 0 1 Tujivunie Kiswahili 2 1 0 Hadithi 0 1 I Matokeo yalionyesha kuwa walimu katika viwango vyote walikuwa na zaidi ya kitabu kimoja cha kufunzia (Jedwali 3.9). Walimu wengi walionekana kupendelelea kutumia Kiswahili Mufti. Kitabu cha Masomo ya Msingi kilifuata kwa umashuhuri, na kisha ,,I ",I "~ Kiswahili Sanifu. Kadhalika walimu walizingatia mapendekezo ya silabasi katika kuchagua makala ya kusoma. Walimu wengi walieleza kuwa walifuata mpangilio wa vitabu vya kiada kwa sababu mada zilipangwa kulingana na muhula. Hata hivyo "11il ,I 11,I II ,I, walimu katika darasa la kwanza hawakutumia Kiswahili Mufti, bali walitumia vitabu tofauti wakati wa kufundisha. Mwalimu mmoja alieleza kuwa Kiswahili Mufti kilikuwa kigumu kwa watoto wa mashambani. Walimu walieleza kuwa walikitumia kwa kuwapa watoto mazoezi pekee kwa sababu kilikuwa na mazoezi mengi. Vile vile mwalimu mmoja alieleza kuwa hukirejelea wakati wa kuandaa mafunzo. Mawazo haya yanaafikiana na Kitengo cha Uteuzi wa Makala cha Krashen yanayoonyesha umuhimu wa kuzingatia uwezo na tajriba ya watoto ili kuamsha hamu na maendeleo ya stadi ya kusoma. Mwalimu mmoja kati ya sita alieleza kuwa watoto wanapoingia 82 darasa la kwanza, huanza kwa kuwafanyisha mazoezi ya mambo ya kimsingi katika kusoma kwenye mchanga kabla ya kuanza kutumia kitabu kilichopendekezwa. Hakuna aliyetaja vitabu vya hadithi ama makala yoyote mengine mbali na yale yaliyotajwa. Kwa mujibu wa Kitengo cha Uteuzi Makala, kuna haja ya kushirikisha vitabu vya hadithi; uchaguzi wenyewe uzingatie Kitengo cha Utaratibu wa Kiasili ili kuamsha hamu ya kusoma. Katika darasa la pili na la tatu walimu walitumia Kiswahili Mufti kufundishia. Walimu walikuwa na maoni tofauti ya kukitumia. Mwalimu mmoja katika darasa la pili na mwingine katika darasa la tatu walieleza kuwa walikipendelea kwa sababu kilikuwa na upana wa msamiati kikilinganishwa na hivyo vingine. Mwalimu mwingine katika darasa la pili alieleza kuwa kina mpangilio mzuri na wengine wawili walisema kilipendekezwa na jopo la walimu wanaoshughulikia mambo ya kiusomi shuleni mwao. Mwalimu mmoja katika darasa la tatu alieleza kuwa mtihani wa kitaifa wa darasa la nane ulitungwa kutoka kwa Kiswahili Mufti. Hata hivyo, hakuna mwalimu aliyetaja ugumu wa kitabu hiki. Kama ilivyodhihirika (Jedwali 3.9) ni mwalimu mmoja tu katika darasa la pili na mwingine darasa la tatu ambao walikuwa na vitabu vya hadithi. Hii ni kinyume na matakwa ya silabasi ambayo inapendekeza matumizi ya maktaba katika madarasa yote. Aidha, katika viwango vyote walimu walieleza kuwa walikuwa na vitabu vya kutosha. Walivigawa ama 1:2, 1:3 au 1:4. Kuhusu kukamilisha silabasi, katika darasa la kwanza, la pili na la tatu, walimu watatu, watatu na wanne mtawalia walikamilisha silabasi. Hii inaonyesha kuwa 83 UN~ LI~""il'r1l walimu walijitahidi katika kukamilisha silabasi ikichukuliwa kuwa walikuwa na changamoto nyingi k.v. kufunza idadi kubwa ya watoto. 3.4 Mbinu za Kutathmini Usomaji wa Watoto Kuna njia mbalimbali za kutathmini viwango vya watoto katika kila darasa kama ilivyoelezewa kwenye silabasi (K.I.E, 2002). Sehemu hii inanuia kuonyesha mbinu ambazo walimu walipendelea kutumia kutathmini viwango vya usomaji wa watoto darasani (Jedwali 3.10). Mbinu ya watoto kusoma mmoja mmoja ina maana ya watoto kusoma kwa zamu darasani au kila mtoto kujisomea makala kwa sauti mwalimu akizunguka darasani akiwasaidia. Kujaza mapengo, walimu walitarajia watoto kujaza mapengo kwa kuandika herufi au neno mwafaka. Kuchanganua picha ni mbinu, ambapo watoto walibainisha picha au michoro kwenye kitabu cha kiada au kwenye chati. Kadhalika, mwalimu aliweza kutathmini uelewa wa watoto kwa kutazama mambo mbalimbali ambayo watoto walishiriki darasani. Mambo kama vile kushiriki katika kuongea, kujibu maswali, kuandika, kuigiza na katika kushiriki nyimbo na michezo darasani. Matokeo yalionyesha kuwa walimu walikuwa na njia mbalimbali za kupima usomaji wa watoto darasani. Ilidhihirika kuwa walimu katika madarasa yote walitumia mbinu ya kusoma mtoto mmoja mmoja (Jedwali 3.10). Walimu walisema kuwa huu ndio mtindo waliotumia katika kuhakikisha kila mtoto ana ujuzi wa kusoma darasani. Vile vile waliutumia kwenye mtihani wa kati na wa mwisho wa muhula, ambapo kila mtoto alimsomea mwalimu kwa zamu maneno machache na sentensi chache fupi (Kiambatisho 3, 4, 5). 84 J d r 310 A' T h ' 'T r w K ik D I 1-3e wa I , : IDaza at mIDI a izopewa atoto ab a arasa a Tathmini Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Kusoma mmoja kwa sauti 6 6 6 Zoezi la Kujaza Mapengo 2 2 3 Kuchanganua Picha 0 0 2 Kutazama darasani 2 2 0 Imla 0 0 3 Mazoezi mengine yalikuwa kujaza mapengo kwa herufi au maneno mwafaka kwenye daftari. Walimu wengine wawili katika darasa la kwanza na la pili walitumia mbinu ya kutazama namna watoto walivyoshiriki katika shughuli mbalimbali darasani. Katika darasa la kwanza na la pili hakuna mwalimu aliyechukulia kuchanganua picha kama njia ya kutathmini usornaji. Inadhihirika kuwa tathmini zilijikita katika kupima ujuzi wa chini. Hata hivyo, darasa la tatu lilifuata Modeli Husishi ambapo lilitathmini uchanganuzi wa picha. Hii ni kwa sababu makala kwenye vitabu vya kiada yaliambatanisha picha zilizooana na habari kwenye makala. Kadhalika, walimu watatu walisema kuwa waliwapa watoto mazoezi ya imla. Hii ina maana kuwa watoto walikuwa wamemudu ujuzi wa kusoma wa chini kwa hivyo walikuwa na ujuzi wa kupambanua walichosikia na kuweza kuendeleza kwa usahihi. 3.4.1Idadi za Tathmini Katika swali hili walimu walieleza jumla ya tathmini walizowapa watoto na kurekodi alama za watoto mbali na mazoezi ya kila siku waliyowapa watoto. Matokeo ya majibu ya walimu yalibainisha kuwa walimu walikuwa na idadi tofauti ya tathmini walizowapa watoto. Kwajumla walimu wote katika darasa la kwanza, la pili na la tatu 85 waliwapa watoto mitihani ya kati na ya mwisho wa muhula (Jedwali 3.11). Hii ni kwa sababu hizi zilikuwa tathmni rasmi ambazo zilitengewa wakati wa kufanya na matokeo yake kupelekewa mkuu wa elimu katika tarafa ambaye alizikabidhi kwa mkuu wa elimu katika wilaya. Matokeo ya tathmini rasmi ilijikita katika ushindani. Hii ina maana kuwa shule ama katika eneo la kielimu au tarafa walifanya mitihani ya kati na ya mwisho wa kila muhula iliyofanana ili kupima maendeleo ya ujifunzaji katika masomo yote. Matokeo haya hutumiwa kupanga madarasa katika eneo au tarafa kulingana na namna walivyofuzu katika kila somo. Kwa njia hii shule zinaweza kufahamu wanavyofuzu wakilinganishwa na shule zingine . Jedwali 3.11: Idadi za Tathmini Katika Muhula Idadi za Tathmini Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Majuma mawili 2 3 4 Kila mwezi 0 1 1 Kukamilisha mada 1 1 1 Kati ya muhula 6 6 6 Mwisho wa muhula 6 6 6 :' Kulingana na majibu Jedwali 3.11 walimu wawili, watatu na wanne katika darasa la I I •-I ,--II ~q I ; kwanza, la pili na la tatu mtawalia walieleza kuwa waliwapa watoto tathmini baada ya majuma mawili. Mwalimu mmoja katika kila darasa waliwapa watoto tathmini baada ya kufunza mada fulani. Mwalimu mmoja katika darasa la pili na la tatu waliwapa baada ya kila mwezi. Inavyodhihirika ni kwamba kuna walimu watatu katika darasa la kwanza na wawili katika darasa la pili ambao hawakuwapa watoto tathmini mbali na tathmini rasmi. Walimu hawa walielezea kuwa waliwapa watoto mazoezi kutoka kwa 86 kitabu cha kiada badala ya kutayarisha tathmini. Walimu waliowapa watoto tathmini aidha walieleza kuwa waliweka rekodi ya alama za tathmini walizowapa watoto. Hata hivyo, hakuna aliyeweza kutoa nakala kuonyesha rekodi ya tathmini walizowapa watoto isipokuwa zile za mitihani ya kati na ya mwisho zilizowekwa na walimu wakuu. Bila kuweka rekodi mwafaka ni vigumu kwa mwalimu kukumbuka matatizo ya kila watoto. 3.4.2 Umuhimu wa Kuweka Rekodi za Tathmini Walimu walitakiwa kueleza jinsi wanavyotumia alama za tathmini za watoto katika kuimarisha usomaji wa sauti. Kulingana na walimu alama za watoto zinaweza kutumiwa kwa njia zifuatazo Jedwali 3.12. Matokeo haya yalionyesha kuwa walimu wengi katika madarasa yote walitumia tathmini kwa maksudi ya kubainisha maendeleo ya watoto ili kujua kama mtoto anaendelea mbele au anarudi nyuma (Jedwali 3.12). Mwalimu mmoja katika darasa la kwanza alieleza kuwa alitumia tathmini kuangalia kama daraja fulani lilimfaa mtoto. 87 J d r 312 M wr K h U h· R k die wa I . : aODIva a nnu u usu mu imu wa e 0 I Maoni Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Maendeleo ya Mtoto 3 5 6 Kumweka daraja 1 0 0 Kutambua shida 2 1 0 Mwalimu kujitathmini 1 0 1 Mwalimu alifafanua kwa kutoa mfano wa mtoto akiwa mgonjwa wakati wa mtihani wa mwisho wa mwaka; mwalimu anaweza kutumia rekodi ya alama za tathmini alizofanya awali kujua kama mtoto atakwenda darasa linalofuata ama la. Kadhalika, walimu wawili katika darasa la kwanza na mmoja katika darasa la pili walitumia kubainisha matatizo yanayowakumba watoto ili kuweza kuwapa mazoezi mwafaka. Mwalimu mmoja katika darasa la kwanza na mwingine katika darasa la tatu walitumia alama hizi kutathmini ufundishaji wao kama watoto walielewa au walikuwa na shida. 3.4.3 Asilimia ya Watoto Wenye Ufasaha Ufasaha katika swali hili ilichukuliwa kuwa ule uwezo wa mtoto kuweza kusoma maneno au sentensi bila kusitasita. Aidha, kutamka silabi moja moja ama kugusa neno au silabi wakati wa kusoma ni ishara mojawapo ya kutokuwa na ufasaha. Mbali na hayo, umumunyaji wa maneno kabla ya kulitamka neno na kutozingatia alama za uakifishaji hutinga kusoma kwa sauti. Sehemu hii inanuia kujadili makadirio ya asilimia ya watoto wenye ufasaha kama ilivyotolewa na walimu baada ya kuwafundisha kwa muda fulani. 88 Matokeo haya yanaonyesha makadirio ya asilimia ya watoto walioweza kusoma kwa ufasaha katika madarasa ya kwanza kwenye Jedwali 3.13. I1idhihirika kuwa shule tatu (Chomo, Kirwara na Gichumbu) zilikuwa na asilimia 50 na zaidi. Shule hizo zingine tatu zilikuwa na asilimia 25 au chini ya alama hizo. Hii inaashiria kuwa watoto wengi walikuwa hawajumudu ujuzi wa chini. Katika madarasa ya pili madarasa yote yalikuwa na asilimia 50 na zaidi katika usomaji. Hii ilidhihirisha maendeleo ya wastani ambapo watoto walionekana kuwa katika viwango vilivyokaribiana isipokuwa shule moja ambayo ilikuwa na asilimia kubwa ya 75. Kando na maendeleo hayo kulikuwa na watoto ambao walikuwa hawajamudu kusoma kwa ufasaha. J d r 313 M k di . U w Kr wre wa ( . : a a (no ya soma ( wa atoto u mgana na a (mu Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Shule Idadiya %ya Idadi ya %ya Idadi ya %ya watoto Usomaji watoto Usomaji watoto Usomaji Chomo 42 50 42 60 47 70 Gatura 56 25 48 50 46 75 Gatunyu 46 25 50 75 54 80 Kirwara 30 75 33 60 33 75 Rwegetha 58 20 65 50 37 50 Gichumbu 45 75 48 50 50 75 Kulingana na silabasi, watoto katika darasa la tatu huwa wameimarika katika ujuzi wa chini na huzingatia zaidi kuendeleza ujuzi wa juu wa kusoma kwa sauti na kimoyomoyo. Hii ina maana walimu huzingatia zaidi kukuza matamshi, alama za uakifisho na ufahamu wa kinachosomwa. Matokeo Jedwali 3.13 yaiionyesha kuwa 89 madarasa haya yalikuwa yameimarika zaidi katika usomaji. Hata hivyo, shule ya Rwegetha ilionyesha maendeleo ya chini ikilinganishwa na shule hizo zingine. Shule hii ilikuwa na asilimia 50 wakati madarasa mengine yalikuwa na asilimia 70 na zaidi. Ikumbukwe darasa hili lilitenganishwa katika darasa la tatu baada ya kuajiriwa kwa mwalimu mwingine. Inawezekana maendeleo ya watoto iliathiriwa na idadi kubwa ya watoto. 3.5 Uchanganuzi wa Matokeo ya Hojaji ya Walimu Katika sehemu ya 3.2 maelezo ya walimu katika hojaji yaliwasilishwa. Kutokana na maelezo yao ilidhihirika kuwa walimu waliofunza madarasa haya ya chini walikuwa wamehitimu katika ualimu. Walimu walikuwa wa mifumo tofauti wengi wao wakiwa wenye kufuzu katika mfumo wa 8-4-4. Matokeo yalionyesha kuwa mtazamo wa mwalimu kuhusu lugha ya Kiswahili ulibeba uzito kuliko mfumo aliohitimu. Hii ni kwa sababu katika mifumo yote kulikuwa na walimu ambao hawakupendelea kufundisha somo la Kiswahili. Walimu walitumia mbinu mbalimbali katika kufundisha kusoma kwa sauti. I1idhihirika kuwa walimu wa darasa la kwanza walizingatia Modeli ya Chini-Juu na kupuuza ufahamu. Katika madarasa ya pili na tatu walimu walitilia mkazo Modeli Husishi, ambapo mbinu ya silabi iliendelea kutumiwa. Hii inaonyesha kuwa walimu walitumia mikakati mbalimbali kuimarisha usomaji kwa sauti. Kulingana na majibu ya walimu kulionekana kuwa na maendeleo ya wastani katika stadi ya kusoma kwa sauti kadri watoto walivyoendelea kupanda juu. Hata hivyo, kufikia darasa la tatu, kulikuwa na watoto ambao walikuwa hawajamudu ujuzi wa chini kinyume na 90 mapendekezo ya silabasi. Jambo jingine ni kuwa, mazingara ya darasani hayakusisimua kwa sababu ya uchache na ukosefu wa ubunifu katika matumizi ya nyenzo ili kuwatia watoto ari ya kusoma. Kuna haja ya kuzingatia kitengo cha Hisi ili kuinua kiwango cha usomaji. Kulingana na maoni ya walimu walikuwa na vitabu vya kiada vya kutosha kwa matumizi ya watoto darasani. Kadhalika watoto walikuwa na vitabu zaidi ya kimoja. Vitabu vilivyotumiwa vilikuwa vya aina mbalimbali kwa mujibu ya mapendekezo ya silabasi. Aidha, kitabu 'Kiswahili Mufti'kilipendelewa na walimu wengi. Hata hivyo ilidhihirika kuwa walimu hawakuwa na vitabu vya hadithi darasani. Hii inaashiria kuwa walimu wanahitaji kuhamasishwa kuwa na maktaba darasani kama ilivyopendekezwa na silabasi. Watoto walipewa tathmini rasmi na zisizo rasmi. Alama za tathmini rasmi tu ndizo zilionekana kurekodiwa. Walimu waliohojiwa hawakuwa na rekodi zenye kuonyesha matatizo yaliyokumba mtoto binafsi. Rekodi ya tathmini inaweza kumwongoza mwalimu kujua shida za mtoto kama vile: ni kipengele kipi kinamsumbua mtoto, shida za kihisia, na maumbile. Bila kukabiliana na matatizo kwa njia ifaayo maendeleo ya mazoezi ya marudio yatakuwa yakujikokota. 3.6 Uchunguzi wa Darasani Sehemu hii ya pili ilijadili matokeo ya uchunguzi wa darasani. Maelezo yatatumiwa kuthibitisha majibu yaliyotolewa na walimu katika hojaji. Aidha mtafiti alichunguza ufundishaji wa kipindi kimoja cha kusoma katika kila darasa. Uchunguzi uliongozwa 91 na ratiba ya kukagua funzo na kurekodiwa kwa kinasa sauti. Maelezo yalitolewa katika kila kitengo cha maswali ya hojaji. 3.6.1 Aina za Vitangulizi. Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa darasani walimu watatu, wawili na wawili katika darasa la kwanza, la pili na la tatu mtawalia walitanguliza mafunzo yao kwa nyimbo. Kati ya nyimbo zilizoimbwa mbili katika darasa la kwanza na la pili zilioana na mada ya siku hiyo na zilishughulikiwa kwa dakika chache sana; watoto hawakupata nafasi ya kuchangamka. Katika darasa la tatu wimbo mmoja ulioana na mada ya funzo la siku hiyo. Aidha nyimbo hizi zilikuwa ndefu na zilionekana kuwasisimua watoto. Matokeo haya yanaafikiana na matokeo katika (Jedwali 3.4) yaliyoonyesha kuwa walimu katika madarasa haya walipendelea nyimbo kama vitangulizi ili kuwatia motisha watoto. Mbinu nyingine iliyotumiwa ilikuwa ya kukariri silabi. Walimu wawili darasa la kwanza, mmoja katika darasa la pili walitumia mbinu hii ambayo waliambatanisha na ama kadi au chati kabla ya kuanza kusoma. Mbinu nyingine zilizotumika ni kama vile; kusoma maneno ubaoni mwalimu mmoja, kuchanua picha walimu watatu, na kueleza maana ya msamiati walimu wawili; darasa la kwanza, la pili na la tatu mtawalia. Matokeo ya uchunguzi yalidhihirisha ukosefu wa ubunifu katika vitangulizi vilivyotumiwa darasani na walimu. Walimu walitarajiwa kubadilisha badilisha vitangulizi ili kuwafanya watoto kuwa wasikivu kwa mujibu wa Kitengo cha Hisi. 92 Pengine walimu hawakuwa na wakati wa kutosha wa kujiandaa kwa sababu ya kazi nyingi ikichukuliwa kuwa walihitajika kufunza masomo yote. 3.6.2 Mbinu za Kufundishia Majibu ya walimu katika hojaji yalionyesha kuwa walimu hawakupendelea mbinu ya abjedi. Mbinu ya silabi ilionekana kupendelewa na walimu wote na walitumia katika madarasa yote (Jedwali 3.5). Katika uchunguzi wa darasani mbinu ya abjedi na kutamka herufi zilishirikishwa katika matumizi ya mbinu ya silabi. Hii ni kwa sababu wakati wa kufundisha silabi waliwaongoza watoto kusoma kila herufi kwanza kabla ya kusoma silabi ili kuweza kupambanua herufi. Katika ufundishaji wa watoto darasa la kwanza, walimu wanne walitumia Ll kufafanua maelezo wakati wa kufunza kusoma katika lugha ya Kiswahili. Walimu walieleza kuwa hii ndiyo lugha waliyozoea kwa mawasiliano. Walimu wote walitumia mbinu ya silabi katika ufundishaji tofauti i1ikuwa katika namna walivyowasilisha funzo. Kuna walimu ambao walitayarisha silabi kwenye kadi na kuwaongoza watoto kuzisoma. Kwa mfano mwalimu mmoja alipitia kadi zenye silabi 'sa, se, si, so, su' na kisha kuziandika ubaoni zikiwa zimechanganywa. Watoto walisoma silabi hizi kipindi kizima bila kuunda maneno. Watoto walionekana kukosa usikivu na wengine kuanza kupiga kelele kufikia mwisho wa kipindi. Matokeo haya yanaafikiana na Kitengo cha Hisi ambacho kinaeleza umuhimu wa mwalimu kuwa na ubunifu ili kudumisha usikivu wa watoto katika kipindi kizima. Walimu wanne waliwaongoza watoto kusoma silabi wakitumia ama silabi kwenye kadi au chati. Baadaye walimu waliongoza watoto kuunda maneno na kuyaandika ubaoni na kisha 93 wakasoma sentensi fupi. Mwalimu mmoja kwa mfano aliandika sentensi zifuatazo kwenye ubao: 1. Dada amevaa vazi lake. 2. Mvuvi anavua samaki 3. Bibi arusi amevaa veli 4. Tunasoma vokali a e i ° u. Mwalimu mwingine alianza kwa kuandika majina ya wanyama ubaoni na kuyapitia pamoja na watoto bila kutumia nyenzo. Hata hivyo, katika kusoma aliwaongoza watoto kutamka kila silabi katika neno kabla ya kusoma neno nzima. Usomaji ulijikita katika kuwaongoza watoto kupambanua herufi na silabi wakati wa kusoma kwa sauti. Kusoma kulilenga zaidi kumudu silabi wala si ufahamu. Aidha, walimu walizingatia ujuzi wa chini kama inavyobainishwa na Modeli ya Chini-Juu. Walimu katika madarasa ya kwanza, pili na tatu waliotumia mbinu ya silabi walianza kwa kutaja herufi zinazounda silabi kama inavyoonyeshwa (Jedwali 3.14). Jedwali 3.14: Namna Walimu Walivyofundisha Silabi Silabi Uwasilishaji Sa Esi na 'a' ya Kiswahili Va Vii na 'a' ya Kiingereza Ki Kei na ai Cha Sii na 'h' ya kiingereza na a' ya Kiswahihi Ng'o Eni na 'g' ya ; kangongo na 'a' ya; Mbe Emu na 'b'ya Kiingereza na 'e'ya ; 94 Katika usomaji kuna watoto waiiokanganywa na silabi 'nga' na 'nja'. Hii ni kwa sababu ya jinsi fonimu /g1 na /j/ zilivyotamkwa mara kwa Kiswahili mara kwa Kiingereza. Wengine baada ya kutambua kila herufi walishindwa kuzishikanisha na kusoma silabi yenyewe badala yake walisoma vokali iiiyounda silabi ile kwa mfano ikiwa ni 'cha' walisoma kama 'a', oche' kama 'e'. Pengine kule kutamka silabi mara kutaja herufi zenyewe kwa Kiingereza mara kwa Kiswahili kuliwatatiza watoto katika kukumbuka herufi. Kadhalika uchunguzi ulionyesha kulikuwa na watoto wachache ambao waliweza kupambanua silabi na kusoma maneno mafupi. Watoto wengi katika darasa la kwanza walionekana kuwa na matatizo ya kutambua ama herufi au silabi. Baadhi ya watoto walisoma herufi lakini wakashindwa kushikanisha herufi zilizounda silabi. Wengine walisoma silabi lakini wakashindwa kuunganisha maneno yenye zaidi ya silabi mbili kama vile 'mawili', 'maandazi' n.k. Watoto wengine walionekana kusoma silabi za herufi mbili kwa urahisi zaidi ikilinganishwa na kusoma silabi zenye herufijozi kama vile 'cha, sha, nga, nja, bwa.' Kulikuwa na haja ya kuzingatia Kitengo cha Utaratibu wa Kiasili ili kukuza hamu katika stadi ya kusoma. Hii pia inaashiria umuhimu wa uteuzi wa makala ya kusoma. Kadhalika watoto walipokuwa wakisoma ama silabi au maneno waliyagusa kwa kidole. Isitoshe, kulikuwa walimu ambao walikuwa na matatizo ya matamshi na ilikuwa vigumu kwao kusahihisha watoto athari za Ll. Ilidhihirika kuwepo walimu wengine ambao aghalabu walijaribu kuepuka kuwaongoza watoto kutamka maneno. Ikumbukwe katika ufunzaji wa sifa bainifu za kusoma kwa sauti watoto wanahitaji kuiga usemi wa mwalimu. 95 - Katika darasa la pili walimu watatu walitumia mbinu ya silabi kabla ya kusoma maneno au makala kwenye kitabu cha kiada. Pia katika madarasa ambapo silabi hazikufunzwa kulikuwemo chati au sehemu ya ubaoni iliyotengwa na kuandikwa silabi. Hii iliashiria kuwa walimu wakati mwingine walirejelea mbinu ya silabi kama ilivyoonyeshwa katika Jedwali 3.4. Kadhalika, ilidhihirika wakati wa kusoma makala, baadhi ya watoto waliochaguliwa kusoma kifungu, walisikika wakitamka silabi moja moja. Hii iiionyesha kuwa kulikuwa na watoto ambao walikuwa bado kumudu silabi. Matokeo haya yalidhihirisha kuwa mbinu changamano zilitumiwa katika darasa la pili. Hii ilimaanisha kuwa ujuzi wa chini na ujuzi wajuu ulishirikishwa na walimu ili kujenga na kukuza utambuzi na uelewa wa kile kinachosomwa. Modeli Husishi inaeleza umuhimu wa kutumia mbinu changamano ili kuibua hamu ya kusoma. Aidha makala yanayovutia huweza kusisimua watoto na kujenga usikivu badala ya ukariri wa silabi na maneno yasiyo na maana. Walimu wawili katika darasa la tatu walitumia mbinu ya silabi. Walimu walitumia silabi zenye herufujozi kama vile 'cha, mbe nga ng'a tha, ,bwa, nda,ngwa, njwa. Hii inaashiria kukua kwa kiwango cha usomaji cha watoto kwa mujibu wa Kitengo cha Utaratibu wa Kiasili. Baadaye, walimu waliwaongoza watoto kuunda maneno yenye silabi hizo. Mwishoni, waliwapa watoto mazoezi ya imla. Walimu wengine wanne waliwapa watoto kifungu cha habari kusoma ambapo wawili waliwauliza watoto kusoma kwa pamoja kifungu. Baadaye waliwachagua watoto wachache kusoma aya au sentensi chache kwenye kifungu. Aghalabu kuna watoto waliosoma kwa ufasaha lakini kuna wengine waliotamka silabi moja moja huku wakigusa kwa kidole kila 96 neno na kwa mwendo wa kujikokota. Aidha, ilikuwa vigumu kupata maana ya kile kinachosomwa. Matokeo haya yanaafikiana na majibu ya walimu (Jedwali 3.4) kuwa kulikuwa na watoto ambao walikuwa hawajamudu ujuzi wa kiwango cha chini. Watoto waliofanya mazoezi ya imla, wengi walifanya makosa aina mbalimbali. Baadhi ya daftari chache ambazo zilikusanywa kutoka katika darasa moja la tatu makosa yanaonyeshwa (Jedwali 3.15). Jedwali 3.15: Namna Watoto Walivyoendeleza Maneno Katika Imla Neno Sahihi Neno lilivyoendelezwa Mayai oyai, mayi, mae Wazazi asase, cana, uiboi, wnsi Chochote okoke, ketoa, yoye, yoyote Matokeo yalionyesha kuwa watoto walikuwa hawajamudu ujuzi wa chini wa kusoma. Hii ni kwa sababu walishindwa kuendeleza maneno mepesi waliyosomewa. Kando na hayo, mwalimu aliyesoma zoezi la imla aliwapa watoto muda mrefu kati ya maneno na kurudia neno zaidi ya mara tatu kama inavyohitaj ika katika zoezi la imla. Hata hivyo, ilionekana watoto wengi walishindwa kupambanua sauti walizosikia. Kwa hivyo, mbali na kushirikisha mbinu za ujuzi wa chini na ujuzi wa juu katika kusoma kulikuwa haja ya walimu kutathmini uwasiiishaji wao wa stadi ya kusoma. Matokeo haya hayaafikiani na malengo ya kusoma katika darasa la tatu kwenye silabasi (K.I.E., 2002). Silabasi ilichukulia kwamba tayari watoto walikuwa 97 wamemudu silabi na herufi za Kiswahili. Malengo katika darasa hili yalifaa kuzingatia ujuzi wa juu, kusoma kwa ufasaha na ufahamu wa habari. 3.6.3 Mpangilio wa Darasani Maelezo yafuatayo yanaonyesha namna watoto walivyoketi darasani, usomaji ulivyotekelezwa na mazingara ya darasani yalivyoathiri ufunzaji. Kulingana na majibu ya walimu kwenye hojaji yalionyesha kuwa walimu walitumia mitindo tofauti kutekeleza ufunzaji wa kusoma kwa sauti darasani. Matokeo ya uchunguzi darasani hayaafikiani na maelezo ya walimu katika Jedwali 3.7 yaliyoonyesha kuwa walimu waliwaongoza watoto kusoma kwa kutumia mitindo mbalimbali kama darasa lote, kusoma mtoto mmoja mmoja kwa zamu na kusoma katika makundi. Uchunguzi wa darasani ulithibitisha kuwa watoto katika madarasa ya kwanza na ya pili waliwekwa katika makundi. Mpangilio wa makundi ulijikita katika safu aghalabu matatu na manne ambapo madarasa yalikuwa na watoto wengi. Safu zilipangwa kulingana na uwezo wa watoto, wenye uwezo, uwezo wastani na uwezo wa chini. Katika safu lenye watoto wenye uwezo aghalabu hawakujaza safu nzima walilotengewa kwa sababu watoto wachache walikuwa wamemudu ujuzi wa chini. Watoto wachache wenye uwezo wa kusoma aghalabu waliwekwa mbele katika safu walilotengewa kisha watoto wengine wenye uwezo wa wastani waliingizwa kujaza nafasi zilizobaki. Hii ni kwa sababu wakati wa kusoma, sauti ilisikika kutoka sehemu ya mbele mara ya kwanza lakini wakati wa kurudia mara ya pili silabi, neno au 98 sentensi iliyosomwa, watoto wengi zaidi walishiriki kusoma. Hii ina maana kuwa watoto wengi walikuwa wakiiga sauti walizosikia tu. Vile vile kuna walimu ambao walionekana kutazama upande fulani kila wakati wa kuwaongoza watoto kusoma na hata wakati wa kuchagua mtoto mmoja mmoja kusoma Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa darasani matumizi ya mtindo wa kusoma darasa lote ulikithiri katika madarasa yote ya kwanza, ya pili na ya tatu. Huu ulifuatwa na ule wa makundi kisha wa kusoma mtoto mmoja mmoja uliotengewa muda mfupi. Kadhalika, ilidhihirika kuwa ingawa watoto walikuwa na uwezo tofauti walipewa kazi iliyofanana kutoka kwa kitabu cha kiada. Yamkini, shughuli ya kufanya kazi ilionekana kuchukua muda kuwaelekeza watoto kwenye safu kwa sababu ilibidi mwalimu kwenda kwa kila dawati kuwaelekeza na kusahihisha makosa ya watoto. Pengine dawati zingepangwa kwa njia ya kuwawezesha watoto kukaa katika makundi. Hii ingewezesha mwalimu kuwaelekeza kwa urahisi watoto wenye uwezo tofauti kwa pamoja. Matokeo ya uchunguzi katika darasa la tatu yalidhihirisha kuwa watoto hawakuwekwa katika makundi kulingana na uwezo wao bali walichanganywa kama ilivyoonyeshwa katika Jedwali 3.7. Walimu wanne waliwaongoza watoto kusoma makala au sentensi kama darasa lote. Hii ilikuwa kinyume na maelezo ya walimu katika Jedwali 3.7. Aidha kuna mwalimu mmoja alitumia mtindo wa mtoto mmoja mmoja kusoma. Yamkini, kuna watoto waliosoma kwa ufasaha na wakizingatia uakifisho bila kugusa 99 maneno kwa kidole. Hata hivyo, kulikuwa na watoto wengine ambao waligusa ama kila neno au silabi waliyosoma kwa mwendo wa kujikokota bila kufuata uakifisho. Wengine walimumunya silabi kisha kutamka silabi moja moja kwenye neno. Pia, kulikuwa na watoto ambao walikuwa na matatizo ya kusoma neno ndefu. Mwalimu mwingine aliwaongoza watoto kusoma kimya makala kwenye kitabu cha kiada kinyume na matokeo katika Jedwali 3.7 yaliyoonyesha hakuna mwalimu aliyetumia mtindo huu wakati wa kusoma kwa sauti. Hata hivyo, wakati wa kusoma kulikuwa na kelele kingi sana. Hii ina maana kuwa watoto wengi walikuwa hawajamudu silabi kwa hivyo iliwabidi kumumunya kwanza silabi au maneno wakati wakusoma. Kadhalika, walimu hawakutilia mkazo baadhi ya vipengele muhimu kama vile; matamshi, uakifisho na ufasaha katika kukuza ujuzi wajuu wa kusoma. Matokeo haya hayaafikiani na maelezo ya walimu katika Jedwali 3.5. Kulingana na silabasi watoto katika darasa hili walichukuliwa kuwa wamemudu kusoma, ilidhihirika kuwa watoto wengi wakati wa kusoma hawakuzingatia uakifisho. Ufasaha unajitokeza ambapo watoto wamemudu silabi, wanasoma kwa mwendo wa wastani na wanazingatia alama za uakifisho. Ilionekana kuwa walimu walizingatia zaidi Modeli ya Chini-juu. 3.6.4 Mazingara ya Darasani Sehemu hii inaelezea kuhusu mazingara ya shule na darasani kama yalikuwa ama ya kusisimua au la. Aidha, iliangazia aina ya mbinu na nyenzo zilizotumiwa na walimu na hali ya watoto wakati wa ufunzaji. 100 Uchunguzi ulionyesha kuwa kulikuwa na madarasa matatu, manne na mawili katika darasa la kwanza, la pili na la tatu mtawalia ambayo yalikuwa na nyenzo nyingi kwenye ukuta. Baadhi ya madarasa yalipanga nyenzo kulingana na masomo. Kuhusiana na mradi wa darasani, madarasa matatu, mawili katika darasa la kwanza, la pili na la tatu mtawalia yalikuwa na mradi wa darasani kinyume na mapendekezo ya silabasi. Yamkini darasa moja katika darasa la pili na lingine darasa la tatu yalikuwa na walimu waliokuwa wakifanya mazoezi ya kufundisha. Pengine, ndio sababu walionekana kuzingatia mapendekezo ya silabasi. Madarasa hayo mengine yalikuwa na chati chache, kuukuu na zilizolegea na zilikosa mradi wa darasani. Mazingara kama haya hayawezi kusisimua usomaji kulingana na Kitengo cha Hisi. Kwa kuhitimisha ilionekana kuna shule ambazo zilifuata mapendekezo ya silabasi ingawa hayakuwa na walimu waliokuwa wakitahiniwa. Rata hivyo, matokeo yalionyesha upungufu wa nyenzo katika madarasa yote. Pia ubunifu ulikosekana katika utayarishaji wa nyenzo. Aidha ilidhihirika uhifadhi mbaya wa chati darasani. Hii inaonyesha kuwa walimu hawakutilia maanani umuhimu wa kuwa na mazingara darasani yenye kuamsha hamu ya kusoma kwa mujibu wa Kitengo cha Hisi. 3.6.5 Aina ya Vitabu Watoto katika darasa la kwanza hawakutumia Kiswahili Mufti kamma walimu walivyokuwa wamesema. Mgao wa vitabu darasani ulikuwa kama walimu walivyosema katika Jedwali 3.9. Katika uchunguzi watoto ambao walikuwa na kitabu kimoja kati ya watatu au wanne walionekana kutatizika zaidi kwa sababu haikuwa rahisi kwa watoto wote kukifikia kitabu kikiwekwa katikati. Baadhi ya watoto 101 walisoma kwa mwendo wa kasi kuliko wengine jambo ambalo lilitatiza wenye kusoma kwa kutamka kila silabi polepole. Kwa hivyo, walibaki kumumunya maneno na kujaribu kufikia wanaosoma kwa kasi. Isitoshe, kuna waliogusa maneno kwa kidole hivyo kuzuia wengine kusoma hasa tukichukulia kuwa watoto hawa walikuwa na uwezo tofauti. Kitengo cha Uteuzi wa Makala kinasisitiza kuzingatia uwezo wa mtoto katika uchaguzi wa kifungu. Hii inaweza kufanikiwa ikiwa watoto watawekwa katika makundi na kupewa makala aina mbalimbali kusoma. 3.6.6 Tathmini Tathmini zilichukuliwa kama mazoezi ambayo watoto walipewa darasani na walimu. Kuna walimu waliowapa watoto zoezi kutoka kwa kitabu cha kiada. Wengine walikuwa wametayarisha kazi ya kuwapa watoto kwa mfano zoezi la imla na maswali ya ufahamu yaliyotarajiwa kujibiwa kwa mdomo. Aidha mifano ya tathmini rasmi katika kila darasa zimeonyeshwa (Kiambatisho 3,4,5). Katika darasa la kwanza baadhi ya walimu walitumia silabi kwenye kadi kuunda maneno. Mtoto mmoja mmoja alichaguliwa kusoma neno lililoundwa. Kuna wengine waliochanganya kadi zenye silabi kisha mtoto kuchaguliwa kusoma ili kuonyesha kama anaweza ama kutambua herufi na silabi au kukariri bila kufahamu. Kuna watoto ambao walionekana kuwa na matatizo ya kutambua silabi ama walisoma vokali na kushindwa kusoma herufi ya konsonanti au kushindwa kabisa kusoma silabi waliyopewa. 102 Kuna walimu wengine ambao waliwapa watoto mazoezi kwenye kitabu kama vile kusoma sentensi fupi ambazo ziliambatanishwa na picha. Kwa mfano mwalimu mmoja aliwapa watoto zoezi kutoka kitabu cha Kiswahili Mufti, darasa la kwanza, uk.75. Huyu ni mbuzi Huyu ni ng'ombe Ninamwona ngamia Mbwa anabweka Kadhalika, walipewa zoezi ambapo silabi fulani ziliambatanishwa na picha zenye kuchukua silabi iliyofundishwa. Kwa mfano picha zenye kuchukua silabi 'cha'kama vile: chupa, cheti, chini, choma, na chana. Picha zilitakiwa kusaidia watoto kutambua neno lililoandikwa chini yake. Hata hivyo, watoto wengine walisoma picha wala si maandishi kwa mfano; kusoma 'kitabu' badala ya 'cheti' au badala ya 'choma' anasoma 'samaki' anayechomwa. Mazoezi ambayo watoto walipewa katika darasa la pili na la tatu yalikuwa zaidi ya kupima ufahamu. Kwa mfano, katika darasa la pili watoto walipewa zoezi la kuandika majina ya picha walizopewa. Mazoezi mengine yalikuwa kuchanganua picha zilizoambatana na makala, kusoma makala, kujibu maswali kwa mdomo na kisha kufanya zoezi kwenye daftari zao. Aidha, kulikuwa na watoto waliotatizika kuandika majibu katika daftari zao. Watoto wengi walikuwa na hati mbaya na wengine walishindwa kutenganisha maneno katika sentensi walizoandika. lsitoshe, kuna mwalimu mmoja aliyepitia majibu ya maswali yote kabla ya kuwapa watoto zoezi katika darasa la pili. Mwalimu huyu alieleza kuwa asipoyapitia maswali na majibu yake, watoto wengi watashindwa kupata majibu sahihi. Katika darasa la tatu, kwa 103 mfano kuna baadhi ya watoto katika darasa moja waliopewa zoezi lakini idadi kubwa ya watoto walikuwa na matatizo ya kuandika majibu. Yamkini jumla ya watoto kumi na saba walichukua muda kufikia swali la pili katika zoezi ambalo lilikuwa na maswali manne tu. Kuna watoto wawili ambao walishindwa kabisa kuanza zoezi. Aidha, kulikuwa na watoto watatu wenye akili punguani darasani. Aidha katika darasa.la tatu kulitokea aina tofauti ya mazoezi yaliyofanywa na watoto. Kwa mfano kuna walimu wawili ambao walifunza msamiati kisha wakawapa watoto zoezi la imla. Hii ilionyesha kuwa watoto hawa walikuwa wamemudu silabi na kwa hivyo wangeweza kuendeleza maneno kwa usahihi. Kwa mfano zoezi lililopewa watoto (Jedwali 3.16). J d r 316 N W t t w r dika K tik Z . I I lae wa I . : amna aoo a rvyoan I a I a oezi a m Neno sahihi Lilivyoendelezwa Chakula Chakura, Caklor, chakala, uguu, chii Ng'ombe Ngomde, Ngobo,nyombe, Thelathini Thethethini, Theranini, Therathini Maembe Maebe,coma, maende,mesui Chura Chula, unsim,guiru Lakini matokeo ya zoezi yalidhihirisha kuwa kulikuwa na watoto wengi katika darasa hili la tatu ambao hawakuwa wamemudu silabi za Kiswahili. Pengine kule kuwapa watoto wote tathmini zilizofanana kuliwatamausha wenye uwezo wa chini. Kulingana na Kitengo cha Hisi ni vizuri walimu kuzingatia hisi za watoto katika shughuli zote darasani. 104 3.7 Uchanganuzi wa Matokeo ya Uchunguzi wa Darasani Kwa mujbu wa matokeo ya uchunguzi wa darasani ilidhihirisha kuwa mbinu ya silabi ilikanganya watoto. Walimu watumia mbinu ama ya abjedi au kutamka sauti ambapo watoto walitambua herufi za silabi kabla ya kuzishikanisha. Watoto wengi walitambua herufi lakini walishindwa kusoma silabi katika madarasa ya kwanza na ya pili. Vilevile watoto walibahatisha kusoma na kuiga wengine. Hizi ni ishara za watoto ambao walikuwa hawajamudu silabi. Kutokana na mbinu hii watoto waliendelelea kusoma kwa kugusa silabi na kutamka silabi wakati wa kusoma. Hii ili sababisha watoto kusoma kwa mwendo wa kujikokota. Hata hivyo, idadi ya watoto wenye shida ya kupambanua silabi ilipungua kadri walivyoendelea katika madarasa yajuu. Utekelezaji wa ufundishaji wa kusoma ulionyesha kuwa walimu katika madarasa yote walimu walipendelea watoto kusoma darasa lote kinyume na walivyosema katika hojaji kuwa walitumia mtindo wa mtoto mmoja mmoja. Kulikuwa kwa hakika hakuna makosa kutumia mtindo wowote ule bora tu mwalimu achanganye mitindo tofauti ili wanafunzi wasichoke. Pengine walitumia mtindo huu kwa sababu kwa njia hii ilikuwa rahisi kuficha udhaifu wa watoto. Aidha, kuna haja ya kusisimua hisi za watoto katika ufunzaji kwa mujibu wa Kitengo cha Hisi. Kadhalika ilidhihirika kuwa makundi katika madarasa ya kwanza na ya pili yalipangwa kisafu. Hii ilifanya ufunzaji wa makundi kuwa mgumu. Darasa la tatu watoto walikuwa wamechanganywa. Matokeo ya uchunguzi wa darasani yalionyesha kuwa watoto walikuwa na matatizo mengi ya kusoma kwa sauti katika darasa la tatu. Aidha, kuna watoto wengine walioshindwa kusoma kabisa. Kwa mujibu wa Kitengo cha Kiasili watoto wanafaa kuimarika katika kiwango kimoja kabla ya kuingia kiwango kinachofuata. 105 Kulingana na matokeo ya nyanjani, kulikuwa na vitabu vya kiada vya aina mbalimbali. Walimu walieleza kuwa watoto walikuwa na vitabu vya kutosha. Hata hivyo, kwa sababu ya kiwango cha chini katika ujuzi wa kusoma ilikuwa vigumu kwa watoto kutumia kitabu kimoja wakiwa watatu au wanne. Hii ni kwa sababu kuna watoto waliokuwa hawajumudu silabi kwa hivyo waligusa kwa kidole silabi au neno wakati wa kusoma makala waliyopewa. Aidha, kuna haja ya walimu kuzingatia urefu na ugumu wa makala kulingana na uwezo wa watoto wakati wa kusoma darasani ili kuimarisha kusoma kwa sauti. Watoto walipewa mazoezi kufanya baada ya mada waliyosoma. Kuna walimu ambao walichukulia mazoezi haya yalitosha watoto kutathmini maendeleo ya watoto darasani. Kando na mazoezi ya darasani kulikuwa na tathmini rasmi ambazo zilifanywa katikati na mwisho wa muhula. Mazoezi yalidhihirisha kuwa kulikuwa na watoto ambao katika madarasa yote ambao hawakuelewa mambo ya kimsingi katika usomaji. Hii ina maana kuwa kuna haja ya walimu kutayarisha mazoezi mwafaka yanayolenga matatizo ya watoto binafs mbali na yaliyomo vitabuni vya kiada. Mazingara ya darasani hayakuvutia hata kidogo. Ilionekana kutokana na majibu ya walimu kuwa walikosa ubunifu katika vitangulizi walivyotumia darasani. Katika madarasa mengine nyenzo zilikuwa chache na kuu kuu. Hali hii ilionyesha kuwa nyenzo chache zilitumika katika ufundishaji kwa sababu inachukuliwa kuwa mwalimu baada ya kutumia kwa mfano chati, picha anafaa kuzibandika kwenye ukuta kwa muda. Ilibainika kadri watoto walivyoendelea nyenzo zilipungua kwa asilimia kubwa. Kadhalika walimu walitumia vitangulizi aina moja kila wakati. Kando na 106 hayo, kuna shule moja ambayo madarasa yalikuwa machafu sana. Mazingara kama haya hayawezi kusisimua usomaj i. Muhtasari Sura hii imeangazia matokeo ya utafiti huu. Tumeshughulikia maelezo ya walimu kuhusu vipengele muhimu katika ufundishaji wa kusoma kwa sauti. Tumejadili mbinu, vitangulizi, nyenzo, mitindo ya usomaji, vitabu na aina ya tathmini ambazo walimua walitumia kufanikisha usomaji kwa sauti. Imedhihirika matatizo mbalimbali katika utekelezaji wa kusoma ambao ulichangiwa na mambo tofauti. Mambo kama vile idadi ya watoto, mtazamo wa walimu, mbinu zenye kukanganya, mazingara yasiyovutia, makala yasiyoafikiana na uwezo wa watoto, na tathmini zisizotosheleza. Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa mambo haya ni muhimu kuzingatiwa katika kufanikisha usomaji. Hata hivyo, kulikuwa na mafanikio ya wastani katika usomaji. Maoni yetu ni kuwa athari hizi zikipunguzwa maendeleo ya kusoma itainuka zaidi. Mjadala wa matatizo ya kusoma pamoja na matokeo ya ukusanyaji data utajadiliwa katika sura itakayofuata. 107 SURA YA NNE: MATATIZO YANAYOWAKABILI WATOTO KATlKA UJIFUNZAJI WA KUSOMA 4.0 Utangulizi Sura iliyotangulia tumeshughulikia maoni ya walimu katika hojaji kuhusiana na ufundishaji wa kusoma kwa sauti. Matokeo yalionyesha kuwa walimu walitumia mikakati mbalimbali katika kutekeleza stadi ya kusoma kwa sauti. Kadhalika matokeo ya uchunguzi wa darasani yamejadiliwa. Matokeo ya utafiti wetu njanjani umeonyesha kuwa kulikuwa na changamoto tofauti katika utekelezaji wa stadi ya kusoma kwa sauti. Tafiti nyingi zimefanywa kuhusiana na usomaji. Tafiti hizi zinaonyesha kuwa watoto wengi baada ya kusaidiwa huweza kusoma. Hata hivyo, idadi kubwa ya watoto hawa hushindwa kusoma kwa ufasaha au kwa usahihi. Walimu katika shule hujua watoto wenye matatizo na aina ya matatizo waliyonayo. Lakini tatizo huwa ni kujua chanzo na/au kisababishi cha matatizo yale. Kwa hivyo, itakuwa rahisi kwa walimu kuwasaidia watoto iwezekanavyo wakijua baadhi ya mambo ambayo huchangia matatizo yale. Aidha, itawawezesha kuandaa mazoezi mwafaka ya kuwasaidia watoto. Wataalamu wengi wanashikilia kuwa hakuna jambo moja bali ni mwingiliano wa mambo mbalimbali ambayo huchangia katika matatizo ya kusoma ya watoto. Sababu kadhaa zinatolewa na wataalamu kama vile Moyle (1968), Homer (1974) na Hughes (1975), miongoni mwa wengine. Baadhi ya mambo yanayoathiri usomaji yanahusiana na akili, mazingara ya nyumbani na/au shuleni, kihisia na kimaumbile. Mojawapo ya matatizo ambayo huwakumba watoto hawa ni kama kubainisha maumbo ya sauti na 108 sauti zake. Lakini, hivyo si kusema kuwa watoto hawa hawawezi kujua kusoma. Wanachohitaji ni mazoezi mengi ya kuwatayarisha katika kusoma, subira na motisha kutoka kwa walimu wao. Katika sura hii tunajadili matatizo ambayo yanajitokeza katika ujifunzaji wa kusoma katika kila kiwango kutoka darasa la kwanza hadi la tatu kwa mujibu wa maelezo ya walimu. Aidha walimu sita katika kila kiwango katika shule sita walihojiwa. Uchunguzi wa darasani ulifanywa, matokeo yake yalitumiwa kuthibitisha baadhi ya maelezo yaliyotolewa na walimu. Kadhalika, walimu walitarajiwa kueleza namna walivyokabiliana na matatizo hayo. Matokeo ya majibu ya walimu yamewasilishwa na kuelezewa. Kando na maelezo ya walimu, uchanganuzi wa maelezo ya walimu yametolewa huku yakilinganishwa na baadhi ya maelezo ya wataalamu kuhusiana na stadi ya kusoma. Sura hii ina sehemu mbili kuu. Sehemu ya kwanza ni kuwasilisha na kuchanganua maelezo ya walimu. Pili, ni kuwasilisha na kuchanganua njia walizotumia kutatua matatizo ya kusoma. 4.1 Matatizo katika Darasa la 1 Walimu walinuiwa kueleza matatizo yaliyowakumba watoto katika stadi. ya kusoma kwa sauti. Matokeo yanaonyeshwa Jedwali 4.1 ambapo matatizo yaliyowakumba watoto yanajadiliwa. 109 Jd 1"41 Mtf K k W t t D I 1e wa I . : a a IZO ya usoma wa aoo arasa a Matatizo Idadi ya walimu wenye fikira hii Shule ya malezi 2 Athari ya L1 1 Kutambua silabi 4 Kushindwa kushikanisha silabi 2 Kupindua silabi katika neno 1 Lugha zaidi ya moja 2 Kusoma maandishi -kitabu 1 Mazingara ya nyumbani 2 Kueleza picha si kusoma 1 Sehemu inayofuata itaangazia matatizo yaliyowakumba watoto katika ujifunzaji wa stadi ya kusoma kwa sauti. Baadhi ya walimu walitaja zaidi ya tatizo moja. Shule za Malezi Walimu wawili walieleza kuwa watoto hawakutayarishwa vizuri katika shule za malezi ili kukabili mambo ya darasa la kwanza. Waliongezea kuwa watoto walifunzwa alfabeti pekee na hesabu rahisi katika kuwatayarisha kuingia shule za msingi. Kadhalika walimu hawa walitumia L1 katika kuwafundisha watoto. Kutokana na mazingara ya watoto, lugha ya Kigikuyu ndiyo iliyotumiwa kwa mawasiliano nyumbani na shuleni. Lugha ya kwanza kwa mujibu wa wizara ya elimu ndiyo hutumiwa kama lugha ya kufundishia masomo yote isipokuwa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza katika madarasa ya chini. Kwa hivyo, watoto walipoingia katika darasa la kwanza walikanganywa na lugha mbili mpya. Pia, walieleza kuwa 110 walimu wengi waliofunza watoto katika shule za malezi walikuwa hawajahitimu kuwafundisha. Utafiti huu ulithibitisha kuwa aghalabu shule zilizotembelewa zilikuwa zimetenga sehemu au madarasa kwa matumizi ya shule ya malezi. Hii inamaanisha kuwa watoto wengi waliokuwa darasa la kwanza walisomea katika shule za malezi. Inachukuliwa kuwa watoto hawa walikuwa wametayarishwa kuingia darasa la kwanza. Moyle (1968) anasema kuwa watoto wengi huwa wameimarika katika mambo yanayohusiana na kusikia na kuona wanapoingia shule za msingi. Hii ina maanisha walimu wengi wa shule za msingi walichukulia kuwa watoto wote walikuwa wameimarika katika mambo ya kimsingi yanayohusiana na kusoma. Hata hivyo, utafiti umeonyesha kuwa watoto walikuwa bado hawajaimarika na walihitaji mazoezi ya kimsingi. Kwa mujibu wa Hughes (1978) mtoto anahitaji msamiati kiasi na uwezo wa kutumia lugha simulizi kabla ya kujifunza kusoma. Kama ilivyoonekana watoto kwa sababu hawakuelewa lugha ya Kiswahili ilibidi walimu kuwasiliana na watoto kwa Ll. Uchunguzi wa njanyani ulithibitisha kuwa katika baadhi ya shule walimu walitumia L1 hata katika shughuli za gwaride. Athari za Lugha ya Kwanza Mwalimu mmoja alitaja matatizo ya athari ya Ll , Uchunguzi wa darasani ulithibitisha kuwa watoto wengi walikuwa na matatizo haya kinyume na inavyodhihirika kwenye (jedwali 4.1). Mbali na watoto walimu wengi walionekana kuwa na matatizo ya kutamka baadhi ya vitamkwa kama vile l/r, flv na uchopekaji au udondoshaji wa sauti za vingo'ngo Imf na In!. Jedwali 4.2 linaonyesha baadhi ya vitamkwa vilivyowatatiza watoto. Vitamkwa vyenye makosa vimepigiwa mstari. 111 Jd r42M y r W t t D I 1e wa I .. aneno a iyosomwa na aoo arasa a Maneno sahihi Maneno yasiyo sahihi Mawili Mawirj Maandazi Maandathi Anavua Anafua Chura Chula Kondoo Kodo Mbuzi ~u~i, ~uzi Ng'ombe Ng'obe Kutokana na mifano iliyotolewa ni dhahiri kuwa LI iliathiri matamshi ya baadhi ya maneno. Watoto walikanganywa na vitamkwa 11/ badala yake wakaweka Ir/, Ivl badala yake IfI, IzI bad ala yake Ithi/. Aidha, watoto walikuwa na matatizo ya kutamka sauti ya ving'ong'o ambapo vilitumika katika silabi zenye herufijozi. Watoto waliviondoa vitamkwa hivyo kama inavyodhihirika hapo juu kwa mfano jina 'ng'ombe'likatamkwa 'ng'obe'. Kadhalika watoto walikuwa na matatizo ya kutamka maneno yaliyokuwa na mfuatano wa vokali aghalabu vokali moja iliondolewa kwa mfano neno 'kondoo' lilitamkwa kama 'kodo'. Kuna mwalimu mmoja ambaye alitaja kuwa matatizo mengine ya matamshi yalisababishwa na kung'olewa meno kwa watoto katika umri huu, hivyo ikawa tatizo kutamka vitamkwa ambavyo mahali pa kutamkia ni ufizi/meno. Tena, walimu wanne kati ya sita walitaja kuwa watoto walikuwa na matatizo ya kutambua silabi. Watoto walishindwa kubainisha vitamkwa walivyopewa. Kutokana na uchunguzi wa darasani ilidhihirika kuwa kuna watoto wengi ambao waliweza 112 ma, me, mi, mo, mu badala yake walisoma cha,che,chi,cho,chu ka, ke, ki, ko, ku a, e, i, 0, u kutambua vokali ' a, e, i, 0, u' lakini wengi walikuwa na matatizo ambapo walipewa silabi kusoma. Kwa mfano walipoulizwa kusoma silabi zifuatazo: a, e, i, 0, u a, e, i, 0, u Kuna walimu ambao walitumia kadi zenye silabi kufundishia silabi. Mwalimu aliwaonyesha watoto kadi na kuwauliza watoto kusoma kwa pamoja. Waliposoma kama darasa lote walionekana kuweza kusoma. Lakini baadhi ya watoto walipochaguliwa kusoma kadi zenye silabi, kuna watoto ambao walishindwa kutambua silabi. Watoto wengine walisoma /ha! badala ya /ka! na wengine walishindwa kusoma kabisa. Hili lilidhihirisha kuwa kuna watoto ambao walikuwa wakiiga wale waliojua kusoma. Pia kuna mwalimu ambaye aliandika silabi kwenye ubao zikiwa zimechanganywa kama vile: sa, se, si, so, su se, si, so, su, sa si, so, su, sa, se so, su, sa, se, si su, sa, se, si, so Watoto waliochaguliwa kuongoza wengine katika kusoma walionekana ama kusoma silabi bila matatizo au kukanganyika wakati wa kusoma. Watoto wengi walishindwa na ilibidi kusaidiwa na mwalimu na wakati mwingine watoto waliokuwa na uwezo wa kusoma. Katika uchunguzi wa darasani ilionekana kuwa, kuna watoto ambao 113 walikanganywa na baadhi ya silabi na kuzisoma kama fonimu za lugha ya Kigikuyu kama vile: 'ba, be, bi, bo, bu' walisoma kama 'fa, fe, fi, fo, fu' na 'ga, ge, gi, go, gu' walizisoma kama fonimu za Kigikuyu. Uchunguzi ulionyesha kuwa watoto wengi walikuwa bado kumudu silabi na wengi walikariri silabi bila kuzibainisha pengine kwa kuwaiga wengine. Kwa mfano wengi waliweza kusoma 'sa, se, si, so, su' hapo juu kwa urahisi kwa sababu ya kukariri kwa kukumbuka lakini zilipochanganywa walishindwa kuzisoma. Walimu wengi walijaribu kuwasaidia watoto kutambua silabi kwa kuwakumbusha vitamkwa vinavyounda silabi kama vile Isa! ikawa lesil na la!, lakini bado kulikuwa na watoto ambao walikuwa na shida. Kubainisha Silabi Tatizo lingine ambalo lilitajwa na walimu wawili lilikuwa la kuunganisha silabi katika neno. Walitaja kuwa kuna watoto ambao waliweza kutambua silabi lakini wakashindwa kuunganisha silabi katika maneno. Uchunguzi wa darasani ulithibitisha kuwa madarasa yote ya darasa la kwanza yalikuwa na matatizo haya. Kwa mfano watoto baada ya kujifunza silabi za 'ka, ke, ki, ko, ku' kuna watoto walioshindwa kusoma maneno yaliyoundwa kwa kutumia kadi zenye silabi hizo kama vile: Kaka Kuja kuku haki keki duka Hi kusoma majina ilibidi watoto kuanza kwa kutamka kwanza vitamkwa vinavyounda silabi na baadaye kusoma jina. Kwa mfano jina 'keki' lilisomwa kama 'kei' na 'e' yaani /kel na 'kei' na 'i' yaani /kil kisha kushikanisha pamoja na kutamka j ina nzima 114 'keki'. Walimu wote isipokuwa mmoja katika madarasa ya kwanza walionekana kutumia mtindo huu kufundisha watoto kutamka silabi za Kiswahili. Mtindo huu wa kutamka vitamkwa vinavyounda silabi kabla ya kusoma jina i1ionekana kuwa njia ndefu sana na yenye kukanganya watoto, ikichukuliwa kwamba nyingi za herufi za Kiswahili hutamkwa kwa kuunganisha na vokali. Kwa hivyo, ilionekana kujaribu kutenganisha vitamkwa vya silabi na kuvisoma kivyake viliishia kukanganya watoto badala ya kuwasaidia kusoma. Pengine kuna haja ya walimu kufahamu kuwa ingawa kuna mbinu nyingi za kufundisha stadi ya kusoma, kila lugha ina mbinu ambazo ni mwafaka zaidi kuzingatiwa kuliko mbinu zingine na pia kuna mbinu ambazo hazifai kabisa kutumiwa kufundishia lugha fulani kwa sababu ya muundo wa lugha yenyewe. Mwalimu mmoja alitaja matatizo ya kugeuza au kupindua silabi katika neno wakati wa kusoma jina yaani kuanzia mwisho wa neno na kwenda mbele. Uchunguzi wa darasani ulithibitisha tatizo hili katika darasa tofauti na lile Iililotajwa na mwalimu katika Jedwali 4.1 ambapo katika darasa hili kulikuwa na watoto ambao walisoma majina kama vile: Kiti kama tiki Chana kama nacha Hili Iilidhihirisha kuwa mbali na mwalimu mmoja aliyetaja tatizo hili ni dhahiri kuwa tatizo hili lilikithiri katika darasa hili la kwanza. Moyle (1968) amezungumzia tatizo hili. Anasema tatizo hili husababishwa na shida ya utambuzi, ambapo mtoto anashindwa kubainisha maumbo na kuweza kuyakumbuka. Anasema kuwa mambo mengi yanaweza kuchangia hali hii kama vile mazingara yasiyosisimua, ukomavu wa kiakili na mambo yanayohusiana na kihisia. Anaendelea kusema kuwa watoto wenye 115 matatizo kama haya wakifanyishwa mazoezi mengi kabla ya kuanza kufundisha kusoma kirasmi inaweza kusaidia. Aidha tatizo hili lilithibitisha maoni ya baadhi ya walimu ambao walieleza kuwa watoto walikosa maandalizi mazuri ya kusoma katika shule za malezi ili kuingia darasa la kwanza. Kadhalika, kuna mwalimu mmoja aliyeeleza kuwa kuna watoto ambao waliruka silabi waliposoma. Inawezekana silabi ambazo waliruka ni zile ambazo hawana uzoefu ama hawazitambui. Walimu wengine walitaja tatizo la watoto kuruka neno wakati wa kusoma. Katika uchunguzi wa darasani ilidhihirika kuwa maneno marefu na vilevile maneno yenye herufijozi yaliwashinda watoto wengi kusoma. Pengine haya yalitokea kwa sababu watoto walikuwa bado kumudu silabi na uzoefu wa kusoma silabi zenye herufijozi. Aidha, vitabu vilivyotumiwa vilikuwa na mipangilio tofauti; kuna vile ambavyo vilianza kwa kufundisha silabi zenye herufi mbili na vingine herufijozi ziliingizwa mapema sana. Matumizi ya Lugha Zaidi ya Moja Katika madarasa ya chini watoto walikumbana na masomo mbalimbali. Kati ya masomo haya ni lugha za Kigikuyu, Kiswahili na Kiingereza. Matumizi ya lugha hizi tatu ziliwakanganya watoto katika ujifunzaji wa stadi ya kusoma kwa sauti. Katika uchunguzi wa darasani tatizo hili lilibainika waziwazi wakati ambapo watoto walipewa picha zilizoambatana na majina kusoma mmoja mmoja kwa mfano kwenye Jedwali 4.3. 116 J d r 43 V w M·· K po h D I 1e wa I .. somaji wa atoto wa ajma wenye le a arasa a Neno sahihi Usomaji Mti tree Ndara slipper Ndizi banana Ndoo bucket Ndumakuwili Snake/munyo-ngoro Kama ilivyobainika kutokana na mifano iiiyoonyeshwa Jedwali 4.3, lugha ya Kiingereza ilionekana kuchangia zaidi katika kuwakanganya watoto. Kisha iJifuatwa na lugha ya Kigikuyu kwa mfano kusoma neno 'ndumakuwili' kama 'munyongoro' lenye maana ya 'mchango'. Usomaji huu ulidhihirisha kuwa watoto hawa walikuwa wakisoma picha bali si maneno yaliyoandikwa. Hii inaonyesha picha zinaweza kusaidia katika usomaji lakini pia zinaweza kukanganya ambapo kuna zaidi ya lugha moja ambayo inatumiwa kwa watoto ambao hawajaimarika katika usomaji. Kadhalika jambo hili linadhihirisha udhaifu wa mbinu hii ya kusoma picha, kwa sababu watoto wanaweza kubahatisha neno badala ya kusoma. Pia, ilionyesha umuhimu wa matumizi ya mbinu zaidi ya moja katika ufundishaji wa stadi ya kusoma. Kusoma kunahusisha akili au bongo wala si kukariri kama mashine bila kufikiria. Kushindwa Kusoma Maandishi Kwenye Vitabu Mwalimu mmoja alitaja kuwa kuna watoto ambao walisoma maneno kwa ubao kwa urahisi lakini walishindwa kusoma maandishi kwenye vitabu vya kiada. Tatizo hili linahusiana na mambo ya kimaumbile hususani kuona. Mojawapo ya kisababishi cha tatizo hili kinachotolewa ni shida ya macho ambapo mtoto anaweza kuona mbali 117 lakini hawezi kuona karibu. Sababu nyingine inaweza kuwa mtoto hakupata mazoezi ya kutosha kukuza uwezo wa kubainisha herufi na maumbo yake (Hughes, 1978). Aidha mazingira yenye uchache wa maandishi ama vitabu tofauti au nyenzo yanaweza kumnyima mtoto uzoefu wa maandishi kwa hivyo kushindwa kutofautisha herufi kwenye ubao na kwenye vitabu. Kadhalika, kuna mwalimu mwingine aliyeeleza kuhusu watoto ambao waliruka silabi waliposoma. Inawezekana silabi ambazo waliruka ni zile ambazo hawana uzoefu ama hawazitambui. Walimu wengine walitaja tatizo la watoto kuruka neno wakati wa kusoma. Katika uchunguzi wa darasani ilidhihirika kuwa maneno marefu na vilevile maneno yenye herufijozi yaliwashinda watoto wengi kusoma. Pengine haya yalitokea kwa sababu watoto walikuwa bado kumudu silabi na uzoefu wa kusoma silabi zenye herufijozi. Aidha vitabu vilivyotumiwa vilikuwa na mipangilio tofauti; kuna vile ambavyo vilianza kwa kufundisha silabi zenye herufi mbili na vingine herufijozi ziliingizwa mapema sana. Pia walisema kuwa kuna watoto ambao walikariri maneno bila kuelewa walichosoma. Kwa hakika kuna walimu ambao walieleza kuwa katika darasa la kwanza, usomaji ulikuwa muhimu kuliko ufahamu. Pengine hii ilichangia matatizo ya kusoma kwa sababu kulingana na nadharia ya Krashen kitengo cha Uteuzi wa makala, aina ya habari inayoteuliwa ni muhimu katika kuimarisha lugha ya mtoto. Kitengo hiki kinaeleza kuwa ni muhimu kwa mwalimu kuteua mambo ambayo yamo katika kiwango na tajriba ya watoto ili kuwapa motisha ya kusoma. Kwa hivyo, kuna uwezekano wa watoto kuchoshwa na kukariri silabi ambazo hazina maana yoyote. 118 Wataalamu wa lugha wanasema ni muhimu watoto kutoka mwanzo kuona usomaji una makusudio ili wapende kusoma. Isitoshe, vigezo vilivyotumiwa na walimu katika kuteua makala vinaenda kinyume na maelezo ya kitengo hiki cha Krashen. Vigezo vilivyotumiwa na walimu kuchagua makala ya kusoma ni kama vile; mpangilio wa kitabu, mtihani unatungwa kutoka kwa kitabu fulani, lugha ya kitabu ina kina, n.k. wala si umri au uwezo wa watoto. Mazingara ya Nyumbani Walimu wawili walieleza kuwa mazingara ya nyumbani yaliathiri maendeleo ya usomaji. Wazazi wengi wa watoto walikuwa hawana elimu kwa hivyo hawawezi kuwaelekeza au kuwasaidia watoto na mazoezi waliyopewa kufanyia nyumbani. Kando na wazazi, watoto wengine waliishi na nyanya zao ambao walikuwa wazee na wasiokuwa na elimu. Maelezo haya yanashadidiana na yale ya Hughes (1978) kwamba mazingara ya nyumbani huathiri usomaji ambapo wazazi hawana desturi ya kusoma na hawaoni umuhimu wa kusoma. Ukosefu wa vitabu nyumbani unaweza kuwafanya watoto wasione haja ya kujua kusoma. Watoto ni wenye kuiga haraka sana, kwa hivyo ikiwa wazazi hawajali elimu ya watoto wao ni rahisi kwa watoto pia kupuuza usomaji. Aidha, maoni haya yanaafikiana na kitengo Hisi cha nadharia ya Krashen. Mazingara kama haya ya nyumbani hayawezi kusisimua na hayamtii mtoto ari ya kusoma. Walimu wengine walielezea hali ya umaskini ambapo baadhi ya watoto hawakuwa na lishe bora au chakula cha kutosha. Mathalani, watoto wengine walikosa chakula cha kubeba shuleni kwa hivyo kushinda mchana kutwa bila kula kwa sababu watoto 119 EN -; , ("~-JJERSITV lIBRAII~L I \ walibaki shuleni hadi saa tisa. Watoto hawa walionekana kuchoka na kulala wakati wa mafunzo darasani. Pengine uchovu ulisababishwa na njaa na kushinda mchana kutwa wakisoma jambo ambalo hawakuzoea katika shule za malezi. Yamkini watoto katika shule za malezi huwa na wakati mwingi wa kucheza na pia hutengewa wakati wa kulala. Pia walimu hawakutaja mazingara ya darasani kuwa yanaweza kuathiri ujifunzaji wa kusoma. Kulingana na wataalamu mbalimbali mazingara ya shuleni huathiri usomaji wa mtoto. Mambo kama vile idadi ya watoto darasani, vifaa na nyenzo za kufundishia, ujuzi wa mwalimu na uchovu. Aidha, mabadiliko kutoka shule moja kwenda nyingine ambapo watoto wanatoka shule za malezi na kuingia shule za msingi zenye mtalaa tofauti na ule waliozoea. Kadhalika kitengo Hisi kinasema kuwa mazingara ya darasani yanaweza kuathiri hasi usomaji kama vile darasa likiwa chafu, ukosefu wa nyenzo, uwasilishaji wa funzo kwa njia moja n.k., unaweza kufanya funzo kuwa kavu hivi kwamba watoto kukosa motisha katika usomaji. Uchunguzi wa darasani ulithibitisha hayo ambapo kulikuwa na madarasa machafu sana, kuta zenye nyenzo chache na baadhi yake kuukuu. Ukosefu wa shughuli mbalimbali darasani ambapo watoto walipoteza hamu ya kusoma na kuanza kupiga kelele na wengine kutohusika na kinachoendelea darasani. Kwa mfano kutumia mtindo wa aina moja kama vile kurudia rudia silabi kwa pamoja au kusoma mtoto mmoja mmoja kwa kipindi kizima. 120 4.2 Matatizo ya Darasa la 2 Walimu walitaja matatizo ambayo baadhi yake yalifanana na yale ya darasa la kwanza na pia walitaja mengine ambayo yalikuwa tofauti. Baadhi ya matatizo yaliyofanana ni kama vile: 1. Athari ya LI kwa kuwa kuna vitamkwa ambavyo viliwashinda watoto kutamka na badala yake kuweka vitamkwa vingine kama ilivyoelezewa katika darasa la kwanza. Matatizo ya L1 hususani kutamka maneno yenye ving'ong'o ilidhihirika kwa kuchopeka vitamkwa mahali pasipofaa au kudondosha panapofaa kwa mfano 'gamia' badala ya ngamia 'jugu' badala ya 'njugu' 'ndamu' badala ya 'damu'. Walimu wawili kati ya sita walitaja tatizo hili. 2. Kukariri silabi kutokana na kukumbuka wala si kwa ufahamu wa maandishi. Aidha watoto walishindwa kuchagua silabi sahihi zilipochanganywa. Walimu wanne kati ya sita walitaja tatizo hili. 3. Watoto walishindwa kushikanisha silabi katika maneno. Hawa waweza kusoma silabi lakini hawawezi kusoma neno. Walimu wawili walitaja tatizo hili. 4. Kuna watoto ambao wanaweza kusoma maneno yakiambatana na picha tu. 5. Mazingara ya nyumbani yaliathiri kwa sababu hawakufuatiliwa nyumbani na wazazi. 121 Matatizo tofauti yaliyowakumba watoto wa darasa la pili yanaonyeshwa kwenye Jedwali 4.4. Jedwali 4.4: Matatizo ya Watoto Katika Usomaji Darasa la 2 Matatizo Idadi ya Walimu Idadi kubwa ya watoto 2 Kugusa silabi wakisoma 1 Kukosa usikivu 2 Uzembe 1 Akili punguani 1 (Walimu walitaja zaidi ya tatizo moja). Idadi ya Watoto Walimu wawili walieleza idadi kubwa ya watoto kama mojawapo ya matatizo yaliyowakabili. Kama ilivyoonyeshwa katika sura ya tatu idadi ya watoto katika baadhi ya madarasa ilikuwa kubwa. Wataalamu wanakubaliana kuwa hili ni tatizo katika ufundishaji si wa usomaji bali katika masomo yote katika madarasa ya chini na ya juu. Isitoshe tatizo hili ni kubwa zaidi katika madarasa ya chini ikichukuliwa kuwa watoto hawa hawajaimarika katika dhana za kimsingi katika kusoma na kila mtoto alihitaji muongozo wa mwalimu hata katika kutoa maagizo. Tatizo lingine lilikuwa lile la kugusa silabi kwa kidole wakati wa kusoma maneno au sentensi. Uchunguzi wa darasani ulithibitisha tatizo hili, hivi kwamba watoto walijikokota waliposoma na walisoma kwa mfululizo bila kutenganisha maneno katika sentensi. Walimu wengi hawakuweza kuzingatia alama za uakifisho. Pia kwa 122 sababu walishirikiana vitabu ilikuwa vigumu kwa wengine kusoma kitabu wakati wa kusoma makala pamoja au mmoja mmoja kwa sababu mmoja aligusa kila silabi wakati wa kusoma kwa sauti. Watoto wengine waliruka maneno mengine wakati wa kusoma pengine neno lilikuwa ngumu au refu. Nadharia ya Krashen, kitengo cha Uteuzi wa makala kinasisitiza kiwango cha habari inayoteuliwa na mwalimu iwe yenye kulingana na uwezo wa watoto. Matokeo haya yalionyesha watoto hawa bado walihitaji mazoezi zaidi ya kubainisha herufi na silabi ili kuweza kusoma kwa ufasaha. Kulingana na kitengo cha utaratibu wa Kiasili kuna hatua ambazo sharti zifuatwe moja ikijengwa juu ya nyingine katika ufundishaji wa kusoma kama sivyo watoto wataendelea kuwa na matatizo yale yale katika viwango vinavyofuata. Walimu wanaofundisha kusoma wanahitaji kufahamu utaratibu wa kusoma ili kuwasaidia watoto ifaavyo na kwa utaratibu. Kukosa Usikivu Ukosefu wa usikivu ulitajwa na walimu wawili. Kulingana na Moyle (1968), Homer (1974) na Hughes (1978) wanataja kuwa hali kama hii inaweza kuchangiwa na zaidi ya jambo moja kama vile; mbinu na nyenzo zinazotumiwa na walimu na pia mambo yanayohusiana na kihisia. Mambo yanayohusiana na kihisia yanaweza kuwa na matokeo kama vile kukosa usikivu, kujitenga na uchokozi. Wanafafanua kuwa mambo haya yanaweza kusababishwa na ukosefu wa upendo kutoka kwa wazazi au mtoto kushinikizwa na wazazi kufanya zaidi ya uwezo wake. Aidha walimu wanaweza pia kuchangia kwa kukosa kuwatuza watoto wanapofanya vizuri. Vilevile wanaweza kuwapa watoto kazi inayozidi uwezo wao na hivyo kuwafanya kufa moyo kila mara wanaposhindwa. Haya yanaoana na maelezo ya Nadharia ya Krashen ya 123 Kitengo cha Uteuzi wa Makala ambacho kinaeleza umuhimu wa kuzingatia makala yanayolingana na uwezo wa watoto. Kadhalika Kitengo cha Hisi kinaonyesha kuwa mazingara ya shuleni na/au nyumbani, matumizi ya mbinu mwafaka huchangia katika kutia watoto mshawasha wa kusoma. Watoto wakikosa usikivu itakuwa vigumu kwao kufahamu kusoma. Kusoma kwa sauti kunahitaji watoto wawe wachangamfu na wenye kujiamini, tena wanahitaji kusoma kwa kufikiria wala si kurudia tu mambo kama mashine. Ikiwa akili zao hazijatulia ni vigumu kwao kushika stadi hii ambayo inajikita katika bongo iIi kuweza kubainisha sauti, maumbo na maana ya kile kinachosomwa. Kwa mujibu wa uchunguzi wa darasani ilionekana kuwa baadhi ya makala yaliyosomwa yalikuwa marefu sana na kwa hivyo yalichukua muda mrefu sana kusoma. Kwa mfano kuna mwalimu ambaye alifunza maneno mengi sana kama vile majina takriban tisa katika kila kikundi yenye kuanza na silabi 'mba', 'nda', 'nga,' 'nja', 'nya' na 'nza'. Watoto wachache sana waliweza kusoma wengine walinyamaza na wengine kufuata na kuigiza wanayosikia. Mfano wa makala hapa chini ambayoyalinukuliwa kutoka Kiswahili Mufti, Darasa la Pili uk.86. Kutokana na Jedwali 4.6 baadhi ya maneno yalikuwa magumu sana kwa watoto wa darasa la pili. Isitoshe mwalimu hakutumia nyenzo zozote kufundishia maneno yale na waliyasoma kwa pamoja. Watoto wa darasa la pili hawawezi kutulia kwa muda mrefu na haswa ikiwa makala yanawasilishwa kwa njia ambayo haisisimui. Kadhalika urefu na ugumu wa makala ni muhimu kuzingatiwa na walimu wakati wa kuteua 124 ITV LlBR R , makala ya kusoma darasani. Hii ni kwa sababu walimu wengi walifuata mpangilio wa vitabu vya kiada ambapo mada zilipangwa kulingana na muhula. Jedwali 4.5: Mfano wa Makala Yaliyosomwa na Watoto Darasa la 2 Mba Nda Nga Nja Nya Nz Mbuzi Ndizi Nguruwe Njugu Nyinyi Nzige Mbegu Ndoo Ngiri Njia Nyenzi Kurunzi Mbao Ndovu Nguo Njaa Nyundo Panzi Mbung'o Ndoto Ngozi Njegere Nyumba Nyenze Mbisi Ndege Ngano Njoo Nywele Nzumari Mboga Ndewe Ngazi Njiwa Nyota Nzao Mbaazi Ndimu Ngamia punje Nyumbu Vibanzi mbatata Ndoana Nguvu Njenje Nyani Mwanzi Uzembe Mwalimu mmoja alieleza kuwa kulikuwa na watoto wazembe ingawa hakutoa ufafanuzi. Hughes (1978) anasema watoto wanapoingia shuleni huwa na hamu ya kusoma. Mwalimu akifahamu haya anaweza kutumia fursa hii kuwatia watoto hamu na watoto wakiona kuwa wanapiga hatua katika usomaji wataendelea kuimarika. Mwalimu asipozingatia haya basi matokeo yatakuwa watoto kukosa motisha na kuwa wazembe. Aidha, mambo mengine yanayohusiana na kimaumbile yanaweza kuchangia hali hii kama vile kuchoka kwa haraka, ugonjwa, ukosefu wa usingizi, njaa n.k. (Moyle, 1968). Watoto katika umri huu huwa rahisi sana kuathirika chanya au hasi. Wataalamu wanakubaliana kuwa watoto hawa wamo katika miaka ya kuumbika kwa mambo mengi akili, maungo, hisia na kimaadili. Ikiwa watoto katika umri huu ni 125 wazembe basi kuna mambo mengi ambayo yanasababisha haya kama ilivyoelezewa hapo juu. Hali hii inaweza kuathiri usomaji wa masomo mengine mbali na kusoma kwa mujibu wa Kitengo cha Hisi. Akili Punguani Matatizo mengine yalikuwa ya watoto wenye akili punguani. Uchunguzi wa darasani ulithibitisha haya. Hata hivyo, kuna shule ambazo ziliwaweka watoto kama hawa katika darasa tofauti. Wataalamu wanakubalina kuwa uwezo wa akili ni muhimu katika ujifunzaji wa kusoma. Watoto wenye matatizo yaliyokithiri hawataonyesha mabadiliko hata baada ya mwalimu kujaribu mbinu na nyenzo mbalimbali. Isitoshe watoto wa aina hii ni rahisi kutambua kwani ulemavu hudhihirika kwenye maungo yao ya mwili. Hawa watahitaji kushughulikiwa na watu wenye ujuzi wa mafunzo ya kisaikolojia. Stadi ya kusoma inahusisha uwezo wa kiakili kwa hivyo watoto hawa watahitaji mambo yanayotumia zaidi mkono kuliko akili. Aidha, kuna kikundi kingine cha watoto wenye uwezo wa kiakili wa kiwango cha chini ambao huwa na matatizo ya kusoma. Lakini watoto hawa kinyume na watoto wenye akili punguani wanaweza kusoma wakifanyizwa mazoezi ya kuwatayarisha katika usomaji (Homer, 1974). Moyle (1968) anasema kuwa watoto wengi hushindwa kusoma kwa sababu ya mbinu na nyenzo ambazo zinatumiwa na walimu ambazo haziambatani na hulka ya watoto. Kwa mfano, ikiwa mtoto ana matatizo ya kutambua silabi itabidi mwalimu kutumia mbinu za kimsingi ambazo zitamtayarisha mtoto kwa usomaji. Kwa hivyo, nyenzo zitahitajika kuwa nyingi ili kumsaidia mtoto kubainisha herufi tofauti kabla ya kupewa maandishi kusoma. 126 4.3 Matatizo ya Kusoma kwa Watoto wa Darasa la 3 Kutokana na majibu ya walimu kuna matatizo ambayo yalionekana kufanana kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la tatu. Matatizo haya ni kama vile: 1. Walimu wanne kati ya sita walitaja matatizo ya watoto kushindwa kutambua herufi. 2. Walimu watatu walitaja shida ya kushindwa kushikanisha silabi. 3. Athari ya LI katika matamshi. 4. Watoto kusoma mchoro au picha katika lugha ya Kiingereza. 5. Watoto kusoma neno tofauti na lililoandikwa kwa mfano, 'kuku' asome 'mti'. 6. Kushindwa kusikiza kwa muda mrefu kwa sababu ya kuchoka. 7. Kuruka neno likiwa ngumu. Matatizo yaliyotajwa na walimu yalidhihirisha kuwa watoto wengi katika kiwango hiki walikuwa hawajamudu mambo ya kimsingi ya kusoma. Hii ni kinyume na mapendekezo ya silabasi ambayo yalilenga zaidi katika ujuzi wa kiwango cha juu cha usomaji. Aidha, ilichukuliwa kuwa watoto katika darasa la tatu walikuwa wametayarishwa na wamefuzu dhana za kimsingi tayari kuingia madarasa ya juu. Katika uchunguzi wa darasani matokeo yalionyesha kuwa watoto wengi walisoma ama kugusa kwa kidole silabi katika kila neno au kugusa kila neno. Tena, kuna wengine ambao walisoma kwa mfululizo bila kufuata vituo au nafasi kati ya maneno waliyosoma. Hii ilitatiza uelewa wa kile kilichosomwa. Vilevile watoto wengine walishindwa kusoma na wengine walishindwa kufanya mazoezi mafupi waliyopewa. Matokeo ya uchunguzi yalionyesha kuwa watoto walikuwa na matatizo ya ujuzi wa 127 chini. Kulingana na JedwaJi 4.6 kuna matatizo yaJiyokuwa tofauti na yaJiyojadiliwa katika madarasa ya kwanza na ya pili. Jd r46M ti W t t K K ik D I 3e wa I . : ata IZO ya a ooya usoma ati a arasa a Matatizo Idadi ya Walimu Kushindwa kujibu maswali I Kuwana woga 1 Upungufu wa vitabu 1 Uakifishaji 2 Kujibu Maswali Mwalimu mmoja alieleza kuwa kulikuwa na watoto wengine ambao walikuwa na matatizo ya kujibu maswali ya ufahamu kwa usahihi (Jedwali 4.6). Matokeo ya uchunguzi wa darasani yalionyesha kuwa madarasa mengi yalikuwa na watoto ambao walishindwa kujibu maswali ya makala waliyosoma darasani. Hii ni kwa sababu watoto wachache walishiriki katika kujibu maswali. I1imradi, kama mtoto hajamudu ujuzi wa chini itakuwa vigumu kufahamu anachasoma. Kulingana na Modeli Husishi ni muhimu walimu kushirikisha Modeli ya chini-juu na juu-chini kuanzia darasa la kwanza ili watoto kuimarika katika stadi ya kusoma. Kwa mujibu wa Modeli Husishi matatizo haya hayana budi kutokea wakati ambapo walimu wanazingatia ujuzi wa aina moja na kupuuza ule mwingine. Aidha, maelezo haya yanathibitisha athari za mwelekeo wa aina hii. Katika viwango vyote ni muhimu kutumia Modeli Husishi. Kadhalika, Kitengo cha Uteuzi Makala kinaonyesha umuhimu wa mwalimu kuteua makala kwa makini akizingatia uwezo na tajriba ya watoto ili kukuza ujuzi wa chini na wajuu. 128 Woga Mwalimu mmoja alieleza kuwa baadhi ya watoto walikuwa na woga. Watoto waliogopa mwalimu na pia waliogopa kushiriki katika kusoma kwa sauti peke yao. Hali hii inaweza kusababishwa na mambo mengi. Kulingana na uchunguzi wa darasani kuna watoto walichekelewa na wengine waliposhindwa kusoma. Hii inaweza kumfanya mtoto kutojiamini na kushindwa kusoma kwa sababu ya kuogopa kufanya makosa. Pia mwalimu anaweza kuchangia hali hii kutokana na maoni yake wakati mtoto anapofanya makosa. Kwa mfano, mwalimu mmoja aliwauliza watoto ambao walianguka zoezi la imla wainue mikono yao. Hatua kama hii inaweza kuwavunja watoto mioyo kama Kitengo cha Hisi kinavyoeleza. Kwa mujibu wa Hughes (1978) hi si za woga zinaweza kuwa matokeo ya kushindwa kusoma au kisababishi cha matatizo ya kusoma. Kutokana na uchunguzi wa darasani watoto waliojua kusoma walionekana wachangamfu na pia walikuwa tayari kushiriki katika kusoma. Upungufu wa Vitabu Mwalimu mmoja alieleza upungufu wa vitabu kama sababu nyingine iliyochangia matatizo ya kusoma. Katika maswali ya hojaji walimu wote walisema kuwa walikuwa na vitabu vya kutosha. Hata hivyo, katika uchunguzi wa darasani i1idhihirika kuwa wakati wa kusoma watoto walitatizika walipotumia kitabu kimoja watoto watatu au wanne. Hii ni kwa sababu wengi wao waligusa maneno kwa kidole wakati wa kusoma kwa hivyo kuzuia wenzao kusoma kwa urahisi. Matokeo yalionyesha kuwa watoto wengi walikuwa bado na matatizo mengi ya kusoma pengine ingekuwa bora kama kila mtoto angekuwa na kitabu chake kwa sababu hata ya kufanya mazoezi nyumbani. 129 Kadhalika kuna walimu wawili ambao walieleza kuwa watoto hawakuzingatia uakifisho (Jedwali 4.6). Jambo hili linadhihirisha kuwa watoto hawakufahamu walichosoma kwa sababu ufahamu wa kile kinachosomwa ndio humsaidia msomaji kuakifisha kwa usahihi. Isitoshe kwa sababu watoto wengi walijikokota katika usomaji, hili liliwazuia kuzingatia alama za uakifisho. Kwa hivyo, haiwezekani watoto kama hawa kuelewa wanachosoma kwa kuwa wanatilia makini zaidi utambuzi wa silabi. Kama Kitengo cha Utaratibu wa Kiasili kinavyosema haiwezekani mtoto kufahamu ujuzi wa kiwango cha juu ikiwa hajamakinika katika kiwango cha chini cha usomaji. Hii inamaanisha mwalimu anafaa kuhakikisha kuwa mtoto amemudu kiwango alichomo kabla ya kumwiingiza katika kiwango kinachofuata. Kwa kuhitimisha sehemu hii ni dhahiri kuwa kulikuwa na watoto wengi ambao walikuwa na matatizo ya kusoma kwa sauti. Matatizo yalikuwa ya aina mbalimbali kama ilivyodhihirika. Baaadhi ya matatizo yalihusiana na yale ya ujuzi wa chini na mengine ya ujuzi wa juu. Aidha, tatizo la athari ya lugha ya mama liliwakumba walimu mbali na watoto. Kadhalika kulikuwa na walimu waliotaja kuwa hawapendi kufundisha lugha ya Kiswahili bali walifanya hivyo kwa sababu walitarajiwa kufundisha masomo yote katika madarasa ya chini. Hata hivyo, kuna walimu wachache ambao walipenda kufundisha somo la Kiswahili. 4.4 Namna Walimu Walivyotatua Matatizo ya Usomaji Majibu ya walimu kuhusu namna walivyokabiliana na watoto wenye matatizo yalikaribiana sana. Walimu walitoa zaidi ya njia moja ya kusuluhisha matatizo ya watoto ya kusoma kwa sauti. Majibu yaliyotolewa na walimu yanaonyeshwa (Jedwali 4.7). 130 Jedwali 4.7: Namna Walimu Walivyokabiliana na Matatizo ya Watoto ya Kusoma Suluhisho Darasa 1 Darasa 2 Darasa 3 Mazoezi ya ziada saa nane 5 5 6 Kufanya marudio 1 Kufuatilia mmoja mmoja 1 1 Mazoezi ya ziada nyumbani 1 Kuwatia motisha 1 1 Kutumia watoto wenye uwezo 1 Kufunza mambo ya kimsingi 1 Kutokana na Jedwali 4.7 walimu karibu wote isipokuwa wawili waliwapa watoto mazoezi ya ziada saa nane. Karibu shule zote watoto walibaki saa nane isipokuwa shule moja ambapo watoto katika darasa la kwanza na la pili walikwenda nyumbani kwa sababu walimu wao walifunza madarasa ya juu saa nane. Aidha, kuna shule ambazo hazikufunza lugha ya mama kwa hivyo walitumia kipindi hicho kuwapa watoto mazoezi zaidi. Baadhi ya mazoezi ambayo yalitajwa na walimu watatu kati ya sita ambayo waliwapa watoto katika darasa la kwanza ni kamavile; kuchanganua picha na kusoma silabi. Katika darasa la pili walimu watatu kati ya sita waliwapa watoto mazoezi ya kukariri silabi, mazoezi ya kujaza mapengo maneno mepesi na kufanya marudio ya kazi waliyokuwa wamefanya wakati wa kipindi darasani. Darasa la tatu walimu wanne waliwapa watoto mazoezi ya kusoma silabi na mwingine mmoja, mazoezi ya imla. Kutokana na maelezo ya walimu ilionekana kuwa wengi wao walirudia kufundisha silabi kwa sababu watoto wengi walishindwa kubainisha herufi na silabi ambazo ni mambo ya kimsingi katika ufundishaji wa kusoma. Pia, 131 kuna walimu wengine ambao walifundisha masomo mengine saa nane mbali na Kiswahilili ili kukamilisha silabasi ya madarasa yao. Kadhalika, wengine walitaja kuwa walitumia wakati ule kufanya marudio ya dhana ambazo ziliwatatiza watoto katika masomo mbalimbali waliyokuwa wamefunzwa siku hiyo. Mtoto akiwa na matatizo ya kusoma atahitaji zaidi mwongozo wa mwalimu. Kufanya marudio ya kazi iliyomshinda mtoto haiwezi kumsaidia. Mtoto huyu atahitaji kufanya kazi ambayo inalingana na kiwango alichomo. Kulingana na kitengo cha Uteuzi wa makala mtoto akipewa makala ambayo inashinda uwezo wake mtoto atakosa kuona maendeleo na kwa hivyo kuzoroteka katika usomaji. Kwa mfano kuna mwalimu mmoja katika darasa la pili ambaye kwanza, alipitia maswali na majibu sahihi ya zoezi kabla ya kuwapa watoto kufanya. Alifafanua kuwa asipofanya hivyo watoto wengi sana hushindwa kufanya zoezi. Matokeo ya uchunguzi wa darasani yalionyesha kuwa hata baada ya kupitia majibu ya zoezi walilofanya bado watoto wengi walianguka zoezi walilopewa. Jedwali 4.7 linaonyesha kuwa mwalimu mmoja katika darasa la kwanza na mwingine mmoja katika darasa la pili, walishughulikia mtoto mmoja mmoja wakati wa kufanya marudio. Kulingana na wataalamu njia ya kushughulikia mtoto mmoja mmoja ndio mwafaka. Kupitia njia hii mwalimu anaweza kumsaidia mtoto vyema zaidi ikichukuliwa kuwa watoto wana uwezo tofauti. Aidha, mwalimu ataweza kutathmini matatizo ya watoto na kujua kiwango walichomo ili kuweza kujua mbinu atakazotumia badala ya kubahatisha. Mwalimu pia atahitajika kufahamu utaratibu wa kusoma ili kukabiliana na viwango tofauti vya watoto. Kadhalika atatarajiwa kutumia 132 mbinu na tathmini mwafaka ili kupata matokeo yafaayo. Lakini bila rekodi ya tathmini itakuwa vigumu mwalimu kukumbuka matatizo ya mtoto binafsi. Mwalimu mmoja alieleza kuwa huwapa watoto mazoezi ya ziada kufanyia nyumbani. Mwalimu alifafanua kuwa watoto waliokuwa na ndugu katika madarasa ya juu aliwauliza kuwasaidia nyumbani. Hata hivyo, njia hii ina changamoto zake ikichukuliwa kuwa kulikuwa na upungufu wa vitabu, umaskini, wazazi wasiojali elimu na akina nyanya ambao hawakujua kusoma. Kuwapa motisha ilikuwa njia nyingine iliyotumiwa na mwalimu mmoja katika darasa la pili na mwingine katika darasa la tatu. Watoto wanaoshindwa kusoma huathirika sana kama ilivyojadiliwa hapo awali. Watoto hawa wanahitaji kuvumiliwa na kutiwa motisha kama ilivyojadiliwa katika sura ya pili. Njia moja ya kufanya hivyo ni kuwapa kazi kulingana na uwezo wao ili waweze kupata mafanikio madogo madogo kadri wanavyoendelea. Aidha Kitengo cha Hisi kinaeleza umuhimu wa kuzingatia hisi za mtoto kwa sababu huchangia katika uimarishaji wa kusoma. Njia nyingine ni kama vile kupongeza watoto wanapojaribu na kuwapa mazingara darasani yenye kusisimua usomaji. Aidha kutokana na uchunguzi wa darasani kuna walimu ambao waliwapongeza watoto kwa kutumia makofi au maneno ya kuwahimiza kutoka kwa watoto wenzao. Lakini kuna walimu wengine ambao hawakuwapongeza watoto. Walimu wengine waliwatumia watoto wenye uwezo kuwasaidia wenye uwezo wa chini. Mwalimu mmoja alifafanua kuwa njia hii huwasaidia watoto hususani ambao wanaogopa mwalimu. Watoto hawa huwasaidia wenzao kusoma silabi, kuwasomea 133 maagizo ya mazoezi na kuwaelekeza. Pengine walimu walitumia njia hii kwa sababu ya idadi kubwa ya watoto darasani. Hata hivyo, watoto hawa hawana ujuzi wa kuweza kujua shina la matatizo ya wenzao ili kuwasaidia vyema. Aidha njia hii inaweza kuwavuta nyuma watoto wenye uwezo ili wasifikie kilele cha usomaji wanachotaraj iwa. Mwalimu mmoja katika darasa la kwanza alieleza kuwa huzingatia mambo ya kimsingi katika usomaji kwanza kabla ya kutumia vitabu. Wataalamu wanapendekeza watoto kupewa mazoezi mengi ya kuwatayarisha kusoma kabla ya kuanzisha usomaji wenyewe. Kwa njia hii watoto wataimarika katika mambo ya kuona na kusikia ambayo ni ya kimsingi ili kuweza kubainisha herufi. Wanaendelea kusema kuwa hata mtoto mwenye akili nzito akipewa muda na mazoezi mengi na mwafaka atajua kusoma. 4.5 Uchanganuzi wa Matatizo ya Watoto Kutokana na maelezo yaliyotolewa na walimu kuhusu matatizo ya watoto ilionekana kuwa watoto walikuwa na matatizo mbalimbali. Baadhi ya matatizo yaliingiliana katika madarasa yote matatu. Matatizo ya kupambanua silabi katika madarasa ya pili na tatu yalionyesha kuwa watoto walikosa msingi mzuri katika kuwandaa watoto katika mambo ya kimsingi ya kusoma. Hii ni kwa sababu kulikuwa na watoto wachache katika darasa la tatu ambao walikuwa na matatizo ya kupambanua silabi. Kadhalika walimu hawakutilia maanani uwekaji wa rekodi mwafaka yenye kuonyesha maendeleo ya watoto. Walimu wengi walikosa shughuli mbalimbali za 134 kuwapa watoto wenye matatizo ya ujuzi wa chini. Pengine matatizo ya watoto yalikithiri kutokana na mbinu na nyenzo ziIizotumiwa na walimu. Hii ni kwa sababu watoto kutoka darasa la kwanza waIibaki saa nane kwa mazoezi ya ziada. Jitihada hizi kwa upande wa watoto na walimu hazionekani kuzaa matokeo yaIiyotarajiwa. Kuna haja ya kutathmini mbinu, vitabu na mazoezi ambayo walimu waliwapa watoto. Muhtasari Sura hii imeangazia matatizo yanayokabili watoto katika usomaji na namna waIimu walivyokabiliana na matatizo yale. Imedhihirika kuwa kuna matatizo mengi katika kila darasa lakini kuna mengine yaliingiliana katika madarasa yote. Kutokana na matokeo haya ilionekana kuwa watoto wa darasa la tatu walikuwa na matatizo ya kutambua herufi na silabi, kinyume na mapendekezo ya silabasi ambayo yanaonyesha kuwa watoto wameimarika katika ujuzi huu. Matokeo ya namna walimu walivyokabiliana na matatizo ya watoto yalionyesha kuwa walimu walitumia karibu njia moja kushughulikia matatizo ya watoto. Aidha ilidhihirisha upungufu wa aina mbalimbali ya mazoezi ili kuimarisha usomaji wa watoto ikichukuliwa kuwa baadhi ya matatizo yalikuwa ya kimsingi. Pengine walimu hawakufahamu hatua za kumudu kusoma ambazo mtoto anatakiwa kupitia ili kuimarika katika usomaji. 135 SURA YA TANO: MUHTASARI, IDTIMISHO NA MAPENDEKEZO 5.0 Muhtasari Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika madarasa ya chini katika shule za msingi. Nia hasa ya kufanya uchunguzi huu ilikuwa ni kubainisha mbinu na nyenzo zilizotumiwa na walimu kufundishia stadi ya kusoma kwa sauti. Malengo mengine yaliyozingatiwa yalikuwa ni vitabu vilivyotumiwa kufundishia na tathmini zilizotumiwa kupima viwango vya usomaji wa watoto. Aidha, kazi hii ililenga kubainisha matatizo yaliyowakumba watoto katika usomaji na namna walimu walivyoyakabili matatizo yale. Kwa minajili ya kutimiza malengo haya, mtafiti aliwapa walimu hojaji ili kupata maoni yao kuhusu namna walivyolikabili funzo la kusoma kwa sauti. Vilevile uchunguzi wa darasani ulifanywa kwa kufuata ratiba ya kukagua funzo. Shughuli hii ililenga hasa kuchunguza utekelezaji wa stadi ya kusoma kwa sauti kama ilivyoendelezwa darasani na walimu. Kadhalika, matokeo ya uchunguzi wa darasani yalitumiwa kuthibitisha maoni yaliyotolewa na walimu kwenye hojaji. Sura ya kwanza inatoa maelezo ya kijumla kuhusu kazi hii. Sura hiyo imeonyesha swala la utafiti, sababu za kuchagua mada hii, na malengo ya utafiti yamejadiliwa. Fauka ya hayo upeo na mipaka ya utafiti, misingi ya nadharia iliyoongoza utafiti huu na mbinu za ufafiti zimejadiliwa. Katika sura ya pili, dhana muhimu katika stadi ya kusoma kwa sauti, sifa zake bainifu, mbinu za kufundishia zimejadiliwa kwa jumla. Pia umuhimu wa nyenzo na tathmini katika ufundishaji yameangaziwa. Maelezo haya 136 yanatupa mwongozo wa mambo ambayo walimu wanafaa kuzingatia ili kutimiza malengo ya stadi ya kusoma yaliyopendekezwa katika silabasi. Sura ya tatu na nne zinahusu uwasilishaji wa data na mjadala kuhusu namna walimu walivyotekeleza stadi ya kusoma kwa sauti. Mbinu walizotumia ni kama vile mbinu ya abjedi, silabi, kutamka herufi, kutazama na kusema neno, kusoma sentensi na kusoma hadithi. Uchunguzi umeangazia vifaa na nyenzo zilizotumiwa kufanikisha usomaji. Aidha matatizo yanayowakabili watoto na namna walimu walivyoyashughulikia matatizo yale yameonyeshwa katika sura ya tano. Ufunzaji wa darasani ulirekodiwa kwa kutumia kinasa sauti iIi kushadidia kauli zetu kwa kurejelea ufundishaji wa kusoma kwa sauti darasani. 5.1 Hitimisho Kusoma kwa sauti ni stadi muhimu katika ufundishaji wa kusoma hususani watoto katika madarasa ya chini. Kwa njia hii mwalimu anaweza kuimarisha matamshi ya watoto ili waweze kueleweka kwa usahihi. Pia anaweza kupanua ufahamu wa watoto kwa kushirikisha makala mbalimbali yenye kulenga uwezo na tajriba ya watoto. Yamkini hii ni njia mojawapo ambayo mwalimu anaweza kutumia kuamsha hamu ya watoto kupenda kusoma na hata kupima maendeleo ya watoto ya usomaj i. IIi kufahamu maendeleo ya usomaji wa sauti wa watoto katika viwango hivi vya chini uchunguzi ulifanywa kuhusu namna walimu walivyotekeleza jukumu hili. Matokeo yalionyesha kuwa walimu wote waliofunza madarasa haya walikuwa wamehitimu katika masomo ya ualimu na baadhi yao walikuwa na tajriba kubwa. Hii ina maana 137 walikuwa na ujuzi ufaao kufundisha somo la Kiswahili. Kando na hayo, walimu walifahamu mbinu na nyenzo mbalimbali za kufundishia stadi ya kusoma kwa sauti. Rata hivyo, mbinu hizi zina uzuri na udhaifu wake katika ufundishaji wa kusoma kwa sauti. Ilionekana katika uchunguzi huu kuwa watoto walikuwa na matatizo ya kubainisha maumbo ya herufi na sauti zake, ambao ni ujuzi wa kiwango cha chini cha usomaji. Ilidhihirika kuwa baadhi ya walimu walijikita katika kufundisha ujuzi wa kiwango cha chini katika madarasa ya kwanza bila kushirikisha ujuzi wa juu ambao unajikita katika ufahamu. Kulingana na wataalamu wa lugha kuchanganya mbinu za ujuzi wa chini na juu huwa na matokeo bora zaidi. Aidha Modeli Husishi inapendekeza kuwa walimu washirikishe viwango vyote vya ujuzi wa chini na vyajuu katika ufundishaji wao. Kwa hivyo kuna haja ya walimu kuzingatia viwango vyote vya ujuzi ili kuimarisha usomaji. Kadhalika mazingara ya nyumbani na shuleni ni muhimu katika kusisimua usomaji wa watoto. Rata hivyo, uchunguzi ulionyesha ukosefu wa mazingara mwafaka. Ingawa walimu walionekana kujua umuhimu wa kutumia nyenzo kulikuwa na kuadimika kwa nyenzo darasani. Vilevile ubunifu ulikosekana katika kutayarisha nyenzo hizi. Walimu walipendelea aina moja ya nyenzo kama vile chati ukutani na picha kwenye vitabu vya kiada. Aidha, nyenzo hazikuthaminiwa kwa sababu ya uhifadhi wake, nyingi zilionekana kuchakaa na kubandikwa bila uangalifu. Nyenzo zikitumiwa vizuri husadia kurahisisha maelezo na pia kuvuta usikivu wa watoto na kuamsha hamu ya kusoma. Aidha husaidia kuwafikia watoto wenye uwezo tofauti kwa urahisi. Kulingana na kitengo cha Hisi, mazingara ni muhimu katika ujifunzaji wa watoto. Nyenzo huchangia katika kufanya mazingara ya darasani kusisimua. 138 / Kadhalika kutuzwa kwa watoto kwa njia tofauti huinua ari ya watoto na kujenga kujiamini katika kazi wanazopewa kufanya darasani. Kwa hakika si rahisi kubadilisha mazingara ya nyumbani, lakini walimu wakijitahidi wanaweza kufanya mazingara ya shuleni kuwa bora na yenye kusisimua usomaji. Yamkini, watoto katika mazingara ya mashambani walikumbwa na changamoto nyingi kwa hivyo walihitaji mazingara yenye kusisimua zaidi. Makosa mengi ya watoto yalikuwa kushindwa kubainisha maumbo ya herufi, kusoma silabi, kushikanisha silabi na kufahamu maana ya kilichosomwa. Watoto wengi walionekana kubahatisha wakati wa kusoma makala waliyopewa. Watoto wengi katika darasa la tatu walikuwa hawajamudu ujuzi wa chini wa kusoma kinyume na malengo ya silabasi. Kulingana na kitengo cha Uteuzi wa Makala ni muhimu makala yanayotumiwa kuchukuana na kiwango cha uwezo wa watoto. Kuna haja ya walimu kuchagua makala ya kusoma kwa makini kuendeleza usomaji wala si kutatiza usomaji wa sauti. Kadhalika hii ina maana kuwa, watoto wanatakiwa kuimarika katika kiwango kimoja kabla ya kuingia kiwango kinachofuata. Makosa ya kusoma yakivuka hadi madarasa ya juu ambapo kuna ongezeko ya shughuli za darasani itakuwa vigumu kuyatatua kwa sababu ya athari za kihisia kwa mwanafunzi. Ikumbukwe msingi bora utarahisisha shughuli za darasani katika madarasa yajuu. Sifa bainifu za usomaji wa sauti kama vile mkazo, kiimbo na hata uakifishaji hazikuzingatiwa na walimu. Ukosefu wa matumizi sahihi ya sifa za kiarudhi ina maanisha kuwa watoto hawatafahamu wanachosoma. Aidha hali hii yaweza kuwafanya watoto kukosa ari na maksudi ya usomaji na kuishia kuvunjika moyo. 139 Kulingana na uchunguzi, watoto wengi walishindwa kuzingatia sifa hizi. Hata hivyo, sifa hizi zinaweza kuimarishwa tu ambapo watoto tayari wamemudu kiwango cha chini cha ujuzi wa kusoma. Haina budi walimu kushirikisha viwango vyote viwili vya usomaji ikiwa watoto wataona maksudi ya kusoma na kwa hivyo kupenda somo la Kiswahili. Kadhalika makala yanayotumiwa yawe yenye kusisimua hisia za watoto. Vile vile ni vyema walimu kuwapa watoto mwongozo ili waweze kuwaiga na kukuza sifa bainifu za kusoma. Uteuzi wa mitindo ya kutumia katika kutekeleza ufundishaji wa kusoma kwa sauti ni muhimu. Kila mtindo una uzuri na udhaifu wake kama ilivyojadiliwa na wataalamu wa lugha. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa walimu walipendelea usomaji wa darasa lote kwa sauti. Ilionekana kuwa watoto wenye matatizo ya kusoma ama walinyamaza au kuiga waliyosikia kutoka kwa wale ambao walikuwa na uwezo wa kusoma. Kufuatia uchunguzi huu inabainika kuwa mtindo unatakikana kutathmini matatizo ya usomaji na kuyapunguza. Kwa hivyo, kuna haja ya kushirikisha mitindo mingine ya usomaji kama vile, kusoma mmoja mmoja, kusoma kwenye makundi ili kuwafikia watoto wenye uwezo tofauti. Walimu walitumia kigezo cha uwezo katika kuwapanga watoto katika makundi hasa madarasa ya kwanza na ya pili. Njia hii husaidia kushirikisha watoto wote katika ujifunzaji. Pia mwalimu hupata fursa ya kusaidia kila kikundi na kuwapa mazoezi mwafaka kulingana na uwezo wao. Kwa njia hii watoto wenye matatizo wanaendelea kuimarika na wenye uwezo hawavutwi nyuma na wale wengine. Hata hivyo, mpangilio wa makundi haya ulifanya njia hii kukosa matokeo yaliyotarajiwa. Katika NYAnA UNc 140 madarasa yote watoto walipangwa katika masafu. Ilionekana vigumu kwa mwalimu kuwasilisha malengo yake kwa kikundi kizima. Hivyo, ilimbidi mwalimu kuenda kwa kila dawati yenye watoto wawili au watatu akiwasaidia. Njia hii ilionekana kuchukua muda mrefu zaidi kuweza kuwafikia watoto ikichukuliwa kuwa idadi ya watoto i1ikuwa kubwa katika madarasa haya. Aidha katika madarasa ya chini watoto walihitaji usaidizi wa mwalimu zaidi. Ilivyobainika katika uchunguzi huu ni kuwa, mengi ya madarasa yalikuwa na nafasi ya kutosha kupanga watoto katika makundi. Hii ni kusema kuwa walimu wanahitajika kuwa na ubunifu zaidi ili kuwapanga watoto katika makundi mwafaka ambayo yatachangia uelewa wa watoto kwa muda mfupi. Kuhusu vitabu, uchunguzi wetu ulionyesha kuwa watoto walikuwa na vitabu vya kiada vya aina mbalimbali. Shule nyingi zilikuwa na zaidi ya kitabu kimoja cha kusoma. Kitabu kilichopendelewa zaidi kilikuwa ni Kiswahili Mufti kikifuatwa na Masomo ya Msingi. Hata hivyo, kuna watoto ambao walionekana kushindwa kusoma makala waliyopewa. Baadhi yao walikuwa na matatizo ya kuruka maneno, kushindwa kusoma maneno marefu na kubahatisha maneno. lsitoshe vitabu vya hadithi vilikosekana katika shule hizi isipokuwa shule moja ambapo vilikuwepo kinyume na mapendekezo ya silabasi. Vitabu vya hadithi ni muhimu katika kupanua msamiati wa watoto na hivyo kuwezesha ufahamu wa kilichosomwa. Kulingana na nadharia ya Krashen, kitengo cha Uteuzi wa makala kuna haja ya kuchunguza kama vigezo vinavyofaa kuzingatiwa katika uteuzi wa makala kwenye vitabu hivi vimezingatiwa. Hii ni kwa sababu yanaweza kuchangia chanya au hasi katika stadi ya kusoma kwa sauti. 141 Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa walimu walikuwa makini katika kutoa na kurekodi alama za tathmini rasmi za kati na za mwisho wa muhula. Mbali na alama, tathmini, zinaweza kutumiwa kubainisha matatizo ya watoto na maendeleo ya watoto katika usomaji. Uchunguzi huu ulibainisha kuwa watoto wenye matatizo walipewa kazi za ziada nyakati za alasiri. I1ivyoonekana ni kuwa watoto katika viwango vyote walikuwa na matatizo mengi ya ujuzi wa chini na wa juu hata baada ya kupewa kazi za ziada. Hii ina maana kuwa kuna haja ya walimu kuchunguza tathmini wanazowapa watoto na kuhamasishwa kuhusu kutayarisha tathmini zao wenyewe kutokana na matatizo yaliyokithiri darasani. Ikumbukwe, aina za tathmini wanazopewa watoto ndio muhimu wala si idadi ya tathmini. Utafiti huu pia umeweza kuonyesha kuwa walimu walijua matatizo yaliyowakumba watoto katika usomaji wa sauti. Matatizo haya yanaonyesha kuwa mambo mbalimbali yalichangia hali hii. Walimu walijaribu kukabiliana na matatizo yale lakini utafiti huu ulionyesha uhaba wa kuwepo mikakati mbalimbali ya kuimarisha usomaji. Aidha ni muhimu kwa walimu kuelewa namna stadi ya kusoma inavyofanyika katika bongo za watoto. 5.2 Mapendekezo Kusoma kwa sauti ni mojawapo wa stadi muhimu za lugha. Mtoto akiimarika katika usomaji inakuwa rahisi kwake kufahamu masomo mengine. Kadhalika inamfanya mtoto kujiamini na kukuza utamaduni wa usomaji ambao umekuwa tatizo kubwa nchini Kenya. Kwa sababu ya umuhimu wa kusoma kuna haja ya walimu kufahamu hatua za usomaji na pia kuibua shughuli ambazo zinaweza kuzingatiwa kuimarisha 142 stadi hii. Aidha, walimu wa madarasa haya walionekana kutokuwa na shughuli mbalimbali za kujenga uwezo wa watoto kubainisha herufi na sauti zake. Kwa vile walimu katika viwango hivi walikuwa hawana budi kufundisha masomo yote, walimu wengi hawakujiamini katika kufundisha somo hili la Kiswahili. Hii ni kwa sababu baadhi yao walitaja hawakuwa na msingi mzuri katika somo hili. Mwalimu ambaye hajiamini ni vigumu kwake kutekeleza jukumu hili ifaavyo na kuwafanya watoto kuonea fahari lugha ya Kiswahili. Isitoshe kutokana na tafiti zilizofanywa hatuwezi kupuuza mchango wa mwalimu katika ujifunzaji wa watoto. Kwa hivyo tunapendekeza kuwepo ama zaidi ya mwalimu mmoja au kushirikiana pamoja kwa walimu katika madarasa haya. Hii itasaidia walimu kufundisha masomo wanayopenda. Aidha kulikuwa na malalamishi kutoka kwa walimu kuhusu shule za malezi. Kuna haja ya utafiti wa aina hii kulenga shule za malezi ambazo ni za kibinafsi na za umma katika mazingara yanayofanana na haya ya utafiti huu ili kubainisha tofauti katika kuwaandaa watoto. Hii ni kwa sababu watoto wengi waliendelea kushindwa kusoma hata baada ya kuwa shuleni kwa kipindi kirefu. Inadhirihika kuwa kuna pengo ambalo linahitaji kuzibwa. Kutokana na matokeo ya utafiti huu ni dhahiri kuwa kuna haja ya utafiti kama huu kufanywa katika vyuo vya walimu vinavyowaandaa walimu kwa shughuli ya ufundishaji. Hii ni kwa sababu walimu wote, ambao walikuwa wa mifumo tofauti na tajriba tofauti walionekana kuwa na njia zinazokaribiana katika ufundishaji wao. Pia 143 walikosa ubunifu katika kutayarisha nyenzo. Ikumbukwe wengi wa wahadhiri katika vyuo hivi huwa wametayarishwa kufundisha shule za sekondari. Ni muhimu utafiti kuthibitisha kama walimu hawa hupelekwa katika warsha ili kuongezea ujuzi wao ili kuweza kuwaandaa walimu wa shule za msingi kwa njia ifaayo. Walimu wakuu wajizatiti katika majukumu yao ya kuwahamasisha walimu kuhusu umuhimu wa tathmini. Wanapokagua kumbukumbu za walimu wahakikishe kuwa watoto wanapewa tathmini zingine mbali na tathmini rasmi. Aidha walimu wakuu wachukue majukumu yao ya kukagua madarasa na kuhakikisha mazingara ya watoto shuleni yanasisimua badala ya kuwaachia wakaguzi wa shule kufanya kazi hii peke yao. Utafiti huu ulihusisha shule za umma katika eneo la mashambani. Kuna haja ya utafiti mwingine kama huu kufanywa kwa kulenga shule za kibinafsi katika mazingara sawa na ya utafiti huu. Utafiti kama huu unaweza kusaidia kuangazia namna wanavyoshughulikia usomaji wa kusoma kwa sauti na kulinganisha na shule za umma. 144 MAREJELEO Beaty, J.1. 1988. Skills for pre-school Teachers: (3rd ed.): Macmillan Publishing Co. U.S.A. Bwen, B.M. 1982. Look Here! Visual Aids in Language Teaching: Macmillan Press. London. Claessen, A and D. Stephen 1988. Language Education Resource Book. H.O. Ayot (ed.): British Council. Dalton, C. and B. Seidhhofer 1995. Reading: Oxford University Press: New York. Eskey, D.E. 1988. Holding in the bottom: An interactive approach to second language reading: Cambridge. New York. Gage, N.L. 1967. Handbook of Research on Teaching: Rand McNally and Co. Chicago. Gathumbi, A. W. and C.M. Ssebunga. 2005. Principles and Techniques in Language Teaching: Jomo Kenyatta Foundation. Nairobi. Goodman, K. S. 1969 Reading: A Psycholinguistic guessing game. Journal of reading specialist, 6, 126-135. Goodman, M. and Burke, C.L. 1972. Reading miscue inventor: Macmillan. New York Gough, P.B. 1972. One second of reading. In language by ear and by eye, J.F. Kavanagh and I.G. Mittingly (eds): Cambridge, Mass. MIT Press. Grant, M. 1960. School Methods with Younger Children: Evans Brothers Ltd. Ibadan. Gray, W.S. 1956. The Teaching of Reading and Writing: Evans Brothers Ltd. London. Habwe, J. na P. Karanja. 2004. Misingi ya Sarufi ya Kiswahili: Phoenix Publishers Ltd. Nairobi. Horner, P. 1974. Reading: Activity in Primary School: Heinemann Educational Books. London. Hughes, J.M. 1978. Reading and Readingfailures: Evans Brothers Ltd. London. Kenya Institute of Education (K.I.E). 2002. Silabasi ya Kiswahili kwa Shule za Msingi. Nairobi. K.I.E. 2006. Mwongozo wa silabasi ya Kiswahili kwa shule za Msingi-2002. Nairobi. 145 Kawoya, V.F. na Ryanga, C.W. 2003. ECT.313: Mbinu za Lugha na Fasihi. Institute of Open Learning. Kenyatta University. Kimani, N. na Wenzake. 2006. Sarufi ya Kiswahili: Uchanganuzi na Matumizi: Jomo Kenyatta Foundation. Nairobi. Kirigia, E. 1991. Assessment of English reading comprehension of pupils completing Primary Education. A case study of Meru municipality. (M.A.unpublished thesis) Kenyatta University. Krashen, S.D. and Terrel, T.D. 1988. The natural Approach: Prentice Hall International UK. Ltd. Britain. Krashen, S.D. 1982. Principles and Practise in second language acquisition: Pergamon Press. Oxford: Krashen, S.D. 1985. The Input Hypothesis: Issues and Implications: Longman Group Ltd. England. Laberge, D. and Samuel, S.S.1975. Basic processes in reading perception and comprehension: Hillsdale, N.S. Lawrence Elrbaum Associates Lansdown, R. 1974. Reading: Teaching and Learning: Sir Isaac Pitman & Sons Ltd. Nairobi. Matuu, H.M. 2000. An investigation of the Instructional practices used by Teachers to teach Reading and Writing in Mother-Tongue in selected schools from Tree Divisions of Kitui District. (Unpublished M.Ed Thesis) Kenyatta University. Massamba, D.P.B., Kihore, Y.M. na Hokororo, J.1. 2001. Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Oar es Salaam: TUKI. Mbaabu, I. 1987. Facilitating the Adoption of African Languages as Educational instruments in African countries-The case of Kenya. Mbaabu, I. 1996. Language Policy in East Africa: A dependency Theory Perspective: ERAP. Nairobi. Mberia, H.K. 2002. A survey of the teaching of reading in English Lower primary classes of Gatundu Division in Rural Thika District. (Unpublished M.A. Thesis) Kenyatta University. Mbua, A. 2000. Factors influencing the Performance of Kiswahili in KCPE in Dagoretti Division Nairobi Kenya (Unpublished M.Ed. Thesis) Kenyatta University. Mclaughlin, B. 1987. Theories of second Language Learning: Chapman and Hall, Inc. New York. 146 Mgullu, R. S.1999. Mtalaa wa Isimu: Longhorn Publishers (K) Ltd. Nairobi. Milroy, L. 1987. Observing ana Analysing Natural Language: Basil Blackwell Ltd. Oxford Mohammed, M.A. 2001. Modern Swahili Grammar: E.A.E.P. Dar es Salaam. Moyle, D. 1968. The teaching of Reading: Ward Locke Educational. Musau, P.M. 1993. Aspects of Interphonology. The study of Kenyan learners ofSwahili: Bayreuth African Studies. Germany. Newman, H.M. 2000. Psycholiguistics and reading: A dissenting point of view. Reading World. Vol. 18No. 4. 0' Connor, J.D. 1967. Better English Pronounciation: Cambridge University Press. New York. Ogunniyi, M.B. 1984. Educational Measurement and Evaluating: Longman Group Ltd. Nigeria. Onyamwaro, A.A.O. 1990. A study of factors that affect the teaching of reading in Kiswahili, lower primary classes in selected schools. Kisii Municipality. (Unpublished M.ED Thesis) Kenyatta University. Pearson, H. 1981. The Teaching of Language Skills: Oxford University Press. Nairobi. Pearson, K. 1987. Children's Writing and Reading: Analysis classroom Language: Basil Blackwell. U.S.A. Quist, D. 2000. Primary Teaching Methods: Oxford University Press. New York. Reason, R. and B. Rene. 1990. Learning Difficulties in Reading and Writing : A Teacher's Manual: Infer-Nelson Publishing Co. Ltd. Rumelhart, D. 1977. Toward an interactive Model of reading in attention and performance, VI, S. Dorni L. (Ed): Hillsdale NJ. Erlbaum. Seefeldt, C. (ed) 1976. Curriculum for the Preschool-Primary Child: Bell &Howell Co. U.S.A. Shipley, C.M. et al 1968. A synthesis of Teaching Methods 2nd edition: McGraw-Hill Co. of Canada Ltd. New York. Smith, F. 1971. Psycholinguistics and Reading: Holt, Rinehart & Winston. New York. Stanovich, K.E. 1980. Intelligence, Cognitive skills and early reading progress. Reading research quarterly xix 3. 147 Teal. 1994. Reading Ability: Oxford Press. New York. Tuki. 1981. Kamusi ya Kiswahili Sanifu: Oxford University Press. Nairobi. Uljn, J. 1980. Foreign language Reading Research. Recent trends and futureprospects Journal of Research in Reading 3. Vincent, D. 1985. Reading Tests in the Classroom: Nfer Nelson Co. Ltd. Gr. Britain. Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi Istilahi na Nadharia: Focus Publishers. Nairobi. Wanyoike, E. 1982. A teacher training reading methodology manual in Kiswahili for lower primary. (Unpublished Postgraduate Dip. Ed. Thesis) Nairobi University. Wario, H. 1981. Reading attainment and its relationship to some school conditions. (Unpublished M. Ed. Thesis) Nairobi University. WiIliams, D.J. 1973. English Teaching in the Primary School: Evans Brothers Ltd. Ibadan. Yule, G. 1996. The study of Language: Oxford University Press. New York 148 KIAMBATISHO 1 HOJAJIKWA WALlMU SHULE . WILAYA . TARAFA . DARASA . 1. Maelezo kuhusu mwalimu: (1) Jinsia: Mwanamke[ ] Mwanamume[ ] (2) Umefunza Kiswahili kwa miaka mingapi? 0-3 [] 4-6 [] 7-10 [] zaidi yaI 0 [] (4) Kiwango chajuu cha elimu KJSE [ ] EACEIKCE/KCSE [ ] yoyote nyingine (5) Cheti cha taaluma Graduate/Approved [] SI PI P2 [] [] [] 149 11.Mbinu ,vifaa na nyenzo za kufunzia (6) Taja mbinu ambazo umekuwa ukitumia katika kufunza kusoma kwa sauti MBINU (i) Abjedi (ii) Silabi (iii) Kutamka herufi (iv) Kusoma neno (v) Kusoma kirai (vi) Kusoma sentensi (vii) Kusoma hadithi (7) Toa sababu zako zinazoonyesha umuhimu wa kila mojawapo wa mbinu ulizoorodhesha katika kufundisha kusoma kwa sauti (6) katika kiwango hiki cha madarasa ya chini MBINU UMUHIMU (i) Abjedi (ii) Silabi (iii) Kusoma neno (iv) Kusoma kirai (v) Kusoma sentensi (vi) Kusoma hadithi 150 (8) Je, kuna wakati wowote umetumia zaidi ya mbinu moja katika kufundisha kusoma kwa sauti katika kipindi kimoja? Ndio [] La [] (8bToa sababu (9) Ni vitangulizi vipi ambavyo unawapa watoto katika kutanguliza mada ya kipindi cha kusoma kwa sauti? (9b) Taja umuhimu wa mazoezi haya? (10) Unatumia mtindo gani kuhakikisha kila mtoto anashiriki katika funzo. (i) kusoma darasa lote [ ] (ii) kuchagua mmoja mmoja [ ] (iii) kusoma katika makundi [ ] (iv) Yoyote nyingine [ ] (11) Unayapanga vipi makundi katika darasa? (11 b) Makundi ni ya kudumu? (12) Unashughulikia vipi makosa ya kusoma kwa sauti yanapotokea? (i) Nasahihisha mwishoni mwa funzo [.] (ii) Sisahihishi [ ] (iii) Nasahihisha kila yanapotokea [] 151 III Vitabu na makala ya kusoma (13) Unatumia vitabu gani kuandaa kipindi cha kusoma kwa sauti? (i) Kitabu kilichopendekezwa kwenye silabasi. Toa mfano (ii) Makala yako mwenyewe (14) Nini unazingatia unapochagua makala itakayosomwa na watoto kwa sauti? (i) Silabasi. (ii) Umri wa watoto. (iii) Uwezo wa watoto (iv) Yoyote nyingine (14b) Je, ulikamilisha silabasi ya mwakajana? {swali kwa walimu wa darasa la 2 na 3} Ndio []....... La [ ] Kama la kwa nini ? . IV Utathmini (15) Unatathmini vipi viwango vya watoto vya usomaji? (i)Kila mmoja kusoma kwa sauti (2) Zoezi la kujaza mapengo (3) Kuchanganua picha (4) Kutazama wanaposoma darasani 152 (16) Unawapa watoto tathmini mara ngapi kwa muhula? (i) Baada ya wiki mbili [ ] (ii) Katikati mwa muhula [ ] (Hi) Mwisho wa muhula [ ] (iv) Yoyote nyingine . (17) Je, unaweka rekodi ya tathmini unazowapa watoto? . (17b) Kwa nini unaweka rekodi? . (18) Ni asilimia ngapi ya watoto wako wanaweza kusoma kwa ufasaha? A. 100% B. 75% C. 50% D.25% (19) Taja baadhi ya matatizo unayokumbana nayo? . (18b) Unakabiliana vipi na matatizo hayo? . 153 KIAMBATISHO 2 RATmA YAKUKAGUAFUNZO Darasa . Jina la Mwalimu . Idadi ya wanafunzi . I. Ratiba ya kufundisha somo la Kiswahili . 2. Andao la funzo ; . 3. Mbinu iliyotumiwa na mwalimu (i) Abjedi [ ] (ii) Silabi [ ] (iii) Kusoma neno [ ] (iv) kusoma kirai [ ] (v) Kusoma sentensi [] (vi) Kusoma hadithi [] 4. Kinachotiliwa mkazo (i) Matamshi (ii) Kiimbo (iii) Shadda (iv) Uakifishaji [ ] [ ] [ ] [ ] 5. Vifaa na nyenzo zilizotumiwa na mwalimu (i) Vitabu (ii) Picha (iii) Chati (iv) Ubao [ ] [ ] [ ] [ ] 154 (v) Kadi za maneno/herufi [] (vi) Mradi wa darasani [ ] (vii) yoyote nyingine [ ] 6. Mbinu alizotumia kutathmini viwango vya usomaji wa watoto (i) Kusoma mmoja mmoja [ ] (ii) Kusoma katika makundi [] (iii) Kuwapa zoezi daftarini [] (iv) Kusoma darasa lote [] 7. Kusahihisha makosa ya watoto kulifanyika (i) Mara moja kosa lilipotokea [ ] (ii) Baada ya funzo [ ] (iii) Yalipuuzwa [ ] 8.Usomi wa mwalimu (i) Mwendo wa kasi [ ] (ii) Mwendo wa kiasi [ ] (iii) Alizingatia kiimbo [ ] (iv) Alizingatia shadda [ ] (v) Alizingatia mkazo [] (vi) Alizingatia uakifishi [ ] (vii) Alizingatia matamshi [ ] 9. Mazingara ya darasani (i) Watoto wana motisha . (ii) Darasa safi . 155 KIAMBATISHO 3 JARIBIO LA MTllIANI DARASA LA KW ANZA MWISHO WA MUHULA WA KW ANZA 2007 KUSOMA Soma majina Soma sentensi hizi 1) Baba 6) duka Mimi ni mtoto. 2) Mtoto 7) Paka Huyu ni paka. 3) Kaka 8) Ua Hii ni meza. 4) dada 9) Mti Mtoto analia. 5) Kuku 10) Meza Duka la mama. 156 KIAMBATISHO 4 JARIBIO LA MTffiANI DARASA LA PILI MWISHO WA MUHULA WA KWANZA 2007 KUSOMA Soma majina Soma sentensi hizi 1) Bata 6) Seremala 1) Huyu ni mwalimu wetu 2) Fedha 7) Duka 2) Leo ni Jumatatu 3) Firimbi 8) Peremende 3) Hii ni fedha ya Kenya 4) Ghorofa 9) Kinyozi 4) Baba anasoma gazeti 5) Msichana 10) Ndizi 5) Mama anapika chakula 157 KIAMBATISHO 5 JARIBIO LA MTmANI DARASA LA TATU MWISHO WA MUHULA WA KWANZA 2007 KUSOMA Soma majina haya Soma sentensi hizi 1) Kikapu 6) Kabati 1) Kitabu chako ni cha samawati. 2) Ndumakuwili 7) Muuguzi 2) Watoto hawa ni watukutu. 3) Mlingoti 8) Mwavuli 3) Mwalimu wetu ni mzuri. 4) Dhahabu 9) Nyepesi 4) Baba huwakaribisha wageni. 5) Omboleza 10) Shemeji 5) Nyumba yao imechomeka. 158