Usilimishaji wa Vielelezo Katika Fasihi ya Watoto: Mfano Kutoka Wasifu wa Mwana Kupona (2008) na Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (2015)
Loading...
Date
2021
Authors
Mwendwa, Stephen M
Ngugi, Pamela M.Y
Ndungo, Catherine
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu Cha Dar es salaam
Abstract
Makala hii inachunguza usilimishaji1
wa vielelezo vilivyotumika katika
hadithi ya Wasifu wa Mwana Kupona (King‟ei, 2008) na Alisi Ndani ya Nchi
ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) na mchango wake katika kuendeleza ujumbe.
Tafiti chache za usilimisho wa vielelezo katika hadithi za watoto zimefanywa
(taz. Muthubi, 2005; Kaui, 2011; Sohaimi, 2011; Balodis, 2012; Ratiba, 2014;
Omuya, 2017). Hata hivyo, tafiti hizi za awali hazijahusisha moja kwa moja
hadithi ya Wasifu wa Mwana Kupona (2008) na Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu
(2015). Ni katika msingi huu ndipo makala imeshughulikia aina za vielelezo
vilivyotumika katika hadithi teule na mchango wake katika kuendeleza
ujumbe. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Usilimisho ya George
Bluestone (1957) na baadaye ikaendelezwa na Goodman (1976), Andrew
(1984) na Starrs (2006). Nadharia ya Usilimisho inahusu uzalishaji wa kazi
nyingine huru baada ya kazi ya awali kuzalisha kazi nyingine. Data
iliyotumika katika makala hii imetokana na kusoma machapisho mbalimbali
maktabani kama vile majarida, tasnifu na vitabu. Vilevile, usomaji,
uchambuzi na hata unakili wa vipengele muhimu vinavyohusiana na
masilimisho teule ulifanywa. Matokeo ya utafiti yamebainisha kwamba aina
za vielelezo vilivyotumika katika hadithi teule ni vibonzo, ramani, picha
zilizotiwa rangi na michoro. Aidha, imebainika kuwa vielelezo vinaweza
kutumika kupasha ujumbe iwapo vitatumika ipasavyo.
Description
Article
Keywords
Citation
Mwendwa, S. M., Ngugi, P. M., & Ndungo, C. (2021). Usilimishaji wa Vielelezo katika Fasihi ya Watoto: Mfano kutoka Wasifu wa Mwana Kupona (2008) na Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (2015). Kioo cha Lugha, (18).