Uwezo wa Lugha katika Matini ya Siasa Nchini Kenya Kuanzia Mwaka 2002 hadi 2005.
Abstract
Utafiti huu unaangazia uwezo wa iugha katika matini ya siasa nchini Kenya.
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kudhihirisha vile lugha hutumiwa na
wanasiasa ili waweze kuonyesha itikadi zao na pia kupata mamlaka. IIi
kuonyesha uwezo wa lugha katika matini za siasa nadharia ya uchanganuzi
usemi hakiki ndio imetumiwa.
Katika utafiti huu sura ya kwanza ambayo ni utangulizi wa tasnifu inashughulikia
swala la utafiti, sababu za kuchagua mada, nadharia, madhumuni, upeo wa
utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pili inaangazia na
kueleza dhana muhimu zilizotumiwa katika utafiti. Pia inaelezea mwingiliano
uliopo kati ya lugha, siasa, mamlaka na itikadi.
Sura ya tatu inahusu uchanganuzi wa data ya hotuba za kisiasa na
kuzichanganua kimuktadha na kimaana. Inatoa maelezo ya hotuba zilizotolewa
katika kipindi cha siasa kinachozungumziwa. Sura ya nne ni uchanganuzi wa
data na kueleza uwezo huo wa lugha katika hotuba za kisiasa nchini Kenya. Sura
ya tano ni matokeo ya utafiti, mapendekezo ya utafiti mwingine na matatizo
yaliyoukumba utafiti.
Collections
Related items
Showing items related by title, author, creator and subject.
-
Factors affecting performance of tourism sector in Kenya. ( A case of Kenya Tourism Board, Bomas of Kenya, Kenya Utalii College and Kenya Wildlife Service)
Okemwa, Ogwoka (2012-03-01)The main objective of this study was to look into the factors that affect performance of the tourism sector in Kenya. A sample of 27 respondents was drawn from Kenya Tourism Board. Bomas of Kenya Ltd., Kenya Wildlife Service ... -
Factors Affecting Performance of Tourism Sector in Kenya (Case of Kenya Tourism Board, Bomas of Kenya, Kenya Utalii College and Kenya Wildlife Service)
Ogwoka, Okemwa (Kenyatta University, 2005)The main objective of this study was to look into the factors that affect performance of the tourism sector in Kenya. A sample of 27 respondents was drawn from Kenya Tourism Board. Bomas of Kenya Ltd., Kenya Wildlife ... -
Effects of Information Literacy on Adult Consumers of Kenya National Library Services in Embu County: A Case Study of the Kenya National Library Services Embu Branch, Embu County, Kenya
Karimi, Phyllis Njeri (Kenyatta University, 2017-06)The study aimed at assessing the effects of information literacy programs on adult users in public libraries in Kenya by conducting a case study at Embu County public library. Public libraries have been operating with ...