Maigizo katlka fasihi simulizi: mfano wa kirarire katika nyimbo za tohara za wameru
Abstract
Mada ya utafiti huu m maigizo katika fasihi simulizi kwa kurej elea mifano
kutoka kirarire katika nyimbo za tohara za Wameru. Mtafiti ameangazia
umuhimu wa maigizo katika utanzu huu wa nyimbo kwa lengo la kudhihirisha
jinsi ambavyo wahusika katika nyimbo hizi huwasilisha ujumbe wao kwa njia ya
ubunifu. Mtafiti pia alinuia kuwaonyesha baadhi ya watafiti wa awali ambao
hushikilia kuwa hakuna maigizo katika bara la Afrika kwamba kweli yapo.
Utafiti huu uliongozwa na Nadhariaya Maigizo ambayo husisitiza umuhimu wa
kuonyesha mitagusano ya wanajamii katika maisha yao halisi kupitia vitendo vya
jukwaani. Nadharia hii pia huonyesha umuhimu wa hadhira katika kuwatathmini
waigizaji wanapoendelea na vitendo vyao jukwaani.
Tasnifu hii imegawanywa katika _sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa
tasnifu. Hapa, mtafiti ameifafanua mada ya utafiti, sababu za kuchagua mada na
upeo wa utafiti. Udurusu wa maandishi pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti
pia zimefafanuliwa. Mbinu za utafiti zilizotumiwa katika utafiti huu
zimefafanuli wa.
Sura ya pili inaangazia historia ya jamii ya Wameru ambao ndio watafitiwa.
Mtafiti amefafanuamifumo ya kisiasa na kijamii ya Wameru, fasihi simulizi na
utamaduni wao pamoja na vipawa vyao vya kisanii. Lengo kuu hapa ni
kudhihirisha kuwa ingawa bara la Afrika limepitia mabadiliko makubwa ya
kitamaduni, bado kuna jamii ambazo zingali zinauthamini utamaduni wake.
Sura ya tatu i?1echunguza sifa za maigizo katika kirarire. Baadhi ya
yaliyoshughulikiwa ni njia ya mawasiliano, jukwaa, tukio la kuigizwa, mila na
tamaduni zinazohusika na ujumi na itiksadi ya mawasiliano katika kirarire.
Sura ya mwisho inatoa muhtasari wa matokeo, hitimisho na mapendekezo ya utafiti. Hatimaye kuna marejeleo ya utafiti huu.