Maigizo ya kienyeji ya watoto nchini Kenya: nafasi ya kuyatumia katika ufundishaji
Abstract
Tasnifu hii imechunguza namna za kuchuma vipengele vya kiufundishaji na kimawasiliano kutoka katika maigizo ya watoto ya kienyeji kama njia ya kuuhudumia ufundishaji wao katika shule za msingi nchini Kenya.Tumetazama jinsi tajriba za kisanaa zinazotokana na mazingira ya nje ya shule zinavyohusu uigizaji zinaweza kutumika katika mfumo rasmi wa shule za msingi.
Mkeketo tunaozungumzia na tuliokutana nao wakati wa utafiti ni wa kati ya miaka 5 na 15.Aina za uigizaji wa kienyeji unaowahusu watoto tulizozitalii ni pamoja na utambaji ngano,utegeanaji vitendawili,uimbaji/ukariri wa mashairi, uchezaji michezo mbalimbali ya watoto na uimbaji/uchzaji wa ngoma/nyimbo.
Sura ya kwanza ni Utangulizi ambamo kuna maelezo ya msingi kuhusu mada ya tasnifu hii. Sura ya pili inahuluti baadhi ya yaliyoandikwa kuhusu maeno yanoyoihusu mada ya tasnifu hii na kuyaambatanisha na tuliyotafitia. Sura ya tatu imenakili njia tulizozitumia kunafidhishia matokeo ya utafiti tulioufanya. Sura ya nne inachanganua matokeo ya utafiti na kuyatia katika dhana na mtazamo nasibishi wa ufundishaji. Sura ya tano ni hitimisho ambamo tumetoa mapendekezo yetu.
Katika sehemu ya ziada zipo habari kuhusu watoto tuliowashirikisha katika utafiti.Sehemu hii pia ndio iliyo na mihutasari ya baadhi ya matini za kienyeji zilizotumika katika uigizaji halisia.Kadhalika katika sehemu hii zipo nyaraka zilizoandikwa na baadhi ya wanafunzi kuhusu shughuli tulizowashirikisha wakati wa utafiti.