• English
    • français
  • English 
    • English
    • français
  • Login
View Item 
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

Maoni ya jamii katika tamthilia za Chacha Nyaigotti Chacha: swala la uongozi

Thumbnail
View/Open
Abstract (5.554Kb)
Date
2012-05-09
Author
Mahero, Ann Judith
Metadata
Show full item record
Abstract
Tasnifu hii imejishughulisha na ubainishaji wa mano ya taasisi ya uongozi katika jamii jinsi yanavyojitokeza katika tamthilia za msanii Chacha Nyaigotti Chacha. Tunaamini kuwa mazingira ya msanii pamoja na tajriba zake katika maisha huathiri kwa kiasi kikubwa jinsi anavouona na kuuwasiri ulimwengu. Mtazamo huu humwelekeza katika mapendekezo anayoyatoa kwa jamii. Mambo yakiwa hivyo, kadri mazingira yake ya kibinafsi na ya kijamii yanavyoendelea kubadilika na kuathiri tajriba zake, zake, ndivyo maono yake yanavyoendelea kubadilika. mabadiliko haya yanaweza ama kuboresha maono ya msanii au yakayadunisha. Jinsi maono ya Chacha kuhusu uongozi wa jamii yanavyobadilika ama kwa kukua au kwa kudunishwa kadri anavyoendelea kuandika tamthilia baada ya nyingine ndilo lengo la tasnifu hii. Sura ya Kwanza ni utangulizi ambamo tumezingatia somo la utafiti, madhumuni yake, sababu za kulichagua somo hili na upeo wake. Pia tumezungumzia mandishi mengine yanayohusiana na somo hili kwa ufupi na kuifafanua nadharia ambayo tumeitumia kama msingi wa utafiti wetu. Mwisho, tumeonyesha njia za utafiti tulizotumia katika kazi hii. Sura ya pili inamulika tajriba muhimu katika maisha ya msanii na jinsi zilivyoathiri usawiri wake wa kudhia katika tamthilia alizoandika. Athari muhimu tulizozingatia ni za kisiasa, kiuchumi, kifasihi na kidini. Katika sura ya tatu tumechambua maudhui katika tamthilia ya Mke Mwenza (1982). Tumeonyesha namna athari za mfumo wa ubepari pamoja na elimu ya kikoloni imemkinaisha mwafrika na kumkengeusha kutokana na mahitaji ya mazingira yake halisi. Sura ya nne ni uchambuzi wa maudhui katika tamthilia za Marejeo (1986) na Wingu Jeusi (1987). Tumeonyesha jinsi ufisadi na unafiki umekithiri katika ngazi za juu za uongozi barani Afrika. Pia tumejadili swala la wito wa wasomi kwa jamii ya Afrika. Sura ya tano inachambua maudhui katika tamthilia ya Hukumu (1992). Tumeonyesha jinsi mtazamo wa msanii unabadilika na kupevuka kuhusu swala la uongozi kuliko ulivyokuwa katika kazi zake za awali. Sura ya sita ndicho kiini cha utafiti wetu. Katika sura hii tumejadili jinsi maono ya msanii ya uongozi katika jamii yanavyokua kutoka tamthilia yake ya kwanza mpaka ya mwisho. Halikadhalika, tumehitimisha tasnifu katika sura hii kwa kufafanua matokeo yetu na kupendekeza maeneo ambayo yanastahili kufanyiwa utafiti zaidi katika tamthilia za mwandishi huyu.
URI
http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/4520
Collections
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages [234]

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback

 

 

Browse

All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

My Account

LoginRegister

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback