Show simple item record

dc.contributor.advisorKimemia, J.
dc.contributor.advisorSheila C. W. Ryanga
dc.contributor.authorMose, Patrick Obwocha
dc.date.accessioned2012-04-12T12:42:40Z
dc.date.available2012-04-12T12:42:40Z
dc.date.issued2012-04-12
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/3935
dc.descriptionDepartment of Kiswahili and other Foreign Languages,74p.The LB 1044.6 K4M6 2011
dc.description.abstractRedia ni chombo cha ufundishaji na ujifundishaji kinachotumika katika nchi nyingi duniani. Ufanisi wake nchini Kenya umekuwa jambo la kubahatisha. Kwa miaka mingi, vipindi vya redia vimekuwa vikitumika shuleni kwa ufadhili wa Serikali ya Kenya. Hata hivyo, mwaka wa 1995 upeperushaji wa vipindi vya shule ulikatizwa kutokana na gharama za juu za kuandaa na kupeperusha vipindi hivyo ambavyo serikali ilishindwa kusitiri. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza ukubalifu wa vipindi vya redio vya Taasisi ya Elimu Nchini Kenya hasa mielekeo na uelewa wa walimu na wanafunzi na kubaini vipengele vya lugha vinavyoweza kufunzwa vema kupitia kwa redio. Nia ya utafiti huu ilikuwa ya kuchunguza uelewa na mielekeo ya walimu na wanafunzi kuhusu vipindi vya Taasisi ya Elimu Nchini Kenya. Utafiti huu ulifanyiwa Nairobi, Kenya. Walengwa wa utafiti walikuwa walimu na wanafunzi wa shule za upili za Nairobi. Sampuli ya shule nane iliteuliwa, shule mbili mbili kutoka katika viwango vifuatavyo: shule za kitaifa, mkoa, wilaya na za kibinafsi. Mbinu ya uteuzi wa sampuli kusudio ilitumika kuteua sampuli ya shule za upili. Jumla ya watafitiwa mia mbili na kumi na sita ilikuwa ndiyo sampuli ya utafiti. Vifaa viwili vya utafiti vilitumika kukusanya data: hojaji na mahojiano. Data ilichambuliwa kwa njia ya maelezo. Uchanganuzi wa data ulifanyiwa kupitia kwa mfumo wa tarakilishi wa SPSS. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa mielekeo na uelewa wa walimu na wanafunzi kuhusu vipindi vya Taasisi ya Elimu Nchini Kenya ni chanya. Walimu na wanafunzi walipendekeza hatua muhimu za kuimarisha vipindi vya redio. Utafiti huu ulikuwa wa manufaa hasa katika kutatua changamoto zinazosababishwa na mielekeo na uelewa wa walimu na wanafunzi kuhusu vipindi vya Taasisi ya Elimu Nchini Kenya.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.language.isoenen_US
dc.subjectRadio in education --Kenya --Nairobi
dc.subjectEducation broadcasting --Kenya --Nairobi
dc.titleMielekeo na uelewa wa walimu na wanafunzi wa sekondari kuhusu vipindi vya redio vya taasisi ya elimu nchini Kenya: utafiti wa Nairobien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record