• English
    • français
  • English 
    • English
    • français
  • Login
View Item 
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

Usawiri wa maudhui ya ndoa katika ushairi wa Euphrase Kezilahabi na Kithaka Wa Mberia

Thumbnail
View/Open
Full text Thesis (47.09Mb)
Date
2012-02-21
Author
Gicuku, Margaret
Metadata
Show full item record
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia usawiri wa maudhui ya ndoa kama yanavyodhihirika katika ushairi wa Kiswahili. Katika kuendeleza kazi hii, mtafiti ameteua ushairi wa Euphrase Kezilahabi; Kichomi (1974) na wa Kithaka wa Mberia Bara Jingine(2001) na Msimu wa Tisa (2007). Ndoa ni asasi muhimu na ya kimsingi katika maisha ya binadamu. Ni mojawapo ya asasi zinazohakikisha kukua na kuendelea kwa jamii. Utafiti huu umechochewa na imani kwamba ndoa ina manufaa kwa jamii. Ndiyo msingi wa familia na pia ndiyo hujenga jamii. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya umuundo-utekelezi. Nadharia hii hueleza kuwa jamii ni mfumo unaochangiwa na vipengele vyake vyote ili kuleta mshikamano na utangamano. Nadharia hii husisitiza juu ya utekelezaji wa majukumu ya wanajamii ili waendelee kuwa vipengele muhimu vya jamii. Ndoa ni mojawapo ya vipengele vinavyochangia mshikamano huo. Data ya kimsingi imepatikana maktabani kutokana na kazi teule. Aidha mtafiti amesoma makala, vitabu na tasnifu kupata ujumbe unaohusiana na mada hii. Amezingatia pia mtandao ili kufahamu maswala ibuka yanayohusiana na ndoa. Data imechanganuliwa kwa kuzingatia mihimili ya nadharia iliyoteuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo. Tasnifu hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, malengo ya utafiti na pia sababu za kuchagua mada hii vilevile zimejadiliwa, pamoja na udurusu wa maandishi yanayohusu mada ya utafiti pamoja na misingi ya nadharia. Mbinu za utafiti zilizotumika katika utafiti huu pia zimeangaziwa. Sura ya pili imetalii athari za kijamii katika usawiri wa maudhui ya ndoa katika fasihi andishi ya Kiswahili. Sura ya tatu imebainisha namna mtunzi E.Kezilahabi alivyosawiri changamoto katika asasi ya ndoa, pamoja na hatua zinazofaa kuzingatiwa kukabiliana na changamoto hizo. Sura ya nne imebainisha usawiri wa changamoto katika asasi ya ndoa kaina unavyojitokeza katika ushairi wa Kithaka Wa Mberia na namna ya kukabiliana na changamoto hizo. Sura ya tano ni hitimisho na muhtasari wa sura zote pamoja na matokeo ya utafiti huu. Mapendekezo ya tafiti za baadaye pia yametolewa.
URI
http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/2768
Collections
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages [234]

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback

 

 

Browse

All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

My Account

LoginRegister

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback