Show simple item record

dc.contributor.authorNg’etich1, Daniel Kiprugut
dc.contributor.authorWafula, Richard Makhanu
dc.contributor.authorMaitaria, Joseph Nyehita
dc.date.accessioned2023-07-14T09:38:05Z
dc.date.available2023-07-14T09:38:05Z
dc.date.issued2022
dc.identifier.citationNg’etich, D. K., Wafula, R. M., & Maitaria, J. N. (2022). Maongezi Katika Riwaya Za Kiswahili. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 5(1), 224-233.en_US
dc.identifier.issn2707-3467
dc.identifier.issn2707-3475
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/26232
dc.descriptionArticleen_US
dc.description.abstractMakala hii inaangazia dhima ya maongezi katika riwaya ya Kiswahili. Riwaya ni mojawapo wa tanzu muhimu za fasihi ya Kiswahili ambayo inaendelea kukua kwa upande wa wahusika, dhamira, maudhui, mtindo na upeo. Utanzu wa riwaya ya Kiswahili ulianza mwanzo wa karne ya ishirini wakati James Juma Mbotela alipoandika riwaya ya Uhuru wa Watumwa (1934). Ukuaji wake umeshika kasi zaidi katika mwongo wa mwisho wa karne ya ishirini na mwanzo wa karne ya ishirini na moja. Ni muhimu pia kutambua kuwa, utungaji wa riwaya umeendelea kukua sambamba na uhakiki wake. Katika karne ya ishirini na moja, riwaya ya Kiswahili imefikia utungaji wa kimajaribio (Mwamzandi, 2013:48-66 na Mohamed 2003:78-79). Katika riwaya za kimajaribio, watunzi hujumuisha nadharia, visasili pamoja na kuzungumzia masuala ya utandawazi na soko huru. Ni riwaya ambazo hukiuka miundo ya riwaya iliyozoeleka. Kwa upande wa maongezi, usemaji wa wahusika katika riwaya umekua kutoka sahili hadi changamano kutokana na masuala yanayojadiliwa katika riwaya mahususi. Ni maoni ya waandishi wa makala hii kuwa, usemaji wa wahusika unaweza kuathirika na vipindi vya kihistoria hivyo basi kuwa na mchango muhimu katika maendeleo ya riwaya. Madhumuni ya makala hii ilikuwa ni kuainisha maongezi katika riwaya za Kiswahili. Riwaya ambazo zilichanganuliwa kwa mujibu wa makala hii ni Kusadikika (1951), Mafuta (1984) na Kufa Kuzikana (2003). Riwaya hizo ziliteuliwa kuwakilisha vipindi mahususi vya ukuaji na maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi wa Usemi Hakiki. Kutokana na uchanganuzi huo, makala hii imebainisha mchango wa maongezi kwa ukuaji, maendeleo na uumbufu wa utanzu wa riwaya kwa ujumlaen_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherEAST AFRICAN NATURE & SCIENCE ORGANIZATIONen_US
dc.subjectMaongezien_US
dc.subjectRiwaya ya Kiswahilien_US
dc.subjectUainishajien_US
dc.subjectDhimaen_US
dc.subjectUkuajien_US
dc.titleMaongezi Katika Riwaya za Kiswahilien_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record