• English
    • français
  • English 
    • English
    • français
  • Login
View Item 
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

Tathmini ya Hadithi Fupi Zilizowasilishwa Katika British Broadcasting Corporation: Mtazamo wa Edgar Allan Poe na Leech (1969)

Thumbnail
View/Open
Full text thesis (850.6Kb)
Date
2021
Author
Macharia, Francis Maina
Metadata
Show full item record
Abstract
Utafiti huu umetathmini hadithi fupi zilizowasilishwa katika BBC kwa kuzingatia mtazamo wa Edgar Allan Poe. Katika kufanya hivyo, mtafiti amejihusisha na uhakiki wa mikusanyiko: Mapenzi ni Kikohozi (1970), Vituko Duniani (1970), Pavumapo Palilie (1971) na Kinywa Jumba la Maneno (1977) za kipindi kati ya 1970 hadi 1977 maarufu kama “Hekaya za Kuburudisha” zilizochapishwa na shirika la Longman Kenya wakishirikiana na BBC. Mikusanyiko hii inajumuisha hadithi ambazo zilitokea kuwa bora na hivyo zikasomwa hewani na shirika la utangazaji la BBC na hatimaye zikachapishwa kwanzia 1970 hadi 1977. Mtafiti amezingatia mtazamo wa Edgar Allan Poe (1842; 1846) na kipengele cha uhakiki cha mtindo katika kutalii hadithi hizi na kukadiria usanii wa watunzi wa hadithi fupi teule. Kwa kufanya hivyo, ametathmini hadithi fupi zilizowasilishwa katika BBC. Nadharia ya uhakiki ya mtindo pamoja na misingi ya hadithi fupi iliyowekwa na Poe (1842; 1846) imetumika katika kufanikisha utafiti huu. Leech na Short (1981) wanafafanua mtindo kama namna mwandishi anavyotumia lugha kuzingatia muktadha maalumu na kwa lengo mahsusi. Mtindo ni ule upekee wa kujieleza katika maandishi au mazungumzo. Poe (1842; 1846) anaweka misingi ya hadithi fupi kwa kuorodhesha vigezo muhimu ambavyo vinafaa kuzingatiwa ili kufanya hadithi fupi kuvutia na kuwa bora. Nadharia ya mtindo na misingi iliyowekwa na Poe imesaidia katika kutathmini hadithi fupi zilizoko katika mikusanyiko hii ya awali zaidi. Mbinu ya utafiti iliyotumika ni ya kimaelezo ikirutubishwa kwa kiasi fulani na mbinu ya kitakwimu. Mbinu ya kimaelezo imetumika pale ambapo mtafiti amedondoa sentensi au matukio ya kimaelezo na kuchanganua hadithi teule. Aidha, mbinu ya kitakwimu imetumika wakati wa kuteua hadithi mbalimbali kutoka mikusanyiko ya hadithi fupi tuliyoorodhesha. Sampuli imeteuliwa kimaksudi. Utafiti umekuwa wa maktabani. Inatarajiwa utafiti huu utakuwa na mchango hasa kwa upande wa muundo, maudhui na usawiri wa wahusika katika mtindo kwa kuonyesha namna hadithi fupi inastahili kusukwa ili kuwafaa waandishi chipukizi katika kusanii kazi zenye ubora wa muundo, mtindo na maudhui.
URI
http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/22884
Collections
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages [234]

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback

 

 

Browse

All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

My Account

LoginRegister

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback