• English
    • français
  • English 
    • English
    • français
  • Login
View Item 
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

Ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi katika shule za upili

Thumbnail
View/Open
Full text thesis (81.49Mb)
Date
2012-01-04
Author
Mwangi, Jacinta Wangeci
Metadata
Show full item record
Abstract
Utafiti huu unahusu misingi ya ugumu wa ushairi wa Kiswahili katika shule za upili. Misingi hii imeelezwa na kujadiliwa kulingana na maelezo ya walimu, wanafunzi, wakuza mitaala kutoka Taasisi ya Elimu Kenya, pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Nadharia changamano iliyoongoza na kuelekeza utafiti huu ilikita misingi yake katika nadharia ya umaumbo na ya ushirikiano. Kwa kuzingatia misingi ya nadharia hizi, misingi ya ugumu wa mashairi imetathminiwa. Kadhalika, lugha ya kishairi imechanganuliwa, na kuonyeshwa namna inavyokiuka na kupotosha lugha ya kawaida. Imeelezewa namna lugha ya kishairi inavyokiuka lugha ya kawaida katika viwango tofauti. Kwa mfano, ina ukiushi wa kilahaja, kitahajia, awamu ya kihistoria, kisajili na kisemantiki. Pia mna maelezo kuhusu uchanganuzi wa lugha ya kishairi katika viwango vitatu; kiwango cha tamathali za usemi, cha mikakati ya kujielezea na cha kisauti. Tasnifu hii imegawika katika sura tano. Sura ya kwanza ina utangulizi wa tasnifu. Katika sehemu hii, mna mada ya utafiti, sababu za utafiti na madhumuni ya utafiti. Upeo wa utafiti pia umeshughulikiwa katika sehemu hii. Pia, ina maelezo kuhusu yale yaliyoandikwa kuhusiana na mada hii, mbinu za utafiti pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti huu. Sura ya pili ina maelezo juu ya fasili za dhana ya ushairi na namna zinavyoweza kuathiri ujifunzaji na ufundishaji wa ushairi. Vile vile sura hii ina maelezo kuhusu malengo ya kielimu ya kufundisha ushairi katika shule za upili pamoja na umuhimu wake. Sura ya tatu ina maelezo na mjadala kuhusu misingi ya ugumu wa mashairi kama ilivyoelezwa na wanafunzi. Lugha, umbo, uhaba wa vifaa, mielekeo hasi na uhaba wa wakati, ndiyo msingi iliyotajwa na wanafunzi. Sura ya nne inahusu maelezo ya walimu na maafisa wa elimu kuhusu ufundishaji wa ushairi wa Kiswahili na matatizo yake. Matatizo yanayoukumba ufundishaji wa ushairi ni Lugha ya kishairi, uhaba wa vifaa na wakati, mielekeo hasi pamoja na mbinu zisizofaa. Sura ya tano inahusu uchanganuzi wa viwango mbalimbali vya Lugha ya Kiswahili. Kura ya sita ina muhtasari wa tasnifu, mahitimisho, pamoja na mapendekezo kutokana na utafiti.
URI
http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/2239
Collections
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages [234]

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback

 

 

Browse

All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

My Account

LoginRegister

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback