Show simple item record

dc.contributor.authorMose, Ezra Nyakundi
dc.date.accessioned2011-12-30T08:18:27Z
dc.date.available2011-12-30T08:18:27Z
dc.date.issued2011-12-30
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/2184
dc.descriptionThe PL 8704.T3M6en_US
dc.description.abstractKatika tasnifu hii, taashira za kifo katika fasihi ya Kiswahili zimechunguzwa. Tamthifa za Kiswahili ambazo zimenakidiwa katika utafiti huu ni pamoja na Mukwava wa Uhehe (Mulokozi, M. 1979), Kilio cha haki (Mazrui, A. 1982), Amezidi (Mohamed, S. A 1995) na Visiki (Ongeti, K. 1984). Kazi hizi zimehakikiwa kwa mujibu wa nadharia ya vikale ifyoaziziwa na Northrop Frye kutoka Kanada katika mwaka wa 1947. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kutathimini jinsi kifo kimetumika kif'ani na kimaudhui katika utunzi wa tamthilia za Kiswahili. Aidha,utafiti huu ulilenga kuchunguza taashira mbalimbali za kifo zinazojitokeza katika tamthilia za Kiswahili. Kufikia malengo haya na kama ilivyotajwa hapo juu, nadharia ya vikale iftanuliwa kwa kutumiwa katika uhakiki wa tamthilia zilizoteuliwa. Hivyo, katika utafiti huu imcbainika ya kwamba kifo kimetumika katika utunzi wa tamthilia za Kiswahili na katika kujenga na kuimarisha maudhui katika tamthilia hizo. Miongoni mwa taashira za kifo ambazo zilidhihirika katika tamthilia za Kiswahili ni ushujaa, usaliti, uzalendo, utupu wa maisha, na uozo wa mawazo. Vilevile, kifo kimetumika kisanaa katika tamthilia zilizoteuliwa kama mbinu ya utunzi ya kuwapisha na kuwaondosha wahusika kutoka jukwaani. Sura ya kwanza na ambazo inatanguliza tasnifu, imeshughulikia sNvala la utafiti, sababu za kuchagua mada, madhumuni ya utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada, mbinu za utafiti na uchanganuzi wa data. Katika sura ya pili, usuli na historia ya matumizi ya kifo katika kazi za fasihi yameelezwa. Aidha dhana kifo kama kikale imefafanuliwa na mifano mahsusi kutolewa. Vilevile, wahakiki mbalimbali katika vipindi mahsusi vya historia wamerejelewa katika sehemu hii. Sura ya tatu imeshughulikia uhakiki wenyewe wa tamthilia mbili ambazo ni za Mukwava wa Uhehe na tamthilia ya Kilio cha Haki. Tamthilia hizi zimejumuizwa katika sura moja kwa vile zimeakisi maswala ya ukombozi wa haki za Waafrika katika kipindi cha historia cha ukoloni. Sura ya nne imeshughulikia uchanganuzi wa tamthilia za Amezidi na Visiki. Tamthilia hizi vilevile zimehakikiwa kwa pamoja kwa sababu zimetathimini maudhui ya uongozi mbaya wa nchi za Afrika katika kipindi cha baada ya ukoloni. Tamthilia hizi zote zimehakikiwa kwa mapana na marefu katika sura hizo mbili kwa mujibu wa mihimili ya nadharia ya vikale. Sura ya tano na ya mwisho ina hitimisho la uchunguzi na matokeo ya utafiti kwa jumla. Mapendekezo ya utafiti mwingine ambao unaweza kufanywa hapo baadaye vilevile yametolewa katika sura hii. Kutokana na utafiti huts, imedhihirika ya kwamba kifo kimeweza kutumiwa kisanaa katika utunzi wa tamthilia na katika kujenga na kuimarisha dhamira za mtunzi.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.language.isoenen_US
dc.subjectMulokozi, mumukwara wa uhehe//Mazrui,A; kilio cha haki//Mohamed,S.A; Amezidi//Ongeti,K; Visiki//Deathen_US
dc.titleTaashira za kifo katika tamthilia za mukwava wa uhehe, amezidi, kilio cha haki na visikien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record