Matumizi ya majazi kama mkakati wa kuepuka upigaji marufuku katika riwaya za G.K Mkangi za mafuta(1984) na walenisi(1995)
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia swala la upigaji marufuku na matumizi ya majazi katika riwaya teule za Kiswahili. Riwaya zilizohahakikiwa ni Mafuta (1984) na Walenisi (1995) za G.K Mkangi. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya mtindo. Nadharia hii imeegemea kitengo cha kimajazi. Majazi yameonyeshwa jinsi yalivyotumika katika viwango mbalimbali katika riwaya teule. Tasnifu hii ina sura sita. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti Tumeshughulikia mada ya utafiti, malengo ya utefiti, sababu za za kuchagua mada, yallyoandikwa kuhusu made na vilevile upeo wa utafiti. Pie tumejadili nadharia na mihimili yake na vilevile mbinu za utafiti. Sura ya pili imejadili historic ya upigaji marufuku Ulimwenguni, Afrika na nchini Kenya. Sure ya tatu imejadili maisha ya mwandishi G.K Mkangi. inahusisha maisha yake ya awali, elimu, kazi na uandishi wake. Sura ya nne na tano zinachunguza jinsi riwaya za Mafuta na Welenisi zinavyotumia majazi kuepusha upigaji matufuku. Sura ya site imeshughulikia matokeo ya utafiti,matatizo yaliyokabiliwa katika utafifi na mapendekezo ya utafiti wa baadays.
Kutokana na utafiti huu,imebainika wazi kwamba Mkangi anatumia majazi kimakusudi. Anatumia majazi kuepuka kupigwa marufuku kwa kazi yake. Majazi yanamwezesha kushambulia wenye mamlaka bila ya kuamsha hasira yao. Hivi anatoa hadharani upungufu wa jamii na kuitaka ijirekebishe.