Show simple item record

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorNyangena, Thomas Arege
dc.date.accessioned2018-02-13T08:09:13Z
dc.date.available2018-02-13T08:09:13Z
dc.date.issued2013-07
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/18205
dc.descriptionTasnifu hii imetolewa ili kutoshelesha baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Julai, 2013en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umechanganua matumizi ya tasifida katika jamii ya Abagusii kwa madhumuni ya kuwahamasisba wanajamii kubusu matumizi ya lugha ya adabu na heshima dhidi ya lugha isiyostahili wakati wanapowasiliana. Matumizi ya lugha isiyostahili katika mawasiliano yanazua mafarakano, utengano, chuki na hata buyakatisba mawasiliano na hivyo lengo lake kutofikiwa ama ujumbe unaowasilishwa kutopitishwa ipasavyo. Hali hii ilimtia mtafiti motisha ya kuchunguza na kuweka bayana namna tamathali ya tasifida inavyotumiwa katika kuunda maneno ya hesbima pamoja na maelezo kwa njia ya mzunguko yanayofaa kuchukua mahali pa maneno yasiyostahili ili kuyakamilisha mawasiliano. Nadharia ya Ethnografia ya mawasiliano iliongoza utafiti wetu hadi ukakarnilika. Maelezo ya kimsingi kubusu jamii ya Abagusii iliyotafitiwa yalitolewa ili kumpa .msomaji wa tasinifu hii msingi imara wa kuyaelewa matumizi ya lugha kuhusu jamii hii. Matumizi ya maneno ya staha katika mazungurnzo, yanawafanya wanajamn kutambua umuhimu wa kuwa na besbima pamoja na kulinda utamaduni wao. Tasifida inapotumiwa katika mawasiliano, inzifanya mada ambazo sizizotamanika kuwa za kupendeka na kufuraikia wakati wanajamii wanatoa boja zao hadharani. Matumizi ya maneno yasiyostahili katika mawasiliano, huwafanya wanajamii kuona fedheha na hivyo wanaogopa kuyazungurnzia maswala mengi hadharani. Lugha inayostahili kwa mawasiliano inapotumiwa kuwasiliana, inawezesba wanajamii kuzipitisha tamaduni zao kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Mbinu kadbaa zinatumiwa katika kuunda tasifida. Vlll Baadhi ya mbinu hizo ni mafumbo, taashira, sitiari na tashbihi. Kupitia kwa mbinu hizi, maneno ya heshima yanaundwa na kutumiwa ili kuyatimiza mahitaji katika mawasiJiano. Utafiti wetu unadhihirisha kwamba matumizi ya tasifida katika mawasiliano yanaiboresha lugha ya mawasiliano. Aidha tasifida hupunguza makali ya maneno yasiyostahili. Hali hii inayafanya mazungurnzo baina ya wanajamii kuwa ya kutamanika Kwa upande mwingine tasifida katika lugha ya mawasiliano yanaufanya ujumbe kuwafikia wanajamii wote bila kuwabagua. Vile vile, matumizi ya tasifida katika mazungurnzo yanachangia kwa kiwango kikubwa kujenga uhusiano mwema pamoja na kuhifadhi maadili miongoni mwa wanajamii. Lugha inayostahili inapotumiwa katika mawasilaino, inachangia katika kulinda na kuhifadhi tamaduni za jamii husikaen_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.language.isootheren_US
dc.titleTasifida katika jamii ya Abagusti: Mtazamo wa isimujamiien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record