Show simple item record

dc.contributor.authorMalenya, Mary
dc.date.accessioned2011-11-15T09:30:00Z
dc.date.available2011-11-15T09:30:00Z
dc.date.issued2011-11-15
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/1639
dc.descriptionThe PL 8701.M34en_US
dc.description.abstractKatika tasnifu hii tumechunguza lugha na jazanda alizotumia marehemu Jacob Luseno katika nyimbo zake. Kazi hii imeshughulikia jinsi Luseno alivyoteua tamathali za usemi kulingana na vipindi vitatu vya utawala nchini Kenya na pia kuonyesha vile lugha ilivyooana na matukio mbalimbali nyakati hizo. Sura ya kwanza imetupa mwelekeo wa utafiti wetu. Tumejadili swala la utafiti na kuelezea nadharia itakayotuongoza katika kuchanganua nyimbo tulizochagua. Tumeeleza kwa nini tulimchagua mwimbaji huyu na vile vile kujadili kazi za waandishi wengine zinazohusu nyimbo. Tumeonyesha pia upeo wa tasnifu yetu na kusisitiza kwamba tutalenga nyimbo tano kutoka kila kipindi cha utawala. Sura ya pili imejadili historia ya Luseno na maisha yake kwa ujumla. Tumeeleza bendi mbalimbali alizojiunga nazo pamoja na washirika wenzake katika uimbaji. Tumechanganua, japo kwa ufupi, maudhui katika baadhi ya nyimbo za Luseno ili tupate kutambua na kufafanua jinsi alivyotumia lugha. Tumeonyesha kuwa kuna nyimbo ambazo hazina tamathali zozote, lakini Luseno ametiririsha maudhui ipasavyo. Sura ya tatu imejadili nyimbo alizoimba Luseno katika kipindi cha kwanza cha utawala nchini Kenya. Tumeteua nyimbo tano na kuzichanganua. Tumejadili tarnathali zilizotumika kama vile misemo, tashbihi, chuku, balagha na takriri. Tumepata kwarnba Luseno alizitoa katika jamii yake kwa hivyo zinaoana vilivyo na kipindi husika. Sura ya nne imejadili nyimbo zilizoimbwa katika kipindi cha pili. Tumetaja baadhi ya nyimbo hizo, tuliteua nyimbo tukazitafsiri na kuzichanganua kwa misingi ya matumizi ya lugha. Vile vile tumepata misemo, takriri, chuku, kinaya na tashbihi zilizotumika. Katika sura ya tano tumejadili nyimbo tano alizoimba Luseno katika kipindi cha tatu. Tumechanganua kwa undani lugha aliyotumia Luseno na kupata kuwa anazungumzia matukio halisi katika jamii yake. Analalamika jinsi wanawake walivyobadili tabia waliporudi kutoka Beijing. Pia anakashifu tabia mbaya kama vile ulevi na uasherati inayoendelezwa na baadhi ya wanajamii. Sura ya sita ni hitimisho la utafiti wetu. Tumeeleza matatizo yaliyotukumba, mapendekezo na mafanikio ya utafiti huu. Mapendekezo tuliyotoa yanaonyesha baadhi ya vipengee muhimu ambavyo vinafaa kutafitiwa katika nyimbo. Kutokana na utafiti huu tumethibitisha kuwa nyimbo nyingi za Luseno zinaweza kugawanywa katika vipindi vitatu vya utawala nchini Kenya kama ifuatavyo: Kabla uhuru hadi baada ya uhuru 1958 - 1978 (Agosti), Kipindi cha pili: 1978 - 2002 (Disemba) na Kipindi cha tatu: 2003 - 2006. Baadhi ya nyimbo hizi zinaweza kuwekwa katika zaidi ya kipindi kimoja. Hii ni kwa sababu miongoni mwa matatizo yaliyoikumba nchi ya Kenya kabla ya uhuru yangali yanaendelea hata baada ya uhuru na basi kumfanya mtunzi kuyarejelea katika nyimbo zake. Kwa mfano, matatizo kama ya unyang' anyi wa mali ya watu yalizungumziwa katika wimbo `Makuru' kwenye kipindi cha kwanza. Katika kipindi cha pili, Luseno ameendeleza maudhui haya kwa kuimba wimbo wa `Itembel Katika kipindi cha tatu, Luseno ameimba wimbo `Basololi' wenye maudhui ya unyang'anyi. Ingawa nyimbo hizi zimeimbwa katika vipindi tofauti vya utawala nchini Kenya, kuna uoanifu mkubwa wa maudhui na hivyo tunaweza kuziweka katika zaidi ya kipindi kimoja. Hatimaye, tumethibitisha kuwa lugha na jazanda zinazotumika na Luseno katika nyimbo zake zinalandana vizuri na mazingira yake, maudhui na dhamira zake.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.language.isootheren_US
dc.subjectSwahili language -- Figures of speech//Luseno, Jacob -- Songs and music -- Kenyaen_US
dc.titleMatumizi ya lugha na jazanda katika nyimbo za Jacob Lusenoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record