• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Master Theses and Dissertations(MST)
    • MST-School of Humanities and Social Sciences
    • MST-Department of Kiswahili and African Languages
    • MST-Department of Kiswahili and African Languages
    • View Item
    •   Repository Home
    • Master Theses and Dissertations(MST)
    • MST-School of Humanities and Social Sciences
    • MST-Department of Kiswahili and African Languages
    • MST-Department of Kiswahili and African Languages
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uchanganuzi wa usemi katika sajili ya dini: sifa bainifu za lugha ya mahubiri

    Thumbnail
    View/Open
    Thesis full text (64.76Mb)
    Date
    2001
    Author
    King'ei, Kitula Osore, Miriam
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Katika tasnifu hii, tumechunguza sifa bainifu za lugha ya mahubiri kama zinavyojitokeza katika sajili ya dini katika lugha ya Kiswahili. Tumetumia data kutokana na mahubiri mbalimbali na kuyachanganua ili kudhihirisha sifa zake. Utafiti huu ulikuwa na malengo mawili ambayo ulitekeleza. Kulikuwa na utambuzi wa sifa bainifu za lugha ya mahubiri na utambuzi wa aina za mshikamano na jinsi zinavyounganisha. mahubiri. Katika kufanya hivi, mtazamo wa kimtindo na wa mshikamano katika nadharia ya uamilifu wa lugha ilitumika. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi wa tasnifu imeshughulikia swala la utafiti, sababu za kuchagua swala lenyewe, madhumuni ya utafiti, upeo wa utafiti, misingi ya kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu somo lile na mbinu za utafiti. Ni katika sura ya pili ambapo tumejishughulisha na baadhi ya sifa bainifu katika lugha ya mahubiri kama vile jinsi wahubiri wanavyoanza mahubiri yao, njia wanazoturnia kuendeleza ujumbe, na namna wanavyohitimisha. Kutokana na uchunguzi wetu tuligundua ya kwamba kuna mianzo maalum ya kuanza mahubiri. Kwa jumla wahubiri huanza kwa maamkuzi na pia kutaja kiini cha ujumbe wao.Wahubiri hutumia njia nyingi kuendeleza ujumbe kama vile matumizi ya mifano takriri, kubadilisha sauti, maswali na kadhalika. Pia, kuna njia maalum za kutamatisha mahubiri. Katika kila ruwaza iliyojadiliwa, maelezo ya kiisimu yametolewa. Sura ya tatu yaonyesha kuwa mahubiri yana sifa ya kuchanganya msimbo. Kuchanganya msimbo kumeshughulikiwa kama mojawapo ya sifa bainifu katika kuendeleza ujumbe. viii • Aina muhimu za kuchanganya msimbo na JlOS1 zinavyojitokeza katika matini za uchanganuzi zimejadiliwa. Sura ya nne yaonyesha kuwa lugha ya mahubiri ina aina mbalimbali za mshikamano. Kwa mfano, kuna mshikamano wa kimsamiati, urejeshi, uunganishi, ubadilishaji na udondoshi. Sura ya tano na ya mwisho inajumuisha muhstasari na matokeo ya utafiti kwa jumla. Mapendekezo ya utafiti mwingine unaoweza kufanywa katika uwanja huu pia yamewekwa katika sura hii
    URI
    http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14837
    Collections
    • MST-Department of Kiswahili and African Languages [213]

    Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Browse

    All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
    Contact Us | Send Feedback