Masuala ibuka katika riwaya za kisasa: kidagaa kimemwozea na mhanga nafsi yangu
Abstract
Utafiti huu unatathimini namna masuala ibuka yanavyosawiriwa katika riwaya za kisasa. Katika kuendeleza kazi hii, mtafiti anateua riwaya mbili za kisasa ambazo ni: Kidagaa Kimemwozea(2012) ya Walibora Kenna Mhanga Nafsi Yangu (2012) ya Mohamed S.A. Masuala ibuka ni mambo halisi yanayoikumba jamii ya kisasa ambayo inapitia mabadiliko mengi. Mabadiliko haya huwa ni ya kijamii, kisiasa, kiuchurni, kidini na kiteknolojia na huiathiri jamii katika mawanda yote. Waandishi wa riwaya wanateua masuala yenye mguso kwa jamii na kuyasimulia kwa kiwango cha juu cha ubunifu. Maudhui haya yanaangazia hali halisi, maingiliano, mivutano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira yao. Malengo ya utafiti huu ni kuangazia mbinu za kisasa zilizotumiwa kuwasilisha masuala ibuka katika riwaya ya kisasa na kubainisha jinsi riwaya ya kisasa inavyoyaangazia masuala ibuka katika jamii ya mwandishi na kufafanua. Utafiti unaongozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia ya uhalisia inaeleza kuwa kazi ya msanii inapaswa kuwasilisha ukweli kama ulivyo katika mazingira, matukio yanayosimuliwa sharti yawe yanatokea katika ulimwengu halisi na msanii anayaangalia matatizo ya jamii na kuchunguza vyanzo vyake. Mihimili ya nadharia hii inaturnika kama dira katika kutafiti huu. Uteuzi wa sampuli ni Kidagaa Kimemwozea ya Walibora Ken naya Mhanga Nafsi Yangu yake Mohamed S.A. Riwaya hizi zinatupa data faafu katika utafiti huu. Data ya kimsingi inakusanywa maktabani kutokana na kazi teule, majarida, magazeti, tasnifu na kwa mtandao. Data inayopatikana inachanganuliwa kwa kuzingatia maswali ya utafiti, malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia teule. Matokeo yanawasilishwa kwa njia ya maelezo.