Mgongano wa tamaduni katika hadithi fupi za kiswahili
Abstract
Mtafiti alihakiki kazi za waandishi teule wa hadithi fupi. Kazi zilizochanganuliwa ni kutokana na
vitabu vinne vya hadithi fupi ambavyo ni pamoja na Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi
Nyingine kilichohaririwa na K.W.Wamitila(2004), Kiti cha Moyoni na Hadithi Nyingine
kilichohaririwa na Ken Walibora na Said Mohamed(2007), Mwendawazimu na Hadithi Nyingine
kilichohaririwa na Mwenda Mbatiah(2000) pamoja na Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine
kilichohaririwa na Ken Walibora na Said Mohamed(2007). Utafti huu unaongozwa na nadharia
ya udhanaishi. Udhanaishi ni falsafa inayoshughulikia masuala kuhusu maisha. Ni mtazamo
unaokagua .kwa upembuzi hali na nafsi ya mtu katika ulimwengu anaoishi. Pia ni falsafa
inayozungurnzia uhusiano uliopo kati ya mtu na Mungu na iwapo mtu anapaswa kuamini
kuwepo kwa Mungu. Nadharia hii hujaribu kueleza uhuru wa mtu binafsi, uwezo wa mtu
kujifikiria na kujiamulia ni wajibu wa binadamu katika ulimwengu. Kupitia nadharia hii ni
dhahiri kwamba jinsia ya kike na kiurne wanaathiriwa pakubwa na utamaduni huu hasi. Rata
hivyo kuna matumaini ikiwa binadamu mwenyewe atajinasua katika mtego huu kwa kuzielewa
na kuzipigania haki zake.