Usimulizi katika riwaya za; adili na nduguze, walenisi na babu alipofufuka.
Abstract
Usimulizi ni dhana iliyohusishwa kwa muda mrefu na hadithi. Hadithi ni mojawapo ya
tanzu za fasihi simulizi, ambayo hutolewa kwa maelezo ya nathari. Huhusisha vipera
kama vile; ngano, rnighani, hurafa, hekaya, visasili, visakale ngano za mtanziko na visa
vingine. Kihistoria, fasihi ya Kiafrika ilisimuliwa na kupitishwa kwa vizazi kwa njia ya
mdomo na kuhifadhiwa katika kurnbukumbu. Fasihi andishi ni utanzu mpya uliokuja
kufuatia kuanzishwa kwa maandishi ili kuweza kuhifadhi sanaa ya fasihi ya Kiswahili.
Riwaya kwa hivyo, ni ngeni katika Kiswahili kwa vile ililetwa na majilio ya hati za
kirurni zilizoletwa na Wazungu na kuturnika kuihifadhi fasihi. Utafiti mwingi uliofanywa
unaonyesha kuwa, riwaya ambayo huturnia maelezo ya nathari inaelekea kuwiana na
simulizi na wengine wanapinga kabisa kuwa, hakuna uhusiano kati ya riwaya na simulizi.
Hata hivyo, kumezuka riwaya mbalimbali katika nyakati mbalimbali ambazo zimetatiza
ufasiri na uhakiki wake. Kwa sababu ya riwaya kuwa ya nathari kama ngano,
yawezekana sifa za usimulizi zipatikanazo katika simulizi (zilizo pia na mtindo wa
nathari) kuturnika katika utunzi na uhakiki wa riwaya ya Kiswahili. Ifaharnikavyo ni
kuwa, simulizi zina muundo maalumu wa kifomyula ambao zinaturnia kupitisha ujumbe
wake na hivyo, kuna makisio kuwa, ndani yake kuna vipengele maalumu vinavyoweza
kuturniwa kufasiri vipengele muhimu riwayani. Hadithi ndizo zinazohusishwa sana na
rniundo na maumbo ya usimulizi. Katika uhakiki wa ngano uliosharniri huko Ulaya,
walihakiki masimulizi kifomyula. Hata hivyo, uhakiki wa riwaya umefungika kwa muda
mrefu kwa rnisingi ya maudhui, wahusika na mtindo huku umbo na muundo wake
ukipuuzwa, hali ambayo inaathiri ufasiri na uhakiki wake. Kuna haja ya kutalii nafasi ya
rniundo na maumbo ya usimulizi katika riwaya ili kuyahusisha na utunzi na uhakiki wake
na kupata uelewa wa kina kuihusu.