Nadharia za Uhakiki kama Mchakato wa Kutaalamisha Usomaji wa Fasihi
Abstract
Utunzi na uhakiki wa fasihi ya Kiswahili umepanuka sana katika miongo mitano iliyopita. Makala haya yananuia kuonyeshe dhima ya nadharia katika kutaalamisha usomaji wa fasihi. Nadharia za uhakiki (na wakati mwingine za utunzi) zimepevusha usomaji na uhakiki kwa viwango ambavyo havingeweza kukadirikeahapo awali. Kwa njia hii, lugha ya Kiswahili
imeweza kueleza maarifa anuwai kwa viwango vya juu. Nadharia na mikondo ya uhakiki kama usemezano na udenguzi vimetuwezesha kuchanganua matini ya kifasihi kwa jicho la upekuzi. Kwa upande mwingine, changamoto katika utumiaji wa baadhi ya nadharia hizi zimejitokeza na zinapaswa lwtathminiwa katika mazingira ambamo lugha ya Kiswsbili inaendelea kutumiwa lwfafanulia ujuzi wowote ule. Makala haya yanatalii manufaa ya matumizi ya nadharia katika uhakiki na kuweka wazi matatizo yanayoandamana na matumizi ya baadhi ya nadharia hizo.
Hatimaye, njia mwafaka ya kufuatwa imependekezwa.