Mtindo na dhamira katika mashairi ya kiswahili ya washairi chipukizi kutoka kaunti ya Bungoma
Abstract
Utafiti umechunguza mtindo na dhamira katika mashairi ya Kiswahili ya washairi chipukizi
kutoka kaunti ya Bungoma. Kwa kutumia mbinu kusudio, Toili Khisa, Martin yongesa na
Brian Mutambo waliteuliwa ili kuwawakilisha washairi wengine chipukizi kutoka kaunti ya
Bungorna nchini Kenya. Malengo ya utafiti yalikuwa kubainisha mtindo katika mashairi ya
washairi chipukizi kutoka kaunti ya Bungoma, kubainisha dhamira zilizofumbikwa kwenye
mashairi ya washairi hawa na kuchunguza jinsi mitindo iliyotumiwa na washairi hawa
ilivyofanikisha uwasilishaji wa dhamira lengwa katika ushairi wao. Kwa ambavyo mtindo
unahusu jinsi mtunzi anavyojieleza kwa kutumia lugha na hufanikisha mawasiliano ya
kifasihi ukiwerno ushairi, utafiti huu uliongozwa na rnihimili miwili ya nadharia ya mtindo na
mwingine mmoja wa nadharia ya maadili. Kwa mujibu wa Leech (1969), nadharia ya mtindo
inashughulikia jinsi lugha inavyotumiwa na mtunzi katika kuwasilisha rnaudhui ya kazi yake.
Kwa upande mwingine, Tolstoy (1960) anasema kuwa ujumi na uzuri wote wa sanaa
hutegemea maadili ambayo hupitishwa kwa wanajamii. Vile vile, sanaa nzuri ni ile ambayo
inaweza kupitisha ujumbe kwa watu wengi na inaeleweka na kila mtu. Kwa kutumia mihirnili
ya nadharia hizi, utafiti huu umeyachanganua mashairi yaliyokusanywa kutoka kwa washairi
chipukizi ili kupata data iliyokidhi mahitaji ya utafiti. Data iliyopatikana ilirekodiwa na
kuchanganuliwa kulingana na malengo na maswali ya utafiti pamoja na mihimili
changamano ya nadharia zilizotumiwa katika utafiti huu. Uwasilishaji data umefanywa
kimaelezo. Utafiti huu umelenga kuwafaa wasomi, watafiti wa ushairi na wakuza mitaala
nchini Kenya. Tasnifu hii imegawanywa kwa sura tano. Sura ya kwanza ya tasnifu
imetanguliza mada, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka. yaliyoandikwa
kuhusu mada, sababu za kuchagua mada na misingi ya nadharia. Sura ya pili imeshughulikia
chimbuko na maenezi ya ushairi nchini Kenya. Katika sura hii, kando na kutoa fasili mbali
rnbali za ushairi na shairi, tumefafanua asasi na njia mbalirnbali zilizochangia ushairi kuenea
hadi maeneo ya bara ikiwemo kaunti ya Bungoma kwani inaaminika kuwa asili ya ushairi ni
pwani. Katika sura ya tatu, tumechanganua maumbo mbali mbali yanayojitokeza kupitia
mashairi ya washairi chipukizi kutoka kaunti ya Bungoma. Sura ya nne imeshughulikia
tamathali za usemi na jinsi uteuzi wake mwafaka ulivyofanikisha uwasilishaji wa dharnira
lengwa. Mwisho ni sura ya tano ambayo imetoa hitimisho, matokeo ya utafiti na
mapendekezo ya utafiti.