Viwango vya uhalisi na ubunifu ka tika riwaya teule za Kiswahili
Abstract
Katika utafiti huu, tumeshughulikia viwango vya uhalisi na ubunifu katika riwaya teule za Kiswahili: Cheche za Moto (2008) ya Habwe John, Kaburi BUa Msalaba (1969) ya Kareithi P.M. na Kusadikika (1951) ya Shaaban Robert.IIi kuafiki hili, tumeangalia mbinu
zilizotumiwa na waandishi kusawiri uhalisia na ubunifu katika riwaya za Kiswahili. Kila mwandishi ana njia yake ya kipekee ya kuwasilisha kazi yake. Kuna wanaoeleza yaliyotendeka katika jamii kwa uaminifu na kwa narnna ambayo atakayesoma kazi yake ataona ni mambo yanayosadikika au yaweza kutendeka katika jamii. Njia zinazotumiwa na waandishi kama hao zimeangaziwa katika utafiti huu. Zaidi ya hayo kuna waandishi wanaovuta fikra zao na kusimulia visa ambavyo vinaonekana kuwa ni vya kufikirika tu wala haviwezi kutendeka katika ulimwengu halisi. Kazi hizo ndizo tumeita 'ubunifu' katika
utafiti huu. Hivyo basi kazi hii imejaribu kuangazia mbinu hizo na kuona iwapo kuna uhusiano wowote kati ya kazi hizo za kihalisia na kibunifu. Katika kuangalia uhusiano huo, utafiti huu umeangalia namna ambavyo waandishi wa rriwaya zilizotajwa, wameeleza visa
'kibunifu' na namna ambavyo uhalisia unajitokeza katika 'ubunifu' huo. 'Ubunifu' unaojitokeza katika kazi za kihalisi pia umeangaziwa. Nadharia iliyotumiwa ni nadharia ya uhalisia. Nadharia hii imechaguliwa kwa misingi kuwa mihimili yake itatuwezesha
kuchambua vitabu vilivyoteuliwa na kuafiki malengo ya utafiti. Data ya utafiti ilipatikana kwa kusoma vitabu vyote vilivyochaguliwa na yaliyoangaliwa ni namna waandishi wamewasawiri wahusika wao, matukio na mandhari yao. Uchanganuzi ulifanywa kwa njia
ya maelezo na mahitimisho kutolewa kimaelezo. Utafiti huu umeeleza nafasi ya uhalisi na ubunifu katika maendeleo ya riwaya za Kiswahili. Utatoa mchango katika uchambuzi wa riwaya za Kiswahili na matokeo yake kutumiwa katika kuainisha riwaya hizo.